Dynamic Productivity; Tija na Maarifa

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Heri ya Pasaka na Iddi.

Kwa wengi wetu hapa JF ambao tunakaa nje ya Tanzania, iwe Japan, Russia, Finland, US, UK, SA, Malaysia, France, Swiss, Ujerumani, Brazil, Canada na nchi zingine za ulimwengu wa kwanza au wa pili, si siri kuwa chimbuko la maendeleo yao halikuwa katika sera pekee, hotuba au hata kama tukidai ni matunda ya ukoloni na utumwa (unyonyaji), bali ni kutokana na uchapakazi ulioambatana na ufanisi, uvumbuzi, tija na maarifa.

Kwa wastani, Wamarekani wa middle class. huwa wanafanya kazi takriban masaa 50-60 kwa wiki. Wale wa KCC ndio huvuta dabo shifti, kazi tatu ili kujikimu na hawa hufikia hata kufanya kazi kati ya masaa 80-100 kwa wiki.

Hata matajiri au tabaka la juu, nao ni wachapa kazi na wao mara nyingine hupita hata masaa 100 kwa wiki wakiwa katika kuhamasisha uzalishaji mali, kupelekeshana puta na uvumbuzi hata ufanisi, ili waendelee kuwa tabaka la juu na kuendelea kuwa na ongezekop marudufu la kipato (utajiri).

Nitatoa mfano wa Warren Buffet, tajiri kuliko wote duniani. Anakaa Omaha, anaamka saa 10 asubuhi, baada ya kupiga tizi, anakimbilia magazeti kabla ya kuanza mikutano na wafanyakazi wake, matajiri wenzake au kwenda kazini kwenye shughuli 100 ambazo huishia kwenda kulala saa 4 hadi saa 5 usiku, kisha siku mpya huanza tena saa 10 asubuhi, hivyi kuwa na mzunguko wa kufanya kazi.

Mtu wa kima cha chini Jane/Jone Doe, huamka saa 10 asubuhi, na kuondoka nyumbani kwake baada ya kumuacha mwenza aangali watoto kabla ya kwenda shule. Nitamtumia Jane/John Doe ambaye kazi yake ni kusafisha ofisi, dereva wa basi, mpishi au mlinzi. Kazi anaanza rasmi saa 12 asubuhi au mapema, hufanya kazi kwa masaa 8 kisha huenda kwenye kazi nyingine ambayo anaingia saa 10 jioni na huko hufanya kazi kwa masaa 5 kabla ya kwenda nyumbani hoi bin taabani, kulala na kuamka mapema tena siu inayofuata.

Mimi huamka saa 12 asubuhi, natakiwa kazini saa 2 asubuhi, kila siku hutoka kazini kurudi nyumbani kati ya saa 1 hadi saa 3 usiku. Muda wangu wa kwenda lunch ni saa 1. Huingia kitandani saa 5 au 6 usiku (pamoja na kuleta kazi nyumbani kumalizia kiporo, pia hupata fursa kuchungulia JF kama sikuibia kuchungulia JF na kuchangia nikiwa kazini). Kisha huamka tena siku inayofuata asubuhi na mapema kuanza sakata jipya.

Kwa wastani, Mmarekani au wale wanaoishi marekani hufanya kazi takriban si chini ya masaa 12 kwa siku. Kuna wanaolipwa kwa saa, na kuna wanaolipwa mshahara bila kujali masaa.

Ikiwa mimi nalipwa mshahara bila kujali masaa na kwa wastani nafanya kazi karibu masaa 50-60 kwa wiki na wale direct reports wangu wanaofanya kazi kwa kulipwa ujira wa saa nao hufanya kazi na mimi (huenda wana kazi nyingine za ziada) kwa masaa 40 ya kwanza na yale yote ya ziada ni OT, najiuliza, je ni ajabu kuwa wenzetu kama Taifa kwa kupitia viwanda, na hata shughuli za huduma mpaka kilimo wanaendelea kuitwa nchi zilizoendelea?

Ikiwa kuchapa kazi bila kubangaiza ndio tabia na utamaduni wa Mmarekani, Mchina, Mjapan hata Mbrazil, je sisi Watanzania tuna utamaduni na tabia gani mbele za kazi?

Nakumbuka nikifanya kazi nyumbani (TZ), kwanza ukichelewa kazini (unatakiwa kazini saa 2 asubuhi), unalaumu Uda na vipanya, ukishaingia na kuonekana, unatoweka kwenda kupata kifungua kinywa, unapotea kwa muda wa nusu saa hadi saa kamili (unalipwa kwenda tafuta kifungua kinywa!), mchana ukiwadia, Lunch ni saa moja na ushehe, kisha saa tisa alasiri kuna kupata kitafunwaji kingine, ikifika saa kumi jioni, ni kufungasha makabrasha haraka kuwahi basi la kukurudisha nyumbani au kukimbilia "stoo" kwa mama vitunguu kuziguguda!

Ukiangali kwa watsani, muda niliofanya kazi ni masaa 5.5-6 na mawili katika hayo masaa 6 ni kubangaiza kwa stori za mpira, wanawake, siasa, kupekenyua JF au Dar Hotwire na kupanga mikakati ya kilauri!

Najiuliza leo hii, pamoja na kuwa twadai nidhamu ya kazi imerudi (kwa wale wanaofanya kazi kwenye makampuni binafsi na ya kigeni!), lakini tija na ufanisi wetu ni bado unagota, tunatarajiaje kuwa tutapiga hatua?

