E-SIM imefika Tanzania. Hii inamanisha nini kwetu watumiaji?

Tech Africa

New Member
Feb 25, 2021
2
12
E-SIM ni teknolojia inayomsaidia mtumiaji wa simu kwa na laini zaidi ya moja kwenye simu hata kama simu hiyo inakisehemu kimoja tu cha kuweka laini.

Vitu vya kuzingatia ili kuweza kupata huduma ya E SIM ni vipi?
1. Lazima simu yako iwe ina uwezo wa kupokea mipangilio ya E-SIM, kwa maelezo zaidi nenda google na uangalie kama simu yako ina uwezo huo.
2. Lazima uwe umesajiliwa na mtandao unaotoa huduma ya E-SIM, kwa hapa Tanzania ni Airtel.

Faida za E-SIM.
1. E-SIM inasidia sana pale ambapo unahitaji kutumia laini mbili za simu lakini simu yako inakisehemu kimoja tu cha kuweka laini, au unataka kutumia laini tatu lakini simu yako inasehemu mbili tu za kuingiza laini.
2. Hakuna tena haja ya kununua laini za simu, na mtu akiiba simu yako basi unaweza kufuta na kundoa mpangilio wa E-SIM ukiwa mbali hivyo basi mwizi hawezi kupata laini yako.

kama una swali lolote karibu kuuliza kwenye sehemu ya comment.
 
Ni aina gani za simu zenye kupokea huduma hiyo?
Zipo simu nyingi zinazosupport lakini kuna hii list nimeipata mtandaoni unaweza kuicheki;

Apple​

  1. iPhone 14
  2. iPhone 14 Plus
  3. iPhone 14 Pro Max
  4. iPhone 14 Pro
  5. iPhone 13, 13 Pro, 13 Pro Max, 13 Mini
  6. iPhone 12, 12 Pro, 12 Pro Max, 12 Mini
  7. iPhone SE
  8. iPhone 11, 11 Pro, 11 Pro Max
  9. iPhone XS, XS Max
  10. iPhone XR
  11. iPad Pro 12.9‑inch (4th generation)
  12. iPad Pro 12.9‑inch (3rd generation)
  13. iPad Pro 11‑inch (2nd generation)
  14. iPad Pro 11‑inch (1st generation)
  15. iPad Air (4th generation)
  16. iPad Air (3rd generation)
  17. iPad (8th generation)
  18. iPad (7th generation)
  19. iPad mini (5th generation)

Samsung​

  1. Samsung Galaxy S22 5G, Ultra 5G, S22
  2. Samsung Fold LTE model
  3. Samsung Z Flip 4
  4. Samsung Z Fold 4
  5. Samsung Galaxy Z Fold 3 5G
  6. Samsung Galaxy Z Flip 5G
  7. Samsung Galaxy Z Flip
  8. Samsung Galaxy Z Fold2 5G
  9. Samsung Galaxy Fold
  10. Samsung Galaxy S21+ 5G
  11. Samsung Galaxy S21 Ultra 5G
  12. Samsung Galaxy Note 20 Ultra, Ultra 5G
  13. Samsung Galaxy Note 20 FE 5G
  14. Samsung Galaxy Note 20 FE
  15. Samsung Galaxy S20, S20+ and S20 Ultra

Google Pixel​

  1. Google Pixel 7 Pro
  2. Google Pixel 7
  3. Google Pixel 6 Pro
  4. Google Pixel 6
  5. Google Pixel 5a 5G
  6. Google Pixel 5
  7. Google Pixel 4a
  8. Google Pixel 4
  9. Google Pixel 3 & 3XL (Limited support)
  10. Google Pixel 2
 
Iphone 11 pro max line moja haina option ya esim shida ni nn

Labda ya kwako
IMG_3511.png

Mi mbona ndo nnayo na natumia eSIM tena inaenda hadi 5 eSIMs
 
Esim ni teknolojia inayomsaidia mtumiaji wa simu kwa na laini zaidi ya moja kwenye simu hata kama simu hiyo inakisehemu kimoja tu cha kuweka laini. Vitu vya kuzingatia ili kuweza kupata huduma ya Esim ni vipi?
1. Lazima simu yako iwe ina uwezo wa kupokea mipangilio ya Esim, kwa maelezo zaidi nenda google na uangalie kama simu yako ina uwezo huo.
2. Lazima uwe umesajiliwa na mtandao unaotoa huduma ya Esim, kwa hapa Tanzania ni Airtel.

Faida za Esim.
1. Esim inasidia sana pale ambapo unahitaji kutumia laini mbili za simu lakini simu yako inakisehemu kimoja tu cha kuweka laini, au unataka kutumia laini tatu lakini simu yako inasehemu mbili tu za kuingiza laini.
2. Hakuna tena haja ya kununua laini za simu, na mtu akiiba simu yako basi unaweza kufuta na kundoa mpangilio wa Esim ukiwa mbali hivyo basi mwizi hawezi kupata laini yako.

kama una swali lolote karibu kuuliza kwenye sehemu ya comment.
Natumia pixel 5a, kwenye connection settings inaonyesha kuwa in support eSIM. But airtel wanasema haisapoti. Ishu inaweza kuwa ni nini?
 
Back
Top Bottom