Duru za siasa: Ndani ya Bunge

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
15,626
32,047
UTANGULIZI

Ndugu wanajamvi

Kwanza, tumshukuru mdau aliyetufikia kwa maoni.

Mdau ameshauri kuwepo na uzi endelevu utakaoangaza shughuli za Bunge kila mara

Hili litasaidia sana katika kutenga hoja mbali mbali zinazohusu masuala ya jamii yetu

Tumeafiki na kuanzia sasa uzi huu utakuwa endelevu ukieleza kinachoendelea Bungeni

Uzi utajjadili kila kinachosemwa kwa umuhimu wake na yoyote ndani ya Bunge

Tutafuatilia majadiliano na kudadavua hoja za washiriki kwa ukamilifu wake.

Hoja zitaangaliwa kwa jicho la utaifa bila kuegemea , kuonea au kupendelea

Tupo katika jitihada za kuhamisha mabandiko mengine yaliyogusa shughuli za Bunge hili.

Lengo ni kuleta mtiririko mzuri wa majadiliano kuanzia uzinduzi wa bunge hadi sasa

Tunawaomba uvumilivu wakati tunaendelea kuweka mambo sawa

Tusemezane
 
Janaury 27, 2016


SERIKALI YA RAIS MAGUFULI
NIA IPO NA JE DHAMIRA IPO KWELI?


Nia ni matamanio ya kuona/kutaka au kufkiri kwa namna dhamira inavyomtuma mtu

Dhamira ni nguvu inayomsukuma mtu kutenda ili kufikia matarajio kama nia ilivyomtuma

Tunayoyaona awamu hii (kwa mtazamo wa baadhi ya watu) ya kupambana na rushwa/ufisadi. Kubana matumizi, kukusanya kodi pengine yana nia njema kwa Taifa

Swali la kujiuliza, je, dhamira ya kufikia nia ipo?

BUNGE

Miaka ya karibuni limechukua jukumu lake la asili la kusimamia serikali.
Awamu ya 4 ililazimika kubadili serikali na hata viongozi kutokana na shinikizo la Bunge.

Ingawa maazimio hayakufanyiwa kazi na serikali,Taifa limeona tatizo tulilo nalo na chanzo

Viongozi na waaathirika wa hatua za bunge hawapendi kuona Bunge likiwa na meno.

Wanataka bunge liwe 'sehemu ya serikali' badala ya kuwa chombo cha uwakilishi

Awamu ya 5 ingalikuwa na nia na dhamira isingekinzana na yanayotokea bungeni

Ili 'kushinda' vita ya ufisadi, ubadhirifu na uzembe ni lazima kufanya kazi kama timu moja

Mathalan, hakuna kinachofanyika wapinzani hawakuwahi kukizungumzia.

Wapinzani walisema bandari ni chanzo kikubwa cha mapato, CCM/wabunge walibeza.
Leo walichobeza ndicho wanachotekeleza kwa jitihada kubwa

Serikali ikifanya kazi na wapinzani, mafanikio ni ya Taifa na sifa ni za serikali

Upangaji wa kamati za wabunge unatia shaka juu ya dhamira ya Awamu ya 5.

Hakuna namna Spika na Naibu wake wanaweza kutengwa na uongozi wa serikali.

Wote kama Rais wamepitia CCM na utiifu wao kwanza ni kwa CCM kabla ya eneo jingine

Upatikaji wa Naibu Spika ulitia shaka ndani ya CCM yenyewe akitoka nje ya bunge na bila kutarajiwa. Aliteuliwa ubunge na Unaibu muda mfupi

Alikuwa mjumbe wa bodi ya Bandari ilivyovurunda

Kwanini alichomolewa serikalini na kupewa unaibu? Dhamira inaanza kuingia mashaka

Muhimu ni la jinsi Spika alivyopanga kamati za bunge, hapa dhamira ya shaka inapojitokeza

Tuendelee sehemu inayofuata
 
January 27, 2016

SPIKA WA BUNGE NA KAMATI

Tumeeleza nia na dhamira, tunaona dhamira ya awamu ya 5 inavyotia shaka kuliko tumaini

Mh Spika akihutubia bunge aliahidi kasi ya hapakazi kwa maana mhimili wa bunge kumsaidia Mh Rais kufikia malengo yake.

Uundaji wa kamati za bunge ni kazi ya Spika na sehemu mhimu ya shughuli za Bunge
Tulitarajia uundwaji uweke masilahi ya nchi mbele badala ya uchama.

Hali ni tofauti ,kinachoonekana ni Bunge kupoteza nguvu zake.

Kamati 2 ambazo zinazongozwa na wapinzani hazina wenye viti baada ya wapinzani kususa
Kuna point muhimu kwa wapinzani. Kamati wanazotakiwa kuongoza zimejaa CCM

Maana yake ni kumnyima mwenyekiti uwezo kwasababu ya majority.

Wabunge wa CCM wakipewa maagizo na chama watamkwamisha mwenyekiti kwa njia tatu.
(1) Kumzunguka katika hatua nyeti
(2) Kutokubaliana naye
(3) Kupiga kura ya wingi ukiwa wao. Kuna maana gani wapinzani kuongoza kamati hizo?

Kwanini jambo hili limetokea? Kuna dhamira ya kupambana na maovu kweli!

Pili, wabunge wa upinzani wamejazwa kamati moja ya jamii pengine kwa makusudi kabisa.

Ni kujenga hoja hata wapinzani ni wengi kamati fulani bila kueleza uzito wa kamati hizo

Tatu, kamati zilizopo baadhi zinaongozwa na majina yaliyochafuka katika Taifa hili

Nne, wabunge wanaoonekana moto wote wa upinzani na CCM wamewekwa kando kiaina

Ipo hoja kamati zote zina hadhi sawa.
Ni kweli zina hadhi sawa kama kamati lakini hazina nguvu sawa

Ni sawa na kusema mawaziri wote wana hadhi sawa, ukweli ni kuwa waziri wa fedha, mambo ya nje au Ulinzi ni waandamizi miongoni mwa mawaziri.

