EBay testimonial...!!!

donlucchese

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Posts
17,258
Reaction score
22,129
Habari wakuu,
Natumai mu wazima. Kwanza nitoe shukrani zangu za dhati kwa mkuu chief mkwawa kwa ule uzi wake kuhusu how to activate PayPal account. Kwa mimi nilishajiunga paypal kitambo simce 2012 na ever since nimekua nikifanya online transactions marakwa mara. Wengi huogopa kwa kuhisi wanaweza tapeliwa ila this is my testimony na mzigo huu nimeupokea leo, nlinunua EBay.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uliagiza mzigo gani kaka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weka updates kidogo.

Imechukua siku ngapi
Umetumia njia gani kusafirisha(free/kampuni za usafirishaji?)
Umepikelea posta au nyumbani kwako n. K n. K
 
Mkuu Mimi naomba kujua kuhusu myus na kama kodi walikutoza ama laaah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weka updates kidogo.

Imechukua siku ngapi
Umetumia njia gani kusafirisha(free/kampuni za usafirishaji?)
Umepikelea posta au nyumbani kwako n. K n. K
Haswaaa...
 
Weka updates kidogo.

Imechukua siku ngapi
Umetumia njia gani kusafirisha(free/kampuni za usafirishaji?)
Umepikelea posta au nyumbani kwako n. K n. K
Mkuu, ilitumia three weeks kutoka United States mpaka hapa kunifikia. Nimetumia Fedex mkuu, nilijiunga pia na coy ya myus.com ambapo wanakupatia US physical adress,hii inasaidia incase ukiingia ebay ukakutana na sellers ambao hawaship mzigo kwenda kwenye nchi yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu donlucchese
Kuhusu kutumia 'fedex na myus.com', please fafanua kidogo mkuu;
ni kwamba unanunua mzigo wako online alafu hao online retailers (either wa ebay au wengine) ndio wanatuma mzigo wako huko 'myUS', alafu 'myUS' ndio wanautuma huku tanzania kwa kutumia kampuni ya fedex?

Na kuhusu mambo ya ushuru/kodi, je, kodi inawekwa pamoja na postage charges? Au ni kwamba hakuna kodi kabisa? Unanunua mzigo tu na kulipia postage basi, alafu unatumwa tanzania?

Je, kuna resentative wa fedex US hapa bongo? Ndio wanaokuletea mzigo mpaka nyumbani?
 
Ok mkuu, ni hivi,
Ebay ni kuhusu manunuzi tu. Je, baada ya hapo mzigo wako unakua shipped wapi? Hapo sasa tunakuja katika swala zima la ma sellers. Kuna sellers wengine hawafanyi shipping to third world countries, therefore kutatua tatizo hili ndipo wanaingia myus.com. je. Hawa ni kina nani? MyUs ni kampuni ambayo inakupa uwezo wa kumiliki physical adress ya USA. Why USA? USA ni taifa kubwa ambalo linafanya business almost na nchi zote ulimwenguni. Kwahiyo basi, inapotokea katika maelezo ya sellers kwamba haship mzigo labda kwa mfano tuseme tanzania, you ain't got to worry abou nothing. Kwa physical address ambayo myus wanakupatia, ni kwamba seller yeypte ulimwenguni hata kama yuko Alaska,atautuma mzigo kwenda us kwenye adress yako. Sasa kule ndio watafanya mchakato wakuutuma mzigo kuja katika your destination popote ulipo. Payment inategemea na uzito wa mzigo, . Nimejitahidi kujibu kadri ya maswali yako ila kama kuna sehemu sijawa clear nikumbushe mkuu nikudadafulie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kodi hakuna mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reps wa fedex wapo mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kodi hakuna mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app

Hapa kidogo hatupo sawa!
Kodi ipo mkuu mie mwenyewe mhanga wa hili ila tu kuna baadhi ya items ndogondogo (simu, tablet, hhd nk) ndio hazina kodi.

Mzigo wangu nimetumiwa na hao hao myus kuna iterms 8 ndani ya package 1 upo tra mpak muda huu japo nishafanya clearence tayr nasubiri mzigo kutoka.
Kodi ni allmost 40% ya kila iterm kwenye package kilichonisaidia price ya kila iterm iliomo kwenye invoice sio actual purchased price zaidi ya hapo ningeumia mana mzigo wa 256 usd costum duties ni 271,000 tsh!!!!

Nb
Sishauri mtu kutumia fedex hawa jamaa hawafai na hawapo tayari kukusaidia chochote zaidi ya kukukandamiza
 
una itumiaje iyo address na wewe upo tanzania... na gharama ya kujiunga na fedex na myus ni kiasi gani kwa mwezzi au mwaka... wewe flash ime kughalimu kiasi gani kuisafilisha tu hachana na kuinunua....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…