Duru za siasa
Tukianza na CCM tumeiona ikiyumba ama kuelekea kukosa ubunifu tumeona mkutano wake wa hivi karibuni kwenye viwanja vya Jangwani umeacha somo kwa wale wapendao kujifunza.
Kuna CCM tatu ndani ya chama kimoja, CCM inapaswa kurudisha uhai wa chama ili watu waione CCM iliyo hai na pia waone faida ya CCM kwenye maisha yao, watu wanataka wasikie CCM inasema nini badala ya watu wanasema nini, kwenye mkutano wa pale Jangwani CCM haikuwa moja na pia CCM haikusema chochote badala yake watu binafsi ndio waliosema kwa kutumia nyadhifa zao na na nafasi zao.
Ninapozungumzia kauli ya cha nina maana pana, kwanza kuna mengi ambayo CCM inapaswa kuyatolea kauli ama kuyatolea ufafanuzi ili watu wasikie chama kimesema nini. Kitendo cha kuwaalika Wawaziri ili waje wawaeleze Wananchi mazuri yanayofanywa na Serikali ya CCM ni kujikanyaga, chama ndicho kinapaswa kuitetea serikali na sio serikali kujitetea mbele ya Wananchi ili kukisafisha ama kukinufaisha chama tawala.
Mawaziri wanalo jukwaa lao ambalo wananchi huwasubiri na kuwasikiliza ni bungeni wakati wa kuwasilisha makadirio ya matumizi ya wizara zao.Tutaendelea na Duru za siasa.
Ritz, Suala la kuyumba kwa CCM ni dhairi kabisa.
Ona jinsi ambavyo Nape alivyosusiwa kampeni. Amebaki anazunguka mikoani kueneza uhai wa chama peke yake.
Wakati anafanya hayo wazee wa chama akina Makamba wanasubiri kumsulubu katika vikao kama kilichokwisha cha NEC
Uenezi wa chama siyo one man show ni kazi ya pamoja (team work). Katika kufanya hivyo Nape anakosa timu ya mkakati na matokeo yake ni ima kutoa matusi au kujibu tuhuma na wala si kueleza sera za chama.
Chama tawala sasa hakiongozi bali kinaongozwa kwasababu CDM wakitoa hoja CCM haielezi kwa ufaha hoja husika bali kujibu hoja. CCM imebaki na sera za kueneza udini na ukabila na wala siyo zile sera za chama au ilani ya uchaguzi
Kuna kundi linalosubiri chama kidhoofike ili litumie mbinu zao kukirudishia uhai. Hili ndilo lililowatuma wazee wamkaange Nape kuwa anaua chama na Mkama si kiongozi mzuri. Kundi hili linaloundwa na mafisadi linasubiri wakati muafaka na nakuhakikishia kuanzia mwakani utaliona likiibuka kwa kasi. Sasa hivi linafanya kazi ya kuhamasisha na kuchochea chuki
dhidi ya wenzao ndani ya chama linatafuta kuungwa mkono na hasa taasisi za kidini.
Wale uliowaona Jangwani si kwamba walikuwa wanaeneza chama, ni kundi la pili linalojitutumua kukipa uhai chama kwa kutambua kuwa Watanzania wengi wamechoshwa na ulaghai na kwamba kwa kujipambanua kuwa linapigania haki za wanyonge katika misingi ya chama lina nafasi ya kutoa mgombea.
Kwa vile lengo ni mgombea ndiyo maana hakuna aliyekuwa 'anahubiri' sera za chama bali kila mmoja anajitafutia ka nafasi.
Na wala kundi hili haliwezi kuitetea serikali kwakuwa serikali yenyewe ni mzigo tosha na kujinasibisha nayo ni kujipalia makaa.
Pia tuelewe kuwa hakuna kundi linaloweza kukitetea chama kwasababu chama kimekosa uongozi.
Hivi fisadi anawezaje kusimama na kukitetea chama au serikali kwa hasira zilizopo za wananchi?
Hivi wapambanaji wa ufisadi wanawezaje kukitetea chama au serikali ili hali wameshindwa kuwatia nidhamu mafisadi?
Mfano mzuri wa jinsi wanachama wasivyoweza kukitetea chama, ni wa waziri mwanadamizi Membe anayenyemelea nafasi ya kuongoza nchi. Membe anajinasibu kuwa mtetezi wa rasilimali za nchi kama tulivyoona akishupalia suala la Rada.
Ni membe huyo huyo hawezi kutaja hata mhusika mmoja na kila akiulizwa anasema yeye hahusiki.
Sasa kama yeye hahusiki kujua nani mwizi anawezaje kuitetea serikali yake yenye mkono ndani ya kashafa ya Rada?
Hivi Membe anawezaje kusimama na kutetea sera za chama za kupinga ubadhirifu na ufisadi tukijua kuwa hawezi kumtaja achilia mbali kuchukua hatua dhidi ya wahusika!
Hapa ni wazi Membe amepoteza 'moral authority' ya kutetea serikali yake au kukemea ufisadi.
Sasa katika mkanganyiko wa wanamna hiyo Membe anawezaje kusimama na kurudisha uhai wa chama.
Kwa ufupi ni kuwa CCM imetekwa nyara na wahuni wachache na uongozi uliopo una ombwe kubwa la kiuongozi, ni uongozi dhaifu ambao sidhani kama unaweza kurudisha uhai wa chama tena.
Vyovyote vile wavyo muda wa CCM kutawala iwe bungeni au serikalini hauna ashirio la mwisho mzuri.