Eti! Mchawi wa Manchester United ni Ed Woodward

Kisiwa Cha Harishi

JF-Expert Member
Jun 15, 2019
1,016
2,000
MANCHESTER, ENGLAND.
TANGU Sir Alex Ferguson aondoke, Manchester United imebadili makocha mara nne. Kila anayekuja, anaonekana hafai na kufunguliwa mlango wa kutokea.
David Moyes hakumaliza mwaka, akafunguliwa mlango wa kutokea. Akaja Louis van Gaal, naye akaonekana hafai. Kaja, Jose Mourinho na uzoefu wake wote, naye mambo yamemshinda na sasa yupo, Ole Gunnar Solskjaer, ambaye naye yanaonekana mambo yanamwendea kombo.
Lakini unaambiwa hivi, majanga yote ya Man United yanaanzia kwa Makamu Mwenyekiti wa Man United, Ed Woodward. Ed Woodward ndiye tatizo.
Katika kipindi chake Moyes, alihitaji wachezaji wengi, akiwamo Cesc Fabregas, Thiago Alcantara, Toni Kroos na Mats Hummels, lakini wote hao hakuna hata mmoja aliyempata, Ed Woodward anayehusika na usajili, hakufanikiwa kuwanasa, licha ya mambo kuonekana kwamba yangekuwa safi kama jitihada kidogo tu zingeongezwa.
Badala yake, Moyes alisajiliwa Marouane Fellaini majira ya kiangazi, kabla ya kuongezewa Juan Mata Januari, kabla ya kufukuzwa kazi baada ya miezi 10 huko Old Trafford.
Kocha Van Gaal aliwataka Thomas Muller, Sergio Ramos na Cristiano Ronaldo, lakini hakuna aliyekuja kwenye kikosi hicho cha Old Trafford, huku akipewa wachezaji Ander Herrera, Memphis Depay. Bastian Schweinsteiger, Angel Di Maria na Luke Shaw kwa kuwataja kwa uchache.
Baadaye, akaja Mourinho, ambaye alikuwa na orodha ndefu ya mastaa aliowataka, akiwamo Gareth Bale, Neymar, Antoine Griezmann, Raphael Varane, Dani Alves, Edinson Cavani na wakali wengine kibao, lakini Woodward alifeli, kama alivyomfelisha Solskjaer pia kwenye kumpatia mastaa aliokuwa akiwasaka kama Paul Dybala, Kalidou Koulibaly, De Ligt na wengineo, ambao hakuwanasa na hivyo kupata huduma ya Harry Maguire, Aaron Wan-Bissaka na kinda Daniel James.
Makocha watatu, Moyes, Van Gaal na Mourinho wote wamefutwa kazi, huku wakidaiwa kwamba wameondolewa kimakosa.
Mashabiki wa Man United kwa sasa wamemka na kumtaja Woodward ndiye aondoke kutokana na kuwa kikwazo kwa makocha wengi kwa kushindwa kuwapatia wachezaji wanaopendekeza wasajiliwe, badala yake amekuwa akisajili tu kwa kupaniki, pindi anapoona mambo yanakwenda kombo. Makamu mwenyekiti huyo amekuwa akishindwa kukamilisha dili za usajili na matokeo yake, wachezaji wamekuwa wakitimkia kwenye timu nyingine. Man United ya sasa ingekuwa imejaa mastaa kibao kama wale wachezaji wote waliopendekezwa na makocha wangenaswa na bosi huyo. Hiki hapa kikosi ambachp Ed Woodward ameshindwa kukisajili, wakati walikaribia kabisa kutua Old Trafford.


HUGO LLORIS.
Kwa hali ilivyo kwa sasa, David De Gea atakuwa na uhakika wa kupata namba hata kama kiwango chake kitashuka kwa sababu hakuna anayemsogelea kwa ubora kwenye timu hiyo. Sergio Romero ni mzuri, lakini hali ingekuwa tofauti kwa De Gea kama Woodward angekamilisha ile dili ya kumsajili Hugo Lloris.


DANI ALVES.
Mkataba wa Alves ulikuwa unafika mwisho huko Barcelona na Man United ilionyesha dhamira ya kumsajili, lakini baadaye ikajichelewesha, Juventus ikamwahi staa huyo na kumtia kwenye kikosi chao, huku Man United ikiishia kwenda kumsajili, Matteo Darmian kutoka Torino.


