Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,504

Msanii wa filamu kutoka nchini Marekani, Eddie Murphy na mchumba wake, ambaye ni mwanamitindo Paige Butcher, wanatarajia kupata mtoto hivi karibuni atakayefikisha idadi ya watoto tisa wa msanii huyo.
Murphy mwenye umri wa miaka 55, ameweka wazi kupitia mtandao wa Instagram kwamba yeye na mchumba wake wa miaka mitatu wanatarajia mtoto wa kiume.
Kwa sasa Murphy ana jumla ya watoto nane ambapo wa kiume watatu na wakike watano.
Mtoto wa kwanza wa msanii hiyo ana umri wa miaka 25, anajulikana kwa jina la Bria, wengine ni Shayne (21), Zola (15), Bella (13), ambao alizaa na mpenzi wake wa zamani Nicole Murphy kabla ya kuachana 2006 baada ya kukaa miaka 22 kwenye ndoa.
Nadhani mnamkumbuka huyu jamaa kwenye movie yake iliyobamba enzi hizo ya Coming to America.