Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,714
- 33,969
Katika miaka ya hivi karibuni, huduma ya afya inayolenga kudumisha hali nzuri ya afya ya uzazi imekuwa maarufu. Lakini suala hili sana sana linahusu afya ya wanawake wakati wa uja uzito, baada ya kujifungua na kuzeeka.
Ukweli ni kwamba wanaume pia wanahitaji kuyapatia umuhimu masuala yanayohusiana na afya ya uzazi.
Kabla ya kuangazia shida ya mkojo kwa wanaume husababishwa na nini, ni vyema kufahamu kuwa wao pia wanatakiwa kuwa na afya katika mfumo wao mzima wa uzazi ambao unahusisha ubongo, mfumo wa hewa na mishipa ya mfumo mzuri wa uzungukaji wa damu.
Viungo vya uzazi vya mwanaume vimegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni viungo vya uzazi vya ndani na vya nje.
Viungo vya ndani vinahusisha mirija ya mbegu za kiume, tezi dume, ubongo, mfumo wa hewa na uzungukaji wa damu pamoja na afya ya mishipa ya damu.
Viungo vya nje ni kama uume na mfuko wa korodani.
Lakini je kinachosababisha shida ya mkojo kwa wanaume ni nini?
Matatizo ya korodani
Maumivu ya korodani hutokea endapo zitaumizwa kwa kuumia au maambukizi.
Maambukizi haya yanaweza kuwa makali na ya muda mfupi, yanakuwa makali kwa muda fulani halafu yanapoa yenyewe au kwa dawa baadaye yanarudi tena yakiwa makali sana kama mwanzo.
Tatizo hili huhitaji upasuaji wa dharura.
Wakati mwingine tatizo hili hutokea kwa korodani kuwa na tabia ya kupanda au kushuka, ikishuka mgonjwa hupata nafuu, hali huendelea vivyohivyo kwa vipindi fulani. Hali hii inapotokea mgonjwa hutapika na kukosa nguvu.
Maambuziki ya korodani huambatana na maambukizi katika mkojo au 'UTI' na homa.
Uvimbe kama jipu la korodani ni mbaya kwani korodani inakuwa kama inaoza. Uvimbe huwa kama busha au jipu kubwa lakini ndani yake hakuna maji wala usaha.
Ni tatizo ambalo linaweza kumuathiri mwanaume yeyote na lisiposhughulikiwa mapema linaweza kumfanya mgonjwa kupoteza uwezo wa kuzaa.
Maambukizi ya njia ya mkojo
Kulingana na madaktari bingwa wa magonjwa ya uzazi, maambukizi ya njia ya mkojo husababishwa na vimelea au bakteria hatari ambao huzidi uwezo wa kinga ya mwili katika mfumo wa mkojo. Maambukizi haya yanaweza kuathiri figo, kibofu cha mkojo na mirija inayopita katikakati ya viungo hivyo.Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa UTI ni mojawapo ya aina za maambikizi yanayowakumba watu wengi zaidi duniani na watu takriban milioni 8.1 hutembelea hospitali au kliniki kila mwaka kuwaona madaktari kutokana na maradhi haya.
Maambukizi ya mkojo yanaweza kugawanywa katika aina mbili ya njia ya juu ya mkojo na ya njia ya chini. Njia ya juu inajumuisha figo na mrija unaopeleka mkojo katika kibofu cha mkojo (ureter), na njia ya chini ya mkojo yenye kibofu cha mkojo na mrija unaoelekea sehemu ya nyonga.
Kwa wengi maambukizi ya njia ya mkojo husababishwa na bakteria aina E. coli, ambayo kwa kawaida hupatikana katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.
Dalili za maambulizi ya UTI zinategemea una umri gani, jinsia na ni sehemu gani imeathiriwa ya njia ya mkojo.
Madaktari bingwa wanashauri ni vyema kwa mtu kufanyiwa vipimo vya maabara vya mkojo na damu kabla ya kupewa dawa za kutibu UTI ili kubaini ni aina gani ya bakteria wanaosababisha maambukizi uliyonayo.
Dalili za kawaida za UTI ni pamoja na:
- Haja ya kwenda haja ndogo kila mara
- Kupanda kwa joto la mwili
- Kuhisi baridi mwilini
- Maumivu ya mgongo
- Mkojo mzito wenye harufu kali na damu
- Maumivu au muwasho unapokwenda haja ndogo
- Kichefuchefu na kutapika
- Maumivu ya misuli na tumbo
Maelezo ya picha,Maambukizi ya UTI yanaweza kuathiri figo yasipotibiwa haraka
Kuzuia maambukizi ya mfumo wa mkojo
- Kunywa maji mengi ,lita tatu hadi nne kila siku. Maji huzimua mkojo na kusaidia kutoa bakteria kwenye kibofu na njia ya mkojo.