LEIGHTON B AINES.
Wakati David Moyes anatua Old Trafford kuchukua mikoba, chaguo lake la kwanza kwenye beki ya kushoto aliyotaka ni Leighton Baines.
Lakini Woodward alishindwa kukamilisha usajili huo na kuendelea kumwaangusha kocha huyo kwa kumletea beki wa maana wa kushoto kabla ya kwenda kumsajili Luke Shaw, ambaye muda mwingi tu amekuwa majeruhi kikosini.


NICOLAS OTAMENDI.
Hakuna kitu ambacho mashabiki wa Man United kinawauma kama kitendo cha bosi wao, Woodward kujichelewesha kwenye usajili wa beki wa kati, Nicolas Otamendi na hatimaye kunaswa na mahasimu wao, Manchester City. Man United iliendelea kuteseka kwa majanga ya kina Chris Smalling na Phil Jones kwa kitendo cha Woodward tu kuzembea kwa Otamendi.


MATS HUMMELS.
Chaguo jingine la beki wa kati lililosakwa na Man United. Beki huyo alianza kufukuziwa na Moyes, kisha akaja Van Gaal, lakini Ed Woodward aliikosesha tena Man United nafasi ya kuwa na huduma bora kabisa ya beki wa kati wa kiwango cha dunia na matokeo yake kuendelea kuteseka ikicheza bila ya mabeki wa kati wa maana, ambapo wakati mwingine ililazimika kumtumia Daley Blind kwenye beki ya kati.


CESC FABREGAS.
Kiungo wa Kihispaniola, Cesc Fabregas alikuwa kwenye rada za Man United wakati alipokuwa kwenye kikosi cha Barcelona. Kila kitu kilionekana kama vile kinakwenda sawa, lakini Ed Woodward alijichelewesha na matokeo yake kiungo huyo kwenda kujiunga na Chelsea mwaka uliofuatia. Hadi sasa, Man United haijapata kiungo mchezeshaji fundi wa mpira.


ARTURO VIDAL.
Tangu mwaka 2013, Man United imekuwa ikihusishwa na viungo wengi sana, akiwamo Arturo Vidal. Staa huyo wa kimataifa wa Chile, alikuwa kwenye rada za Man United wakati huo alipokuwa akikipiga Juventus na mambo yalionekana kama vile anakwenda kutua huko Old Trafford, lakini Man United ilijichanganya hadi Bayern Munich ikamnasa kiungo huyo, ambaye kwa sasa amechukuliwa na Barcelona.


TONI KROOS.
Chaguo jingine hilo la Kocha Van Gaal wakati alipokuwa Man United. Kipindi hicho, Toni Kroos alikuwa na mpango wa kuachana na Bayern Munich, lakini Ed Woodward alishindwa kukamilisha dili la Mjeruhi huyo aliyekuwa akitaka kabisa kutua Old Trafford na matokeo yake, staa huyo akatimkia zake Real Madrid. Kiungo mwingine aliyesakwa sana na Man United ni Thiago Alcantara, lakini Woodward alifeli.


GARETH BALE.
Karibu makocha wote waliotua kwenye kikosi cha Man United baada ya Sir Alex kuondoka, walihusishwa na mpango wa kumtaka staa Gareth Bale. Moyes alikaribia kumnasa staa huyo, kisha ikaja zamu ya Van Gaal na baadaye Mourinho.
Solskjaer naye kwenye dirisha lililopita la usajili, alidaiwa kumpigia hesabu staa huyo, lakini Ed hakuwa na mpango wa kwenda kukamilisha biashara licha ya kwamba Madrid walikuwa tayari kufanya biashara.


PEDRO.
Wakati anaondoka Barcelona, staa wa Kihispaniola, Pedro alidaiwa anakwenda Man United, lakini Ed Woodward alijifungia tu ofisini kwake na kushindwa kufanya mambo ya maana kwenye kuwasaka wachezaji na badala yake staa huyo alitua zake Chelsea, ambapo amekwenda kuisaidia kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England na Man United ikibaki inashangaa tu.


THOMAS MULLER.
Kocha Van Gaal alihitaji yake na Muller alikuwa tayari kwenda kukipiga Man United, lakini Woodward alishindwa kukamilisha dili hilo na kujichelewesha kwake kulimfanya fowadi huyo wa Kijerumani kubaki zake Bayern Munich.
 

Pain killer

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
2,951
2,000
Nashangaa sana mnavosema man u inapesa, ile hali hawana hata kikosi kipana, cha kumzid man city

Man u sijui wanafeli wapi, kwamba hawana pesa za usajir au?, mbona pep man city anakikosi kipana hadi kero,
 
Top Bottom