Duru za siasa - Mgongano wa mawazo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Discussion in 'Great Thinkers' started by Nguruvi3, Aug 26, 2011.

 1. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #1
  Aug 26, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  DHANA YA 'DAMAGE CONTROL'

  Kwa mara ya mwisho tuligusia namna ambayo siku 14 zilipita bila uongozi wa Chadema kutoa ufafanuzi , maelezo au majibu sakata la AR.

  Siku 14 ni nyingi sana kuachia mada ijieleze na kujijibu yenyewe. Ndipo tulisema dhana ya damage control haikutumika kwa gharama kubwa kisiasa.

  Hili halikuwa tukio la kipekee kwa Chadema, vyama kama CUF, NCCR vimepita katika majaribu kama hayo na vimeumia sana.

  Kwa ukongwe wa kisiasa, CCM wameweza kufanya damage control ingawa kutokana na siasa za chuki na makundi kazi hiyo inakuwa ngumu. Mfano, waliunda kamati ya mzee ruksa kutafuta muafaka wa chuki baada ya mashambulizi yenye hasira kutoka pande zinazohasimiana.

  Ilifika mahali siri za chama na viongozi zinamwagwa hovyo na kukidhalilisha Chama, ndipo kamati ikaundwa kuepusha malumbano.

  CCM imekuwa ikijitenga haraka na watu au mtu wenye kashfa, ndiyo maana mara zote wanatoa matamko kama yale yasemayo chama si fisadi ila ufisadi ni wa watu binafsi, wakati mwingine kufikia hatua hata za kuwachachafya watuhumiwa ili kupata 'damage control' mapema kabisa.

  Damage control inatumika katika serikali, taasisi na mashirika katika ngazi zote za kitaifa hadi kimataifa. Inafanyika kwa njia nyingi.

  Kwa mfano Obama alipoandamwa na tuhuma za mchungaji 'Right' ilimchukua muda mrefu kujibu tuhuma kiasi kwamba kampeni yake iliyumba sana. Bahati nzuri Obama ni Orator mzuri aliugeuza uharibIfu kwa manufaa katika hotuba yake Pennyslavania.

  Hata hivyo kuzembea kujibu shutuma, tuhuma au kauli umekuwa ni udhaifu mkubwa sana wa kampeni za Obama na humgharimu.

  Tofauti na Obama, Hillary alizusha yake aliposema akiwa Bosnia alipokewa uwanja wa ndege risasi zikivuma angani.

  Ukweli ni kuwa alipokelewa na maua na ilionekana kuwa kama kashfa kubwa ya uongo. Hillary alikwenda kwenye vyombo vya habari na kutetea kauli zake na kuhudhuria vipindi 'talk show' ambapo aligeuza tuhuma kuwa mzaha akiwa na comedians na kupoteza nguvu.

  Wakati hayo yakiendelea watu wanaojulikana kama Political pundits walikuwa wanatafuta hoja mbadala itakayokuwa na nguvu.

  Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza bw.Godon Brown alinaswa na vipaza sauti kabla hajavivua vikimkariri akimwita mwanamke mmoja Bigots.

  Ilipotokea katika vyombo vya habari asubuhi akaenda nyumbani kwa yule mama kumtaka radhi. Alifahamu uharibifu utakaotokana na maelezo au malumbano yasiyoisha ni mkubwa sana kuliko kusema samahani.

  Tunakumbuka mwandishi aliyemwagiwa tindikali, baada ya minong'ono iliyohusishwa na habari za ufisadi, siku iliyofuata Rais aliagiza serikali igharamie matibabu je! hii ilifanyika ili kuua minong'ono kwani ni wakati huo shauri la marehemu Bilali lilikuwa moto.

  Mwandishi alipokuwa anakaribia kurudi alisema ataweka wazi waliohusika akifika Dar. Baada ya muda wakakamatwa vibakwa kwa kubambikiwa shitaka. Hapo shitaka likawa mahakamani na hakukuwa na uhalali wa kuliongelea.Baada ya miaka 3 nguvu yake ikapungua vibaka wakaachiliwa.

  Hii ilikuwa ni sehemu ya mkakati wa damage control kwasababu ni kipindi hicho EL alikuwa na Richmond na hili la mwandishi lingefunua mambo makubwa kama lingeachiwa kuongelewa hovyo.

  Katika taasisi au mashirika nayo hujikuta katika gharma kubwa ima za kuwalinda au kuwaweka sawa watumishi wao ili pamoja na mambo mengine wasijehusishwa na uharibifu wa heshima (reputation). Hakuna shirika litakalofurahi kusikia manager au CEO ameokotwa chakari mitaani, au CEO anahusishwa na biashara chafu kama za madawa au umalaya. Taasisi na mashirika huchukua hatua za awali kuzuia kama njia ya awali ili wasifikie hatua ya damage control ambayo si njema na ni ghali.

  Nimelitolea mfano hili kwasababu gharama zake zilikuwa kubwa kwa chama cha CUF kilichokuwa na wafuasi wengi wa ukanda wa pwani.

  CUF waliposhutumiwa kuwa chama cha Kidini (Kiislamu) badala ya kufanya damage control (hata kama haikuwa kosa lao) wao wakaacha kwanza jambo hilo likaaminishwa vichwani mwa watu kwa muda mrefu sana. Walipotakiwa kujibu walichofanya ni kuchochea uharibifu kwa kusema CCM nayo ina viongozi wengi wakristo, ni chama cha Kikirsto. Hawakuwa na political strategists, pundits, observers au analysts kwasababu chama kilijengwa kwa personality hasa ya maalimu Seif na si idara au wanachama.

  Kwa kukosa watu muhimu kama Pundits, Observers, commentators n.k katika idara za CUF, makosa yakaendelea kufanyika na kuharibu zaidi.

  Chama kikawa kinafanya mikutano siku ya Ijumaa baada ya swala! Hii ikashadidia hoja iliyokuwepo awali hata kama ilikuwa ni ya uongo. Uharibifu huo ukawa mkubwa sana na damage control haikuwezekana na kupelekea chama kubaki katika vitabu vya historia.

  Chadema, chama cha upinzania ni makini sana lakini bado hawajajifunza kutoka CUF au NCCR kwa undani. Nasema hivi kwasababu chama kimekuwa kama mtu au watu na si idara. Haiwezekani Dr Slaa awepo kila mahali kutoa kauli hata kwa mambo madogo.

  Ni mara chache kumsikia msemaji wa chama, au watu wanaolinda maslahi ya chama (pundits, strategists etc) wakitoa ufafanuzi au kauli. Matokeo yake siku zote watu husema Dr mbona hajasema au kasemaje! Hiki ni chama na idara zake ni lazima zifanye kazi kikamilifu.

  Kwani tatizo la Chadema ni ukosefu wa watu wenye sifa au kutokuwa tayari kuajiri wenye sifa au kutoona umuhimu tu!!!

  Chadema wapo Slow katika ku-seize opportunity hasa CCM wanapobofoa. Ni slow katika kujibu tuhuma, na ni slow katika ufuatiliaji.

  Inawezekana kuwa ni mkakati wao ndio maana wapo makini sana, lakini in politics timing is very important.

  Ndio maana nasema haiwezekani damage control ifanyike baada ya siku 14 halafu useme huo ni mkakati na sio mapungufu.

  Hitimisho:

  CCM wanaijua vema dhana ya damage control, timimg and who is to say what.

  Vyama vya upinzania bado dhana hii haieleweki. Hoja ya Nape haijibiwi na Katibu mkuu wa Chadema inajibiwa na 'counterpart wa Chadema'.

  Upinzani ujue ku react promptly with precisions na ikitokea kuna dalali li za uharibifu damage control ifanyike mapema sana kuepuka gharma zisizo za lazima kisiasa. Lakini pia wawe innovative si kila jambo wafanye kwa 'template ya CCM'.

  Ni wakati tusemezane ili kuviimarisha vyama vya siasa tusijerudi kule kule kwa NCCR au CUF.
  Hatuna muda wa kulelea vyama vipya kila msimu, tulee vilivyopo ili tuwe na demokrasi ya nguvu na kweli.
   
 2. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0


  Kuna Damage Control kwa sababu huwa kuna damage imefanyika. Na hususan damage imefanyika na nani katika mazingira gani. Halafu kuna njia tatu za damage control;

  NJIA YA KWANZA.

  Kama inahusu personality kujidamage kwa hiyo kudamage institution huwa wanachukua RESPONSIBILITY kuanzisha hiyo control wenyewe au taasisi zao. Mfano wa hitilafu kwenye magari ya Toyota, ili kulinda wajihi na hadhi ya Toyota yalikuwa recalled. Nakubali relevance ya mifano yako in context. Lakini hazikuwa technically managed kwa sababu ya maudhui potofu.

  NJIA YA PILI

  Kifupi kama nilivyosema hapo juu, kwa jamii zilizo komaa KUNA KUWAJIBIKA kwa mtu binafsi kuachia ngazi kuokoa taasisi. Kujiuzuru kwa Strauss wa IMF ili kutunza heshima ya IMF. Sina uhakika kama Mzee mwinyi alijiuzuru kwa utamaduni wa kuwajibika kwa sababu waathirika hawakupata cho chote ikawa imetoka.

  NJIA YA TATU

  Kulazimishwa mtu kuwajibika (KUWAJIBISHWA), Hapa inategemea muwajibishaji. Anaweza kuwa ni Mkuu wa Kaya au Taasisi. Mimi napenda umma ndio umwajibishe mtu.

  Baada ya hayo napenda kuchangia kidogo kuhusu vyanzo vya damage. Kwa mawazo yangu damage lazima itokee palipo na mgongano (Confrontation) au msuguano (Conflagration). Kwenye siasa zetu vyanzo vya damage ni siasa kwa itikadi, siasa za maji taka, maovu ya utendaji (ufisadi), maonezi kwa nguvu yo yote ile.

  Ni kweli kuna gharama kubwa kufanya damage control, ila kwenye taasisi yo yote gharama hizi huwa "liability" ambazo dawa yake ni kuwatema kwa njia yo yote wahusika kama taasisi yenyewe ni makini. Nina wasi wasi hapa nchini ni nadra kuna taasisi za aina hiyo.