Kukitokea msiba kwa jirani, twachukua siku tatu (tena unalipwa mshahara!) kuomboleza, Ng'ombe akikata kutoa maziwa, twaenda kazini na kuaga "nakwenda kwa veti" huku muda ambao haupo, unaendelea kulipwa, mbaya zaidi, tunataka mwajiri atulipie huduma za afya, nauli ya basi na lanchi!

Jee tutafika na kufanikiwa ikiwa tumejijengea hii tabia ya kuwa wabangaizaji na wavivu?

Hivi leo Mkandara, Mzee ES, Mwk, Nyani, Rev., Mwanakijiji na wengine waishio nje ya nchi wakirudi nyumbani wakapewa nafasi ya kuongoza na waanze kuongoza na kufanya utendaji kama walivyojifunza huko waliko uchapakazi wa kuhenyeka na ufuatiliaji makini si Tanzania itaanza badilika na hasa kama tutakwenda Serikalini (kisingizio kikuu cha nchi kukosa maendeleo kila siku ni eti Serikali mbaya!) na kuanza kupaa kwa mwendo wa Kipanga na sii kasungura?

Au tukija na hizi tija za "kinyamwezi" kuchapa kazi na kutaka uwajibikaji wa kuchapa kazi tutaitwa "wazungu" na kuendewa Bagamoyo au Mpanda ili tufundwe? Au vijembe vya chini chini kama vile vilivyompata yule mkuu wa TPRI Dr. Bamwenda au yule Kaburu wa Muhimbili Trigonometry vitatukumba na kutufanya tuachie ngazi na kutafuta nauli kurudi "utumwani" unyamwezini ambao juhudi za kufanya kazi kwetu zinaheshimika?

Hivyo basi ni nini kinatakikana katika kujenga utashi wa Mtanzania awe na jitihada na uchacharikaji kama Mchaga au Mpemba katika utafutaji na kuchapa kazi?
 
mzee hapa umeleta hoja.. tena ina nguvu ndani yake.. ngoja hili pilau lishuke kidogo tuanze kujadili..
 
Rev. Kishoka,
Awali ya yote napenda kukupongeza kwa posting yako hii, kwani kwa kiasi kikubwa inatutaka tujadili tatizo ambalo mimi ninaliona ni kubwa sana katika nchi yetu na inawezekana pia lipo katika nchi nyingi za kiafrika. Ulichokiandika sina haja ya kukirudia lakini ndiyo hali halisi ya utendaji wa kazi wa waajiriwa wengi Tanzania.

Mbali ya kuwa wafanyazi hatumii muda sehemu kubwa ya muda wao kwa kuzalisha au kufanya kazi ilikusudiwa, pia ufanisi huwa ni wa hali ya chini pasi na uwajibikaji.

Aidha katika Ofisi nyingi za serikali, Taasisi za Umma na mashirika ya umma wafanyakazi na wasimamizi wa kazi hawatimizi au hawafanyi kazi kwa kuzingatia maelekezo ya kazi zao (Job Descriptions) kwa kuzingatia nini cha kufanya kwa siku, wiki, mwezi na hata mwaka. Sitaona ajabu kwamba kuna wafanyakazi hadi leo hawajui maelekezo yao ya kazi ni yapi. Sitaona ajabu kwa wasimamizi wa kazi kutokuwa na repoti ya kazi ya siku iliyoisha.
Sasa basi majumuisho yote haya yanaonesha udhaifu mkubwa sana katika usimamizi katika taasisi mbalimbali za umma. Ukilinganisha namna ya utendaji wa kazi katika ofisi za umma na ule wa ofisi zisizo za umma utaona kwa kiasi kikubwa ni usimamizi mzuri unafuata taratibu zote za kazi.

Jambo lingine Rev. Kishoka ambalo mimi linanikera ni ile tabia ya baadhi ya wafanyakazi hufikiria ni nini atafaidika kwanza kwa kuwepo katika eneo lake kazi kabla ya kufikiria wajibu wake. Hii tabia ndiyo imekuwa ni kichocheo cha rushwa, uzembe, kutowajibika na kiwango duni cha huduma kwa wateja.

Ni vema katika mabadiliko yanayofanywa katika upande wa serikali hasa katika mfumo wa utumishi wakaangalia kwa undani sana mapungufu mbalimbali yatokanayo na tabia zisizoridhisha za utendaji kwa upande wa wafanyakazi na na usimamizi wa kazi kwa upande mwingine.

Ni vema pia perfomance appraisal method zikatumika ipasavyo ili kuleta tija na kuwabaini wale wafanyazi wabovu.

Kuna hili tatizo kutokuwa na UAMINIFU miongoni mwa wafanyazi katika ngazi mbalimbali. Tabia hii ni kama donda ndugu kwani linatia doa kubwa sana sifa nzuri za Nchi yetu. Kuna baadhi ya wafanyakazi katika taasisi mbalimbali ziwe za umma, binafsi na hata mashirika ya kimataifa ambao hawajui kitu kingine zaidi ya kumwibia mwajiri wao. Tatizo hili linawaogopesha baadhi ya waajiri kutoa ajira fulani kwa watanzania na badala yake kutoa ajira nyingi kwa nafasi za chini na chache katika nafasi za katikati.

Endapo tutaweza kupambana na tabia hizi mbaya nina hakika watanzania wataweza sio tu kujipatia ajiri nyingi zaidi ndani na nje ya nchi bali pia kuweka misingi ya kuboresha maisha ya wale ambao wapo njiani kuingia katika ajira.

Ninakushukuru Rev. Kishoka kwa mawazo yako hayo.
 
Pundamilia,

Nashukuru sana kwa kuongeza wigo wa hoja hii hususan kuhusiana wajibu wa kazi za watu (job description).