Kunajengeka hisia ni jitihada za kudhibiti bunge kwa serikali ya awamu ya tano

Hivi kwanini bunge linaloongozwa na CCM yenye serikali linafanya jitihada za kuunda kamati si za kumsaidia Rais kutumbua majipu, bali kuficha majipu yasioonekane?

Ukiyaangalia yote na tamthilia inayoendelea, tunapaswa kujiuliza, nia ipo , dhamira ipo?

Iko wapi dhamira ya kupambana na maovu, ikiwa kuna jitihada za kuficha maovu?

Iko wapi dhamira ya kupambana na maovu kwa njama za kuwadumuza wapiganaji?

Ipo wapi dhamira ya kupambana na maovu ikiwa bunge linaelekea kukosa meno ?

Jitihada za kudhibiti bunge ni jitihada za kuficha uovu, mapambano juu ya kapeti chafu!!

Nia ya kupambana na maovu haikamiliki kama hakuna dhamira.

Tunachokiona ni kukosekana kwa dhamira ya dhati

Na kwavile dhamira haipo, watu watabaki wakishangilia.

Mwisho wa siku ni anguko letu sote

Tusemezane
 
January 28, 2016

VYOMBO VYA UMMA VINAPOTUMIKA KAMA MALI BINAFSI

WANANCHI WANAISOMA NAMBA, WARUDISHWA ENZI ZA MZALENDO/UHURU


Vurugu bungeni kufuatia tamko la waziri wa habari limetawala habari katika jamii

Tamko ni la kuzia kuonyeshwa kwa bunge 'live' na TV ya Taifa, hadi marudio ya usiku

Hili si tamko jipya, Bunge lililopita ilisemwa 'live' inadhalilisha bunge.

Kwanza, kutoa 'monopoly' kwa TBC kitakachorusha matangazo ili kuzuia 'dhalili'
Hii ilikusudia kuiwezesha TBC kufanya ipendavyo katika kutoa habari.

Kauli ya Nape si jambo geni, kilichoonekana kigeni ni jinsi alivyobadili sababu

Katika kutapatapa Waziri ametoa sababu zisizo weza kutetewa na kuukasirisha umma.

TBC : Ni chombo cha umma kinachoendeshwa na ruzuku. Ili kukiwezesha ,chombo hicho kinapewa upendeleo maalumu (Monoply) jambo lililowahi kulalamikiwa na wamiliki binafsi

Aliyekuwa mkurugenzi wa TBC bwana T.Mhando, alibadili sura na mtazamo wa chombo hicho. Alianzisha jitihada za kujiendesha chenyewe kama vingine katika ushindani wa habari. Yaliyomkuta Tido tunayajua, alitumikia umma badala ya CCM, akawekwa kando

TBC ina matatizo ya kukosa ubunifu na kutumika kama chombo cha propaganda

Pamoja na hayo waziri hatambui katiba inatoa uhuru wa kutoa na kupokea habari.
Kufinyanga habari ni kuunyima umma haki ya kikatiba ya kufatilia majadiliano ya bunge

Tendo hilo ni matumizi yasiyo mazuri (power abuse) hata kama kisheria uhalali upo

Kwamba, mtu/kikundi kidogo cha watu kinadhibiti matumizi ya walipa kodi bila kujali athari/faida kwa Taifa.

TBC si chombo cha CCM kama baadhi wanavyoelewa, ni cha umma


Inaendelea....
 
(Sehemu ya II)

HOJA YA NAPE NA TBC :
Kwamba TBC inatumia bilioni 4 kutangaza bunge haina mashiko.

Kubana matumizi hakulengi kupunguza huduma za lazima kwa jamii.

Bilioni 4 ni pesa za mfanyabiashara mmoja tu aliyekwepa kodi.

Kiasi hicho hakiwezi kuwa mzigo kwa Taifa. Austerity measures inatumiwa kama kisingizio

Mh Nape anasema kupunguza muda ni kuondoa matangazo ya shughuli za kawaida za bunge.Mh hatambui muda huo ungetumika katika matangazo ya biashara! Anajua hilo?

Mh pengine hafahamu muda wa shughuli za bunge ungetumika kufafanua miswaada, majadiliano, kuchambua hoja kama sehemu ya elimu kwa umma.

Kutangaza live si kuonyesha picha, kuna mengi nyuma yake yenye manufaa kwa taifa
Mh aelewe TBC hailazimishwi kutangaza . Ina wajibu kwa kuendeshwa kwa kodi za nchi

Endapo bilioni 4 ni nyingi, TBC iondoe uhodhi (monopoly), kuachia wenye uwezo
Hoja za waziri Nnauye hazina mashiko, hazisimami zenyewe na zinatia shaka #Hapa kazi

NINI KINAFICHWA?

CCM na Serikali ni waathirika wa vyombo vya habari.
Hoja zilizoibuliwa na waandishi wa habari ni chanzo cha umma kutambua na kuichukia CCM

CCM hawana namna isipokuwa kukabiliana na waandishi na kuhodhi habari.Kinachokusudiwa ni TBC kuchuja habari kwa kiwango ambacho CCM ingependelea

Matangazo ya kurekodi ni ya kuondoa sehemu '' chafu'' na kuwalisha wananchi habari zao
Dhamira ya CCM na serikali yake ni kuvinyamazisha vyombo vya umma kuhusu uovu

Tumesema, nia ya serikali ni kupambana na maouvu ipo, Dhamira ipo?

Serikali haiwezi kupambana na uovu bila kushirikisha sekta ya habari.
Wanapofunga midomo ya habari ni kujitenga na washiriki wa mapambano ya uovu

Awamu ya 5 inatengeneza mazingira ya kushindwa. Kuchukua haki za wananchi milioni 45 ili kulinda kundi dogo liendelee na maovu nyuma ya ''Camera'' ni dalili za awali za kufeli.