  Sikubaliane na wewe kuhusu CDM, kwa sababu ulizozitoe mwenyewe. Hawawezi kuwa makini wakati huo huo wawe na upungufu ulioutaja. Kwenye suala unaloelekeza nani wahusika wa "damages"? Ni ndani au nje ya chama? Kwa bahati nzuri kwa sisi wana hesabu UMAKINI NI TIME FACTOR yaani kufanya maamuzi kwa wakati muafaka kama walivyofanya CDM. Je kulikuwa na damage kwa chama nachelea kusema hapakuwa na damage bali fursa iliyojitokeza yenyewe. Sijafanya utafiti lakini consensus ni kuwa CDM imejiimarisha na kujiongezea umaarufu. Kama ni damage kwa madiwani waasi na mawakala wao nakubali lakini haiwahusu CDM. Kwanza chanzo cha hali yenyewe ni msuguano wa kiitikadi. Kwa mantiki hiyo kila role player wa CDM anastahili merit kwa alichokifanya.

  Nakuomba jielekeze kwenye matokeo (result) ya yaliyotokea utagundua hakukuwa na haja ya kukimbilia kupapambana bila kujizatiti na facts. Kwa mimi siwasifu kwa sababu nadhani ndiyo hulka yao ya utekelezaji na uendeshaji wa uongozi na shughuli zao.

  Si kweli hawaijui kabisa dhana ya damage control bali wanatumia vibaya vyombo vya dola, hawatasimama hata siku moja bila kuegemea dola. CDM hawana dola lakini wanajitegemea kwenye kufanya maamuzi

  Sasa wewe ndiyo unataka CDM wawe 'template ya CCM'. Ninachokiona uelewa wa damage control unatofautiana kama vidole vya mkono. Si kwa vyama vya siasa bali hata wananchi wa kawaida. Mchango wangu ni kuwa ni vyema tuisadie nchi yetu iliyokuwa damaged left and right kufanya hii damage control. Kwenye siasa wapo akina Nape, Dr. Slaa and the likes nguvu yao ni sisi ambao tunakuwa damaged kwa kushindwa kuwawajibisha damagers. Naomba tusaidiane siyo kujifunza damage control bali kujenga utamaduni wa damage control kwenye maisha yetu ya kila siku.


   
 3. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #3
  Aug 26, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  well said
  Kamaipo itakuwa ni taasisi ya kimataifa.
  Yes, nimesema ni makini kwa kuangalia ujumla wa mitazamo, approach zao na maamuzi kwa mambo mengi.Baada ya hapo nimeonyesha mapungufu kwasababu ni vitu ambavyo kimoja haki nullify kingine.

  Kwenye suala ninalosema tayari kulikuwa na damage. Kwamba muafaka umefikiwa kinyemela, haukutangazwa na chama, haukukidhi haja ya maandamano. Hii tayari ilishasababisha damage katika credibility ya chama, ilisabababisha kupotea kwa morality katika political base na ilitumiwa na wapinzani(CCM) kama silaha ya kuharibu image ya Chadema. Kuna factor mbili zinazohusika, exterenal na internal.

  Katika hili suala la external factor hutuwezi kuilamu kwasababu ilikuwa inafanya kazi kama ilivyotarajiwa, kwamba kuhakikisha inavuruga Chadema.
  Muhimu ni internal factors (1) Madiwani (2) Chama kitaifa, hawa ndiyo wanahusika katika damage
  Damage ipo, na ni vema tukaiangalia kwa mapana. Muafaka ulitangazwa baada ya maandamano nchi nzima. Ni kipindi hicho waziri Wassira na Sophia walikuwa wanapita kwenye vyombo vya habari kuhubiri 'ghasia' zinazotaka kuletwa na Chadema ingawa ulikuwa uongo mkubwa. Tatizo ulijirudia mara nyingi sana.

  Muafaka ulipotangazwa CCM wakaunganisha kuwa Chadema walikuwa wanagombea kitu bila sababu na wamesababisha vifo na ulemavu.
  Katika nchi kama Tanzania watu wangapi wanaweza kuweka hali hiyo katika mizania ili kujua ukweli na uongo?

  Damage ya pili, Ilionekana wazi kuwa lengo la maandamano lilikuwa kupata umeya au unaibu na siyo kusimamia haki ya uchaguzi.

  Tatu,malumbano yaliyotokea kati ya madiwani, mbunge na viongozi wa taifa yameacha kovu, kupunguza umoja kwa kiasi fulani na kujenga hofu katika political base kuhusu uimara wa chama kwenye masuala nyeti na ya dharura.

  Nne, in long term watu watajiuliza maswali kabla ya kuunga mkono na swali litakuwa 'isije ikawa movement hii ni kama ya Arusha'!! Hilo si swali zuri kisiasa.

  Kuhusu timing, sikubaliani na wewe kuwa ilikuwa nzuri. Kilichofanyika ni pressure kutoka kwenye base na kejeli kutoka CCM.Je ilileta matokeo mazuri, yes! ilipangwa hivyo, No! ililkuwa ni coincidence ya action na timing, yes.Ina nafasi ya kujirudia, questionable!

  Ninachosema hapa ni kuwa vyama vya upinzani vinaiga hata miundo kutoka CCM.Ni lazima viwe na model zao. Kuunda tume ni template ya CCM na mimi sikuona mantiki ya tume endapo mwenyekiti wa taifa alijua nini kinaendelea. Kwa kupunguza pressure kama ilivyozoeleka CCM kwa kuunda tume hata kuchunguza kuwa bendera yao ni ya kijani, Chadema walifanya hivyo. Mfano, kwanini wasimwite mwenyekiti wa Wilaya, Mkoa, Mbunge na Wabunge AR kupata ukweli!!
  Na ndipo umuhimu wa kuimarisha wananchi kupitia vyama vyao unapohitajika.

  Nakiangalia Chadema kama chama cha upinzani na ambacho kinataraji kuchukua dola kwa wakati au ikibidi. Kuna uhuhimu wa Chadema kuwa na mambo kama (1) kuwa tayari kupambana na CCM kisiasa (2)Kujenga imani kwa wananchi kuwa kipo tayari kuendesha dola (3)Kuonyesha kuwa kitafanya mambo kwa njia tofauti lakini bora n.k
  Ndipo linapokuja hili ; Utayari wa kuona matatizo na kuyashughulikia, haraka kwa wakati na njia sahihi
   
 4. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Hapo kidogo ningependa ni tofautiane na wewe!
  Kwa muda sasa toka baada ya uhuru wetu, kumekuwa na hii dhana ya kuwajenga watz katika kuamini katika vyama vya siasa kila linapokuja suala la siasa!

  Kuna haja ya kuwajengea watz uwezo wa kimtazamo katika kujitambua zaidi wao kama wao,
  Ni lazima tujenge kada nje ya hizi za kisiasa, kwa mfano za kijamii ambazo zitakuwa na jukumu lakujenga UMMA wenye nguvu..

  Automatically UMMA wenye nguvu utazaa vyama vya siasa vyenye nguvu na vyenye kuleta tija tarajiwa!
  Ukiangalia njia ambazo tunapita kama taifa, utagundua kuwa kuna nafasi ya chama chenye nguvu cha siasa (CHADEMA)... hata kikishika dola kitakuwa kama vyama vingine vilivyoleta uhuru Afrika- kwamba kinapokelewa kama mwokozi na kinapata ushindi wa kutosha na anayekipinga anaonekana msaliti.... enzi za "chama kushika hatamu".... hii hutokea kwa UMMA usioamka na unaotegemea mustakabali wake kwa chama cha siasa. Hii si sahihi!

  Mjadala nadhani ni lazima tuwe na taasisi za UMMA ie vyama vya kijamii, vyama vya kumlinda mlaji, vyombo vya habari na hii mitandao ya kijamii kama JAMIIFORUMS na Blog makini na vingine,

  Hivi vyote vikifanya kwa ukaribu hakika tutakuwa UMMA wenye nguvu, UMMA wenye kuweza kujenga mustakabali wake wenyewe bila kutegemea vyama fulani kwamba hivyo vyama vitatokana na msimamo wa huo UMMA...!

  Hivyo naomba nikubaliane na "MimiBaba", kuwa tunahitaji kujenga WATU imara sababu huo ndio msingi wa mamlaka zote na vyama vyote..

  Na hamna damage inayoumiza zaidi historia kama ile inayoathiri UMMA kwa ujumla wake.

  Tujifunze Libya!
   
 5. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mimi nilikuwa ndiyo namaliza Primary School mwaka tulipopata Madaraka, na wakati Jamhuri nilikuwa naanza middle school darasa la tano. Naeleza hivi kwa sababu ya ubora na umakini wa elimu kuwatayarisha fikra huru toka chini. Na nadhani kwa observation sisi wa mwaka 47 angalau kwa uwezo wa kifikira tuko tofauti. Sasa nini kilikwenda mrama na kwa sababu gani?

  Kwanza ni fikira potofu kuwa wakoloni ni wabaya kwa kila kitu pamoja na misingi na falsafa ya elimu yao. Nakiri labda kulikuwa na msisitizo mkubwa sana kutii mamlaka kiasi cha kusababisha woga fulani. Kinyume chake utii wa mamlaka haukuwa unazuia kutoa maoni mbadala.

  Na hapo ndiyo dhana ya ukoloni ilikuwa na nguvu kwa sababu ilikuwa na uwezo wa kumtambua mwenye NGUVU ya hoja (kitu ambacho kimenyeng'anywa toka kwa umma).

  Hoja yangu najaribu kuonyesha kasoro kubwa ya kwanza ya umma kunyang'anywa nyenzo za fikra kwenye mazingira yao. Kilichotokea darasa la nane au mfumo wa elimu ya msingi wa "kikoloni" ulikamilika kubadilishwa ilipofika 65/66.

  Pili pamoja na uchanga, miaka hiyo kulikuwa ni kilele cha ushindani wa kambi ya magharibi na mashiriki, nchi mpya huru zilikuwa limbukeni na uongozi wa serikali zao mpya. Yapo mengi lakini kikubwa sana kulikuwa na kuzipindua nchi hizi kwa kupanua himaya za kambi hizi mbili.

  Kwa sababu hiyo viongozi ndani ya serikali changa mmoja mmoja walikuwa na mwelekeo uliojisalimisha kwa moja ya kambi (Kambona Vs Nyerere ndani ya TANU). Ndipo hapa kwetu kukazaliwa AZIMIO LA ARUSHA ili kuielekeza nchi mwelekeo mmoja. Mimi wakati huo nasoma sekondari lakini napiga mguu JKT kila baada ya likizo (kwa sababu nilikuwa yatima kiukweli) na serkali ilikuwa imechukua jukumu kutupa fursa mbali mbali hasa za elimu.

