ECOWAS wabaini kemikali ya sumu Ikulu ya Gambia

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,537
Banjui. Askari wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) wamegundua kemikali ya sumu kali iliyokuwa imetegwa kwenye vyumba vya Ikulu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Ecowas kupitia gazeti la Freedom la Gambia, kemikali hiyo ilitegwa kwa lengo la kuua mtu yeyote atakayeingia ndani ya Ikulu hiyo.

Kutokana na hali hiyo, kiongozi mpya wa Gambia, Adama Barrow anatakiwa kuendelea kukaa Senegal kwa usalama wake huku uchunguzi ukiendelea kufanyika.
Source: mwananchi online.
WEDNESDAY, JANUARY 25, 2017
 
Hawa najamaa sometime hata walinzi wao uwa nawashangaa sana .....

Kuna watu ni wakupiga risasi tu wafe hawana faida yeyote.............
 
Gambia mbali kote huko !! Ofisi za meya wa halmashauri ya jiji la Mwz Mr. Bwire aliwekewa kitu kama hicho na mtangulizi wake mzee Shomari alimwagiwa Tindi kali. Africa tunafanana
 
>>>>>Huyu jamaa ana kichaa cha Madaraka ...Ametawala Gambia kwa 22Yrs... Bado anataka kuendelea ilihali wananchi wameshamkataa.

>>>Anafikiri Gambia ni mali yake??
 
Maelekezo ya mungu nanihii yule wa kule nanihii aliyesema akipenda atatawala miaka bilioni.
 
Yahya Jammeh hamnazo kabisa. Wakati anaondoka amekwapua mamilioni ya dola, pia alipakia baadhi ya magari ya kifahari kwenye ndege.......hiyo haitoshi akatege sumu ili kudhuru watu.
 
Banjui. Askari wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) wamegundua kemikali ya sumu kali iliyokuwa imetegwa kwenye vyumba vya Ikulu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Ecowas kupitia gazeti la Freedom la Gambia, kemikali hiyo ilitegwa kwa lengo la kuua mtu yeyote atakayeingia ndani ya Ikulu hiyo.

Kutokana na hali hiyo, kiongozi mpya wa Gambia, Adama Barrow anatakiwa kuendelea kukaa Senegal kwa usalama wake huku uchunguzi ukiendelea kufanyika.
Source: mwananchi online.
WEDNESDAY, JANUARY 25, 2017

Hilo jamaa kusema kote allah kumbe haikuwa bure. Linaubia mkubwa sana na wa moja kwa moja na allah? Kweli kimtokacho mtu ndicho kiujazacho moyo wake. Jamaa linachuki na unafiki kiwango cha hallah. Jamaa kazi yake ni kuiba, kuua na kuharibu vile vile alivyo hallah!.

Kweli mtot wa nyoka ni nyoka.
 
DUh !! yaani binadamu ni mdudu wa kuogopwa kuliko viumbe vyote duniani, yaani mtu anadiriki kuweka sumu kuuwa binadamu mwenzio kisa madaraka!!:mad::mad::mad::mad: Halafu huyu rais alietoka si ni alhaji alikwenda kuhiji macca?

waliompa hifadhi ya kisiasa wamrudishe kwake hafai hata kufadhiliwa shetani mkubwa huyo
 
hifadhi ya kisiasa kaenda kupewa na dikteta mwenzie wa equatorial Guinea ambaye yuko on line since 1979.birds of a feather...
 
Ha ha ha! Yahaya kweli ni mwendawazimu. Angalau hizo kemikali zimeweza kugundulika kwa njia za kawaida za kisayansi, n.k. Ila inajulikana Jameh alikuwa pia mshirikina nguli duniani wa level ya profesa; hapo Ikulu atakuwa ameacha majini na vibwengo vya kutosha. Njia mbadala za kuondoa uchafu wake huu ni muhimu zikatafutwa.
 
Back
Top Bottom