Safi sana
Bukyanagandi...... kwanza uhuru wa kujadiliana si sawa na ya kutaniana. Na post hii ni ya kufanya uchanganuzi hasa nini kinachozuia maendeleo ya kasi barani na haswa Afrika mashariki. Tunataka pia kueleza au kujibu maswali magumu kuhusu kama ni mwendo wa kasi wa maendeleo ulioiboronga Euro-zone na kufanya yakawa watumwa wa mikopo. Tunataka pia tujikumbushe na tufahamu kama shughuli ya mungano wa Euro na kutia saini kwa nchi kumi na mbili za Ulaya katika mkataba wa
"Maastricht Treaty" ulikuwa na ulbuniwa kwa lengo zuri au baya? Tunaeza jiuliza pia kama tunezipa mgongo suala hadharani la kuzorota kwa njia za ubunifu an utekelazaji sera ndani ya safu za uongozi EU.
Mkuu wala husipoteze muda kujadiliana nao maswala ambayo yako obvious, si rahisi kubadirisha mind set za baadhi yao. Mkuu, baadhi ya hawa jamaa wana malengo fulani katika forum hii na wako well organized, wanafikili wakisema sema Tanzania basi hilo tu litatufanya tubadirishe misimamo yetu thabiti kuhusu certain issues ambazo wanaona tulisha washtukia siku nyingi na siku hizi tumewazidi kete, wanatuona kero kweli kweli. Kuikasikilia TANZANIA kunatokana na msimamo wetu huo wa kukataa shotgun wedding ya Federation vile vile na kutokubali ku-sign an open ended clauses zilizo wekwa kimaksudi kula kwetu.
Leteni mambo ya kujenga kwenye FORUM hii na sio ridiculous rhetoric ambazo hazisadii chochote Tanzania, Kenya au wana JF, mimi binafsi sipendi mambo ya kutuniana misuri kama wendawazimu.
Mkandara, nikirudi katika mada, swali ni
Kasi ya maendeleo ni nzuri kwa mataifa ya Afrika au una ubaya wake? Kuna mifumo aina nyingi ya serikali lakini zote matokeo haziridhishi. Hivi niliambiwa na Mkandara nielezee nini kiini cha Uispania, Italia, na Ureno kupata pigo katika uchumi.
Historia ya Demokrasia nchini Spain, Portugal, na Greece:
Nchi hizi ndizo the most affected katika Eurozone na demokrasia hizi zilianza mwaka wa 70. Hali inayodhihirishwa na "ustawi wa demokrasia" hizi ni ya kutatanisha. Kuna sababu nyingi kando na ubadhirifu wa fedha Uhispania zinazochangia kuanguka kwa uchumi (ambao huendeshwa na mapato zinazotokana na biashara ya "real-estate"). Matumizi ya fedha ya kitaifa katika miradi ya kawi katika bajeti iliongezeka, huku ikiongeza deni la kitaifa/national debt kuwa kubwa.
Uhispania:
Msimu huu Uhispania imefikia katika "njia-panda" katika matumizi ya fedha ya kitaifa/government spending. Je! Uhispania itazuia/katiza matumizi mengi ya fedha ya kitaifa kupunguza deni, au itasalia/kuzidi kukopa mikopo kutoka IMF na Banki ya dunia (ambapo credit-rating itashuka hadi "junk-levels"). Yafaa itiliwe maanani kuwa ni vigumu wigo wa uchumi kupanuka na kuzaa mapato pasipo na matumizi ya fedha. Ndiposa, ninaposikiza malalamishi ya wtz wengi kuhusu muungano wa sarafu, ninakubali hali ilivyo hapo na huwa sipingi. Hakika, sera hizi za serikali za kisocialisti zimewekwa/au zitawekwa katika katiba na afadhali Tz isalie hapo SADC kuliko EAC...(NB..mataifa mengine yanapopigania kuingia EAC, inaonekana jambo ls kutafuta ufadhili wa ardhi, fedha, au CHAKULA).
Taswira tunayoipata kati ya SADC na EAC ni ukubwa wa populations katika SADC ambao ukitizama ni rasilimali ambao hujatiliwa maanani. Umaskini katika bloc hii ni ya kusikitisha mno, licha ya mataifa mengine kutangaza kuboreka kwa uchumi kutokana na uvumbuzi wa madini/rasilimali kama gesi, makaa-ya-mawe, na uchimbaji mafuta. Nusu ya watu wanaishi chini ya dola-kwa-siku. Poor population intergration katika mataifa SADC pia inatisha/XENOPHOBIA(jambo halizungumziwi lakini ni wazi/hadharani). Tena picha halisi ya HIV/AIDS, inadidimiza sehemu ya tija ya populations.