Ni jambo la kustaajabisha kuwa katika karne hii ya nano technology, sisi bado tunafanya mambo kama tuko kwenye mfumo wa Ludism, au ndio tunakaribia kuwa na mapinduzi ya viwanda!

Nilipopigia kelele mfumo mbaya wa Elimu na mapungufu ya wasomi wetu katika kuleta tija, motisha, ubunifu na ufanisi katika kazi, nilikuwa in mategemeo yangu kuwa kwa kutumia uwezo wetu wenyewe na si "wataalamu" wa kuagiza kutoka Japan, Norway au Kenya, tungeng'amua ni nini tunapaswa kufanya ili kuboresha maendeleo.

Azimio lilisema tunahitaji Watu, lakini tumechukulia kuwa kuwa na mlundiko wa watu ndio suluhisho la maendeleo?

Kama Tanzania tungebadilisha nidhamu zetu katika kazi, tungeweza kupiga hatua kubwa sana na hata kuwa katika maendeleo makubwa ambayo yangepunguza ushawishi wa kutafuta njia fupi fupi za kujipatia vipato vya kukidhi mahitaji.

Najua kuna wengine tutasema kwa sauti na vinubi kuwa ni jukumu la Serikali, mimi na sema ni jukumu la jamii na hili lianzie nyumbani, liendelezwe mashuleni na ndipo utakuta nidhamu unakuwa na kujijenga kwa ushamiri pindi mtu anapofika kuajiriwa kwa maana ameshapandikizwa mbegu ya tija na ufanisi na kila hatua anayopanda kielimu ni kuongeza ubunifu na maarifa.

Lakini hata hivyo, hatujachelewa kuanza kuleta mabadiliko ya nguvu katika uchapa kazi makazini na hata mashambani. Kinachohitajika ni mwongozo na kutokuogopana au kupoa na kuweweseka kwa kuitwa "Wakuda"!
 
Pundamilia,

Nashukuru sana kwa kuongeza wigo wa hoja hii hususan kuhusiana wajibu wa kazi za watu (job description).

Ni jambo la kustaajabisha kuwa katika karne hii ya nano technology, sisi bado tunafanya mambo kama tuko kwenye mfumo wa Ludism, au ndio tunakaribia kuwa na mapinduzi ya viwanda!

Nilipopigia kelele mfumo mbaya wa Elimu na mapungufu ya wasomi wetu katika kuleta tija, motisha, ubunifu na ufanisi katika kazi, nilikuwa in mategemeo yangu kuwa kwa kutumia uwezo wetu wenyewe na si "wataalamu" wa kuagiza kutoka Japan, Norway au Kenya, tungeng'amua ni nini tunapaswa kufanya ili kuboresha maendeleo.

Azimio lilisema tunahitaji Watu, lakini tumechukulia kuwa kuwa na mlundiko wa watu ndio suluhisho la maendeleo?

Kama Tanzania tungebadilisha nidhamu zetu katika kazi, tungeweza kupiga hatua kubwa sana na hata kuwa katika maendeleo makubwa ambayo yangepunguza ushawishi wa kutafuta njia fupi fupi za kujipatia vipato vya kukidhi mahitaji.

Najua kuna wengine tutasema kwa sauti na vinubi kuwa ni jukumu la Serikali, mimi na sema ni jukumu la jamii na hili lianzie nyumbani, liendelezwe mashuleni na ndipo utakuta nidhamu unakuwa na kujijenga kwa ushamiri pindi mtu anapofika kuajiriwa kwa maana ameshapandikizwa mbegu ya tija na ufanisi na kila hatua anayopanda kielimu ni kuongeza ubunifu na maarifa.

Lakini hata hivyo, hatujachelewa kuanza kuleta mabadiliko ya nguvu katika uchapa kazi makazini na hata mashambani. Kinachohitajika ni mwongozo na kutokuogopana au kupoa na kuweweseka kwa kuitwa "Wakuda
"!

Sasa kama tunajua nidhamu yetu ya kazi ni mbaya na tunajua kwamba tunajua kwa nini sasa hatuibadilishi? Au mnaojua hivyo mko wachache mno na wengine walio wengi hawajui? Na nyinyi mnaojua mmeshabadilika?
 
Rev:

Kuna mambo mengi yanayosababisha ulelemama maofisini mwetu:

1)Uongozi Bora
Kama ilivyokuwa kwenye sekta nyingine lukuki, ukosefu wa uongozi bora ni moja ya sababu kubwa inayochangia wafanyakazi kutojali nidhamu ya kazi. Wakurugenzi wenyewe hawajali maslahi ya kampuni, sasa surbordinates watatoa wapi guts za kuchapa kazi?

2)Motisha
Hakuna motisha kabisa huko maofisini. Wafanyakazi hawawi recognized pale wanapo kwenda "above and beyond". Na hata kama recognition ipo, huwa inatolewa kwa upendeleo.

3)Heshima baina ya wafanyakazi
Hapa ndipo kuna kasheshe yote. Huko maofisini mwendo mdundo tu. Yaani kuanzia wakurugenzi mpaka wafagizi, kazi ni kusarandiana tu. Tumeshasikia sana habari za ma-DG kuwa na vimada kila department. Wanadiriki hata kupikana majungu na kufukuzana kazi kwa uzinzi. Mambo kama umbea, majivuno na dharau zisizokuwa na msingi, ushirikina ni baadhi ya mambo mengine yanayosababisha uvunjaji wa heshima baina ya wafanyakazi.

