FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,065
Rais Wa Ufilipino, Rodrigo Duterte amenukuliwa akisema kwamba 'hutumia bangi ili kukaa macho' katika mikutano ya kimataifa.
(Rais Rodrigo Duterte)
Rais Rodrigo Duterte, ambaye vita vyake dhidi ya madawa ya kulevya vimechukua maisha ya maelfu huko Ufilipino, alisababisha mshtuko na hasira baada ya kudai alivuta bangi ili kujizuia asilale, ingawa baadaye alidai kwamba maneno hayo yalikuwa ni utani tu.
Akizungumza katika sherehe katika Idara ya Mambo ya Nje, Duterte alidai kwamba wakati wa mkutano wa hivi karibuni wa Asean huko Singapore, alikosa mikutano kadhaa muhimu ili akalale.
Duterte alieleza kuwa mikutano ya muda mrefu ya kimataifa ambayo alipaswa kuhudhuria kama rais mara nyingi imemfanya asilale usiku kwa sababu ya kusoma muda mrefu na kujiandaa kwaajili ya mikutano hiyo.
"Lakini Kwa umri wangu, mimi sina wasiwasi sana kwa sababu huwa navuta bangi ili nibaki macho," aliuambia umati wa watu, ambao uliangua vicheko.
Akizungumza baadaye siku hiyo, Duterte, alitupilia mbali mashtaka yaliyosababishwa na maoni yake kuhusu bangi.
"Ulikuwa ni utani, bila shaka ulikuwa ni utani, lakini hakuna mtu anayeweza kunizuia kufanya nipendacho," akasema, akiongeza kuwa mtu yeyote ambaye aliichukua kauli ile kwa uzito alikuwa "mjinga".
Hata hivyo, utani huo haukuchukuliwa kiwepesi sana na watu wengi huko Ufilipino, nchi ambayo ukikutwa na 'marijuana' utatumikia kifungo cha muda mrefu gerezani.
Chanzo: The Guardian
==========
(In English)
Rodrigo Duterte said he ‘takes marijuana to stay awake’ at international summits.
President Rodrigo Duterte, whose war on drugs has taken the lives of thousands in the Philippines, caused outrage after he claimed he smoked marijuana to stay awake, though he later claimed the comment was just a joke.
Speaking at a ceremony at the Department of Foreign Affairs, Duterte addressed claims that during the recent Asean summit in Singapore he had missed several key meetings in order to take power naps.
Duterte described lengthy international meetings he had to attend as president as a “killing activity” and bemoaned that the reading and preparation often kept him up late into the night.
“But at my age, I am not really bothered because I take marijuana to stay awake,” he told the crowd, who laughed in response.
Speaking later in the day, Duterte, known for his brash style, brushed aside allegations he had caused offence with his marijuana comment.
“It was a joke, of course it was a joke, but nobody can stop me from just doing my style,” he said, adding that anybody who took it seriously was “stupid”.
However, the joke was not taken lightly by many in the Philippines where possession of marijuana carries a lengthy prison sentence.
Source: The Guardian