Kuwanyima wananchi uhuru wa kikatiba kuudhalilisha umma. CCM hawapaswi kulaumiwa. Wananchi wajilaumu. Waliondoa jicho kwenye hoja za msingi na kuimba #Hapakazi

Tusemezane
 
January 30,2016

SERIKALI NA TBC (Bungeni)

Mosi, si kazi ya serikali kupangia watu muda wa kuangalia habari.

Pili, kama lengo ni kupunguza gharama, TBC ifunge matangazo ya mchana wakati wa kazi na kujipunguzia gharama pamoja vituo vinavyotangaza TBC kupitia ving'amuzi

Tatu , kauli ya viongozi wa serikali ni ujumbe kwa wafanyabiashara, taasisi na mashirika yanayotumia TBC kuwa matangazo yao hayaangaiwi wakati wa mchana. Hili linaiumiza TBC

Serikali inasema watu hawaangalii TV ya TBC mchana. Hili litawakosesha TBC mapato ya matangazo. Hakuna mtu anayetangaza wakati 'rating' ya watazamaji haipo

Serikali ilishatoa kauli ya kulazimisha vituo binafsi vitangaze taarifa ya habari ya TBC wakati mmoja. Kauli ilipingwa na wadau na watu mbali mbali kwasababu nyingi

Kwamba, TBC yenye kila fursa bado inataka kutumia fursa za vituo vingine kwa lazima
Hapa kulikuwa na ujumbe mmoja, kwamba hata 'prime time' wananchi hawaangalii TBC

Kwa mtazamo binafsi, wananchi kutoangalia habari ni udhaifu wa kituo kutoa habari zenye mvuto, bila upendeleo(biased) na za kuaminika. Hapa ndipo viongozi wangejiuliza kuliko?

UDHIBITI WA HABARI

Zama hizi za teknolijia udhibiti wa habari ni jambo gumu sana.
Tumeshudhudia vijana wadogo wakileta matangazo kwa njia tofauti za internet

Kudhibiti habari kunawaelekeza wananchi vituo vingine na hata vya nje.

Ni jambo baya, wananchi wanapokosa imani na vyombo vya serikali yao

TBC ina matatizo ya kitaaluma na hapo ndipo pa kuanzia.
Tatizo si 'live or recorded news' ni uchujaji wa habari unapoteza na kupotosha habari

Hasira za wananchi ni ukweli kuwa TBC ni chombo cha umma wanacholipia kodi.

Serikali inayotaka kupambana na maouvu inapodhibiti watoa habari inasikitisha na kufikirish

Tusemezane
 
May 10, 2016

SPIKA WA BUNGE LA JMT ATETEA TAASISI YAKE

UTETEZI WA RUSHWA NI 'KUHALALISHA' RUSHWA

Spika amenukuliwa na gazeti moja akisema wabunge kuchukua rushwa ni kutokana na pressure wanayoapata majimboni kuchangia shughuli za misiba sherehe , madawati n.k.

Amesema, masilahi madogo ya wabunge yanachangia hali ya rushwa.

Kauli ya Spika imekuja baada ya 'mabadiliko ya kawaida' ya kamati za bunge.
Mabadiliko yaliyotokana na tuhuma za wabunge kula rushwa

Spika hakusema tatizo la rushwa, alichokifanya ni ' kuficha' tatizo kwa kauli za kisiasa

Haishangazi anawatetea wabunge wala rushwa kwa sababu zisizo na mashiko

Maisha ya Watanzania hayana tofauti na Wabunge. In fact wabunge ni sehemu ya jamii.
Sote tunachangia madarasa, misiba,sherehe n.k.

Ni mambo katika jamii yoyote yanayomgusa mtu yoyote si lazima awe mbunge

Mh Spika angejiuliza majukumu ya mbunge asingefikia hapo alipofika.

Kazi za mbunge ni uwakilishi, na kuunganisha nguvu za wananchi wa jimbo na taifa

Si kazi ya mbunge kutoa pesa za sherehe, madarasa, madawati kwa pesa zake.

Mbunge anaweza kuchangia kama Raia, hayo hayawezi kuwa pressure kwake.

Kwa upande mwingine, mbunge ana afadhali kwasababu ana mfuko wa jimbo ambao kazi zake ndizo hizo za ujenzi wa madarsa, madawati n.k. tofauti na mwananchi wa kawaida

Mbunge ana nafuu ana mshahara mkubwa ukilinganisha na wakazi wa jimbo lake.

Majimboni 10,000 ni hela nyingi,mbunge anapata 200,000 kukalia kiti cha kazi.
Pressure inatoka wapi?

Spika anaposema masilahi ya wabunge ni madogo, hapa anadhihaki umma.

Ni mfanyakazi gani wa jimbo anayelipwa mshahara na marupu rupu kama ya Mbunge?

Mh Spika angetambua kazi ya wabunge kuisimamia serikali ijenge madarasa, na kutoa madawati asingeweza kutoa utetezi wa pressure.

Si kazi ya wabunge kuchangia harusi au misiba, hayo si majukumu yao kikazi na wala yasifanywe kama shughuli rasmi za kibunge

Spika anazungumzia mikopo ya bunge kama tatizo lingine.
Wabunge wana haki ya kukopa na kulipa madeni yao.

Si jukumu la wananchi kubeba mzigo wa ujenzi wa nyumba binafsi ya mbunge, au kumsomesha mtoto wa mbunge nje ya nchi. Kukopa ni shughuli binafsi si ya kibunge

Si jukumu la wananchi kulipia magari, mwananchi anapolipa 45% ruzuku ni kumuonea.

Mbunge kama mfanyakazi mwingine anatakiwa kutumikia umma kwa nyeNzo zilizopo.

Kwanini anunue Prado na si Rav4 katika kutekeleza majukumu yake?