4)Mission Statement
Mashirika mengi either hayana mission statement or hayatilii maanani iliyopo. Mission statement ndio kioo/kanuni za shirika. Wafanyakazi wote wanapaswa kutenda kazi kwa kuzingatia MS. Mfanyakazi yeyote anayepindisha MS hafai kuendelea kulitumikia shirika.

5)Mengineyo.....
 
Sasa kama tunajua nidhamu yetu ya kazi ni mbaya na tunajua kwamba tunajua kwa nini sasa hatuibadilishi? Au mnaojua hivyo mko wachache mno na wengine walio wengi hawajui? Na nyinyi mnaojua mmeshabadilika?

Nyani, nimekupa mfano wa Dr. Bamwenda, na zaidi, nimesema mwamko wa mabadiliko hauanzii makazini pekee, bali ni nyumbani tangu mtoto anapokua. Ikiwa mtoto atalelewa kuruhusiwa kuwa mvivu na goigoi, basi hata akipata mvi ataendelea kuwa na tabia hizo hizo za kizembe na kivivu!

KWa makazini, kinachohitajika ni shria kali ambazo zinawawajibisha Watendaji (maofisa wakuu) na pia kuwapa Watendaji hawa wakuu, msumeno kuhakikisha kuwa from top to bottom, same demandsza efficiency and productivity are being demanded and met.

Kuna haja pia ya kuhakikisha kuwa nyenzo hizi za nidhamu za kazi, hazita zidiwa nguvu na sheria mbuzi za Kazi au mamlaka za vyama vya wafanyakazi ambao hukimbilia kutafuta mianya kulinda maslahi ya wafanyakazi wazembe.

Nakubaliana na QM kwenye vigezo alivyoleta kuhusiana na shida ya kuimarisha uzalishaji mali mahiri.
 
Lakini swali ambalo pia lazima lijadiliwe katika suala hili la tija na ufanisi ni je, mfanyakazi wa chini na wangazi ya kati Tanzania aweza kukaa ofisini masaa 40 (or whatever is required) bila kwenda kuchakarika na akaishi kwa kutumia kipato chake kukidhi mahitaji yake na ya familia yake?

Na swali linaloendana na hilo pi ni kuwa ni kuna uhusiano gani kati ya tija na kuridhika na kazi au maisha? Je mtu asiyeridhika na maisha yake aweza kweli kuwa na tija? Ni jinsi gani tunaweza kufanya wafanyakazi waishi vizuri ili waongeze tija? Ukiangalia wakati mwingine hata watu wanaolipwa vizuri na kupewa kila aina ya masurufu na wenyewe tija yao inaweza isiwe ile inayotarajiwa.
 
Nyani, nimekupa mfano wa Dr. Bamwenda, na zaidi, nimesema mwamko wa mabadiliko hauanzii makazini pekee, bali ni nyumbani tangu mtoto anapokua. Ikiwa mtoto atalelewa kuruhusiwa kuwa mvivu na goigoi, basi hata akipata mvi ataendelea kuwa na tabia hizo hizo za kizembe na kivivu!

KWa makazini, kinachohitajika ni shria kali ambazo zinawawajibisha Watendaji (maofisa wakuu) na pia kuwapa Watendaji hawa wakuu, msumeno kuhakikisha kuwa from top to bottom, same demandsza efficiency and productivity are being demanded and met.

Kuna haja pia ya kuhakikisha kuwa nyenzo hizi za nidhamu za kazi, hazita zidiwa nguvu na sheria mbuzi za Kazi au mamlaka za vyama vya wafanyakazi ambao hukimbilia kutafuta mianya kulinda maslahi ya wafanyakazi wazembe.

Nakubaliana na QM kwenye vigezo alivyoleta kuhusiana na shida ya kuimarisha uzalishaji mali mahiri.

Sasa kwa nini mwamko haupo majumbani wakati tunajua inatakiwa iwe hivyo...?
 
Lakini swali ambalo pia lazima lijadiliwe katika suala hili la tija na ufanisi ni je, mfanyakazi wa chini na wangazi ya kati Tanzania aweza kukaa ofisini masaa 40 (or whatever is required) bila kwenda kuchakarika na akaishi kwa kutumia kipato chake kukidhi mahitaji yake na ya familia yake?

Mkjj
Jibu la swali ni lazima liwe hapana haiwezekani. Sio tu kipato kipo chini, bali pia ugawaji wa kipato finyu hicho sio mzuri. Unajua katika moja ya systems ninazo zi-admire za nchi za wenzetu ni jinsi wafanyakazi wanavyolipwa....Ninazumguzia weekly, every other week, 15th and last, and so forth. Sasa nyumbani, mshahara wenyewe hautoshi, halafu inabidi usubirie mpaka kila baada ya siku 30. Inabidi tu kutumia muda wa kazi kuchakarika mitaani kujaribu kuokoteza vidili vya hapa na pale.

Pengine kama tungeanzisha mfumo wa kulipa biweekly, motisha ingeongezeka kwa namna fulani huko makazini.

Na swali linaloendana na hilo pi ni kuwa ni kuna uhusiano gani kati ya tija na kuridhika na kazi au maisha? Je mtu asiyeridhika na maisha yake aweza kweli kuwa na tija? Ni jinsi gani tunaweza kufanya wafanyakazi waishi vizuri ili waongeze tija? Ukiangalia wakati mwingine hata watu wanaolipwa vizuri na kupewa kila aina ya masurufu na wenyewe tija yao inaweza isiwe ile inayotarajiwa.

Sticky!!
 
Zenj unaweza kujenga uwadui mkubwa na wafanyakazi wako iwapo utashindwa kuwapa ruhusa ya kwenda kutafuta kitoweo! Hii imekuwa kama ni haki yao na wasipo ipata inakuwa kazi kweli kweli. Kwa kawaida Zenj watu haingia kazini kwa king'ora na kutoka kazini kwa king'ora vilevile.