Ureno:
Taswira ya Ureno ni kinyume na ya Uhispania bila kusahau pia Ireland ni mojawepo ya mataifa ina hili tatizo. Si mara ya kwanza Ugiriki kupata mkopo/bail-out kutoka EU, na mikopo hii imezidisha kusambaratisha uchumi. Hivi sasa IRELAND na GREECE zimesalia "financial-basket-case". PORTUGAL imesalia katika biashara kuuza sehemu ya hisa za kitaifa/government shares/bonds kuhifadhi Uchumi na kuvutia wawekezaji kutoka nje. Uchumi ureno unaoendeshwa sana na ukulima, hutegemea sana ununuzi wa bidhaa za mafuta kutoka mataifa mengine kukithi mahitaji ya kawi na uzalishaji wa viwanda. Hili ni jambo huchangia pakubwa katika utumizi mkubwa wa fedha ya kitaifa na kuongezea mapungufu katika bajeti.
Italia:
Kinyume na taswira za nchi zingine, kuna tofauti kubwa ukijaribu kulinganisha uchumi wa ITALY na mengine Eurozone. Sekta nyingi/asilimia kubwa ya biashara huendeshwa na watu/familia binafsi/makundi ya wafanya biashara mashuhuri ambao ni wamiliki viwanda. Kimaendeleo, taifa hili linaorodheshwa kama ishirini na tatu (technologia, na mawasliano). Tukizingatia mambo haya, ni rahisi kwa nchi hii kupata mafanikio katika panda-shuka yake ya kuimarisha/kuhifadhi uchumi maana deni sio la taifa, ila ni watu binafsi ambao wana jukumu la kulipa deni kwenye Banki kuu/European Central Bank. Uchumi wao unaweza kufananishwa kimsingi na ya Uchina.
..........Uchumi/Italy ni mara mbili zaidi katika ukubwa ukishikanisha ule wa Greece na Ireland.
Yaonekana uchumi wa taifa hili halijarudi hatua nyingi nyuma sababu kuu ikiwa umeegemea kwenye sekta ya ununuzi na uuzaji hisa/sovereign bonds kati yake na European central bank. Yaonekana kama likizo la afueni, lakini swali ni lini/njia ipi itatumika kulipa deni?
Taswira halisi ya URUSI/mtazamo wa uchumi na hadhi yake:
Sekta ya ununuzi na uuzaji wa bidhaa ndani ya Russian Federation mathalan ya mataifa mengine Europa yaliyostawi (Germany, France, na Britain) na uchimbaji madini/almasi, ndio vipengee ambavyo vimekuwa msingi wa upanuzi wa wigo wa uchumi na huchangia pakubwa katika uendeshaji wake. Uzalishaji wa kawi na uuzaji wa mafuta huchangia kwa asilimia ndogo katika kuimarisha uchumi. Pia, tofauti nyingine na inayodhihirika wazi ni sifa yake katika umilikaji wa hazina kubwa ya fedha. Licha ya sifa hiyo, sekta ya ununuzi wa bidhaa unagharimu serikali kiasi kikubwa kutoka kwa hazina ya taifa/Russian Federation huku sekta yake ya uuzaji inayoendeshwa na ukulima/ukuzaji wa mimea ikipata pigo kutokana na janga ya kitaifa kama ukame na kupanda kwa ghafla katika bei za bidhaa muhimu kama vyakula.
Kuna taswira pia mataifa mengi yanaambatanisha uchumi zao na Russian federation katika kufadhiliwa/subsidies mfano nchi za Ukraine na Georgia. Tofauti ya maendeleo/mwanya ulioko kati ya nchi za Russia na jirani zake ni kubwa mno, ambalo kwa muda mrefu imefanya nchi hizi kutegemea nchi za Magharibi, Asia, na Europa kwa ununuzi wa bidhaa na tena kama njia ya kuepuka ubepari unaodhihirishwa na Russian Federation. Bidhaa za kutengenezwa kutokwa kwa uzalishaji ya kawi hujumuisha asilimia 20% tu ikilinganisha na 65% zinazotoka kwenye viwanda.
Hatuwezi lenga kushughulika kuleta mambo ya kujenga wakati kuna sekta zingine zimeorodheshwa duni. Ni heri EAC kama muungano uvunjwe maana licha ya kujaribu kuondoa vikodi, haileti manufaa maana kila nchi ina sera zake. Ninavoona katika siku za baadaye, EAC itabaki tawi unganishi la SADC. Manake tukitarajia kuingilia intergration na kuruhusu uhuru wa uhamiaji, mataifa yote EAC yatakubali lakini, isiwe moja ya mataifa inakataa huku ikitumia ardhi kama sababu. Hali hii haifai kuwa ngumu kama wadau wengine wanjaribu kuonyesha. Mradi tu kuna viwanda na biashara inaoendelea, labor-force ya Afrika mshariki itakuwa rasimali yenye maana.