Haiingii akilini kila baada ya miaka 5 walipa kodi wanatoa ruzuku kwa mbunge yule yule kununua gari la kifahari. Wapo wananchi wana magari kwa miaka 15 au 20.

Na Spika ajiulize , je wabunge waliopoteza nafasi zao wananunua magari kila miaka 5?

Kauli ya Spika inaonyesha ugumu wa kupambana na tatizo la rushwa.

Kwamba, rushwa imeenea hadi katika taasisi zinazopaswa kupambana na rushwa

Ni jambo la mfumo, hila zinatumika kuhalalisha rushwa.

Kauli ya kuwatetea wabunge ni hatari, kwamba, rushwa inatetewa kimfumo sasa.

Bunge linakosa heshima linaposimama kujenga hoja dhaifu na mbovu

Kwamba rushwa katika bunge inatisha sana kuliko rushwa yenyewe

Hili la Spika linatisha na kusitisha

Tusemezane
 
May 13, 2016

SAKATA LA WAZIRI ALIYETUMBULIWA LAZAA MENGINE
UDHAIFU WA BUNGE WAONEKANA

Baada ya kutimuliwa waziri i, mengi yanajitokeza kuhusiana na sakata hilo

Baadhi ya wabunge wameeleza kumuona waziri akiwa amelewa kabla ya kuingia bungeni

Hata alipojibu swali la msingi, ni dhahiri hakuwa katika hali ya kawaida

Kilichojitokeza,uongozi wa bunge kuruhusu shughuli ziendelee kana kwamba lilikuwa jambo la kawaida, tena kiti kikiridhika na majibu

Mkurugenzi wa shughuli za uendeshaji wa bunge amesema 'hakuna kanuni zinazozungumzia kuhusu mbunge anayeingia bunge akiwa amelewa' Kauli hii inaonyesha udhaifu mkubwa

Kwanza, serikali ambayo ni mdau ndani ya bunge imejinusuru na kadhia hiyo kwa kumwajibisha waziri husika haraka kwa muda amabao bunge lilikuwa kimya

Pili, kauli ya mkurugenzi inaonyesha udhaifu mwingine.

Endapo kuna kanuni zinazoongoza mavazi bungeni, iweje kusiwe na kanuni zinazoongoza maadili yanayoambatana na mavazi,maadili kama haya ya ulevi?

Muonekano wa mtu kimavazi haukamiliki bila kuambatana na tabia ndani ya vazi husika

Leo kuna sheria na kanuni zinozoongoza matumizi ya lugha chafu, hakuna kanuni zinazoongoza maadili ya wabunge kuhusiana na mambo ya kimaadili kama ulevi n.k.

Tumeshuhudia mara kadhaa wabunge wakikemewa kwa kuzungumza lugha zisizo na stara. Hilo peke yake lilipaswa kuwa amsho 'wake up call' kwa bunge ya kuwa huenda matumizi ya lugha hizo yanaambatana na ulevi au sababu nyingine

Bunge lilipaswa, kwanza, kumzuia waziri husika asiendelee na shughuli ili kulinda hadhi ya chombo hicho cha kutunga sheria

Pili, bunge lilitakiwa iongoze ukemeaji wa waziri huyo kabla ya serikali haijachukua hatua kwavile tendo hilo limefanyika ndani ya mhimili huo na kuudhalilisha. Halikufanya hivyo

Utetezi laini na rahisi wa mkurugenzi wa bunge unaonyesha udhaifu wa chombo hicho

Kwamba, chombo hicho kinageuka kuwa sehemu ya Serikali badala ya mhimili pekee

Pengine ikitokea siku nyingine kuna mbunge aliye na kilevi tutasikia bunge likikemea.

Aidha zitatungwa kanuni kuhusiana na ulevi baada ya serikali kuonyesha kuchukizwa

Kwa msingi huo, ule msemo wa mhimili unayoijetegemea una maana yoyote?

Je, udhaifu huu wa bunge unalisaida taifa kufikia malengo yake kupitia chombo hicho?

Sakata la waziri mtumbuliwa linatuonyesha sehemu nyingine wengi walishinda kuiona ' udhaifu mkubwa wa bunge'

Tusemezane
 
Ukimaliza tutajadili, ila naona unajadili kauli za Wabunge wa upande mmoja. Usisahu na upande mwengine na huo unatambulika kama serikali kivuli..

Labda kama sio lengo la huzi huu.. Kama lengo Serikali na shughuli za bunge.. Bunge ni la mchanganyiko
 
May 29 2016
VIONGOZI WA WABUNGE WA CCM(CAUCUS) CHUKUENI HATUA

AIBU HII KWA TAIFA HADI LINI?

NDIO AIBU ILIYOFICHWA KWA 'BUNGE LIVE'

Tunakushukuru chinchilla coat kwa video hii inayoeleza mambo mawili

1. Kwamba, mpango wa waziri Nape kuzuia matangazo umeshindwa na unawarudi CCM

Kuficha kinachoendelea bungeni kumejenga curiosity kwa wananchi, na video au recorded sound zinapatikana mitaani kwa urahisi sana. Zuio lime backfire vibaya na kuwaumiza CCM

2.Tuliwaeleza CCM na viongozi bungeni kujenga nidhamu ya kuongea kwa utafiti na utaifa.Mnadhimu wa wabunge wa CCM aangalie caucus yake kama ipo sawa

Tulisema kwasababu video ya Mbunge Gekul kama inavyoonekana, inajenga hoja nzito.

Hata kama hatukubaliani na hoja, kitu kimoja tunakubaliana, Gekul anajenga hoja kama mbunge, anajua anaongelea nini na kwa nani na wakati gani.

Bila kujali maudhui, ukweli au upotoshaji, tumsifu kwa namna alivyojenga hoja

Bunge lipo kimya Gekul akieleza anachokiona. Si kuwa wananchi wanafarajika bali wanajengewa imani Dodoma wanaelewa matatizo yao na kuyajadili kwa lengo la utaifa.