Iwapo kusingekuwepo na udhuru wa kutafuta kitoweo, kunywa supu na mambo mengine, ufanisi huko ungekuwa ni mkubwa sana kwani unaingia kazini kama vile unakwenda darasani kwa kengele!

Maalim Seif alijaribu kusimamia nidhamu makazini, na alichoambulia ni kundi kubwa la upinzani dhidi yake..
 
Rev. Kishoka,
Mkuu najua haswa kinachokukuna hapa na jibu utalipata lakini sivyo ulivyotegemea..
La kwanza ni kwamba sisi Wadanganyika bila kupinga ni Wapuuza malengo na wazembe ktk utendaji kazi hata kama tunahitaji kitu.
Binafsi mchango wangu ktk mada hii mbali na sisi wananchi ni lazima nikubali maelezo ya marehemu Mh. JKN kwamba kuna vitu viwili muhimu ambavyo hadi leo hatuna.
Siasa safi in a sense ya (mwongozo) kuwepo System madhubuti inayolinda kisheria sehemu za uzalishaji, wafanyakazi na quality ya kile kinachozalishwa. Yote yaliyozungumzwa hapo mwanzoni ukiyatazama kwa makini utakuta kwamba yameshindikana kutokana na kutokuwepo system bora ya uzalishaji isipokuwa ile inayomlemaza kiongozi na wananchi.

Pili ni Uongozi bora, ambao haupatikani serikalini tu ila hata ktk sehemu za makampuni binafsi. Sisi tumejenga utamaduni wa kufanya kazi kwa kupuuza umuhimu wa kazi hiyo ukilinganisha na maisha yetu sisi wenyewe. Kiasi kwamba leo naweza kosa kazi na bado nikaendelea kulipwa bila kuwepo na sababu muhimu ya kutokwenda kazini. Sina haja ya ku answer to anyone, hadithi yoyote inakubalika.
Mfanyakazi yeyote anapoingia kazini na hakuna chombo (System or leadership)kinacholinda maslahi ya kampuni ama Taasisi anayoitumikia huwa ndio chanzo cha kuitaarifu akili (subconcious mind takes a note) kuwa hapa ni mchezo ule ule wa Kupuuza na kuzembea kazini kwa malipo, hivyo mwili pia hujiandaa kulemaa.

Tatu, Umaskini wa hali na mali.
Yawezekana kuwepo kwa umaskini wa maisha ni mchango mwingine unaojenga Taifa letu kuwa la wapuuzi na wazembe kwani kutokana na umaskini huo akili zetu zimejenga mahitaji yetu ya lazima kutokuwa makubwa (malengo madogo). Ama ni kutokana na kupuuza kwetu mambo muhimu ktk maisha hivyo tumejenga uzembe wa kutofanya kazi kwa malengo ya ufanisi wa hali ya juu tukifahamu kwamba hiyo kazi haiwezi kutuondoa ktk umaskini.
Nakumbuka vizuri nilipokuwa nimeajiriwa mtu yeyote anayefanya kazi huitwa mtwana ama watamcheka na kusema -Duh! jamaa lafanya kazi utafikiri ya babake! - right there, huo ndio Upuuzaji unaotokana na uzembe wa akili kutokuwepo na malengo yanayoweza tokana na ubora wa kazi hiyo..
Hakuna connection kati ya kufanya kazi kwa nguvu na ufanisi kumwezesha mtu kupata mafanikio isipokuwa Ajira yenyewe ndio kielelezo cha mafanikio. Hivyo unapoajiriwa tu akili yako subconciously inakaa macho kutazama opportunities za ziada nje ya masaa ya kufanya kazi kwani hayahusiani kabisa na uwezo wa mtu kufikia goals zake.
Nne, kuna hili swala la Shida (demand) kuzidi supply ambalo ni chimbuko la ufanisi ktk uzalishaji..aidha tuna wataalam wachache sana sehemu za kazi kiasi kwamba mwajiri huwa hana budi kukubaliana na hali halisi ya uzembe kazini. Pia yawezekana tatizo hili chimbuko lake haswa ni pale Quality inapokosa nafasi kabisa zaidi ya Quantity!
Kutokana na demand market level kuwa high zaidi ya supply basi vitu vyote ktk hali yoyote ile vinaweza uzika.
Utakuta Hotel zinapika vizuri siku za Ufunguzi lakini baada ya muda wakisha jenga market fulani basi huanza kupuuza ubora wa chakula kuwa ndio kivutio cha biashara. Mwenye biashara atakata wafanyakazi, wafanyakazi wataanza kujenga kiburi (Kupuuza na kuzembea) wakijua kwamba ufanisi sio guarantee ya kuvuta wateja.. wateja ndio wenye njaa kwani demand ya chakula na mahotel ni kubwa kuliko zilizopo na kama hapati wateja basi kuna mkono wa mtu..

In short, nimeshindwa kujizuia mkuu...
NDIVYO TULIVYO! haaa haaa haa!
 
Ninarudi tena katika kuchangia mada hii lakini hasa nikirejea michango ya waliotangulia.

Suala la kukosa ufanisi katika kazi ni pana sana na kama alivyoanza Rev. Kishoka amejaribu kuangalia mazingira ya nchi tofauti na ya kwetu kwa kutupa hali halisi. Nadhani ni vema basi tuka-share uzoefu wetu halisi kwa yale yanayofanyika nyumbani (Tanzania) na yale yanayofanyika kwingineko.

