ECOWAS yaamuru kupeleka Jeshi Niger

ECOWAS yaamuru kupeleka Jeshi Niger

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
79,195
Reaction score
85,072
Viongozi wa ECOWAS Wametoa amri ya kupelekwa Jeshi Ili wakawanyoe Waliofanya Mapinduzi huko Niger na kurejesha Serikali ya Kiraia.
---

Viongozi wa Jumuiya ya Uchumi wa Afrika Magharibi (ECOWAS) wameamuru kuanzishwa kwa mpango wa kupeleka jeshi katika kuhakikisha kuurejesha utawala wa kidemokrasia na Rais Bazoum aliyepinduliwa na jeshi Julai 26.

Uamuzi huo umeelezewa katika maazimio yaliyofikiwa Alhamisi baada ya majadiliano ya viongozi wa ECOWAS juu ya hali ya kisiasa nchini Niger katika mkutano wao wa pili. Viongozi hao walikutana mjini Abuja, Nigeria.

Mwanzoni mwa mkutano huo viongozi hao walielezea umuhimu wa kutatua suala la mapinduzi nchini Niger, viongozi hao walitoa onyo kali na kukemea mapinduzi au mabadiliko ya serikali kinyume na katiba, waliazimia kuhakikisha kuwa mapinduzi hayaruhusiwi tena Afrika Magharibi.

Akiwasilisha taarifa ya mkutano huo Rais wa tume ya ECOWAS Omar Toure aliwaambia waandishi wa habari kwamba viongozi hao hawakufurahishwa na majibu ya utawala wa kijeshi huko Niger kukataa kukutana na wajumbe wa ECOWAS waliotumwa kuzungumza nao kuhusu hatua za kuchukuliwa ili suluhu ipatikane kwa ajili ya nchi hiyo.

Omar Toure anasema viongozi hao wameamuru kutekelezwa kwa maazimio ya mkutano uliofanyika Abuja Julai 30 pamoja na uamuzi wa matumizi ya nguvu kurejesha demokrasia katika Jamhuri ya Niger.

Toure anasema viongozi wa ECOWAS wameamuru Kikosi cha Usalama cha ECOWAS kupeleka wanajeshi nchini Niger kurejesha utaratibu wa kikatiba huko jamhuri ya Niger.

Hivi sasa inaelezewa kuwa Rais Bazoum amekubali kujiuzulu na kupisha nguvu ya jeshi.

Hali ya kisiasa nchini Niger imeongeza hofu kuhusu ukosefu wa usalama katika eneo la kaskazini mwa Nigeria na watu wanaoishi maeneo ya mpakani wameanza kuhama kuelekea kusini mwa nchi kwa ajili ya uwezekano wa kushambuliwa na magaidi.

Wachambuzi wanasema uwezekano wa kuingilia kati kijeshi unaweza kuiumiza pia Nigeria kwa namna fulani.

Waziri zamani wa mambo ya nje wa Nigeria pia mtaalamu wa uhusiano wa kimataifa, Profesa Nurudeen Mohammed anasema siku hizi ECOWAS haina nguvu au uwezo kama zamani kwa hivyo viongozi wa kijeshi wa jamhuri ya Niger waliweza kukataa kuwaona wajumbe waliotumwa na ECOWAS kuzungumza nao.

Mkutano wa Alhamisi mjini Abuja ni wa pili kwa viongozi wa Afrika Magharibi katika jitihada zao za kutatua tatizo la kisiasa ambalo limesababishwa na kupinduliwa kwa serikali ya kiraia huko jamhuri ya Niger.

Na uamuzi wa kupeleka vikosi vya jeshi la ECOWAS huko Niamey kurejesha demokrasia na utawala wa kikatiba kunaweza kuwa na mapambano ya muda mrefu ya kuchukua madaraka ambayo hakuna anayejua yataisha lini

My Take
Naunga mkono hoja, wakashikishwe adabu Ili mambo ya kipuuzi yakome mara Moja Africa.

View: https://www.instagram.com/p/Cv9kPHbqh9T/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
 
Mapinduzi hayakubaliki na ni upuuzi
---

Umoja wa Ulaya waandaa Vikwazo kwa Niger
.NIGER, Niamey: Umoja wa Ulaya unajiandaa kuiwekea vikwazo serikali mpya ya kijeshi nchini Niger, duru za Ulaya ziliambia Reuters siku ya Jumatano.

Mwanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya na afisa mmoja aliyehusika katika kuunda vikwazo hivyo alithibitisha kuwa umoja huo ulikuwa unabuni vifurushi vya adhabu, vikihusisha "kudhoofisha demokrasia."

