Dyabala vs Manchester United vs Juve vs Lukaku ni vituko

marcoveratti

JF-Expert Member
Sep 21, 2017
968
1,694
Acha nikwambie ,ilikua ni hivi Ile inshu ya Paul Dybala, #Manchester_United na #Juventus

Inter Milan walikua kwenye mazumgumzo na Manchester united kumsajili Lukaku , mazumgumzo hayo yalitumia wiki takribani mbili bila kupata muafa hasa kwenye upande wa bei ya usajili ,Inter Milan hawakuwa na pesa au kiwango cha pesa iliyotajwa na Manchester united.. Ila walikua wanamuhitaji sana Lukaku hasa kocha Antonio Conte . ..

Oooh Lukaku anauzwa basi acha tuone tutampata vipi .. kiwango cha pesa tunakijua je tunaweza kuwa nacho ...?? !! Haya ni maswali waliojiiza Juventus .. tufanyaje sasa .. tuangalie uwezekano wa kuwashawishi .. Nani anaweza kuwa ni ushawishi ili dili hili liafanyike .. fasta Mzee Maurizio Sarr akasema basi mtoeni Dybala kama ushawishi wa dili hilo maana naona yeye hayupo kwenye mipango yangu ..

Aaaaah Mzee umeongea point sana .. Viongozi wa Juve walinena ... Haraka wakapiga simu kwa uongozi wa Manchester united .... "Tunamtaka Lukaku Ila hatuna pesa mpo tayari kufanya dili na Sisi .. ?? ..

Kabla sijaendelea acha nikwambie hili .. Juve ndio walikua na mpango wa kufanya usajili kuliko Manchester united .. Man United wao walikua wanataka pesa taslimu ... Kwaiyo dili hili waliloliibua ni Juve wala Manchester united walikua hawapo kwenye mpango wa dili hilo na ndio maana taarifa za mwanzoni kuhusu dili hilo zilitoka kuwa Juve wapo tayari kumtoa Dyabala na pesa juu coz wao ndio waliokua na uhitaji zaidi ya biashara hiyo ..

Haya basi twende pamoja mtu wangu ..

Baada ya swali lile ,Man United wakasema haya tuambieni mnatakaje kwani ..!!? Juve ni rahisi tu tuna Dyabala na pesa kiasi mtupe Lukaku ....Sasa mnasemaje ..??

Manchester United wakasema basi kama ni hivyo twendeni kwenye mazumgumzo hayo , Juventus wakasema sawa so tufanyaje ..?? United wakasema Sisi tena semeni nyine maana ndio mmeleta dili .. Juve basi sawa sisi hatuna tatizo na nyie na jua hatutashindwana ... Ngojea tumwite Dybala kisha tumwambie mpango uliopo na baada ya hapo mfanye nae mazumgumzo ya maslahi yake .. ??? Ooooook basi fanyeni hivyo ..

Ngriii ,ngriiii .... Halooo ..Eeeh ebana kuna taarifa za mteja wako zipo hivi na vile sasa fanya uje Turin tuzungumze .. hapa alipigiwa simu wakala wa Dybala .. sawa wajomba fasta nakuja hapo ... Wakala alifurahi sana dili hilo maana lilikua manufaa nalo ..

Eheee sasa vipi tunafanyaje ..? Haina tatizo acha tumalizane na klabu husika ambayo ni Manchester united ... Basi sawa Ila kabla ya hapo embu jaribu kuongea na muhusika .. aaaah Dybala taarifa hizi anazo so ni kiasi cha mimi tu kumaliza kila kitu .. Juventus wakasema Yess ... Dili linaelekea pazuri ..

Haya jamaa fasta London kwenda kufanya mazumgumzo ... Akawakuta jamaa hawana hata habari .. oya nimekuja sasa tunafanyaje ..? Tuambie wewe .. basi Mimi kama wakala nahitaji £ 10 mil kisha mteja wangu atahitaji £10 mil .. na kuhusu mshahara basi tunataka £ 210,000 na haki za matangazo yake .. kiasi chote kilikua kinaigharimu kama £300,000 kwa wiki Manchester united ..