Nakubaliana na Rev. Kishoka kuwa si kila jambo baya linaloikabili nchi hii basi limesababishwa na serikali, jamii yenyewe pia ina mchango mkubwa katika kuzorotesha maendeleo ya nchi yetu. Kuna semi mbalimbali za kiswahili zilizosheni busara ndani yake kama vile:

'Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo'

'Samaki mkunje angali mbichi'

Ninachotaka kusema ni kuwa huenda wengi wetu hatukuwa-exposed na mazingira ya kufanya kazi kwa ufanisi na uadilifu kwa hiyo basi inatuwia vigumu hata kuweka mada zetu kwenye mizani na kuzijadili kwa lengo la kupata suluhu ya matatizo yanayolikumba taifa kwa sasa na labda kwa muda mrefu ujao. Kama at this point hatuamini kuwa tuna tatizo linalohitaji kutatuliwa, ni kwa namna gani utaweza kumuhimiza mtoto wako awajibike kwa yale ambayo anatakiwa kuyafanya? je ni kwa namna gani utakuwa tayari kumjengea mtoto wako mazingira ya uwajibikaji? Kama haya yote tunayaona ni mambo yaliyo mbali na ukweli basi dhahiri kuwa hatujui ni nini hasa tunachotakiwa watoto wetu wawe-exposed nacho ili wajenge taswira itakayozaa fikra sahihi.

Kwa mfano katika elimu, ni wazazi au walezi wachache sana wa Tanzania ambao huwajibika vilivyo katika kufuatlia masuala ya ya shule ya watoto wao kila siku. Wazazi hawatimizi wajibu wao wa kupitia kazi za watoto na kuhoji au kuelekezana juu ya yale yaliyofanyika shule. Huku ni kutokuwajibika kwa mzazi na pia ni kumnyima mtoto funzo la kuwajibika.

Sasa tabia kama hizi ndiyo huwa zinabebwa na kuwa ni sehemu ya maisha, ukienda kazini hali inakuwa ndiyo hiyohiyo ya kutokuwajibika na watoto wanakuwa bila ya kupata exposure ya uwajibikaji, na ndipo tunaporudi katika ule usemi wa 'mtoto umleavyo ndivyo akuavyo' na 'samaki mkunje angali mbichi'.

Ni vema wanaJF tukaangalia na kuchambua matatizo halisi yanayoikabili jamii ambayo ni kutokuwa na tija katika kutenda kazi zetu. Tusikimbile kutafuta visingizio kwani havitatusaidia kamwe. Hali ngumu ya maisha isiwe sababu ya kutufanya tutoke katika mstari sahihi wa kupiga hatua za kuelekea kwenye maendeleo ya kweli. Kama umeajiriwa na unaona kipato cha ajira yako hakikutoshi, acha kazi tafuta njia nyingine unayoona itakusaidia kukidhi mahitaji yako yote. Tunahitaji wafanyakazi waliotayari kufanya kazi kwa mujibu wa taratibu za kazi zinavyoelekeza na si vinginevyo.

Namalizia kwa kusema matatizo ya uzembe kazini kwa sehemu kubwa yanaanzia kwenye jamii yenyewe.
 
Lakini swali ambalo pia lazima lijadiliwe katika suala hili la tija na ufanisi ni je, mfanyakazi wa chini na wangazi ya kati Tanzania aweza kukaa ofisini masaa 40 (or whatever is required) bila kwenda kuchakarika na akaishi kwa kutumia kipato chake kukidhi mahitaji yake na ya familia yake?

Na swali linaloendana na hilo pi ni kuwa ni kuna uhusiano gani kati ya tija na kuridhika na kazi au maisha? Je mtu asiyeridhika na maisha yake aweza kweli kuwa na tija? Ni jinsi gani tunaweza kufanya wafanyakazi waishi vizuri ili waongeze tija? Ukiangalia wakati mwingine hata watu wanaolipwa vizuri na kupewa kila aina ya masurufu na wenyewe tija yao inaweza isiwe ile inayotarajiwa.

Nyerere alisema Kazi ni Msingi wa Maendeleo na Utu!

Nitaanza kukujibu kwa kutumia Kipato kama kigezo. Ndiyo hali halisi inafanya wengi wetu tulioko nyumbani tutumie 30% ya muda ambao tunapaswa kumtumikia mwajiri wetu kujitafutia kipato cha ziada. Swali litakuja, je nini chimbuko la kukosekna kwa uwiano wa mapato na matumizi (hali halisi ya ukali wa maisha)?

Jibu ni udhoofu wa mapato katika viwanda, biashara, makampuni, kilimo, ufugaji, uchimbaji madini, n.k. Kama tungekuwa tunaendesha shughuli zetu za uzalishaji mali kwa ufanisi wa hali ya juu (mipango na ufuatiliaji) ambayo inaambatana na Ubunifu (tija, maarifa) na kuhakikihisha kuwa tunapima ukuaji wetu (matumizi na mapato ya uzalishaji) basi tusingeishia kuwa Taifa la Wabangaizaji!

Kuna wengine watasema chimbuko hili la kudhoofu kwa mapato ya Taifa ni kutokana na Azimio la Arusha, Sera za Ruksa, Utandawazi na hata Ufisadi. QM ameongelea Uongozi Bora, sisi wengine tunachukulia Uongozi bora kwa mantiki ya Kisiasa, lakini Uongozi bora huanzia Nyumbani, kisha huenda Shuleni, Kazini na mwishowe Serikalini (kisiasa na utendaji).