  Maana yake ni kuwa kwenye huu msafara wa Azimio la Arusha kulikuwa na Kenge (mfano BM) kwenye msafara wa Mamba. Matokeo yake kenge walitumika kimaslahi na kutekeleza falsafa mbili, wape Elimu duni hasa ya uraia na wanyime fursa za uchumi wa pamoja UWATAWALE kwa urahisi. Kwa hiyo makenge yakawa yanafikiri kwa niaba ya umma (Zidumu fikra za mwenyekiti) na kujinufaisha na raslimali za nchi (kwa ubinafisishaji holela).

  Ninachojaribu kusema ni kuwa Nyenzo hizi mbili elimu na uchumi zimenyang'anywa toka kwa umma. Kinachotakiwa kufanya ni kuwarudishia na kuwawezesha wawe "empowered" kupitia kubuni mfumo wa elimu unaowawezesha kifikra. Mfano uduni wa kifikra ni pale unapoona Profesa mzima anasema Zidumu Fikra za Mwenyekiti na kuacha taaluma yake.
  Hapa umegonga kwenye utosi ni kweli kabisa kwa mahesabu yangu hatujaanza kutengeneza mfumo wa elimu wa kuuwezesha umma kuchukua hatamu za kuamua juu hatima yao kisiasa kwanza. Kwa sababu SIASA ni kila kitu inaweza kumuzesha mtu kushiriki kikalifu kwenye uchumi, kuwa raia mwema muadilifu na kujenga taswira sahihi ya kitaifa.

  Kinyume chake kupokonywa nyenzo hizo, ni kuangalia vyama ambavyo vimekijita kwenye udhaifu wa chama kingine. Kwa mfano wananchi wanaona kwa urahisi udhaifu unavyoelezwa na CDM lakini CDM haijajaribiwa kuongoza serikali, na sera kama ya elimu ya chama hiki haielikei kubadiri kabisa mfumo mbovu elimu uliopo usikidhi mahitaji ya kuwawezesha watanzania kifikra.
  Nachelea kusema kuwa hapa chunguza zaidi; washiriki kwenye taasisi hizi ni elite group ambao pamoja na mimi tuko "disgruntled" na watawala wetu na tuna fursa ya kubadilishana mawazo. Bado nina imani na mabadiriko kamili ya mfumo wa elimu kuwa ndiyo njia pekee.

  Nakumbuka kwenye mwisho wa miaka ya 70 na mwanzo wa miaka ya 80 kulikuwa na msingi mzuri na imara wa elimu ya watu wazima; nakuachia msomaji ujaze sababu za kufa kabisa hiyo programu kwa kuunganisha na sera ya mataji wa chama tawala wa UJINGA NA UMASKINI.
  Kwa mtazamo wangu havitafanyika na vikifanyika vitahujumiwa ili vichukue muda mrefu.

  Mkakati mzuri nionavyo chama mbadala kikiingia kije na katiba inayokubalika, sera ya elimu inayomuzesha mtu kuwa na tafakari sahihi ya mazingira yao, na vyama hivi vya kijamii vijitolee kutumia fursa zote zinazojitokeza kutoa kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu vitu vya msingi kama katiba.
  Ni kweli lakini inawekekana?

  Hakuna cha kujifunza toka Libya. Ni mchanganyiko wa utawala wa muda mrefu na uporaji wa raslimali za Africa. Wale Rebels hawkutokana na umma wa libya.
   
 6. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #6
  Aug 27, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Naam! nimeasoma wote Mimibaba na JouneGwalu na shukran kwa michango yenu yenye kufikirisha na kusisimua sana.

  JouneGwalu; Ni kweli kuwa hatima ya UMMA lazima iwe mikononi mwa Umma, na nakulbali kuwa vyama vya siasa si mahali salama sana katika kuwekeza kimaendeleo. Tunakumbuka Kibaki alivyogeuka kuwa mgumu kwa katiba ile ile aliyopigania kuishughulikia akiingia madarakani.

  Ninaposema umuhimu wa vyama vya siasa nina mambo ninayoyaangalia kwa undani na kujidhirisha kuwa kupitia Umma itachukua muda mrefu na hakika muda huo hatuna. Ni njia sahihi lakini muda si mshiriki mzuri. Ugumu wa vyama vya Umma na kijamii nauona kama hivi:

  1. Mfumo wa elimu uliyojengeka katika mazingira ya kudumaza fikra kama (Mimibaba) alivyoonyesha kwa kina kuanzia uhuru n.k

  2.Sheria kandamizi zisizoruhusu uwepo wa vyama hivyo kwa uhalali na hivyo kuwafanya wanaharakati kujificha nyuma ya mwanvuli wa siasa.
  Si rahisi kumshtaki au kumfunga Lipumba, Mbowe au Zitto kwa sababu wana kinga ya kisiasa na nguvu ya umma lakini ni rahisi kumfunga Nguruvi kwa kisingizio cha kuvuruga amani kwasababu hakuna sheria zinazomlinda mwanaharakati. Mnakumbuka Jenerali Ulimwengu!!!

  Hadi sasa nchi haina sheria ya kuwalinda wapiga mbiu( whistleblowers) na hivi karibuni tumesikia ya CHC bosi kufukuzwa, PPF, na Luhanjo ameahiidi kuwashughulikiwa wote wanotuambia tunaibiwa,kuna ufujaji au hujuma.

  Hawa wanaotuibia siri za ndani ndio wanaharakati wa jamii na ndio wanajamii, ndiyo tunategemea waamshe Umma, bahati mbaya hatuna sheria inayowalinda.

  Lakini pia tujiulize kwanini wananchi wasiandamane kwa kupanda bei za bishaa hadi chama cha kisiasa kiwaongoze? Ni makosa kusema hawako tayari! kinachotokea ni kuwa hakuna kinga yoyote ile kwa wao. Serikali itaingia na maguvu na visingizio vya kuvunja amani ili kuwatawanya.
  Wanapokuwa katika vyama vya kisiasa hali inakuwa tofauti.

  Hoja yangu kubwa hapa ni kuwa tutumie njia ya vyama vya kisiasa ili kuvunja mfumo uliopo sasa usioruhusu vyama vya kijamii au walaji, unaozuia haki za wananchi kuamua na kupanga hatima yao. Njia hii hautakuwasahihi 100% kwasbabu bado ni wa kisiasa lakini utatusukuma mbele agenda.

  Kenya wameweza kupata katiba mpya baada ya Moi kuondoka, Moi hakuondolewa na vyma vya kijamii bali mfumo wa kisiasa.
  Katiba mpya ya Kenya ndiyo inawapa uhuru wa kuwa na vyama vya kijamiii vilivyoweza kushinikiza serikali kushusha bei ya bidhaa, kuhoji mishahara ya viongozi, na hata kutaka uchunguzi wa uhalifu kama ubadhirifu wa mali za umma.

  Kwanini tusitumie short cut tusubiri njia ndefu ya ku-sensitize umma ikiwa ni pamoja na miaka mingi ya elimu inayohitajika.Je tuna muda wa kutembea wakati wenzetu wanakimbia?

  Kuna ushahidi kuwa nguvu ya vyama vya Umma na kijamii katika mfumo babe wa kisiasa kama wetu ni ndogo sana. Katiba ya nchi imepigiwa kelele na vyama hivyo ikiwa ni pamoja na Umma kwa miaka mingi tu. Kuanzia tume za kina Nyalali, Kisanga na zilizowatangulia nyingi tu vyama vya haki za binadamu, usawa na jinsia n.k. Serikali haikushtuka hata kidogo. Hoja ilipochukuliwa na vyama vya siasa na kauli za peoples power kusikika imewastua na japo kukubali kuliongelea hilo.

  Tunachotakiwa ni kuunga mkono nguvu za vyama huku tukiwa makini kuwa katiba iwe mikoni mwetu na si mwao, kwamba sisi ndio tunaweza kuwaambia wafanye nini na sio wao kutumia katiba kutukandamiza. Wakati wao wanapingana kuhusu katiba sisi tutumie fursa hiyo kujenga mazingira ya kuwepo vyama vya UMMA na kijamii baadaye.
   
 7. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #7
  Aug 28, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Hili naliafiki kabisa. Kulikuwa na ulimbukeni wa kujitawala kama tulivyoona kitu kinaitwa Africanization. Ukweli ni kuwa Africanization ililenga kumpa madaraka mwafrika hata kama hana uwezo. Bahati mbaya wanasiasa si watu wakweli na hawakuweza kuwaambia wananchi ukweli huo ila walijitahidi kutumikia mabwana wawili, kwanza africanization ili waendelee kuwepo madarakani, pili, changamoto wataalamu wasio na utaalamu wanotokana na africanization.

  Niliwahi kuuliza kuwa endapo Nyerere alifanya kazi ya kuleta uhuru na hawa watu wa darasa la nane, na kisha katika matatizo wakatuvusha mpaka tukawa na maprofesa, je inawezekana kiongozi yoyote sasa kuwa na vijana wa darasa la saba na kufikia yale ya miaka ya Nyerere! Jibu ni hapana.
  Swali sasa kulikuwa na tatizo gani kubadili mfumo wa elimu? hakuna jibu la maana.

  Hata Katika miaka ya 70-80 mwishoni hali ya kujielewa ilikuwa haijafikia kiwango cha chini kama ilivyo sasa. Wale waliokuwa katika vyuo miaka hiyo mambo ya wanafunzi yalijikita katika shughuli za kijamii. Nakumbuka Chuo kama UDSM kilkuwa kisima cha fikra si kwa mambo ya taifa tu hata ya kimataifa kama ukombozi wa Africa. Hali iliyopo sasa ni tofauti kabisa. Elimu ya Umma wetu inakuwa kama 'radioactive materials, it decays with time) na hapa inamyang'anya mtu kile ulichosema uhuru wa fikra.
  Na wala asitokee atakayesema kuwa Makenge yamefikia mwisho wa safari, big mistake! yapo yanagawana mashamba na mali za umma bila hofu yanawapa watoto wao nyenzo za elimu popote inapopatikana duniani, ndio maana mahali kama bungeni kuna wabunge 47 wanoingia kwa majina ya makenge waliotangulia.Vivyo hivyo katika ajira n.k.

  Ndipo ikifika hapa nasema Shoka lina mpini na mpini unatokana na mti wa msituni, na mpini huo ndio unaotumika kushikiza shoka ili likate msitu. Tutumie vyama vya kisiasa ili kuondoa mfumo babe na kabla ya hao wengine hawajaingia magogoni na kuonja raha ya ving'ora tuwe na katiba ili wakiingia huko waikute. Hapo tutaweza kutengeneza mfumo wa elimu utakaotukomboa.