Tunarudia tena ,Viongozi wa CCM Bungeni wafike mahali wafanye jambo la maana.

Kuwafunza wabunge maana ya bunge, uzungumzaji, uchangiaji, mantiki na Utaifa

Wasipofanya hivyo wakitegemea waziri Nape ataficha uozo kwa marufuku ya bunge live, ni kujidanganya. Kinachoendelea sasa kinaonekana mitaani.

Wala CCM wasije tafuta mchawi au kupiga ramli.

Tusemezane
 
June 22 2016

BUNGE LETU LINAKWENDA WAPI?

NAIBU SPIKA, LITAZAME TAIFA


Bunge linaendelea kwa historia mbaya. Ndilo bunge la vyama vingi bajeti imepitishwa na chama kimoja. Majadiliano ya bajeti za wizara hayakuwa tofuti pia

Mzozo ni baina ya naibu Spika na wapinzani wakimuona anaimnya sauti za wabunge

Pengine saikolojia inachangia katika hili. Wapinzani na baadhi ya CCM wanaona ujio wa naibu spika kama mbunge wa kuteuliwa na Rais aliyepachikwa na serikali
Hali ilikuwa mbaya anaposimamia sharia kwa kukosa uzoefu wa uongozi katika taasisi

Pamoja na mtazamo huo, ukweli unabaki kuwa lipo tatizo kubwa ndani ya bunge.

Wabunge 80 wa upinzani wanaposhindwa kuafikiana na naibu spika lipo tatizo la muhimu

Si kuwa wapinzani hawaafiki uongozi, hoja yao ni kuwa kiti kikiwa na naibu spika wanaona matatizo kwa upande wao. Hawana tatizo na wenyeviti wanaondesha vikao

Hatuwezi kudharau uchache wa wapinzani au umuhimu wao.

Mitazamo tofauti ni jambo lenye afya kwa mustakabali wa taifa.

Wapi mawazo mbadala yatapatikana ikiwa CCM wanafuata maagizo ya 'caucus' yao?

Wapinzani wana uwakilishi wa jamii, kudharau sehemu hiyo ni kujinyima fursa na kutengeneza matatizo makubwa mbele ya safari

Nchi ikiingia katika dharura, tunawezaje kuwa wamoja kama Taifa kwa haya yanayoendelea bungeni ?

Ni wapi na kwa vipi serikali itaungwa mkono na wananchi katika mivutano kama hii?

Haikuwahi kutokea, na mabunge yaliyopita yalionyesha nchi kukomaa katika demokrasia wananchi wakilitegemea bunge. Sivyo ilivyo

Marufuku za bunge kuonyeshwa ,ubabe, na haya ya naibu spika na wapinzani yanatoa picha moja kubwa, kwamba kama Taifa hatupo pamoja na upo ufa mkubwa.

Katika mazingira haya, adui asiyetutakia mema ana nafasi ya kutuvuruga, si wamoja tena

Ifike mahali sasa kuwe na masikilizano na wazee wa nchi hii waingilie kati.

Tutakosea kusema serikali ni mhimili unaojitegemea usioingilia mwingine wakati mzozo huu unachagizwa na teuzi

Kwa upande mwingine, hatuwezi kuwa na watu 80 au Zaidi wenye matatizo.

Tunaweza kuwa na mtu mmoja anayeleta matatizo.

Ni vema basi kila mmoja akajiangalia kama analitendea haki Taifa hili.

Kuzorota kwa shughuli za bunge ni kutolitendea haki Taifa

Ni kwa msingi, kwavile bunge linaweza kuendelea na shughuli kwa kutumia wenyeviti, tungetoa rai kwa naibu spika ajitazame ana sifa za kuendesha bunge vipande

Naibu Spika atalitendea haki Taifa akikaa pembeni ili kuwe na ushiriki wa wabunge.

Endapo yeye si tatizo wananchi tuna macho na wakati ukifika tutawasota vidole wahusika. Kwa sasa ni ngumu kusota vidole watu Zaidi ya 50

Kufukuza wabunge, kuendesha shughuli za nchi kwa mwendo wa 'mkutano mkuu wa CCM' na mambo mengine ni kulidhoofisha taifa kwa kiasi kikubwa sana

Tunarudi kutoa raia kuwa ni wakati sasa naibu Spika anayelalamikiwa akae pembeni ili shughuli ziendelee kukiwa na wabunge wote ndani ya bunge.

Naibu Spika kukaa pembeni kusimuondolee hadhi yake kama Mbunge na Spika.

Wala kusiingilie masilahi yake kama kiongozi. Ni kutoa nafasi kwa nchi kusonga mbele

Kukaa pembeni ni kurudisha Imani ya wananchi ndani ya chombo chao

Kutoafikiana na wawakilishi ni kupoteza Imani 'public trust' na hapa naibu spika hanayo

Tusemezane
 
Mwalimu, post: 16604001, member: 11689"]Mkuu Nguruvi3

Hakuna kitu kibaya kama kutawala nchi ukiwa hujiamini... unakuwa kiongozi uliejawa na woga na kurect vibaya kwa kila kitu kinachoonekana kuwa ni pinzani kwako. Unakuwa sensitive kupita kiasi kwa kila aina ya criticism inayokuja upande wako!

Na hicho ndicho kinachoendelea kwa utawala huu. Ndio maana zinafanyika kila jitihada kuzima sauti zozote zenye mwelekeo wa kuwapinga au kuwakosoa. Walianza kuzuia bunge kuoneshwa live, wamezuia mikutano ya vyama vya siasa, wabunge wa upinzani wanadhibitiwa vilivyo bungeni (sakata la naibu spika), sheria ya mtandao n.k.

Yote yanayoendelea sasa sio bahati mbaya hata kidogo....
 
