ECOWAS yaamuru kupeleka Jeshi Niger

ECOWAS yaamuru kupeleka Jeshi Niger

Acha mawazo mgando kwa iyo wewe huko radhi kuwa mtumwa kisa unataka maisha mazuri?
ebu itumie akili yako vzr , tuache kufanya maamuz kwa hisia sio mzungu wala mwarab wala mchina wala mrusi atakuletea maisha mazuri , wenzetu wanajuwa namna ya kunufaika na sis ila sisi hatujui kunufaika na wao
 
Bado sijakuelewa mkuu kabisa yani

Hilo jeshi lililonpindua nchi husika(Niger) ni jeshi alamu au ni jeshi la wananchi? mpaka nalo livamiwe na jeshi la kikanda (ECOWAS )
Kwan zip njia za kumpata kiongoz mkuu wa kiutawala wa nchi , hujui kipi kinawafanya wasiwe halal
 
Unaunga mkono kwakua ww ni mtanganyika watakao teseka ni wa Niger [emoji1183] uko kuna watoto,wamama na wazee.
Sawa kazi ianze kukuche jumapili bukinabe na mali ndio wanaanza safari ya kwenda kuilinda Niger na watu wake.
Utawala wa kiraia unajuwa maana yake?
 
Aaaha sawa! Sasa kama Jesh likiona uongozi wa kiraia hauwanufaishi raia na raia kutwa wanalalamikia huo uongozi wa kiraia, kutakuwa na hualamau wowote jeshi kuipundua serikali ya kirai,maana moyo wawanajeshi ni kuwalinda Rai
Kaz ya jeshi ni kuingiza na kutoa madarakan viongoz wa kiraia ? AMKA MKUU HATUUNGI MKONO RAIS ALIYEPITA ILA HUYU WA SASA KWANN ASIRUDISHE MADARAKA KWA RAIA , UKIFIKA MUDA UTASHIRIKI NASI KUMLALAMIKIA
 
Nchi za Africa tutatumiwa sana Kwa faida za watu wa ulaya,! ECOWAS Ni njia inayotumiwa ili waendelee kutetea uraji wa ufaransa, yaani tunapiganishwa wenyewe Kwa wenyewe! Harafu mtu mweusi anafurahia kabisa[emoji41]
Tuliza akili uelew nin kinaendelea acha story za urusi na ukraine
 
Raia ni wagumu sana kufanya maamuzi ya kumfurusha raisi kwasababu Huwa wanaliogopa jeshi ambalo linamiliki silaha na ambalo linaonekana kuwatii viongozi.

Ila kama raia wamebariki mapinduzi yanini Sasa ECOWAS kutaka kupeleka jeshi. Kitu kinachoonekana sio Cha busara sana ni jeshi la Niger kukataa mazungumzo ila pia huwenda wanaijua ECOWAS vizuri kuliko sisi na ndo maana hawataki mazungumzo nao.

Kama raia wamebariki jeshi kupindua utawala ambao ulikua unaonekana kama mti mkavu kwao basi Mungu AWABARIKI wafanye taratibu zao vizuri waweke utawala WA kiraia ambao unajua raia wanataka Nini na Jeshi lirudi mahala pake huku moyo wao ukiwa juu ya kuwalinda zaidi raia[emoji123]
Unaezaj kujua maoni ya zaid ya raia million 25?
 
Unafikiri kazi ya jeshi ni kulinda tu CCM isitoke madarakani wewe kunguni wa Lumumba. Mtu ukiwa CCM lazima usiwe na akili jinga hili
Mkuu amka siasa za bongo ni za kukariri sana kwamba kama ni Nyekundu bas kote ni nyekundu , SIIPEND CCMU ILA KUONGOZWA NA JESHI NI HTR SANA TULIZA AKILI UJUE HOJA ZA WAKOSOAJI WA UTAWALA WA KIJESHI , HAO WANAJESHI WAITISHE UCHAGUZ UONGOZ URUDI KWA RAIA
 
Pale Syria palichimbika bila bereshi,vumbi lililotimka pale si la kuhadithia.