  Itachukua mika mingi sana ku sensitize huu umma uliojengewa shule za kata kuelewa ni mfumo gani wa elimu utakomboa kizazi chao. Lakini tunaweza kutumia siasa na kushirikisha umma wa shule za kata kuvunja mfumobabe kwa muda mfupi sana. Kwanini tusitumie hiyo short tukiwa na long term plan.
  Nimekuwa nahoji sana kuwa mbona hatuoni sera mbadala kwa vitendo? kwamfano sera mojawapo ya Chdema ni kuwa na majimbo, lakini haionyeshi kwa namna yoyote ile mfumo huo wanautekeleza vipi kichama. Hata sera zingine bado hazipo wazi. Mathalani nini sera ya Chadema kuhusu muungnao. Kama imeelezwa bado ni vague, kwa umakini haieleweki kabisa.

  Pamoja na hayo kama tunaweza kushirikiana nao kuleta mabadiliko muhimu yatakayotuwezesha kwenda mbele na kubadili mfumo kwanini tusifanye hivyo? Hutatakiwi tuangalie mapungufu yao tu, tunatakiwa tutumie opportunity wanazozitengneza kufanya mabadiliko.

  Kwa mfumo wa utawala uliopo ni vigumu kuleta mabadiliko ya elimu au kichumi hadi hapo tutakapovunja uti wa mgongo unaoiitwa katiba. Kwanini basi tusishirikiane na vyama vya siasa kuvunja mfumobabe na kuzuia wao kutengeneza mfumu wao?

  Amids their confusion, contentions and confrontation let us seize the opportunity to install a new system which will pave a way to sustainable economy and education.


  Hapa sikubaliani nawe kuwa tuwaache kwanza waingie Ikulu. No! tufanye nao kazi kubadili katiba kabla hawajaingia Ikulu. Mwai Kibaki alipoingia Ikulu na kugundua utamu wa viong'ora alitaka kuwarudi wenzake. Tuwe nao pamoja sasa na wakati wanaenda Ikulu waikute ipo tayari.
   
 8. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #8
  Aug 28, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Naheshimu maoni yaliyotolewa kwa sababu kunaelekea kwenye convergence.

  Uzoefu wangu baada ya kufanya kazi miaka 37 katika awamu nne nakuhakikishia katika utungaji iwe wa sera, mikakati hata katiba Tanzania kuna vichwa. Kwenye jumiaya ya AM watekelezaji wazuri wa sera, mikakati hata katiba zinazotungwa Tanzania ni Kenya na nchi karibu zote za SADC.

  Nakueleza kutokana na kuwa mtaalamu mshauri ambaye nimefanya na nafanya kazi kwenye nchi hizo. Kwenye kundi letu tunaita "Just copy from Tanzania, change it to suite the requirement of your client and paste".

  Ninachojaribu kueleza hapo juu ni kutokana na kutofautiana nami hasa kwenye eneo la msingi wa utekelezaji mfumo wa siasa kupitia katiba mpya. Mimi sitoi nafasi kuwa katiba tunayoipigia kelele tutaipata kama tunavyoitaka. Nadhani unaona danadana inavyochezwa kujaribu kuiunga unga katiba angalau iwape muda makenge wakamilishe kazi zao.

  Kwa msingi huo kama wewe ni strategist, utaona muafaka ni kuingia na katiba yo yote ile kwenye kushika dola; halafu hapo ufanye mabadiriko makini ya mfumo mzima. Sababu ni kama ifuatavyo.


  1.
  Mmekiri hapo juu kuwa Asasi/Taasisi za kijamii hazina platform imara ya kusababisha mabadiliko kutokana na njaa na dola inayojihami kwa sababu ya upeo wao mfinyu wa kifikra (zao la elimu duni)


  2.
  Umesikia kwenye hizi asasi ni majina fulani tu yanayotajwa je human capacity base iko wapi? Maana yangu umma unajumuishwaje kwenye maono ya hizi asasi?


  3.
  Vyama hasa CDM kama nilivyoijadiri hapo juu inatumia au inajiimarisha kutokana na udhaifu wa CCM haiuzi sera kwa wananchi kama inavyotarajiwa. Mmelijadiri upungufu huo hapo juu. Nadhani kuna haja ya kuelimisha kwenye eneo hilo.

  a. Ubunifu wa sera unalenga kukidhi ndoto inayotarajiwa (natumia lugha nyepesi) kama vile Tanzania ya baadae, au miundombinu ya uchukuzi ya miaka 10 ijayo nk, nk

  b.
  Mikakati inahitaji kuwepo raslimali zote wakiwepo watu wanaoiamini katiba/sera yenyewe. Hapa tujitazamishe kwenye katiba tuitakayo. Kunahitajika malengo na viashiria vya muda mfupi, wa kati na wa muda mrefu.


  c.
  Kuna kitu ambacho ni mwiko kwa serikali hii toka tupate uhuru. Nacho ni Tathmini na Upimaji (Monitoring & Evaluation) katika kila hatua, mzunguko mzima wa utekelezaji na kutumia mrejesho wake. Hapa ndipo makenge wanamtaji wao kwa sababu ingefanyika kikamilifu upuuzi wote wa kifisadi ungegundulika tu mara unapochongwa.


  Turejee kwenye mada yetu ya dhana ya damage control


  Ni wazi mjadala unaibua maeneo mbali mbali nje ya watu binafsi na nafasi zao kwenye serikali au taasisi. Maeneo yanayokumbwa (suffer damage) ni pamoja na:


  Mustakabali wa katiba tuliyonayo ambayo haiwapi wananchi udhibiti wa utawala na uongozi (umehodhi madaraka ya wananchi kujiamulia ila kwa kupitia chaguzi feki chini ya miamvuli ya makenge)


  Sera mbali mbali katika kila sekta tendaji.

  Mikakati ya kukublika kukiwa na rasilimani za kutosha.
  Tathmini/upimaji endelevu na matumizi ya mirejesho ya tathmini hizo.

  Kitu cha wazi ni kutokuwepo kabisa kwa utamaduni wa UWAJIBIKA kwa umma.
  Ninachojaribu kukieleza kwa maoni yangu ni mapungufu katika mfumo katika kila hatua inayoambatana na uwajibikaji kwa umma. Mfumo wenye tathmini na upimaji katika kila hatua utagundua damage inapotaka kufanyika. Maana yangu tathmini yenyewe na upimaji ndiyo damage control yenyewe.

  Kwa nini haipo ni kwa sababu itawaadhiri wahujumu wa umma katika kila nyanja. Vipi kuhusu vyama vya siasa na damage control? Hapa naona tunazungumzia zaidi matukio (incidences) kuwa ndiyo yanahitaji damage control. Hapa ukitafuta undani wa hoja zangu hapo juu utagundua hayo matukio yanatokana na utekelezaji wa sera zinazotokana na katiba, mikakati programs na projects za chama. Pia tujiulize vyama vina mfumo gani wa kujitathmini ili kubaini mafanikio au mapungufu katika utekelezaji wa sera, mikakati yao?

  Nasikitika kusema nilivyowahi kuviona kwenye kampeni za uchaguzi si sera kama kwa chama cha mapinduzi ndiyo maana wanatumia dola kuwaamisha watanzania kuwa kila kitu ni sawa. Mfano kujenga mioundombinu ya barabara, bandari, anga huwa ni ahadi; umma unachodanganywa kwa ridhaa yao wenyewe (kwa kukosa elimu) hawaambiwi kama utekelezajia wa hayo una rasilimali za kutosha kwa sababu huwa hazipo. Ahadi zikishindikana kutekelezwa hakuna mkakati uliokubalika kabla wa kumuwajibisha mtoa ahadi au chama chake. Je hapo damage haijafanyika kwa umma? Vipi control ya hiyo damage?

  Nizungumzie vyama mbadala si pinzani; kuna walioahidi Katiba mpya, sera ya elimu bure, nafuu ya vyenzo za ujenzi. Je hapa pia kulikuwa na utambuzi wa rasilimali zinazohitajika? Nawaachia mujijibu.


  Tuje kwenye damages baada ya kutambua mianya ya damages hususan suala la CDM. Uchaguzi ulisimamiwa na sheria kanuni na taratibu. Ni wazi rasilimali watu katika hili zilihodhiwa na dola kwa chini ya chama tawala. Wagombea walitokana na vyama nyenye itikadi fulani na “principles” sina uhakika wa tafsiri ya kiswahili kama kama ndiyo imani/uadilifu/miiko au vyote. Principles haziwi compromised hata kama ikibidi kufa.

  Moja ya principle ni kuheshimu mamalaka hii siyo negotiable. Ukiikiuka umevuka mpaka maana yake usirudi umejitoa kwenye chama. Damage ilisababishwa na upande mwingine uliotibua hiyo principle yaani kurubuni wanachama(madiwani in this case) wakiuke principle za chama kwa hiyo kusaliti umma kwa matarajio yaliyoahidiwa na chama kwa maslahi yao (si ya umma).

  Hapa natahadharisha kuwa kwa uelewa mdogo wa umma na kukosekana kwa guarantee ya kuwajibishana siamini umma una chaguo lolote ila kutumika kama tambala la kufutia chemni.


  Madhara ya damage hii kwa kipimo cha wananchi si dhahiri kwa kukosekana kwa nyenzo za kuipimia. Hapa ndiyo maana kukiwa na mfumo wa tathmini na upimaji hata vyama hivi vitakuwa sensitive na suala la damages; muhimu ni kuwa mfumo ukiwa ndani ya utendaji wa shughuli zote za kila siku damage control itakuwa managed na kufanikisha maendeleo makubwa kisiasa, kiuchumi na kijamii.
   
 9. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #9
  Aug 29, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  HOJA YA CHADEMA


  Awali ya yote nimshukuru Mimibaba kwa michango yake yenye kufikirisha na hakika mjadala kuhusu 'dhana ya damage control' unaendelea.

  Pili, kutokana na haja ya hoja yetu ya awali 'Chadema-Big mistake' kama alivyoileta Pasco naonelea tuendeleze vyote kwa pamoja kwasababu kuna thread inayozunguzia muafaka wa CDM na CCM ambao Dr Slaa na Nape wameuchangia.
  Naonelea nihamishebaadhi ya post kama alivyoshauri Pasco ili tulete 'neutrality' katika
  Suala la madiwani lipo mahakani na hapa tunaliangalia kwa ujumla na si kulijadili ili kuepeuka kuingilia uhuru wa mahakama. Sitalijadili chanzo chake bali mtazamo wa jumla wa kisiasa.

