Duuh, wanawake visirani sana

Duuh, wanawake visirani sana

King Savi

Member
Joined
Sep 5, 2014
Posts
71
Reaction score
263
Wakuu heshima kwenu, Mwenyezi Mungu awatie nguvu katika yote mnayopitia zaidi neema yake ikawe juu yenu.

Jana yamenikuta kijana mwenzenu, Shemeji yenu mtarajiwa anafanya kazi ofisi moja na bamkwe wake ila hawajatambulishwa tuu.... Sasa katika mishe za maisha huyu mtarajiwa alifanya matumizi ya kiofisi bila utaratibu sasa wakafanya mpango pamoja na mwenzake waombe hela nyingine kupitia kwa bamkwe ili kuziba hilo gepu, Basi pesa ilipotoka shemeji yenu kamfuata bamkwe kwamba apewe hiyo hela akazibe hilo gepu mzee wa watu akakaza kutoa hela kwamba hawezi kuruhusu hiyo pesa ifanye matumizi mengine.

Bhasi baada ya kikao chao nashangaa natumiwa sms kwamba mimi sina adabu na nidhamu yangu ni ndogo pia simuheshimu na nimkome Kama chu.😂pi.

Kama biblia inavyotuasa kwamba Ishini nao kwa akili bhasi nikakausha sikujibu sms baada ya muda natumiwa sms, Sitaki kusikia chochote kutoka kwako done.😁😂😁😂

Baadae mshua kaniita home akaanza kunieleza kwa makini sana kisa cha kumnyima mkwe wake hela, Nilivyosikia kutoka kwa mshua na sms nilizotumiwa hata sikutaka kumpinga yoyote ila nikamjibu mshua aachane na upuuzi wao, Kama alikula hela za watu arudishe Kama alifanya matumizi apeleke risiti.

Shida inaanzia hapa, mshua anampenda mkwe wake maana Kuna siku nilienda nae usiku home so alihisi tunamahusiano na alichomfanyia kazini ni sahihi ila anahisi amemuumiza na ndio sababu ya kuniita ili kuniambia hayo ila kwangu Mimi nimeshaambiwa nisimuongeleshe namimi nikajibu SAWAAA KWA HERUFI KUBWA.

Katika hili nimejifunza kitu ndio maana nimekuja kushare nanyi, Naamini utajifunza kitu


Ila WAHA wajuaji sanaa😂😂😂
 
Wakuu heshima kwenu, Mwenyezi Mungu awatie nguvu katika yote mnayopitia zaidi neema yake ikawe juu yenu.

Jana yamenikuta kijana mwenzenu, Shemeji yenu mtarajiwa anafanya kazi ofisi moja na bamkwe wake ila hawajatambulishwa tuu.... Sasa katika mishe za maisha huyu mtarajiwa alifanya matumizi ya kiofisi bila utaratibu sasa wakafanya mpango pamoja na mwenzake waombe hela nyingine kupitia kwa
KWA HERUFI KUBWA UMEELEWAKA CC MGALILAYA MWENDA OMO
 
Back
Top Bottom