June 22, 2016

NAIBU SPIKA, LINUSURU TAIFA

UMEKWAMISHA TAIFA, WANUSURU MILIONI 45

Tumeeleza tatizo linalotusibu kama Taifa kule bungeni

Tulitoa raia kuwa watu 50 hawawezi kuwa na tatizo kwa pamoja

Kwamba naibu spika akae pembeni, shughuli za Taifa ziendelee

Tunakumbusha naibu Spika(NS) , kutoafikiana na wabunge kuna maana moja, umma hauna imani naye. Wabunge wana public trust,kutomuafiki NS ni jamii inayozungumza

NS ana nafasi nyingi za kulitumikia Taifa.

Kukaa pembeni kusimuondolee haki yake kama NS au uhalali wa ubunge wa kuteuliwa.

NS anaweza kuendelea na shughuli zingine akiwa bungeni bila kuongoza vikao.

Shughuli kama za kusaidia serikali kukusanya pesa za madawati n.k.

NS atambue uteuzi wake ni imani aliyo nayo Rais kwake na dhamana kubwa

Kwamba , atakuwa miongoni mwa wabunge watakaomsaidia na nchi kwa ujumla

Dahama ya pili ni ya CCM,atakuwa NS na kiungo cha uongozi wa Taifa

Dhamana hizi ni kubwa, anapaswa ajitazame kama amekidhi haja.

Bunge kuvurugika kwa uwepo wake, kUnatia doa taasisi ya Urais iliyomteua na CCM

Taifa limegawanyika na kukwama, Sababu kubwa ni uwepo wa naibu Spika.

Wanasema ''sauti ya umma ni ya mungu' sauti ya umma imeshazungumza

Taifa linaweza kuingia katika udharura utakaohitaji shughuli za bunge na umoja wa kitaifa.

Naibu Spika hataweza kutufikisha tunapohitaji pengine kuwa chanzo cha mgawanyiko

Wananchi tunahitaji kusikia habari za matatizo na maendeleo yetu

Tumefika mahali sasa tunatoa sauti, NS atuache kama Taifa tusonge mbele.

Ni wakati akae pembeni na nyadhifa zake na mafao yake kamili

Muhimu atupe nafasi kama Taifa kusonga mbele.

Naibu Spika wa bunge, kaa pembeni ili Taifa likwamuke na kusonga mbele

Linusuru taifa

Tusemezane
 
NAIBU SPIKA: NCHI KWANZA
KAULI YAKE INASIKITISHA

Bunge la vyama vingi lilianza na wapinzani wachache sana.
Tunakumbuka walitoa hoja ya kufutwa kwa baadhi ya maneno katika viapo vyao

Pamoja na uchache wao usiozidi 20 busara ziliekeza kusikilizwa

Ndivyo ilivyoendelea katika mabunge yaliyofuata. Kupishana kwa kauli vilikuwepo.
Tofauti na sasa ni jinsi ya busara zilivyotumika kufikia muafaka.

Jana naibu spika amesikika akiwaambia wapinzani 'watoke haraka wasipoteze muda....'

Hata bila ya kauli hiyo wapinzani walikuwa wanatoka, na kauli hiyo haikuwa na ulazima kwani iilichochea hisia inatokana na 'kuungwa mkono'

Naibu Spika alikuwa mjumbe wa bunge la katiba. Alikuwa pia mjumbe wa bodi ya bandari ambayo taarifa ya ya gazeti moja, tume iliyoundwa imegundua madudu huko bandarini.

Naibu Spika aliteuliwa haraka kuwa mbunge na kisha kugombea nafasi husika

Hakuwahi kuwa mbunge au kiongozi kama ilivyokuwa kwa Spika Ndugai, Sitta, Makinda

Hili linaeleza uzoefu wake katika uongozi.

Hatudhani aliyemteua au Watanzania walitarajia aina hii ya uongozi.

Bunge ni baraza la wazi na mengi hutokea. Dawa ya matatizo si kuyakimbia au kuzuia yasizungumzwe, ni kutafuta muafaka kwa hekima na busara

Ingawa ''anafanya kazi nzuri'' matatizo yanyoweza kutokea kwa mgawanyiko ni makubwa.

Kwa mfano, si kila jambo linategemea 2/3 ya CCM. Yapo yanayotegemea wananchi.

Katika mparaganyiko uliopo, Taifa halina utengamano jambo baya kuliwaza

Ni wakati naibu Spika akae pembeni akibaki na nyadhifa zake halali na masilahi yake.

Ombi, tunaona kuna tatizo, na suluhu yake ni yeye kukaa pembeni kwanza

Inapofikia wabunge sasa hasalimianii, ni hali ya kutisha.

Naibu Spika ajipime nafasi na wajibu wake wa kulileta Taifa pamoja

Tunahitaji kusikia pande zote, na ili lengo lifikie naibu spika atoe nafasi si kwa bunge tu, kwa mteule wake na Taifa kwa ujumla kuweza kusikilizana, kujadiliana na kupanga

Uwepo wake unajenga ufa, na kwanini Taifa hili liishi katika hali iliyopo?

Naibu Spika akae pembeni, mufaka upo na utapatikana.

Kuwepo kwake kunazidisha hali ya sintofahamu.

Ni wakati sasa masilahi mapana ya umma yazingatiwe

Tusemezane
 
SPIKA MAKINDA NA BUSARA

Hatuwezi kusema Maspika waliopita walitenda kama ilivyopaswa.

Nao wakiwa wajumbe wa kamati kuu ya CCM na waliotokana na CCM walikuwa na mgongano wa masilahi uliopelekea kuegemea upande mmoja. Huu ni ukweli tunaopaswa kuishi nao

Suala la kutosikilizwa kwa wapinzani linachagiza hoja ya kuwa na Spika asiyetokana na chama chochote cha siasa ili kuleta uzani sawa na haki ndani ya Bunge

Hii ni hoja ambayo CCM hawapendi kuisikia wakijua kupitia Maspika 'mambo yao ' yananyoka

Hata hivyo kuna nyakati tupongeze jitihada na busara katika kusimamia maslahi ya Taifa.