  Ni wazi kuwa Nape na Katibu mkuu wake wanasema hakuna haja ya kukaa mezani kuliongelea suala la Arusha kama lilivyoagizwa na ofisi ya waziri mkuu na msajili wa vyama. Hoja yao ni kuwa huo ni mgogoro wa Chadema na madiwani wao na hawapaswi kuuingilia.
  Wanaendelea kusema Meya alishapatikana na hakuna sababu ya kujadili suala hilo.

  Kwa haraka unaweza kuwaona kama hawajui wanachofanya lakini kisiasa wamegeuza meza upande wa Chadema na kutumia udhaifu uliojitokeza kwa manufaa ya kisiasa. Hawa wanacheza karata ya kisiasa baada ya kuwalaghai Chadema.
  Hapa tunasema wapo offensive na Chadema defensive. Nafasi ya kuwa offensive wamepewa na Chadema.

  Mimibaba alisema kuna external factors zinzopaswa kuangaliwa katika mgogoro huu na si Chadema na msimamo wao. Nilikubaliana naye kuwa external factor ni CCM na serikali yake walioutumia udhaifu wa Chadema na hilo lilikuwa kosa kwa Chadema.
  Ni big mistake kama alivyosema Pasco. Ingawa sikubaliani na baadhi ya hoja alizotoa lakini kichwa cha habari sasa kinaonekana kuwa ni dhahiri.

  Kitendo cha Chadema kufanya maandamano na kuiweka CCM na serikali katika wakati mgumu hakikupaswa kufuatiwa na ukimya ulioambatana na muafaka wa madiwani. Ingawa inasemekana kuwa Chama hakikujua lakini tunajua chama kilikuwa na habari.

  Sijui kwanini baada ya serikali ya CCM kuwapiga mabomu, kuua na kujeruhi kulikofuatiwa na maandamano nchi nzima, Chadema waliridhia kukaa kimya kana kwamba suala hilo litajimaliza lenyewe. Matokeo yake madiwani ambao hatujui waliingiaje majadiliano na wenzao na kuchukua dhamana ya chama walipoamua kufanya muafaka. Inaweza kuwa external factor ilitumia nguvu zaidi ya ushawishi.

  Siku mbili baada ya muafaka niliwatahadharisha Chadema(kumbukumbu ipo) kuwa wanatakiwa wachukue hatua mapema kulikabili suala hilo.
  Ikapaita nusu mwezi na ndipo tume ikaundwa. Muda wote damage ikawa inaendelea na 'walaghai' wakaitumia kuwarubuni madiwani kama vile kwenda mahakamani, tukasikia wanalipwa stahiki zao n.k.

  Kwa mantiki hiyo basi CCM sasa hawaongelei utaratibu wa uchaguzi unaolalamikiwa bali wameamua kutumia mgogoro ndani ya chama kujificha. Ikifika hapo Chadema lazima waelewe kuwa suala halikuwa rahisi kama walivyodhani na sasa wanalipa gharama za uharibifu (damage) uliotokana na kukosekana kwa damage control.

  Pamoja na yote mazuri yaliyotokana na hatua za Chadema ukweli ni kuwa uharibifu ulikuwa mkubwa na gharama za kuurepea sasa ni kubwa zaidi.
  Ukifuatilia majadiliano na majibizano ni wazi kuwa CCM wamefanikiwa kuwaondoa watu katika hoja ya msingi na sasa watu wanajadili mgogoro wa Chadema kama chanzo cha tatizo.

  Jitihada kubwa za kuuelimisha umma zainzonekana kupotea kwa hoja ndogo ya kutumia mgogoro wa ndani ya Chama. Lau kana Chadema wangefuatilia kuanzia muafaka uliokuwa unaendelea au basi mara baada ya kutangazwa, walikuwa na nafasi kubwa ya kuziba ufa. Sijui hii itakuwa na impact gani kwa society lakini inatosha kusema upo uharibifu.

  Ningewashauri Chadema wafanye jitahada za kutenganisha matatizo ya ndani na ya nje wakati wa kujadili mambo. Kuna vitu viwili hapa 'donkey'
  na 'Horse' vijadiliwe separate na si kama 'Mule'
   
 10. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #10
  Aug 31, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Mimibaba asante sana kwa maoni yako ya kina na yenye mashiko. Nichangie kuhusu dhana kuwa Tanzania ndio watengenezaji wazuri na wengine wana copy. Ukiangalia kwa undani ni kweli kabisa kuwa sisi tunasera nyingi sana zenye kulilenga taifa kama zitashughulikiwa kama zilivyoandikwa. Bahati mbaya kila mara kumekuwa na matokeo mabaya kuzidi hata wale wanao copy and paste.

  Hapa ndipo nachanganyikiwa kuwa kwanini tuweke mkokoteni mbele ya farasi (cart before horse)! nina maana tuwazuri wa kutengeneza sera lakini hatuna sera nzuri ya kulinda au kusimamia sera. Wenzetu ni wazuri wa copy and paste lakini ni wazuri pia wa kusimamia sera. Sasa kwani hatujitathmini na kujiuliza hivi iweje anayeiba sera afanikiwe na sisi watengenezaji tushindwe? Je si wakati sasa tukaweka farasi mbele ya mkokoteni kwa maana ya kuwa na sera nzuri itakayosimamia sera nzuri zitakazoandikwa.

  Kuhusu katiba, ni kweli kuwa hatuwezi kuwa na katiba 100% kama tunavyotaka katika mazingira haya ambayo watu wamejijengea himaya na sasa himaya zao zinaonekana kutikiswa. Hata hivyo sidhani kuwa ni vema tukatoa nafasi kwa chama chochote kushika dola kwa katiba yoyote.

  Uzooefu unaonyesha kuwa viongozi wa kiafrika wapo tayari kufanya mabadiliko ya katiba zao, lakini hawapo tayari kutoa nafasi ya mabadiliko zaidi mbele ya safari. Kwa mfano, wataweza kukubali mambo mengi lakini si lile litakalowapa nguvu wananchi au kupunguza nguvu zao.
  Wataacha vipengele kama vinavyozuruhusu wao kutangaza hali za hatari au kuchagua viongozi nyeti wa dola kuwalinda.
  Nina maana wakati tunaenda kuandika katiba basi hata kama ni 50% itoe nafasi kwa umma kuwa na nguvu ya dola.
  Kwahiyo sio suala la kuwa na katiba yoyote bali katiba itakayotoa nafasi na nguvu kwa wananchi kwa mabadiliko ya baadaye.
  Pamoja na hayo bado moyo wangu unanisuta, ni wapi viongozi wa Afrika waliwahi kuingia madarakani na kuzikubali katiba walizoahidi kuzibadili bila mikutuo au kasheshe?

  Kuhusu asasi nakubalina pia kuwa human capacity base haipo, na ukweli kuwa nyingi zipo mijini. Hili linatokana na mazingira ya mfiumo yetu iliyotukakarisha kuwa hakuna mabadiliko nje ya asasi. Kwa bahati mbaya pia asasi hizi zinaongozwa na walafi na hivyo kukosa maana yake halisi.

  Hili la vyama kama CDM kutumia udhaifu wa chama kama CCM ni tatizo kubwa. Ingawa hiyo ni sehemu ya mkakati lakini isiwe sehemu kuu ya sera za chama. Tatizo linabaki kuwa vyama vya upinzani havijawa na mikakati mbadala na hivyo kujikuta wakiwa katika level ile ile ya ki-CCM.
  Kwa mfano, sera mojawapo ya CDM ni kuwa na serikali za majimbo, lakini mfumo wa CDM hauonyeshi kuwa wa majimbo na sijui tutaamini vipi sera hiyo kitaifa isiyo na template.
  Walipojaribu sera zao kama Karatu na Tarime wananchi wameonekana kuwaelewa kwa kuondoa ile dhana kuwa upinzani ni vurugu au mafanikio yao ni matokeo ya udhaifu wa CCM. Ghafla naona wamebadili muelekeo na na kuanza kufuata baadhi ya mifumo ya CCM.

  Kuhusu kukokesakana kwa tathmini, hilo ni janga la viongozi kitaifa. Haiwezekani hata mtu binafsi kuishi bila kuwa na mfumo wa kujitahmini. Inashangza pale Rais anapofanya tahtmini miaka 5 baada ya kutoa muongozo! sijui hiyo ni tathmini au ni kitu kinachofanana na hicho.

  Kuna wakati wanakwepa tathmini makusudi kabisa kukwepa kuwajibika. Sidhani Rais Kikwete anaweza kufanya tathmini ya miradi kama ya umeme akijua kuwa yeye ni sehemu ya kushindwa hata bila kutumia kigezo chochote cha elimu.
  Kwahili naweza kusema lazima tuhakikishe kuwa katiba ijayo inaweka vipengele muhimu kama hivi ili tuweze kujua mapema na si baada ya miaka 5 au 10 baada ya uharibifu.

  Utambuzi wa rasilimali wakati wa kampeni: Naweza kutetea kuwa vyama vya upinzani kama CDM vimejaribu kuonyesha japo kidogo wapi rasilimali zinaweza kupatikana katika kutimiza sera zao. Haiwezi kuwa timilifu lakini ina sadikika ukiangalia kwa umakini. Mfano, rasilimali ni pamoja na rasilimali watu, kwahiyo kuwekeza katika elimu ni sehemu ya kuatafuta rasilimali watu. Hapa ndipo wanapoonyesha kuwa wizi wa mabilioni unaweza kuwekezwa katika elimu. Wizi wa rasilimali kama madini na utalii vinaweza kuwa vyanzo vizuri katika uwekezaji wa afya n.k.

  Ninachosema hapa ni kuwa japo ni kwa uchache, wao wameonyesha mbadala ambao CCM kwa zaidi ya miaka 50 hawajaweza kufanya zaidi ya kutafuta 'rasilimali' kwa njia za kawaida kwa serikali yoyote. Hakuna ubunifu na kama upo utaishia kutia maji katika kikapu au ndoo inayovuja.
  Wasi wasi ni pale wanaposhindwa kuzitafsiri baadhi ya sera zao au kuzitetea katika uhalisia hata katika mazingira ngazi za vyama vyao.

  Labda tatizo kubwa katika vyama vya upinzani ni kushindwa kuetetea sera zao na wakati mwingine kuvutika katika mambo yanayomeza sera zao.
   
