Kashishi yetu
JF-Expert Member
- Mar 22, 2014
- 3,634
- 3,941
Mapinduzi
Ni mazuri pale waliochaguliwa wanapojigeuza miungu watuMapinduzi hayakubaliki na ni upuuzi
---
Umoja wa Ulaya waandaa Vikwazo kwa Niger
.NIGER, Niamey: Umoja wa Ulaya unajiandaa kuiwekea vikwazo serikali mpya ya kijeshi nchini Niger, duru za Ulaya ziliambia Reuters siku ya Jumatano.
Mwanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya na afisa mmoja aliyehusika katika kuunda vikwazo hivyo alithibitisha kuwa umoja huo ulikuwa unabuni vifurushi vya adhabu, vikihusisha "kudhoofisha demokrasia."
Mpango huo huenda ukakubaliwa, afisa huyo aliambia chombo cha habari.
"Hatua inayofuata itakuwa vikwazo dhidi ya wanachama binafsi wa serikali ya kijeshi, ambayo inasemekana kuhusika na kuondolewa kwa rais wa zamani Mohamed Bazoum mwezi uliopita," mwanadiplomasia huyo alisema.
Hakuna tarehe ambayo imetolewa ni lini vikwazo hivi vinaweza kutekelezwa, ingawa mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi 27 za umoja huo wanatarajiwa kujadili uwezekano wa vikwazo pamoja na masuala mengine yanayohusiana na Niger watakapokutana Toledo mnamo Agosti 31.
Umoja wa Ulaya umesitisha ushirikiano wa kiusalama na usaidizi wa kifedha katika kukabiliana na umapinduzi ya mwezi uliopita na kundi la kijeshi linaloongozwa na Jenerali Abdourahamane Tchiani.
Marekani na Canada pia zimesitisha baadhi ya programu za usaidizi, na nchi kadhaa za Ulaya - zikiongozwa na Ufaransa, mtawala wa zamani wa kikoloni wa Niger - pia zimekata misaada kwa nchi hiyo.
Shirika la ukadiriaji wa mikopo la Moody lilishusha viwango vya mikopo vya Niger wiki iliyopita siku chache tu baada ya nchi hiyo kupiga marufuku mauzo ya uranium na dhahabu kwenda Ufaransa.
Benki ya Dunia pia imesitisha malipo ya sekta ya umma kwa Niger.
Imeandaliwa na Mashirika
Tembelea //epaper.tsn.go.tz kusoma zaidi
Una maoni usisite kutuandikia