Tuchukulie mfano wa Hospitali ya Muhimbili, je Muhimbili ina uongozi Bora? Jibu i hapana! Alipokuja Mzungu na kuboresha nidhamu ya Kazi, tulilalamika kwa nini hatupewi mwenzetu ambaye ni msomi. Tukamfukuza Mzungu, tukawapa Wenzetu wazawa, Ubangaizaji ukarudi skwea wani!

Uongozi bora si vyeti pekee au ubingwa katika fani fulani! Uongozi bora ni umahiri wa kuongoza watu kwa kuwatia hamasa, kutimiliza malengo na maono (vision) ya kazi na uzalishaji mali, kutumia haki, busara na sheria, kuwajibika kwa kuchochea ufanisi, uadilifu, ubunifu, kutumia vizuri mapato na kudhibiti matumizi hivyo kuongeza mgawanyo wa mapato (Mishahara na huduma nyingine), kutafuta na kuwa wabunifu wa kuongeza mapato, kuongeza ubora wa bidhaa na kustahilimli ushindani wa wazalishaji mali wengine na hata bidhaa za kuagizwan.k.

Naam, kama tungejijenga vizuri kwakutumia nyenzo tulizokuwa nazo tangu tunapata Uhuru na hata vipindi vyote vya mpito, basi vipato vyetu na lile Tabaka la kati lingekuwa kubwa sana. Sera za kujijenga na kulijenga Taifa zilikuwepo tangu awali, tatizo lilikuja kwenye Utekelezaji na Tija.

Kwenye mada ya Agano Jipya kama sikukosea, nimezungumzia suala la Corporate Welfare na lile la kusubiri Nabii afanye kila kitu, afikiri, ahubiri na achimbe handaki! Aidha nilizungumzia upofu wa Watanzania na hasa Wasomi na Viongozi ambao waliacha kuchapa kazi na kutafuta njia nyepesi na fupi kuwa na mali nyingi na kuishi katika anasa kwa kuwa wameona kina Rokifela na matajiri wa Ulaya na Mameneja wanatanua.

Tulichoshindwa sisi ni kuwa na Subira! Badala ya kutokea jasho uzalishaji mali ili tule kivulini, sisi tunakwepa kuvuja jasho na kukimbilia kivulini kutafuta mbinu za kula.

Hivyo basi, kisa cha Mtanzania kubangaiza na kuacha kufanya kazi masaa 40 kwa moyo na dhati, kina sababu nyingi, lakini tukiendelea kuhalalisha sababu hizi na kusema basi tufungie macho Ubangaizaji, kamwe hatutaendelea.

Turudi na kujisuta nadhiri na nafsi zetu, je tukibadilisha mawazo na mfumo wetu wa kufanya kazi, tangu nyumbani, tutaweza kufanikiwa? Ikiwa leo Kila mtu ataamka na kusema "naukataa Ubangaizaji na majaribu yake yote" na kuingia kazini au mashambani na kuchapa kazi kwa nguvu zote, je hatutaona matunda?

Ikiwa tutabadilisha mentality kuhusiana na kufanya kazi, ndipo tunaweza kutibu kuridhika na kazi na hivyo kuongeza tija na bila kusubiri kusukumwa au motisha kufanya kazi kwa umahiri!
 
The only turning point ya kweli kwa mwanadamu kama mtanzania itakuja tu pale michezo yatu ya kizembe itakapokuwa haituwezeshi kuendelea kuishi hata dakika moja ijayo...., vinginevyo tubadilike nini wakati ..... kwa namna tunayoishi .....we are not diying, ulaji upo, unabangaiza kiaina na kinywa kinapata riziki! tunaishi na tunapummua....!! The message is...time is coming mtanzania hatawea kufanya usanii kazini akaendelea kuishi au kuwepo! Makosa yatakuwa makubwa na wazi kiasi amabcho huo mtido utakuwa sio compatible na uzalishaji na ufanisi kwa namna yeyote ile.... Kifo kitakuwa ndio hatua inayofutia...Ni mpaka hii hali ifikiwa ndio tunaweza kuongelea kuhusu ..... Kuamaka na kujenga nchi katika kufikiri katika hali tmamu!

Na wish huo muda ufike mapema...na sifikiri uko mbali!

Sioni namana nyingine ya kuwaleta watu kwenye fikra zenye mantiki zaidi ya Kifo kifo kusogea karibu kabisa mbele yao!!!
 
Kwa bahati mbaya maneno pekee hayajengi nchi wala kuleta maendeleo! Ingekuwa hivyo mbona tungekuwa mbali...
 
The only turning point ya kweli kwa mwanadamu kama mtanzania itakuja tu pale michezo yatu ya kizembe itakapokuwa haituwezeshi kuendelea kuishi hata dakika moja ijayo...., vinginevyo tubadilike nini wakati ..... kwa namna tunayoishi .....we are not diying, ulaji upo, unabangaiza kiaina na kinywa kinapata riziki! tunaishi na tunapummua....!! The message is...time is coming mtanzania hatawea kufanya usanii kazini akaendelea kuishi au kuwepo! Makosa yatakuwa makubwa na wazi kiasi amabcho huo mtido utakuwa sio compatible na uzalishaji na ufanisi kwa namna yeyote ile.... Kifo kitakuwa ndio hatua inayofutia...Ni mpaka hii hali ifikiwa ndio tunaweza kuongelea kuhusu ..... Kuamaka na kujenga nchi katika kufikiri katika hali tmamu!

Na wish huo muda ufike mapema...na sifikiri uko mbali!

Sioni namana nyingine ya kuwaleta watu kwenye fikra zenye mantiki zaidi ya Kifo kifo kusogea karibu kabisa mbele yao!!!