 11. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #11
  Sep 7, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  MAISHA YA WANASIASA

  Katika fani au taaluma zote tunazozijua ukiacha zile za michezo na burdani, siasa ndiyo inayoongoza kwa kuwa na maisha yasiyo na siri(privacy).
  Siajabu majirani kuishi pamoja kwa miaka mingi bila mtu kufahamu jirani yake ni mchumi, mhandisi au daktari.
  Kwa upande mwingine wanasiasa na michezo au burdani kama za art hujulikana hata kwa watoto wadogo.

  Kwa wanamichezo maisha yao yanakuwa na hali tofauti kidogo kwani uwepo wao katika jamii unategemea sana kazi zao na jinsi wanavyoonekana katika matukio. Imefikia mahali wengine huzusha vituko ili kuwa 'viable and vibrant'.

  Nakumbuka Bitney Spear alifanya mkutano na waandishi akiwa hana nguo ya ndani (underwear) ikaandikwa sana magazetini. Baada ya wiki mbili akaita mkutano mwingine kuomba radhi wana habari.
  Haikuchukua muda akaachia single ika hit the market kwasababu yeye alishakuwa habari sasa anauza 'brand' yake.

  Michael Vick alipata kufungwa kwa kugombanisha mbwa. Baada ya kifungo akawa balozi mwema wa mbwa na kuongeza jitihada kidogo michezoni. Leo analipwa zaidi ya wote katika mchezo wa 'American football'.
  Ninachojaribu kusema hapa ni kuwa hawa 'celeb' wana mazingira tofauti yanayoweza kuwa na mvuto kwa mashabiki na wapenzi wao.

  Siasa inataka uwe katika uso wa jamii kila mara na ujue kuwa inashirikisha watu wa rika zote wawe wazee, vijana n.k
  Ingawa wanasiasa ni wanadamu kama walivyo wengine na wanafanya makosa ya kibinadamu mara nyingi jamii huyaangalia makosa hayo kwa undani (scrutiny) na kuyapima kama yanalingana na hadhi ya mwanasiasa husika.

  Maisha ya wanasiasa ni maisha ya umma na ukiamua kuwa mwanasiasa basi ujue wewe ni mtu wa umma, usiyetakiwa kuwa na hasira kwa sababu umma una mchanganyiko wa watu, hutakiwi kuwa na papara au hamaki, usiwe na kiburi au kudhani unaelewa kuliko watu wengine, busara zako zitawale na muhimu ujue kuwa wewe peke yake ni habari kabla ya habari.

  Dereva wa dala dala akigonga mtu inaweza kuwa sio habari, lakini mwanasiasa akiangusha uma wa kulia hotelini inakuwa ni habari kubwa.
  Rais Obama alipokuwa Rose Garden akazungukwa na nyuki hiyo tu ilikuwa habari.
  Waziri wetu anaposinzia bungeni hiyo ni habari kubwa kuliko kilimo kilivyoleta njaa Somalia!!

  Kila anachokifanya mwanasiasa kiwe binafsi au kwa ajili ya umma lazima akiangalie kwa mtazamo mpana.
  Tena kwa bahati mbaya wao wanaongoza kwa kuwekewa kumbu kumbu kuliko taaluma nyingine.

  Leo mgombea urais wa marekani kwa tiketi ya Republican R.Perry anaandamwa kwa kauli yake kuwa ni' bora jimbo la Texas likajitoa marekani' kauli aliyoitoa miaka mingi iliyopita bila kujua kuwa atagombea urais.

  Pamoja nakuwa wanasiasa huwa hawakubali makosa kwa kugeuza kauli ili zilete maana tatai, wanafikia mahali hawana ujanja wa kucheza na lugha na wanalazimika kufanya yasiyotarajiwa.

  Kwa wale waliokomaa kuna maneno rahisi sana wanayoyatumia kuua hoja zinazotishia uhai wa kazi zao.
  Maneno hayo ni kama Samahani, naomba radhi, nakubali makosa, nakiri mapungufu, sikufanya kwa nia mbaya, nitajirekebisha,sikufanya utafiti, ilikuwa poor judgement n.k.

  Godon Brown wa UK aliponaswa akimwita mwanamke 'Bigot' ilikuwa ni habari kubwa kwasababu 'binadamu kauma mbwa na si kinyume chake'.
  Aliwahi asubuhi nyumbani kwa mama yule na kusema samahani kwa kauli zangu, na mjadala ukaishia hapo.
  Tumeona mwalimu Nyerere akikiri makosa kayika awamu yake.

  Wanasiasa wanaochipukia wanapaswa kuelewa matumizi ya meneno kama samahani, sikujua, nilkosea, sikudhamiria n.k ili kuzuia uharibifu 'damage'unaoweza kutokea kutokana na majibu yasiyokidhi haja.
  Kwa bahati mbaya siasa si hesabu ya 1+1=2. Inaweza kuwa na swali moja likazaa maswali mengi zaidi yanayoweza kumtia mwanasiasa matatani.

  Kibaya zaidi majibu yasiyojitosheleza huzua uchunguzi zaidi 'public scrutiny' na kuweza kuzaa maswali yasiyotarajiwa. Mfano, mwanasiasa akiulizwa umeo au umeolewa? akajibu 'hiyo si kazi yenu kujua', swali limetoa nafasi ya kuchunguzwa na hapo utapangwa mlolongo wa wapenzi kuanzia wa shuleni hadi machangudoa katika jitihada za kubahatisha nini kinaweza kuwa jibu la swali. Lakini mwanasiasa huyo angeweza kutumia maneno ya 'social' na kulifanya jambo hilo lifikie tamati.

  Tunakumbuka jibu rahisi la RA kuwa siwajui Dowans lilivyozua maswali na majibu hadi poromoko lake.

  Nimalizie kwa kukusema kukiri mapungufu si kushindwa kisiasa ni kukomaa na kuonyesha uadilifu unaotiliwa mashaka na wananchi kila siku.
  Wanasia wajue wao ni watu wa umma na kwamba kauli zao ni za uma, maandiko yao ni ya umma na kwamba wao ni habari kwanza kabla ya habari, na kuwa habari ni binadamu anapomuuma mbwa na si mbwa anapomuuma binadamu.

  senti sumuni
   
 12. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  http://www.raiamwema.co.tz/ubabe-ndio-unaowaponza-akina-qadhafi…

  Nimeona nianze na hiyo link hapo juu, mahsusi kufafanua hoja ya "kujifunza toka Libya"
  Ambayo "Mimibaba" alinipangua kuwa eti kama taifa hatuna cha kujifunza......

  Binafsi nilivutiwa sana na mawazo ya Ahmed Rajabu na jinsi alivyokokotoa misingi ya "Damage" katika Libya.
  Sipendi kuchukua upande kati ya makundi ya kishabiki (moja likimtetea Qadhafi na jingine likimpinga)...
  Tuchukue mda na kuelewa ukweli toka kwa Ahmed Rajab...

  Nimeamua kusisitiza kwenye hili suala la Libya na hoja hii ya Damage control kama hoja kuu katika muhtadha huu,
  Sababu kuu kuna viashiria vya kufanana kitabia kati ya UMMA wa watz na UMMA wa Libya......

  Wote hatuna uthubutu wa kumkalipia "mnyonyaji" sisi kama umma huru kwa sauti za umma bila msukumo wa ziada.
  Kwa mujibu wa makala hiyo ya Ahmed Rajab, nadhani wenzetu libya bado wana "damage" kali zaidi mbele yao kwa hicho tunachokiita "mapinduzi"

  Naendelea kusisitiza tuna cha kujifunza hasa tena.
  Nilitaka tu kuweka msisitizo katika hilo, zaidi sana nakubaliana na hoja zote kwa upana wake.
   
 13. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #13
  Sep 8, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Nadhani kuna la kujifunza kutoka Libya. Hakuna tukio lisilo na mafunzo.
  Mfano tumegundua kuwa zama hizi bunduki na raisasi haziwezi kutoa jibu, na kwamba watawala wajifunze kusikiliza wananchi wao wanataka nini na kwanini na wakati gani.
   
 14. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #14
  Sep 8, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Jamani Libya si mfano mzuri; hiyo ni project ya NATO. Halafu wale "mapanya" ni matayarisho mazuri ya nchi za magharibi, hamuoni NATO ilivyokuwa inafagia njia wao wanapeta? Hamuoni walivyojizatiti na silaha za NATO kwenye mapigano? Hamujasoma uhalifu wa kivita walioufanya kwa watu weusi na ICC haiwagusi? Kujifunza kutoka kwa labda mambo mawili tu, elimu wanayo kwa msaada wa Gaddafi na kuwa tayari kufia wanachokiamini. Singependa Mtanzania afe ila aelimike kuhusu utanzania wake na haki zake za kuiwajibisha serikali na wanasiasa
   
 15. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #15
  Sep 13, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  TUKIO LA ZANZIBAR: MCHANGANYIKO WA SIASA NA AJALI
  Awali nitoe mkono wa pole kwa wenzetu waliofikwa na matatizo ya ajali katika meli ya Spice Islander. Hakika ni marejeo ya matukio ya ajali zisizo elezeka kwa lugha nyepesi kama ilivyokuwa kwa MV Bukoba, na ile ya Zbar.
  Si nia yangu kuingia katika undani wa tukio hilo kwasababu yapo mengi ya kujiuliza kuliko kujibiwa.

  Kama kawaida tukio hili limejadiliwa katika viwango mbali mbali na vyombo tofauti. Yapo yatokanyo na mjadala ambayo nadhani tunaweza kuayajadili katika viwango vyetu kwa vile tukio zima linachukua muelekeo wa kisiasa na hivyo ndivyo ilivyo katika maisha yetu ya kila siku.

  Niweke sawa baadhi ya kumbukumbu ili kuelewa vema.
  1. Meli ya MV Bukoba ilipozama waziri mkuu Sumaye alikuwa ziarani Namibia. Kama mtendaji mkuu wa serikali alipaswa kuwepo ili kusimamia shughuli zoezi la uokozi na uopoa miili. Hakukatiza ziara yake kama tulivyotarajia.
  2. Mabomu Dar na Nairobi, tukio lilitokea rais akiwa uwanja wa ndege safarini Zimbabwe. Hakukatiza safari kama ilivyotarajiwa
  3. Alipofariki mzee Kawawa Taifa likiwa katika msiba, Rais alikuwa uwanja wa mpira kuangalia mechi ya kimataifa
  4. Tukio la Zbar halikuripotiwa na vyombo vya habari vya umma au binafsi ukiachiwa mitandao ya kijamii.
  Hii ni kwa uchache tu orodha ni ndefu na inaendelea.