Katika hili tunamkumbua Mama Makinda katika moja ya nyakati alizotumia busara za uongozi ambazo leo hatuzioni kabisa

Katika mjadala wa Escrow, Mama Makinda alitoa nafasi kwa wapinzani kujadili hoja hiyo.
Ilikuwa kati ya watu wawili au watu, Zitto, Mbowe, Mwanasheria Mkuu, Spika.

Ilifika mahali ambapo Wapinzani waliamua kutoka. Sauti ya Mama makinda ikasikika ikisema 'Jamani msitoke, rudini tukae na kujadiliana' Wapinzani walirudi na kuendelea na majadiliano

Pamoja na mapungufu yalkiyokuwepo, na kulalia upande mmoja, busara tu za kuwahimiza wapinzani warudi na kukaa ili kuyazungumza ilikuwa busara kubwa.

Tunapollinganisha kauli ya Mama Makinda 'rudini tujadiliane' na hii ya Naibu Spika 'Ondokeni haraka mnapoteza muda' tunaweza kujifunza kitu kuhusu uzoefu na busara

Pili, tunaweza kuona busara kwa tukio jingine.

Mbunge Nasari na Juma Nkamia waliopoleta hoja ya dharura bunge lijadili tatizo la wanafunzi wa UDOM, naibu spika alikataa ombi lao

Kilichofuata ni askari kuingia ukumbuni na kumtoa Mbunge Nasari mithili ya mwizi.

Ingaliwezakana kutumia muda saa moja kuijadili hoja ya dharura.
Hatutegemei hilo likiwa na masilahi ya nchi lingeongeza gharama za bunge kwa namna yote

Majuzi, tumemsikia mbunge wa Ulanga akilalamikakuvuliwa kofia yake na mbunge mwingine. Miongoni mwa hoja zake, ni ile ya Mkewe Mama Gloria 'kuingilia eneo lake'
Mbunge huyo alipewa muda mzuri sana wa kujadili mambo yake binafsi

Mwisho, Naibu Spika kasema atalitafutia suala hilo maoni Zaidi

Hapa unaweza kujiuliza, hivi suala la UDOM na la Mama Gloria yanawezaje kuwekwa katika uzani sawa? Wanafunzi 7,000 wapo matatani bunge halikupewa nafasi ya kujadili hatma zao za kurejea makwao kwa usalama, mbunge anavuliwa kofia hoja inasikilizwa! Busara zi wapi?

Tunapoangalia yote kwa upana, tunabaki kujiuliza tutaendelea hivi hadi lini?

Tusemezane
 
Alichokifanya Gekul katika kuchangia Hoja.. Bungeni, binafsi namsifu ndio Wabunge wanatakiwa kua hivyo, Bila kujali ni live au recorded.. Na video kwa kuiona imetolewa Studio za bunge sio, sasa wanaosema bunge litakua edited wanajisiakiaje huko.. Waliko.. Maana hiyo sio video ya kujirecod
 
Mtakumbuka tumehoji sana kuhusu Lugumi.
Wapo wanaotetea kwa nguvu zote kuwa hakukuwepo na tatizo.

Tulisema ficha ficha ya habari ilieleza mengi zaidi kuliko tuliyokuwa hatuyajui

Soma hapa Utetezi wa Polisi sakata la Lugumi huu hapa | Latest News, Sports, Business, Entertainment, Features, Columnist | IPPMEDIA
Halafu sikiliza hapa kutoka ndani ya Bunge Jeshi la Polisi lapewa siku 90 kuhakikisha mitambo ya LUGUMI inafanya kazi vituo vyote

Je, ''yaliyopita si ndwele tugange yaliyopo na yajayo''?

Vita dhidi ya ufisadi ina maana yoyote kwa wakati tulio nao?

Mahakama za mafisadi zimeanzishwa kwa sababu zipi?

Tutajadili
 
TAARIFA YA BUNGE

Sikiliza taarifa iliyowasilishwa kwa Spika na aliyoiwasilisha Bungeni

Halafu pitia habari hii Utetezi wa Polisi sakata la Lugumi huu hapa ambayo haijakanushwa na chombo chochote cha umma kama ilivyoletwa

Ukisoma na kusikiliza hayo mawaili, utaona nini kimefanyika na kwa hasara ya nani.

Katika bandiko hili tumesema kama lipo litakalo define uongozi wa awamu hii ni Lugumi
Ita define kwa namna mbaya au nzuri, ni wazi Lugumi imeshatatiza jitihada zote za kupambana na rushwa, maovu na ufisadi

Hapa ieleweke, tatizo si Lugumi, bali namna suala la Lililivyoshughulikiwa likiwa na mambo yanayoshangaza.

Kutupiana mpira na mwisho kamati , leo inasomwa taarifa bila kuele kamati imeona nini

Maswali ni mengi sana kuliko majibu, na Lugumi imesha define serikali hii

Tuangalie kwa undani
 
BUNGE LAAHIRISHWA

KAULI YA WAZIRI MKUU NA UTATA WAKE

SAKATA LA LUGUMI LAFIKA MWISHO!

MKutano wa bunge umeahirishwa kwa matukio mawili yanayozungumzwa kwa sasa

Kwanza ni kauli ya waziri mkuu kuhusu vyama vya siasa.

Kauli yake ina utata kwa maana mbili

Ni kweli wabunge wana kinga kwa yale wanayosema ndani ya bunge
Wanasiasa wanaokuwa ndani ya bunge wanalindwa na sharia za haki na kinga

Waziri mkuu alieleza kuwa nje ya hapo wanasiasa hawana kinga
Kwa maana, wanaposema katika mikutano nje ya bunge wanaweza kushtakiwa

Pamoja na ukweli huo, sharia zipo wazi kwa atakayezivunja.
Si kazi ya serikali kuzuia mikutano ya wanasiasa,bali kuchukua hatua kwa wanaokikuka

Hivyo waziri mkuu alijenga hoja kuwa kuzuia mikutano nje ilikuwa sahihi
Hilo si jukumu la serikali.