Azimio,

It is interesting jinsi kukaa Ughaibuni unavyojifunza kutumika! Everything has a price and cost. Nyumbani, ukiishiwa unakimbilia kwa mjomba, shangazi, mshikaji na sehemu nyingine kujishikiza. Maji yakikatwa na Dawasco, unatoboa tundu jipya, Umeme ukikatwa, vibatari milele, simi ikikatwa unakwenda kwa jirani. Ukishindwa kulipa kodi ya pango, mwenye nyumba kukufukuza ni kazi, usipolipa kodi ya nyumba kama ni yako, mamlaka ya mji haina uwezo kukufilisi au kukamata mali.

In Tanzania, everything is made to provide convenience to avoid responsibilities.

In US, hata aliyetajiri anaamka asubuhi kwenda kazini. Maji, Umeme, Gesi, kipasha Moto na Kiyoyozi, Simu, Elimu, Afya na Chakula si vya bure. Ndiyo kuna Welfare programs ambazo Serikali hutoa pesa, lakini ukipima uwiano wa wale ambao ni Wabangaizaji wa kujitakia na ambao hawana kazi kutokana na ukosefu wa kazi (kuridhika kwa kazi au kuchagua kazi) , utakuta sisi Tanzania, asilimia kubwa ya kukwama kwetu inatokana na ubangaizaji na kuwepo kwa mihimili ya "alternative convenience means" kwa mjomba, shangazi, risiti hewa, na upupu mwingine tele wa kujipatia kwa njia fupi!
 
Kwa bahati mbaya maneno pekee hayajengi nchi wala kuleta maendeleo! Ingekuwa hivyo mbona tungekuwa mbali...

Nyani, "unatuvamia";)

Kwanza huanza mawazo, kisha maneno na halafu vitendo. Tunafikiri binafsi, tunazungumza kama gumzo kufundishana na kisha huchukua mbinu bora zilizotokana na mwazo na mazungumzo na kuzifanya vitendo; Kuchapa Kazi.

Natamani sana Tanzania tukipata watu 10,000 katika nyanja za Uongozi na utendaji ambao watakuwa kama Mzee Ben Mulokozi aliyekuwa Utumishi!
 
Rev.Kishoka,

..matatizo yetu yanatokana na MINDSET. chanzo cha mindset hiyo ni siasa za ujamaa na umilikaji mali wa umma.

..wakati wa Ujamaa viwanda na mashirika vilikuwa mali ya umma. matokeo yake tukaajiri watumishi wengi kupita uwezo, na vilevile tukashindwa kufukuza wale wazembe.

..Meneja aliyejaribu kufukuza kazi wazembe, au kudhibiti ajira, alionekana mbaya mbele ya jamii. Alionekana kama mtawala anayejaribu kuhodhi mali ya umma, na kuzuia wananchi kufaidi matunda ya uhuru wao. Mameneja wa aina hiyo waliandamwa na wanasiasa, jumuiya za wafanyakazi, na hata kwenye vipindi vya redio kama mikingamo.

..Kutokana na kushindwa kudhibiti ajira, na kuhimiza uwajibikaji na tija, viwanda na mashirika yakashindwa kuzalisha. Matokeo ya kushindwa kuzalisha na ajira zilizozidi uwezo yakasabisha watumishi walipwa ktk viwango visivyokidhi mahitaji ya lazima.

..Hili tatizo litaisha kwa kuondokana na dhana ya mali za umma. Wengi bado tunalilia mashirika ya umma, lakini tunasahau kwamba utendaji ktk mashirika ya umma ulikuwa ni aibu ya kutisha kwa taifa letu.

..Hata kama tutakuwa na mashirika ya umma, basi kipaumbele kiwe ktk kutengeneza faida na siyo kutoa huduma.

..Vilevile mashirika na idara yajielekeze ktk kuajiri wafanyakazi wachache, wenye nidhamu, na wanaolipwa mafao ya kutosha. Mameneja wawe na nguvu za kuamuandika mtu kazi, au kumfukuza bila kuingiliwa.

..My observation ni kwamba wale ambao ajira zao zinawapatia vipato vinavyokidhi mahitaji muhimu wanachapa kazi kama vile wako nchi za magharibi.

..Tatizo lingine ni huu utaratibu wa watumishi, haswa serikalini, kuishi kwa kutegemea posho za safari na vikao. Kwa kweli ktk safari na vikao watu wanajituma kwelikweli. Hii ni tofauti kabisa na wanapokuwa ktk majukumu yao ya kawaida. Serikali inapaswa iliangalie hilo kwa umakini mkubwa.

..Kwa upande mwingine naamini wakulima wa Tanzania ni wachapa kazi. Wajomba na shangazi zangu wanaamka saa 10 asubihi kwenda shambani. Wanapumzika kidogo tu jua linapokuwa kali. Wengine hurudia hata usiku ikiwa kutakuwa na mbalamwezi kwa shughuli ndogo ndogo.

..Vilevile mama wa nyumbani kijijini anafanya kazi ngumu,kwa muda mrefu, ktk mazingira magumu kuliko wafanyakazi ktk nchi za magharibi.

..Tatizo la wakulima ni vitendea kazi na kutokuwepo kwa incentives za kuwafanya wazalishe ziada.

..Katika maeneo ambapo mkulima akizalisha ziada anakuwa na nafasi ya say, kupata mtaji wa duka, au kujenga nyumba bora, au kupeleka wanae shule, basi utaona wakulima wanajituma zaidi.

..Hoja hiyo hapo juu inakurudisha ktk kuhoji na kuchunguza mahusiano kati ya serikali/chama na wakulima, wafigaji, na wavuvi.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom