mchajikobe
JF-Expert Member
- Aug 14, 2009
- 2,678
- 1,279
Leo wakati natoka kwenye mihangaiko yangu,kama kawaida barabara za mjini zinauhusiano mzuri sana na foleni,wakati tupo kwenye foleni kuna gari kama latatu mbele yetu lilikuwa limezimika katikati ya barabara,aliyekuwa anaendesha gari hiyo ni binti mmoja mrembo,bila kuomba msaada alibaki ndani ya gari na kuanza kupiga simu,hata hivyo kulikuwa hamna usumbufu kwetu kwasababu hata hiyo foleni ilikuwa haisogei,mara wakatokea vijana wawili wakaja kuisukuma ile gari ili kuiweka pembezoni mwa barabara,yule dada hakutoa shukrani wala kuongea nao chochote,zaidi ya kuendelea kupiga simu tuu,wale vijana walipoondoka yule dada akashuka akiwa ametilia kimini cha hatari na kufungua boneti kisha kufunga bila kufanya chochote,akaingia tena ndani ya gari na kuendelea kupiga simu.Mara ikatokea AUDI nyeusi akashuka mwanaume mmoja mtanashati mkononi anagalon la mafuta la lita tano wakaweka yale mafuta kisha yule dada akaiwasha ile gari kama anataka kuondoka na yule jamaa ambaye alionekana kama ni mume au mpenzi wake akaondoka,lakini cha kushangaza nikwamba yule mwanamke alilizima gari nakuendeleaa kukaa pale pale,haukupita muda mrefu ikaja prado akashuka mwanaume mwingine huku akiwa amebeba galon kama yule wa mara ya kwanza,yule mwanamke akafanya vilevile,jamaa akaondoka mwanamke akazima gari na kuendelea kubaki hapo hapo,kitu ambacho kilinishangaza ni kwamba lilikuja Mercedes benzi na mbaba mmoja naye akashuka na galon ya mafuta akamuongezea kisha akampa yule mwanamke kitu mkononi bila shaka ni hela kisha jamaa akaondoka,na yule dada naye akaingia ndani ya gari na kuondoka,hii ni kitu iliyotokea jioni ya leo maeneo ya kinondoni karibu na Hugo Bar!!Sasa huyu mwanamke inaelekea muda wote aliokuwa anaongea na simu alikuwa anamdanganya mmoja mmoja kuwa ameishiwa mafuta mpaka mwisho ametoka na lita kumi na tano,duu wanawake wa mjini hawafai,na unaweza kukuta hapo alikuwa na appointment na mwanaume mwingine!!!!