  Hasira za watu wengi ziehamia katika kampuni ya Vodacom kwa kutositisha sherehe za ma'miss'. Kwa tukio hilo kuna pande mbili za shilingi.

  1. (a)Ukosefu wa busara ulioonyeshwa na vodacom 'poor judgement'
  (b) Matokeo ya Vodacom kushindwa kujisahihisha kwa makosa (damage control)

  2. Kuingizwa siasa katika matukio ya kibinadamu ili kukidhi haja za kisiasa.

  Ufafanuzi.
  1. (a)Katika tukio kama hili kamati ya miss Tanzania ilitakiwa ikae na kujiuliza, je ilikuwa ni busara kuendelea na zoezi hilo ikizingatiwa kuwa waathirika na marehemu baadhi yao kama si ndugu zao ni wateja wa kampuni ya Vodacom ambayo ndiye mdhamini mkuu anayebeba jina la shindano!!
  Na je kulikuwa na njia mbadala ya kuepuka hasara itokanayo kwa kuweka uwiano na hali ya ubinadamu?

  Vodacom walitakiwa watafute jibu kwa kuangalia mambo mengine zaidi ya hasara ya siku moja. Hapa ndipo nukta (b) inapoingia kuwa je walikuwa na mkakati wa kuzuia uharibifu utakanao(damage control). Ni wazi kuwa kama inavyosemwa walitaka kupeleka misaada ikakataliwa(na nina amini hata kama si leo bado wangepeleka) ulikuwa uamuzi mbovu sana kufikiwa. Ubinadamu haupimwi kwa thamani yoyote bali ubinadamu tu.

  Wao wanadhani kutanguliza pesa kunatosha kuwa sehemu ya ubinadamu bila kujua kuwa neno poleni sana ni sehemu ya ubinadamu.
  Hata baada ya kuandikwa na kusemwa sana bado walikuwa na dhima ya kusema, samahani au tupo nanyi n.k.
  Voda hawafahamu kuwa kadri habari inavyojirudia ndivyo inavyowaumiza na hakika sasa wapo katika damage kubwa.

  Damage kubwa kwani wao si waandalizi wa shindano ni wadhani na wapo wadhamini wengine wengi tu lakini kwa vile shindano linabeba jina lao wanajikuta wakiwa machoni mwa watu.
  Walitakiwa wafahamu kuwa wana 'damage' ya tuhuma za kodi ambayo ni ya kisiasa,bosi wao ni mwanasiasa mwenye tuhuma na kiburi, na wana washindani wenye haiba nzuri kuliko wao ambao wangependa kutumia udhaifu wao kibiashara.
  Kitendo cha kukaa kimya na kufanya 'damage control' kwa pesa ni mkakati mbovu sana kwa shirika lenye mtizamo hasi kama lao.
  Busara zingekuwa muhimu zaidi kuliko kuokoa mamilioni au kujiktakasa nayo.

  2)Siasa imeingizwa kwasababu wapo watu wanaohoji tukio hilo na hali ya muungano. Hii ni hoja dhaifu sana kwasababu miss Tanzania ni shughuli binafsi kama harusi na haina uhusiano na serikali ya JMT, lakini pia Vodacom ni sehemu kidogo sana ya jamii ya Watanzani ambao wengi wameungana na wenzao wa Zbar katika msiba huu na wengine kupoteza hata jamaa zao.
  Wanaoiongelea hoja hii ni wale wasio na hoja juu ya muungano bali kutafuta sababu hata kama hawajui zitakuwepo.

  Tayari Wzbar wanaita Watanzania bara (Watanganyika kama wanavyopenda kuwaita) kuwa ni washenzi kwasababu ya miss Tanzania, tena wakishabikia kuwa serikali yao imekataa misaada ya Vodacom. Nao pia hoja yao haina mashiko ni ya kisiasa na chuki zinazoelekezwa hata kwenye majanga ya kibinadamu ili mradi tu kukidhi kiu yao iliyojengeka katika misingi ya chuki na si upendo.

  Wasichoelewa ni kile kile cha kutafuta sababu ya kuzua chuki tu ili kutumbukiza hoja zao za kisiasa katika wakati huu mgumu kkuonyesha 'utukutu' wa Watanganyika. Nao hawana hoja kwasababu ile ile miss Tanzania ni shughuli ya LINO na si JMT

  Wasichokisema ni mchango wa hali na mali utokao bara kwa wenzetu waliofikwa na janga. Hawatamki uungwana wa watu wanaofanya kazi usiku na mchana kwa kusaidiana na wezao wa Zbar.

  Lakini pia kuna unafiki kwasababu iweje Zbar isiyo na shindano la ma miss(kwasababu za kidini) iseme inakataa misaada ya vodacom kwa vile hawakujali msiba? Ina maana kama si hivyo zoezi lile wangeendelea kulifurahia. Hawa nao wana ajenda ya kisiasa kwa kutumia maumivu na machungu ya wananchi wanaoteseka kwa dhiki moyoni leo hii.

  Kwangu mimi Vodacom nisingeifanya hoja kubwa, hoja yangu kubwa ingekuwa kuona watu waliosababisha uzembe huu wakifikishwa mbele ya sheria kutoka bandarini Dar hadi unguja kila mmoja atueleze alishiriki vipi na kwa mamlaka gani katika kutiimiza majukumu yake kwa sahihi.

  Voda wanaweza kufunga biashara leo, lakini je tutakuwa tumesalimika siku za usoni?
  Uzembe huu ni ule wa MV Bukoba, ukajirudia gatini unguja na sasa Nungwi. Ni uzembe wa mabasi na mafuso yanayotuua kila siku bila kuwa wakali kama tunavyowakalia kidete Voda. ndo, yapo mapungufu lakini tusiruhusu yakafunika hoja zetu nzito zaidi.

  Hivi kwanini tusianze kushinikiza waliohusika waachie ngazi na wapelekwe mbele ya sheria tunajadili kampuni ambayo haiwezi kutupa majibu ya siku za baadaye? Kwanini lakini!!
   
 16. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #16
  Sep 14, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  LINO WAOMBA RADHI

  Nimepitia mtandao wa Global publishers nikakuta taarifa ya miss Tanzania.

  YAH: KUOMBA RADHI KWA NDUGU ZETU WALIOPATWA NA MAAFA YA AJALI YA MELI HUKO ZANZIBAR. - Global Publishers

  Yale tunayoyaongea kila siku ndio sasa wanayafanya baada ya kufanyika uharibifu mkubwa.
  Wanasiasa na celeb neno samahani au tunawataka radhi halina maana ya unyonge bali uelewa wa mwanadamu.

  Kinachosikitisha zaidi ni pale samahani hiyo inapotolewa kwa kuunga unga. Mfano Lundenga anataka kusema simba na yanga zikiwa zinacheza hiyo ni excuse kwao. Lundenga lazima afahamu kuwa tukio la miss Tanzania hutokea mara moja kwa mwaka kwa mshindo zaidi ya malumbano ya kila siku ya watani wa jadi. LINO inapaswa kusema samahani na sio kutafuta sababu nyingine kuziba makosa yao yaliyotokana na 'poor judgement'.

  Wao wanafaham kuwa 'reputation' ya mashindo yao nchini inatiliwa shaka hasa kwa mafanikio hafifu kama yapo, malalmiko yanayohusu upatikanaji wa mshindi, historia isiyoridhisha ya washiriki hasa siku za hivi karibuni na tatizo la ' cultural and social ' linaloandama miss T.

  Wakati wote wa kutoa maamuzi au kutetea maamuzi LINO walewe kuwa hakuna justification ya kujicficha chini y amwamvuli wa simba au yanga.
  Hakuna mtu anayeonekana katika TV akinywa Bar na hata siku za maombolezo watu walienda huko lakini hatukuwaona katika TV.
  Lundenga anaposema kwanini baa zilifunguliwe kwahiyo kulikuwa na uhalali wa wao kuendelea bado ni damage kubwa.
  Bar zilifunguliwa jioni na maamuzi ya miss T yalishatoka mchana sasa wao wanapata wapi hoja hiyo.

  Lundenga anafanya damage control kwa voda lakini aelewe ni too late na njia anayotumia kujificha nyuma ya migongo ya vikundi vingine ni mbovu sana. Hata hivyo tumpongeze kwa kuandika 'Tunaomba radhi'
   
 17. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #17
  Sep 25, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Kwangu, Libya ni mfano mzuri kwa mambo kadhaa. Kwanza kuonyesha kuwa nguvu ya umma siku zote ni kubwa wanapochoshwa na madhila. Ingawa inaonekana Libya kuna msaada wa NATO tusishau kuwa Gahadaffi alitumia silaha kali kukabiliana na waasi waliokuwa na majambia na automatic rifles, kwa vyovyote huwezi kusema nguvu ya Ghadaffi illikuwa sawa na ya pinzani.

  Pili, viongozi wa Afrika wanaodhani kuwa demokrasia ni kurithisha watoto wao waelewe kuwa umma hauridhiki na hali hiyo. Tuliyaona kwa Omar Bongo, Kenyatta, Museveni hivi karibuni n.k.

  Tatu, Uhuru si kumpatia mtu kila kitu bali ni zaidi ya hapo. Wafungwa kule the Hague wanapata kila kitu isipokuwa uhuru na ndiyo dhana halisi ya kifungo cha mwanadamu. Huwezi kuwanyima Wananchi uhuru wa kuamua mstakabali wa nchi yao ukajinasibu ni kiongozi mzuri. Hayo tumeyaona Baharain, Saudia na Iran, Ukraine, Ingushetia n.k

  Ni kweli kuwa NATO wana masilahi yao Libya. Ikumbukwe kuwa Ghadaffi alishirki kulipua ndege ya PAN AM kule Lockerbie.
  Libya ilikuwa na sintofahamu na marekani na ilikuwa inaandaa nyuklia. Kwa upande mwingine ilikuwa tishio kwa Israel kwa upande wa kusini.
  Ushawishi wa Ghadaffi ndani ya AU umejenga hofu kubwa sana na hasa alipokuwa anatoa misaada kwa nchi za Afrika.
  Hata hivyo inaonyesha kuwa Ghadafi alikuwa mshari kama alivyoingilia vita vya Kagera Tanzania na kuunga mkono makundi ya ukombozi na uasi barani. Alishafikia mahali ushawishi wake ndani ya AU haukuwa unapingwa kwasababu alitumia rasilimali zake kuziweka mfukoni nchi masikini.

