Quemu
JF-Expert Member
- Jun 27, 2007
- 984
- 128
Kuna mjumbe mmoja kule nyuma amesema kuwa Mtanzania wa kima cha chini hawezi kumudu maisha.Ni kweli.Ila nabishana nae anaposema kuwa Marekani mtu wa kima cha chini anaefanya kazi kwa masaa 40 kwa wiki anayaweza maisha.Hapa nasema NO.
Ukiwa na masaa 40 kwa marekani huku ukilipwa dola 10 kwa saa,ina maana kwa wiki una $400 na kwa wiki una $1600 hapo ni bado hujatoa tax ambayo kwa namna yeyote ile huwezi kuikwepa.Baada ya hapo toa bili ya appartment say $700,gas say $100,Umeme na maji,simu,Chakula,bado Insurances kama za Afya,gari nk bado mkopo wa gari hujamaliza $800.HAKIKA HUTABAKI NA KITU CHOCHOTE MWEZI unaofuata
Majita:
Ni kweli kima cha chini sikuzote hakiwezi kutosheleza mahitaji. Lakini mimi nafikiri system ya utoaji mishahara pia inachangia. Tukitumia mfano wako, tutaona kwamba sio tu hiyo $400 inakuwa earned kila week, bali pia inalipwa kila week. Sasa basi, pamoja ya kwamba gross salary ya $1600 ni ndogo sana, lakini bado inakidhi mahitaji mengi kutokana na kukatwa vipande vipande kila week. Labda nijaribu njia nyingine, ukichukuwa watu wawili ambao wanatengeneza $1600 kila mmoja - mmoja analipwa $400 kila wiki na mwignine analipwa $1600 kila mwishoni mwa mwezi, ni yupi atakuwa na nafasi mzuri ya ku-take care bills zake on time? Ni rahisi kuigawanya $400 kwa 7, lakini ni kazi ngumu mno kuigawanya $1600 kwa 30... Afterall, money is such a brain damager...
Kuugawanya mshahara into multiple payments ni aina ya motivation. Wafanyakazi wanakuwa motivated zaidi wakati wa tarehe za paycheck just before and after, na kufa moyo pale wanapoona tarehe ya mshahara hashikiki kwa umbali.