Mkuu wangu shukran sana na naomba tuvumiliane...Mimi huandika na makosa mengi sana kwa sababu moja kuu. Pengine niwaulize wana JF kina Maxence maana kila napoandika hoja kuna tracing huingia na mara zote znisipokharakisha ku post siwezi tena huwa inaingiwa kiasi kwamba lazima nizime PC kuislafisha na kisha kuanza upya. Hivyo, ni rahisi kuandika haraka na ku post kisha nafanya marekebisho ikisha kuwa hewani. Hapo siingiliwi kabisaaaa!
jmushi1,
Kwenye suala la mafuta ni vita vya kidunia Mataifa matano wanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Marekani, Uingereza, Ufaransa, China, Urusi, hawa ndio wanaomiliki makampuni makubwa sana ya mafuta duniani.
Makampuni haya yanashikilia sasa soko la mafuta kutokana na mitaji yake mikubwa sana ya mafuta duniani, makampuni haya ni Petrochina, British Petroleum (BP), Royal Dutch Shell, Exxon, Texaco, Gulf, Mobil, makambuni ya Kirusi yaliyo chini ya Ikulu, Yukos, Sibneft, Lukoil, kuna Chevron, Total na mengine huunganisha mitaji ili kulikamata soko la mafuta duniani..
Mataifa ya kiarabu yanatumia mafuta yao kama silaha katika uchumi wa dunia.
Ritz,
..suala la utajiri wa mafuta vs haki za wapalestina.
..inasemekana turufu ya mwisho ya kupatikana kwa uhuru wa Zimbabwe ilikuwa ni Nigeria kutishia kutaifisha visima vya mafuta ikiwa Uingereza haitasitisha misaada yake kwa walowezi wa Zimbabwe.
..inasemekana Nigeria tangu enzi za Murtala Mohamed ilikuwa ikitoa msaada mkubwa sana kwa vyama vya ukombozi na nchi zilizokuwa mstari wa mbele wa ukombozi wa kusini mwa Afrika.
..Waarabu wanapaswa kuungana, na kutumia turufu ya utajiri wa mafuta, kushinikiza Wapalestina wapewe haki yao.
Nguruvi3HALI YA MISRI BADO TETE
Rais Morsi alitangaza kurudishwa kwa bunge lililovunjwa na baraza la kijeshi.
Mtafaruku umeendelea baada ya mahakama kupinga agizo la Morsi na kwamba kuliita bunge ni kukaidi amri ya mhimili mwingine. Siku za nyuma tulisema Brotherhood walikaa kimya wakati wa uchaguzi bunge likivunjwa ili wa-focus katika hatua yao ya mwisho ya kuchukua utawala.
Taratibu tunaona kucha za Brotherhood zikichomoza. Ni ukweli usiopingika kuwa Brotherhood walishinda viti vya bunge na Urais. Ni ukweli kuwa baraza la kijeshi chini ya Tantawi halikupaswa kuvunja bunge halali lililochaguliwa na wananchi.
Tunajua kuwa hata uapishwaji wa Morsi ulifanyika mara mbili, moja ikiwa ni mbele ya jengo la mahakama linaloelekeana na Hospitali maarufu ya kijeshi. Hospitali hiyo ndipo alipotangazwa kufariki Anwar Sadat, ndiyo hospitali aliyofia Shah wa Iran na ndiyo anapotibiwa Hosni Mubarak.
Baraza la kijeshi lilitaka Morsi aelewe kuwa kuna mihili mingi ya kikatiba na mingine isiyo rasmi.
Msuguano wa Mhakama, serikali, bunge na baraza la kijeshi unaonekana kupamba moto.
Hili ndilo changamoto tulilosema siku za awali kuwa linamkabili Morsi.
Jambo la kushangaza ni kuwa nchi za magharibi hazijalikemea jeshi kwa kuingilia serikali iliyochaguliwa kihalali.
Huu ni ushahidi kuwa jeshi linaungwa mkono kama lilivyoungwa mkono wakati wa kumuondoa Mubarak.
Bado nchi za magharibi hazijaridhika na uchaguzi halali wa Misri. Wanawajua Brotherhood vema na hakika hawana usingizi
Siku za karibuni tutashuhudia makundi Tahariri Square kumuunga mkono Morsi, na mengine kuunga mkono Jeshi.
Jeshi halitaki kuachia 'utamu' kwasababu linapata msaada wa dola Bilioni 10 kutoka marekani kila mwaka. Hayo ni sehemu ya mkataba wa Camp David.
Uwezekano wa Morsi kupata 'ajali' ya kisiasa ni mkubwa sana hasa kwa jinsi jeshi lilivyochukia kuporwa madaraka.
Ukitaka kujua jinsi jeshi linavyoendesha mambo kichini chini ni pale Mubarak akiwa mfungwa kama wengine bado anatibiwa katika Hospitali ya jeshi. Muda wote wa mashataka alikuwa katika Hospitali ya kijeshi.
Hali ya Misri bado haijatengemaa na tutaendelea kujadili kadri itakavyojuzu
Tusemezane
Katavi ni kweli kabisa unayoyasema. Tatizo ni kuwa utaratibu upi utumike ili kuhakikisha usalama wa kila mmoja wetu.Wakuu Ritz na Nguruvi3 jana mbunge wa Igunga kavuliwa ubunge na mahakama, na hii huenda ikapelekea uchaguzi mdogo jimboni humo. Kwa mtazamo wangu naona tunajiingiza wenyewe katika gharama zisizo za lazima, ni wakati muafaka wa katiba kuangalia hii ishu. Sina utaalamu sana na haya mambo ya demokrasia, je haiwezekani kuwekwa katika katiba kifungu kuwa anayeshika nafasi ya pili achukue nafasi pale inapotokea kesi kama hii??