  Ukiyaangalia hayo yote utaona kuwa uwezekano wa kutokubalika na 'wakubwa' wa dunia ulikuwa mkubwa.
  Jambo tunalokosea ni kulaani NATO kwa kuingilia mzozo wa Libya. Kwanza wao wanafanya hivyo kulinda masilahi yao ambayo AU imeshindwa kulinda yake. Imechukua zaidi ya wiki tatu AU kutoa kauli tena isiyo na majibu kama zile za kuunda tume za Tanzania.

  Ikumbukwe kuwa AU haina historia yoyote ya maana ya kusuluhisha migogoro mezani au kwa mtutu. Ivory coast, madascar na Somalia ni mifano mizuri tu. Lakini kwanini tuwalaumu NATO kwa suala la Libya na tusiongelee Somalia ambako ni failure ya Afrika?

  Zilipoipigwa black hawk kule Mogadishu ulimwengu ukashangilia kuwa marekani wamezidi ubabe, nao wakaachana na Somalia.
  Sasa ni miaka 20 nchi haina serikali na vikosi vya AU havina hata uwezo wa kulipa askari kama ilivyo kwa Burundi na Rwanda.

  Tumeona Darfur ambako bila blue helmet, green helmet zilishindwa hata kununua buti.
  Kule Ivory kama si Sarkozy(hata kama ana masilahi) hali sijui ingekuwaje.
  Bagbo alwavimbia akina Kikwete na hawakuwa na jibu lolote la maana zaidi ya kunywa chai na vitumbua Adis Ababa.

  Ninachotaka kusema ni kuwa NATO wanalinda masilahi yao, je AU inalinda yake? wapi na lini. Sioni kwanini tuwalaumu NATO na tusijalaumu kuiachia Somalia iwe mfano mzuri wa ujinga na upumbavu wa mwafrika.

  Kwa Libya yapo mengi sana ya kujifunza kwa upana wake. Tukiangalia uvamizi wa NATO tu tutakuwa hatujaliangalia jambo zima kwa mtazamo mpana.
   
 18. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #18
  Sep 25, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  IGUNGA NA CHANGAMOTO

  Uchaguzi mdogo wa Igunga unaleta changamoto nyingi kwa chama tawala na vya upinzani. Ni uchaguzitunaouona unatumia nguvu nyingi sana. Chama tawala ambacho kina rasilimali nyingi ikiwa ni pamoja na vyombo vya dola kina haha kufikia hatua za kuwatumia 'wanaovuliwa magamba' na viongozi wastaafu kulichukua jimbo hilo.

  Kuna mambo makubwa matatu ninayo yaona.

  1. Ni dhahiri nguvu inayotumiwa na CCM ni mapungufu ya makali ya chama hicho kimkakati na kiuchakachuaji.
  Ongezeko la wabunge wa upinzani ni kuendelea kumomonyoa ruzuku yao na kibaya zaidi ni kutoa mwanya kwa wapinzani kuchezea anga za nyumbani.Ngome za CCM kama Mwanza, Iringa, Mbeya zote zimesha 'bikiriwa' na sasa kiwewe kipo Tabora.

  CCM imebaki salama Lindi, Tanga, Mtwara, Morogoro, Pwani na Ruvuma. Tabora inaonekana kuponyoka na ndicho chanzo cha kuhaha. Inapofikia chama kinatumia nguvu kiasi hicho kuna jambo kubwa na ishara ya hamkani kutokuwa shwari siku za usoni.

  2. Ni dalili njema kuwa upinzani unakubalika sasa na wananchi wameanza kuwa na imani nao.
  Hata hivyo ni ushahidi kuwa kushindwa kwa upinzani hakutokani na uchakachuaji tu bali ukosefu wa mbinu za ushindi.

  a) Kutokuwa na mkakati wa pamoja na hivyo kugawana idadi ya kura

  b)Kutokuwa na mkakati wa ushindi kwa kuangalia mambo muhimu ya kiufundi.
  i) Ipo thread ya MM ya Igunga iliyoelezea mambo kadhaa yanayotoa ushindi.
  Wachangiaji wengi wameto analysis zao ninazoziafiki kabisa.
  a) Mkakati wa ushindi si mikutano au wahudhuriaji wa mikutano ni idadi.
  Yupo mchangiaji aliyeonyesha idadi ya waliojiandikisha mwaka 2010 na waliopiga kura ikiwa ni chini ya 49%. Hayo yalitokea kule Mbeya na Mwanza katika chaguzi ndogo. Hakuna anayejibu kwa ufasaha kwanini watu wajiandikishe 70% na wapige kura 30%. Zipo dhana za ununuaji shahada ambazo CCM katika chaguzi zake imezionyesha wazi wazi.
  Utakuwa ni ujinga kama tutasema hilo halipo. Swali ni je wapinzani wamejipangaje kukabiliana nalo?

  b)Uchakachuaji: Je wapinzani wana mkakati gani kuzui masanduku ya kura kugawanywa saa 10 jioni? Kama Ubungo waliwahi kupelekewa masanduku saa 11 sijui Igunga itakuwaje.

  c) Je, wapinzani wanajua nani amejiandikisha na kuwa ana shahada yake miongoni mwa wanachama wao?

  d) Kushindwa kutafsiri mauza uza.
  Hili ni kosa kubwa sana wapinzani wameshindwa kuliona mapema na litawagharimu sana.
  Ninaliita mauza uza kwasababu wao wameaminishwa kuwa daftari la kura la mwaka 2010 ni sahihi, kwamba hakuna marehemu, wahamiaji, waliohama n.k.

  Huu ni mkakati wa CCM kwa kushirikiana na tume husika. Wanafahamu kuwa miongoni mwa wapiga kura wengi wapinzani wana vijana waliokuwa likizo na sasa wapo vyuoni na hawataweza kupiga kura. Kutumia daftari la zamani ni kuondoa nusu ya kura za vyama vya upinzani na zilizobaki zitaweza kununuliwa.

  Kwa maneno mengine wao wanacheza na namba ndiyo maana wananunua shahada kutoka kwa wanachama wa upinzani wakielewa kuwa kambi yao ina watiifu ambao wataipatia ushindi hata wa juu ya asilimia 0.5. Ushindi ni ushindi tu.

  Kama wapinzani wangeliona hili mapema wangetaka marejeo ya daftari la kura, bahati mbaya sasa wamechelewa.
  Hapa ndipo CCM watakapocheza na namba kwa uhalali au uharamu na wapinzani watajikuta katika wakati mgumu.

  Ninachojiuliza hivi vyama vya upinzani vitakuwa na wanamkakati lini (strategists) wa kuchambua mambo kabla ya!
   
 19. O

  Ogah JF-Expert Member

  #19
  Sep 25, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Daaahh....Wakulu Nguruvi3, jouneGwalu na mimibaba................nawashukuruni sana kwa shule mnayotoa hapa.....keep it up!

  Nawaomba pia mzungumzie ni namna gani SUALA LA WAGOMBEA BINAFSI litakavyowezesha wananchi kuamua walitakalo............kwa sababu sehemu ya mazungumzo/maandishi yenu mmegusia mabadiliko ya vyama kwenye nchi zingine Vs matarajio ya wananchi (e.g in Kenya).......nafikiri kuna mambo ambayo tunaweza kushawishi wananchi wakayafanya bila kusubiri overhaul ya katiba au mabadiliko ya chama na kuchukua nchi na hatimaye kushika hatamu (risk)!!..............

  ....otherwise wakuu nawashukuru sana kwa shule.........thats why naendelea kuipenda JF...........kwa sababu ya vichwa kama nyie..........
   
 20. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #20
  Sep 25, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nipo safarini nje ya nchi natoa mada kuhusu tathmini ya software ya kupimia MDGs, kwa hiyo sijatulia kupitia mjadala. Nimezisoma hoja zako, siku zote hoja yenye tija ina zaidi pande mbili za mtazamo. Kwenye uchokozi wangu niliibua (upande mmoja wa Libya) mazuri ya Libya ambayo yamegandamizwa na NATO. Umeibua udhaifu wa michango ya Gaddafi katika bara letu na hususan kwa wananchi wake. Ebu sasa tuchambue udhaifu wa hoja zangu na umakini wa wa hoja zako kwa mlinganisho.

  Watu wa Magharibi wana sera isiyotangazwa inaitwa FACTS ON THE GROUND. Watakudunda au kukupora rasilimali ili mnegotiate kwa maslahi yao mfano mafuta ya Libya na kuwepo na taifa la Israel nchini Palestina.

  Uvamizi wa Gaddafi Kagera facts on the ground inaonyesha ulishindwa kwa gharama tunayolipa hadi leo. "Mapanya" wa Libya wamedhibiti sehemu kubwa ya nchi lakini tusubiri kama wataweza kuiongoza Libya kama nchi huru ya Walibya na yenye maslahi kwa walibya.

  Katika mstakabali wo wote endelevu ebu jiulize maswali machache.

  1 Lengo (la muda mfupi, wa kati na mrefu) ni nini?

  2. Mkakati wake unatekelezeka?

  3. Kuna rasilimali za kutekeleza mkakati huo?

  4. Mfumo wa tathmini upo katika kila hatua?

  5. Madhara na changamoto zinatatulika?nani?

  6. Manufaa (ya muda mfupi, wa kati na mrefu) yanatambulika na yanamnufaisha nani?

  Natoa changamoto za tathmini katika hoja hii kwa sababu naamini kwa tukio la NTC huko Libya ni sawa na kuingia kwenye awamu mpya ya ukoloni mambo leo. Kwa kwetu hilo pia ni lakujifunza lakini nani ajifunze nini ndiyo issue.

  Watawala hawakubali ya NTC Libya kwa sababu walinufaika na Gadafi, halafu athari za mabadiriko kwao ni suicide (angalia ya Igunga).

  Bado naamini uduni wa elimu ya msingi ya uraia kwa umma ni kikwazo kikubwa cha kusaidia mabadiriko pamoja ya watawala kujitahidi kuidhafisha jitahada za kuuelimisha umma.

  Kwa bahati mbaya sana fursa ya majadiriano yetu amabayo yangechangia kuelimisha umma yanaishia hapa. Wadau muhimu wa kushiriki kwenye maoni yetu hawana fursa hiyo. Hata hivyo ni matarajio yangu kinachosomwa hapa kitasambaa kikawaida kwa watakosoma humu.
   
Loading...