Jukumu ni kuwachukulia hatua wanasiasa wanaokiuka taratibu
Na vipo vyombo vya dola vya kusimamia hayo kama Polisi na msajili wa vyama

Kazi ya siasa hufanywa katika majukwaa ya nje. Ni haki ya kikatiba ndani ya sheria

Wananchi wana haki ya kikatiba kushiriki shughuli za kisiasa nje ya Bunge
Kauli imechukuliwa kama tangazo la kuzuia wananchi wasishiriki shughuli za kisiasa.

Wakati tunakubali kauli ilikuwa katika muktadha wa ufafanuzi na sahihi, hoja iliyojengwa juu ya uetetezi wa 'kuzuia mikutano ya kisiasa' na kukamata wanasiasa kwa hoja ya mikutano nje ya bunge ni kinyume na taratibu za demokrasia na katiba.

Uhuru wa kutoa mawazo na kushiriki shughuli za kisiasa ni wa kikatiba na kazi za siasa hufanywa ndani na nje ya bunge kwa wakati wowote ikiwa ndani ya sheria za nchi

Waziri mkuu 'anajifunga' hivi yeye au mawaziri wake watawezaje kwenda kukukutana na wananchi ikiwa tayari wameshajiwekea uzio wa kuzungumza bungeni tu!

Lakini pia WM aanatambua wanasiasa kazi yao ni kukutana na wateja wao 'wananchi'

Anachosema ni sawa na kuwaambia wafanyabishara kazi yao ni sokoni tu, si nje ya soko

WM atakapokuwa katika mikutano, anaweza kuulizwa, kinga ya kuongea nje ya bunge ameipata kwa sheria gani ikiwa yeye ni kiongozi ambaye ni mbunge pia kama wengine?


Hoja ya pili ni kuhusu taarifa ya Bunge

Inaendelea..
 
Suala la pili ilikuwa taarifa ya Naibu Spika (NS)Kuhusiana na sakata la Lugumi

NS alitoa taarifa bungeni kufuatana na vifungu vinavyomruhusu kufanya hivyo

Taarifa imeacha maswali na ukakasi, na imeiweka serikali katika wakati mgumu.

Taarifa imepokelewa kwa hisia tofauti kuanzia bungeni na katika makundi ya jamii

Kamati ya bunge iliundwa kufuatia taarifa za mkaguzi mkuu wa serikali (CAG) iliyoonyesha shaka kuhusiana na kazi iliyotarajiwa kufanywa.

Moja ya mashaka ni kufungwa vifaa katika vituo vichache tofauti na ilivyokusudiwa

Ili kuondoa mashaka, kamati ya Bunge ilundwa kufuatilia suala hilo ili kupata ukweli.

Kamati ilundwa baada ya sintofahamu juu ya mkataba halisi na kwanini ilitokea hivyo.

Hivyo,ilikuwa haki ya Bunge kupata taarifa rasmi kwa ukamilifu ikijibu hoja

Kwa mujibu wa NS taarifa ya kamati inaonyesha kazi ya kufunga vifaa haikukamilika.

Na hivyo basi Bunge limeazimia kuitaka serikali ikamlishe kazi hiyo katika miezi 3

Makataba wa kazi ulifanyika katika bajeti ya 2012/2013-gazeti la Nipashe 22 April 2016

Na kwamba mkandarasi alishapewa 99% ya malipo ya kazi

Kutokana na hayo , maswali mengi yanazuka na ambayo yamezungumzwa katika jamii

1. Je, makataba uliiingiwaje? Mkandarasi alipatikana kwa utaratibu gani?

2. Iweje Mkandarasi awe amekamilishiwa malipo endapo kazi ilikuwa haijamalizika?

3. Shaka aliyoonyesha CAG ilihusu nini? kumalizika kazi au matatizo ya mradi mzima?

4. Kwanini taarifa zinakinzana katia ya vyombo husika? Polisi, CAG na kamati ya Bunge?

5. Nani alipaswa kusimamia kazi imalizike na kwanini hakuchukuliwa hatua?

6. Iweje kazi iliyoshindikana miaka 3 imalizwe katika miezi 3?
Nani anajukumu hilo na kwanini alishindwa hapo awali katika miezi Zaidi ya 36?

7. Pesa za kukamilisha kazi hiyo zinatoka funga gani?
Ikiwa ni za kampuni husika, kwanini walilipwa kabla ya kukamilisha kazi?

Nani waliidhinisha malipo hayo? Na ilikuwa uzembe au kuna harufu ya mchezo mbaya?

Haya maswali pengine yangepata majibu kama taarifa ingewasilishwa na kamati.

Uzoefu unaonyesha Richmond ilikuwa katika hali tunayoiona.
Je, suala hili limefikia mwisho au ndio mwanzo kama ilivyokuwa Richmond

Kwanini suala hilo limefikishwa siku na saa ya mwisho ya mkutano wa bunge bila kutoa nafasi kwa wabunge kutoa hoja za kuridhia au kukataa taarifa?

Katika mazingira ya kawaida, huenda suala limefikia mwisho.
Hata hivyo maswali vichwani mwa wanajamii hayaonyeshi kama ndio utakuwa mwisho.

Ni suala litakaloendelea kuitesa serikali hasa katika vita dhidi ya rushwa.

Kukosekana uwazi kunatia shaka kwa dhamira ya kupambana na maovu.

Kwa hili serikali imekosa fursa 'missed opportunity'
Imejiweka katika mazingira magumu machoni mwa jamii.

Vita ya uovu inapiganwa na wananchi na kwa ujumla wake si kwa mashaka

Kwanini serikali ime 'miss opportunity' ? Tutafafanua
 
Back
Top Bottom