- Kukojoa kila baada ya saa mbili au tatu,usihairishe kukojoa,kuweka mkojo kwa muda mrefu huwapa bacteria nafasi ya kukua.
- Kula vyakula vyenye vitamini C ,kama vile matunda.
- Zuia kufunga choo au tibu hali hiyo mara moja.
- Kusafisha sehemu za siri ,mbele na nyuma baada ya kufanya mapenzi,kojoa kabla na baada ya kufanya mapenzi na kunywa gilasi ya maji baadaye.
Ukosefu wa mkojo
Ukosefu wa mkojo kwa wanaume hufanyika wakati ubongo hautumii ishara sahihi kwa kibofu cha mkojo. Mara nyingi, sphincters haifinya kwa nguvu ya kutosha.Misuli ya kibofu cha mkojo inaweza kuambukizwa sana. Uharibifu wa misuli ya sphincter au mishipa inayodhibiti misuli inaweza kusababisha shida hii.
Nini husababisha hali hii?
- Saratani ya korodani - matibabu ya upasuaji inaweza kusababisha UI ya muda au ya kudumu
- Kasoro za kuzaliwa - maswala na ukuzaji wa njia ya mkojo
- Kikohozi cha muda mrefu - huongeza shinikizo kwenye kibofu cha mkojo na misuli ya sakafu ya pelvic
- Shida za neva - hali zinazoathiri ubongo na mgongo
- Unene kupita kiasi - uzito wa ziada unaweza kuweka shinikizo kwenye kibofu cha mkojo, na kusababisha hitaji la kukojoa kabla ya kibofu kujaa.
- Kuzeeka - misuli ya kibofu cha mkojo hudhoofisha kwa muda.
- Ukosefu wa mkojo sawa na magonjwa mengine una dawa na pia uanaweza kutibiwa.
hupelekea maumivu makali ya tumbo, na kuhara damu ambapo hustawisha kusambaa kwa bakteria hao.
Kuvuja kwa mkojo
Mkojo usioweza kudhibitiwa kwa wanaume ni hali ambayo kwa asilimia 11 hadi 34 husababishwa na uzee. Wanaume wadogo pia wanaweza kukabiliwa na hali hii.Hii ni hali ambayo pia huwaathiri wanawake lakini tofauti ni kwamba wanaume wana uwezekano mdogo wa kuzungumza na madaktari wao.
Hali hii inaweza kuzuiliwa kupitia tiba asilia kabla ya kufanyiwa upasuaji. Tiba hiyo inajumuisha kuongeza ufahamu na kuimarisha misuli ya maeneo ya kibofu cha mkojo ili kuzuia uvujaji.
Yote haya yanaweza kufikiwa ndani ya wiki tatu kabla ya kufanyiwa upasuaji, kwa kuimarisha hali ya mwili wa mgonjwa mara baada ya kuja kutafuta huduma ya matibabu. Kuna uwezekano mdogo wa kutokea kwa madhara.
Na hata yakitokea , hayatakuwa mabaya vile.
Licha ya hatua hizi za kinga, kuna uwezekano wa misuli kuathiriwa kwa njia moja au nyingine.
Aina hii ya tiba hujumuisha kukandwa kwa kutumia mikono au mashini, mazoezi ya viungo na kadhalika.
Vidokezo muhimu vya kuzuia maambukizi ya mfumo wa mkojo
Mbinu zote zilizotajwa zinaweza kufanya kazi na tiba zinatofautiana kutoka kwa mgonjwa mmoja hadi mwingine.Mwisho, ni muhimu kufanya jambo la kawaida kujadili hali ya afya kwa wanaume.
Kuzungumza wazi wazi kuhusu changamoto ya kiafya inasaidia kuvunja mzunguko wa kutoelewa. Kitu cha msingi, nikuangazia miiko na itikadi zinazochangia upotoshaji wa habari na kuzua hisia za hofu, uchungu, wasiwasi, hatia.
Wanaume wanaokabiliwa na changamoto za kiafya zinazohusiana na tatizo la mkojo,
wanastahili kuwasiliana daktari au mtaalamu wa magonjwa kupata suluhisho.
Hitimisho :
Kwa Wale Waliotumia Dawa Za Hospitali na Hawajapona Maradhi ya Shida Ya Mkojo Wanione Mimi KwaWakati wao ili nipate kuwatibia Kwa Dawa Zangu zaAsili Wapate Kupona Maradhi yao.