Ngoma ipi kali kati ya mrisho mpoto "chocheeni kuni" na roma mkatoliki "2030"

blaszkowski

Member
Jan 11, 2013
43
10
Kwa ufupi
1. "2030"
"leo Ridhiwani hafanani na Makongoro", kaskazini bila Tanga ni sawa na msondo bila Ngurumo, kwenye njaa kali kula kuku aliye chinjwa na Padri I love.......Tazama gongo la mboto mtoto kamzaa mtoto, ata lelewa na nani baba yake mmemfunga keko. Ona kipindi cha bunge dodoma inanuka ngono, spika hakiairisha bunge wengi mtausapoti mgomo, mnadai posho muwaonge dada zetu.......Mwiisilamu gani unaonga mamilioni bongo movie mama anakufa mwaisela kwa kukosa qwinini....kulichoma kanisa ni sawa nakuuza bibilia Dubai, "Watz tunahuoga tunadanganywa tuna amani"....Waziri ana uza meno na pembe za tembo, nchi imejaa misitu hatuna madawati, tunakula vitu vichafu TBS mpo wapi?.....RPC husitume kikosi kuwaangamiza CDM, Muhimbili unaumwa goti unapasuliwa kichwa......Uchafu wa Mrisho unafanya wasafi tunaonekana wachafu......
2. "CHOCHEENI KUNI"
"Waliopo hatuwataki na wanaotaka tuwape hatuwaamini", katika misimu 4 kwa mwaka haitoshi tuongeze wa 5 tujishtushe, lililotokea mbali tufanye limepita na haliwezi kumdhuru mwengine na kulipamba jeneza hakumfanyi aliye kufa kufufuka,.....Hamjitokezi mpaka yatokee maafa utasikia natoa katoni 20 za sabuni ya unga aliyekuambia wale wachafu nani? kasafisheni kwanza nyoyo zenu ndio mrudi kwa wananchi,........Binadamu ni kama ganda la kitabu ni mpaka humfungue ndio utamgundua,...... Kujipanga kwa mambo mazito, kinaitaji muhuri wa moto au mtaalamu wa magonjwa ya akili zaidi ya kutuambia wewe sahau tu.........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom