Basi naomba kurekebisha kauli yangu na isomeke hivi......"INASEMEKANA kwamba wamiliki wa Easy Finance ndio wenye Travel Mate"
Halafu, mbona wengine mnakuwa wakali sana humu? Au mna hisa Easy Finance nini?
Anaitwa Isack Kasanga,ni mlezi wa umoja wa vijana wa CCM(sikumbukitawi/wilaya ya Kinondoni),aliichangia CCM Tshirt,Kofia kipindi cha uchaguzi mkuu na ilirushwa kwenye luninga.Watanzania tufungue macho,kuna ufisadi mwingi zaidi ya ule wa EPA unaendelea Tanzania,kanuni ni mwenye nacho anaongezewa na asiyekuwa nacho/mwenye kidogo ananyang'anywa!
Kwenye uongozi huu wa serikali ya CCM, maovu tunayoyafahamu ni mfano wa ukubwa wa kigae; hatujaona paa lenyewe.
Siku Kikwete akiona ghorofa, atafanya mara mbili ya yaliyofanywa na Mkapa.
.
Mazee mimi niliongea na mtu ambaye alipata mkopo kutoka kwa hawa Easy Finance na kutokana na maelezo yake hawa watu ni matapeli kutokana na jinsi mikopo yao wanavyoifanya, wanachokifanya ni kuwa-trap watu. Mtu anaanziwa kusainishwa vitu mwanzo na inabidi a-sign kabla ya kwenda process inayofuata na hapo ndio unakuta mtu at the end anaambiwa baadhi ya conditions za huo mkopo ambazo hakuelezwa mwanzo na inakuwa ni sawa na ujambazi au Ufisadi tu.Unakwenda mwenyewe EF kuomba mkopo, unaambiwa masharti ya mkopo na unayakubali. Unapewa mkataba kuusaini baada ya kutimiza masharti ya mkataba huo unausaini unachukua bulungutu lako na kwenda kufanyia shughuli uliyoitarajia kama ni biashara, kumsomesha mtoto au mwenyewe au kuhudumia nyumba ndogo n.k. Ikija kwenye kuanza kurudisha mkopo huo unang'aka na kuruka juu kama vile masharti ya mkopo huo hukuyabukali na wala huyajui na kuanza kuwaita EF matapeli!!!! Wabongo bwana!!! Kazi kweli kweli!!!!
Mazee mimi niliongea na mtu ambaye alipata mkopo kutoka kwa hawa Easy Finance na kutokana na maelezo yake hawa watu ni matapeli kutokana na jinsi mikopo yao wanavyoifanya, wanachokifanya ni kuwa-trap watu. Mtu anaanziwa kusainishwa vitu mwanzo na inabidi a-sign kabla ya kwenda process inayofuata na hapo ndio unakuta mtu at the end anaambiwa baadhi ya conditions za huo mkopo ambazo hakuelezwa mwanzo na inakuwa ni sawa na ujambazi au Ufisadi tu.
Mimi pia nawafahamu watu wengi waliochukua mikopo midogo midogo mpaka ya 50 millioni toka EF na walifurahia huduma za EF na kamwe hawatasita kurudi tena kama wakiwa na shida ya mkopo mwingine. Kwa hiyo shilingi ina pande mbili labda hao wanaolalamika hawasomi kwa makini hayo masharti ili wayafahamu vizuri na matokeo yake wakija kutakiwa kulipa wanawashikia bango EF kwamba ni matapeli.
Unakwenda mwenyewe EF kuomba mkopo, unaambiwa masharti ya mkopo na unayakubali. Unapewa mkataba kuusaini baada ya kutimiza masharti ya mkataba huo unausaini unachukua bulungutu lako na kwenda kufanyia shughuli uliyoitarajia kama ni biashara, kumsomesha mtoto au mwenyewe au kuhudumia nyumba ndogo n.k. Ikija kwenye kuanza kurudisha mkopo huo unang'aka na kuruka juu kama vile masharti ya mkopo huo hukuyabukali na wala huyajui na kuanza kuwaita EF matapeli!!!! Wabongo bwana!!! Kazi kweli kweli!!!!
BAK
Tatizo linakuja kwenye upande wa Watanzania kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu haya mambo ya mikopo. Na huu udhaifu ndio watu kama EF wanautumia kwa sababu wanaujua vyema.
Watu wachache sana huwa wasoma vipengele vyote vya mkataba achia mbali kuelewa kuwa hata koma inacount.
Wale jamaa pale watakuaonyesha yale masharti nafuu ili kukuvutia wakukombe pesa zako. Kwa mfano unaomba mkopo wa millioni tano. Watakuambia riba ni asilimia kumi na tano na utarudisha baada ya muda kadhaa na kila mwezi utakuwa unakatwa kiasi kadhaa. Utaenda home utacalculate vizuri kabisa. Utasign makatasi yako. Tayari kwa kwenda kwenye kuchukua mkopo instantly.
Ukifika huko unapewa breakdown unajikuta jumla utawarudishia say 5.8 millions. Wao wanapata faida ya laki nane toka kwako. Juu ya hivyo wakati unachukua mkopo, unaweza kuambiwa tunakata elfu hamsini au lakini kama loan application fee. Mwanzo hawakukuambia kwamba kuna hiyo application fee. Kwa hiyo mkopo wako ni 4,950,000/= lakini kwenye interest ukatwa based on 5,000,000/=. Chururu si ndondondo.
Wewe una hisa EF si bure, na kama unayoongea ni kweli basi EF unayoiongelea wewe ni ya US si ya Bongo tunayoijua sisi iliyokuwa Kinondoni Mwanamboka na Sasa imehamia Burundi Street
Sina hisa lakini kuna watu ambao nawafahamu kwa karibu katika mazungumzo wameniambia wamechukua hapo EF mikopo kiasi cha 50 millioni watu hawa wamejiajiri wenyewe na ni ni watu maarufu tu na kwa maoni yao wakihitaji mkopo tena hawatasita kurudi EF.
Sasa kama nimeambiwa hivi na wahusika sioni sababu yoyote ya kuficha ukweli eti kwa kuogopa kuambiwa nina hisa EF. Sina hisa EF wala sina mpango wa kununua hisa huko bali nasema nilichoambiwa na baadhi ya wakopaji waliofaidika na mikopo ya EF. By the way I am talking about Tanzania's EF and I know nothing about US' EF.
Mkuu Bubu...tuseme ukweli tu...hivi interest rate ya 30% and above kwa short term loans...na hizo fees tutaendelea mkuu? Hao wanaokopeshwa si inabidi wakauwe "albino" ili waweze kurudisha hizo hela??
Hivi hakuna regulations kwa vyombo vya fedha nchini kwetu? What is BoT up to?
Hamisi F. na Gonzaga