Ka ECOWAS haka Nako,,,[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Tumia akili mpk ww ujue yote hayo basi wenzio wanajua mengi zaid ya hayo
 
Mkuu amka siasa za bongo ni za kukariri sana kwamba kama ni Nyekundu bas kote ni nyekundu , SIIPEND CCMU ILA KUONGOZWA NA JESHI NI HTR SANA TULIZA AKILI UJUE HOJA ZA WAKOSOAJI WA UTAWALA WA KIJESHI , HAO WANAJESHI WAITISHE UCHAGUZ UONGOZ URUDI KWA RAIA
Unafikiri CCM utaiondoa kwa sanduku la kura ? Wewe ndie utulize kichwa.
 
Fuatilia madai ya ECOWAS , nyiny ndo mnafanya tunaitwa nyani , kila kitu unawawaza wazungu
 
Wanamapinduzi wamesema watamchinja huyo rais waliyempindua kama ECOWAS watapeleka jeshi Niger.
Italy keshamuonya Ufaransa aache kuwashwa washwa ya Niger awaachie wenyewe.
Wagner Group wamesema wapo tayari kuwasaidia Wana mapinduzi.
Busara tu itumike kuepuka makubwa zaidi
 
Wanamapinduzi wamesema watamchinja huyo rais waliyempindua kama ECOWAS watapeleka jeshi Niger.
Italy keshamuonya Ufaransa aache kuwashwa washwa ya Niger awaachie wenyewe.
Wagner Group wamesema wapo tayari kuwasaidia Wana mapinduzi.
Busara tu itumike kuepuka makubwa zaidi
Wamchinje tu liwe fundisho
 
Nigeria ndie anawadrive ECOWAS kisa kapata Dili la uwekaji Bomba la gas toka Nigeria kupitia Niger kwenda ulaya, baada ya Mrusi kuwakatia gas mashoga,pia ili kufika Nigeria kwa wepesi na gharama nafuu za ndege ni lazima upite anga la Niger.
Pia mfaransa anataka uranium ya Niger
 
Mapinduzi
Mapinduzi hayakubaliki na ni upuuzi
---

Umoja wa Ulaya waandaa Vikwazo kwa Niger
.NIGER, Niamey: Umoja wa Ulaya unajiandaa kuiwekea vikwazo serikali mpya ya kijeshi nchini Niger, duru za Ulaya ziliambia Reuters siku ya Jumatano.

Mwanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya na afisa mmoja aliyehusika katika kuunda vikwazo hivyo alithibitisha kuwa umoja huo ulikuwa unabuni vifurushi vya adhabu, vikihusisha "kudhoofisha demokrasia."

Mpango huo huenda ukakubaliwa, afisa huyo aliambia chombo cha habari.

"Hatua inayofuata itakuwa vikwazo dhidi ya wanachama binafsi wa serikali ya kijeshi, ambayo inasemekana kuhusika na kuondolewa kwa rais wa zamani Mohamed Bazoum mwezi uliopita," mwanadiplomasia huyo alisema.

Hakuna tarehe ambayo imetolewa ni lini vikwazo hivi vinaweza kutekelezwa, ingawa mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi 27 za umoja huo wanatarajiwa kujadili uwezekano wa vikwazo pamoja na masuala mengine yanayohusiana na Niger watakapokutana Toledo mnamo Agosti 31.

Umoja wa Ulaya umesitisha ushirikiano wa kiusalama na usaidizi wa kifedha katika kukabiliana na umapinduzi ya mwezi uliopita na kundi la kijeshi linaloongozwa na Jenerali Abdourahamane Tchiani.

Marekani na Canada pia zimesitisha baadhi ya programu za usaidizi, na nchi kadhaa za Ulaya - zikiongozwa na Ufaransa, mtawala wa zamani wa kikoloni wa Niger - pia zimekata misaada kwa nchi hiyo.

Shirika la ukadiriaji wa mikopo la Moody lilishusha viwango vya mikopo vya Niger wiki iliyopita siku chache tu baada ya nchi hiyo kupiga marufuku mauzo ya uranium na dhahabu kwenda Ufaransa.

Benki ya Dunia pia imesitisha malipo ya sekta ya umma kwa Niger.

Imeandaliwa na Mashirika
Tembelea //epaper.tsn.go.tz kusoma zaidi
Una maoni usisite kutuandikia
Ni mazuri pale waliochaguliwa wanapojigeuza miungu watu
 
Back
Top Bottom