Mpango huo huenda ukakubaliwa, afisa huyo aliambia chombo cha habari.

"Hatua inayofuata itakuwa vikwazo dhidi ya wanachama binafsi wa serikali ya kijeshi, ambayo inasemekana kuhusika na kuondolewa kwa rais wa zamani Mohamed Bazoum mwezi uliopita," mwanadiplomasia huyo alisema.

Hakuna tarehe ambayo imetolewa ni lini vikwazo hivi vinaweza kutekelezwa, ingawa mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi 27 za umoja huo wanatarajiwa kujadili uwezekano wa vikwazo pamoja na masuala mengine yanayohusiana na Niger watakapokutana Toledo mnamo Agosti 31.

Umoja wa Ulaya umesitisha ushirikiano wa kiusalama na usaidizi wa kifedha katika kukabiliana na umapinduzi ya mwezi uliopita na kundi la kijeshi linaloongozwa na Jenerali Abdourahamane Tchiani.

Marekani na Canada pia zimesitisha baadhi ya programu za usaidizi, na nchi kadhaa za Ulaya - zikiongozwa na Ufaransa, mtawala wa zamani wa kikoloni wa Niger - pia zimekata misaada kwa nchi hiyo.

Shirika la ukadiriaji wa mikopo la Moody lilishusha viwango vya mikopo vya Niger wiki iliyopita siku chache tu baada ya nchi hiyo kupiga marufuku mauzo ya uranium na dhahabu kwenda Ufaransa.

Benki ya Dunia pia imesitisha malipo ya sekta ya umma kwa Niger.

Imeandaliwa na Mashirika
Tembelea //epaper.tsn.go.tz kusoma zaidi
Una maoni usisite kutuandikia
 
Hawa viongozi wanaokua vibaraka wa mataifa ya magharibi ni tatizo sana! Acha wapinduane vizuri ipo siku ile nchi ambayo ina kibaraka wa mataifa ya kiarabu anasaini mikataba kama kichaaa kitamkuta jambo
Unadhani kikimkuta atapata mateso kama wewe?
 
Mapinduzi hayakubaliki na ni upuuzi...
Niger imewaumiza sana Wakoloni wanahaha kama mbwa aliekatwa Mkia.

Urusi itaisaidia Niger haiwezekani tuendelee kuibiwa na vibaraka hawa.

Wanatishia misada kwa miaka yote wametoa misaada ya kijinga imetusaidia nn?

Unasema unatoa dola mil 200.

Halafu kampuni zinazochukua tenda kwa mradi huo ni zao hela zote zinarudi kwao tena na kubakia kutudai stupid
 
Niger imewaumiza sana Wakoloni wanahaha kama mbwa aliekatwa Mkia..Urusi itaisaidia Niger haiwezekani tuendelee kuibiwa na vibaraka hawa...Wanatishia misada kwa miaka yote wametoa misaada ya kijinga imetusaidia nn??? unasema unatoa dola mil 200...Halafu kampuni zinazochukua tenda kwa mradi huo ni zao hela zote zinarudi kwao tena na kubakia kutudai stupid
Au siyo? Mkoloni ndio anaumia au vipi 😂😂😂😂

Saizi Uganda hapo Shilingi Yao imeshaporomoka balaa ,huo ni Mwanzo moto unakuja ,Utajua anaumia mkoloni au wewe
 
Viongozi wa ECOWAS Wametoa amri ya kupelekwa Jeshi Ili wakawanyoe Waliofanya M
.
IMG_20230806_170549.jpg


Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Viongozi wa ECOWAS Wametoa amri ya kupelekwa Jeshi Ili wakawanyoe Waliofanya Mapinduzi huko Niger na kurekesha Serikali ya Kiraia.


My Take
Naunga mkono hoja,wakashikishwe adabu licha ya Jeshi la Niger kupanga kumuua Rais waliyemoindua in case watavamiwa Kijeshi.
Bado sijakuelewa mkuu kabisa yani

Hilo jeshi lililonpindua nchi husika(Niger) ni jeshi alamu au ni jeshi la wananchi? mpaka nalo livamiwe na jeshi la kikanda (ECOWAS )
 
Unaunga mkono kwakua ww ni mtanganyika watakao teseka ni wa Niger uko kuna watoto,wamama na wazee.
Sawa kazi ianze kukuche jumapili bukinabe na mali ndio wanaanza safari ya kwenda kuilinda Niger na watu wake.
 
Back
Top Bottom