Daaah mpango mwingine huu ,mbona ghari sana wakuu .. Juventus wakipigiwa simu Ebanaeeeeeeh imekua hivi sasa tufanyaje ..!!! Juventus wakasema basi kama ni hivyo Sisi hatutahitaji hata senti wala hatutaongeza kitu maana tumeona mteja wetu anathamani ya £90 mil , tufanye biashara ya kubadilishana .. kisha hayo maslahi mengine mtahusika nayo ..??

Mmmh lakini sawa basi poa .siunajua tena nj kama dili la mtende kwao Manchester .. wakakubali fasta Tu maana kwao pesa sio tatizo ...
Acha tuzungumze na mwamba Lukaku ... Ngriii ... Ngriiii ... Mzee baba kuna kadha wa kadha sasa wewe na wakala wako nendeni Turin mkamalize mambo ... Daaah Lukaku "asee mambo si ndio haya ,yaani naenda kucha na CR7 .. !?? Mipicha kibao akiwa safarini .. raha iliyoje kwake ..

Kufika Tunir alipokelewa kwa furaha zote na fasta wakamaliza kila kitu na kiasi alikua achukue kwa mwaka £ 12 mil ..

Oyaaaa wazee Sisi huku kila kitu kucheee .. mambo Safi sawiaaaa .. sasa .. Juventus hao .. Manchester united wakasema sawa acha tumpigie wakala wa kijana aje na dogo london kukamilisha usajili ..

Ngriii .. ngriiii .. ngriii ....!!! Holaaa .... Ohoooo mbona hapokei ... wakawarudia Juventus asee mtu wenu apokei simu .. Juventus ... Nini ?? Ngojea tumpigie .... Oya nini tatizo mbona hauendi kumaliza dili ...wakala wa kijana wetu ..

Daaah yaani hata nashindwa kusema ila dogo kama simuelewi anasema eti anataka kubakia Juve ... Anasema kule kuna plesha sana ,Ila acha nimcheki tuone kwenye mazumgumzo ya mwisho..

Juventus ...daaah mbona kama dogo anataka kuleta shida. .. Mara paaap Manchester united hao hapo kwenye simu ... Oyaaaa muda unakwenda na tunahitaji kufanya program mapema inakuaje ..? Juventus .. unajua babu mzungu ,Bibi ni mmakonde (wakaanza kujigonga gonga ) .. Manchester united ..ooooh haya sawa basi kesho tutawapigia ..

Ngriii .... Ngriiii ...ngriiii ... Manchester united hao tena .. oya wakuu dili hilo hatulitaki tena ,tumelivunja kama mnamtaka Lukaku leteni pesa taslimu .. Juventus kwa mshangao ... Aseee mbona mapema maana kijana alikua anaelekea pazuri tuuu .. !!

Manchester United ... Hautaki tena dili la namna hiyo Ila kama mna cash leteni £ 79 mil .. tumememaliza .... Juventus halooo .. halooo ... Jamaaa wameshasakata simu ..

Baadae .. Ngriii ..Ngriii ... Saivi ni kwa Lukaku .. mwamba sasa halooo .. oya panda ndege uje uendelee na program za mazoezi na wenzako .. !! Ohoo tatioz ni nini tena .. Manchester united ongea na wakala wako yaliyotokea.. ila taarifa ndio hiyo wahi Carrington ..

Daaah Lukaku ..asee huyo dogo bwege kweli .. yaani narudi tena Manchester united.. ..

Basi ndio ikawa hivyo Bana .. !! Dawa ya kiburi nu kuwa na kiburi zaidi yake ..
 
Hueleweki ,Ni inter Milan, Juventus Au Manchester United?

Utamuelewa sana kama ukifuatilia vyombo vya habari vya italy kwa sababu hata Dybala na yeye jana kaanza mazoezi.inter nao wanamtaka lukaku tatizo hela ya united waliowatajia wao kulipa hawataki,yaani juve kiujumla wanataka wawape united mario mandjukic.ni tetesi tu za usajili ila kama unafuatilia usajili hizi tetesi zisikusumbue mpaka pale utakaposikia mchezaji kaweka signature baasi.mengine yoote tupa kule ni kelele tu za kuuza habari.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom