Enzi hizo tulikuwa tunafanya kazi bila komputer masaa nae, tunatumiana barua kwa posta, tunapanda UDA bila foleni barabarani, tunakula mikate ya siha, tunaangalia sinema za bure Drive In, kuna treni kila siku kwenda Mwanza na Kigoma na mara kadhaa kwa wiki kwenda Arusha, tunalala chuma kimoja watu wawili na tunajifungulia chai na maziwa kweye vibomba UDSM, tukipikiwa wali maharage lazima litoke tangazo kutuomba radhi pale UDSM, tunaheshimu wanasiasa, tunaandamana siku kuu za sabasaba na kushona (sio kununua) nguo mpya, tunapangiwa kazi hadi Uganda na Kenya tkiwa shirika la East African au customs, raisi na mawaziri wakitembelea mikoani tunaenda kuwapokea na matawi ya miti mikononi!
Yaani, basi tu!
Mwisho wa mambo mazuri bwana ilikuwa Idd Amin alipochukua nchi Uganda na Arap Moi alipochukua nchi Kenya.
Tukapigana vita Uganda
Tukaanza kupanga foleni ya unga na sukari, tukajua kuna mwendo wa kuruka, tukaujua ugali wa yanga, tukawa na maduka ya kaya, zikaingia dala dala, tukaanza kununua bia na soda kwa vibali, ice cream zikapotea, Blue Band za Kenya zikapotea, tukaanza kununua Colgate na kanga toka Kenya kwa magendo, tuaka tunatakiwa kuwa na kibali kuleta debe moja ya mchele toka Mbeya kuja Dar, tukawa tukienda ulaya tunafanya shopping ya colgate, sabuni Imperial na viatu vya kukimbilia (raba mtoni), suruali za Jeans na kodurai zikawa mali adimu sana, tukawa tunakosa usafiri wa kwenda mikoani kwa sababu mabasi ya Relwe na Kamata na Kwacha yamejaa mwezi mzima.
Mmh, kweli mambo hubadilika.