E-Coli: Gonjwa hili bin mchwa!!!

m_kishuri

JF-Expert Member
Jan 27, 2010
1,484
372
e_coli_bacteria_coloured_scanning_electron_f0010228.jpg

nb: tumuombe muumba atuepushe mbali na hili zimwi E-Coli Bacteria.
 
Mungu ameisha kuepusha.

Kawaweka E.coli kwenye utumbo wako mkubwa, na hawakupi shida yoyote.
Halafu katupa akili na elimu-ukila chakula ambacho kimefikiwa na uchafu wa kinyesi cha binadamu au mnyama, utapelekea E.coli kwenda sehemu nyingine ya mwili ambako wataleta madhara..
 
Ni kweli E. coli wako wengi sana kwenye utumbo mkubwa wa binadamu na hawaleti madhara yoyote. Wako kule kama 'normal flora'. Ni kweli wakitoka kwenye utumbo na kwenda sehemu nyingine ya mwili kama vile kwenye njia ya mkojo wanaletta madhara. Lakini kuna strains chache za E. coli zinaleta madhara kwenye utumbo. Hizi strains zinaitwa Diarrhoeagenic. Ziko aina 6: Enteropathogenic, Diffusely adherent, Enterotoxigenic, Enteroaggregative, Enteroinvasive na Enterohaemorrhagic. Strainya E. coli iliyoleta mlipuko wa ugonjwa wa sasa ni Enterohaemorrhagic ambayo ndiyo ya hatari sana kuliko strains nyingine. Kwa kawaida E. coli "hazaliani" nje ya mwili wa binadamu. Kwa hiyo binadamu wanambukizwa E. coli baada ya kula kitu kilichochafuliwa na kinyesi cha binadamu muda mfupi uliopita.
 
Back
Top Bottom