Ndugu El Jefe Nafikiri tunachanganya mambo mengi mno kiasi cha kuishia kupoteza mtiririko mzima wa mada iliyopo mezani kwa sasa hivi na hii haitusaidii chochote. Hebu tupitie facts moja baada ya nyingine kwa umakini kuhusu sakata la Senate, Barr na Mueler bila kuchanganya mambo mengine kwanza;
Naona na wewe unataka kulisha wana JF matango pori. Kwa ambao wameweza kusoma ripoti yote na underlying evidence wameona wazi kabisa kwamba ugomvi wa Mueller na Barr ni hatua ya Barr kutoa maelezo ya uongo. Barr hakusoma yote na mengi aliyoulizwa jana alikuwa akiyasikia kwa mara ya kwanza na yalimtisha kidogo.
Ripoti ambayo Mueller alitaka iwasilishwe Congress kama ilivyo ilikuwa ni ripoti waliyokwishaifanyia reductions zinazotakiwa kiutaratibu. Hii ndiyo sababu hakupendezwa kabisa na alichokuwa akifanya Barr kwani barua yake ya kwanza ilipotosha kila kitu kilichotakiwa kitolewe kwa umma.
Hiyo ndiyo sababu hata Republicans baada ya kugundua kuwa Barr aliwalisha matango pori katika juhudi za kumlinda Trump, walikuwa wanapiga chenga kujadili ripoti na badala yake wanawaingiza Clinton, Comey, Lisa n.k. kwenye mjadala. Hata mwenyekiti Graham alionekana kushtushwa na baadhi ya maswali kama ya Kamila Harris.
Mag3 , mimi nasimamia FACTS tu.El Jefe, sijui Trump alikulisha nini...unamtetea utadhani uhai wako unamtegemea. Hadi leo hii msimamao wake ni kwamba haamini Urusi waliingilia uchaguzi wao wa mwaka 2016 na kwamba baada ya kumtizama Putin usoni anaamimi maneno yake zaidi ya wana usalama wa US! Barr hili anakwepa kulizungumzia kabisa...!
Who are you kidding...facts according to who? Trump? Maybe you mean alternative facts as Trump's WH would put it! Would your man recognize facts if they were staring at him right in the face? No, El Jefe, I sincerely believe you are not serious, you are just being disingenuous. Immediately Trump enters a room, you can be sure facts will be tossed outside the window and maybe all that will be left are none other but alternative facts, period. We are now entering big time league bigly (sic!), stay tuned.Mag3 , mimi nasimamia FACTS tu.
Naona unaishi US ya kusadikika, je unajua kwa nini Republicans wameanza kumkomalia Mueller? Conservative media sasa hivi iko obsessed na kuhoji credibility ya Mueller, and for what? Well, Watergate had the Nixon tapes. Mueller had Annie Donaldson’s notes. El Jefe, amini usiamini WH wanajua kilichomo ndani ya unredacted report ya Mueller na kama wanajua you can bet na wengine pia wanajua.Habari ya ripoti ya Mueller hata sio habari inayo-trend U.S., ni kama vile umma umeshaichuja na hawana interest nayo tofauti na mwanzoni AG Barr alivyotoa ripoti ya Mueller kwa umma. Uchunguzi wa Mueller unazidi kuchuja kadri siku zinavyoenda.
Kwa taarifa waliyosema ni 'gold std' waliyosema imem'exonerate' Trump"Mag3, post: 31325955, member: 10873" Republicans wameanza kumkomalia Mueller?
Conservative media zimebadilika ghafla. Kama utakumbuka AG Barr aliulizwa kama amewasiliana na WH kuhusu taarifa, alikiri kuwa wamewasilianaConservative media sasa hivi iko obsessed na kuhoji credibility ya Mueller, what? Well, Watergate had the Nixon tapes. Mueller had Annie Donaldson’s notes. amini usiamini WH wanajua kilichomo ndani ya unredacted report ya Mueller na kama wanajua you can bet na wengine pia wanajua.
Trump alisema Mueller ni honorable person baada ya taarifa kutoka. Tuliwaonya wageni wa siasa za DC kuwa suala bado ni bichiJe umejiuliza kwa nini badala ya kumtetea Mueller kwa kutoa ripoti wanayodai imem-exonerate Trump, wameamua kumshambulia?
Ripoti ina makubwa sana ndiyo maana AG Barr hakutumia executive summary ya MuellerRipoti kamili ya Mueller ina makubwa na ni swala la muda tu, kila kitu kitajulikana. Kwa Barr historia inajirudia na safari hii amelikoroga kweli kweli. Aliyetota hajui kutota...
Trump na wapiga debe wake wamekuwa wakishangilia kwamba ripoti haijathibitisha kuhusu tuhuma COLLUSION na urusi. Lakini walipoingia mkenge na kuja kushituka baadae ni kwamba ripoti ya Mueler pamoja na kutosema wazi kuhusu collusion, imeanika ushahidi wa kutosha kuonesha kosa la OBSTRUCTION OF JUSTICE ambalo kisheria ni serious zaidi mtu anaweza kushtakiwa nalo.MUELLER KUTUA NDANI YA HOUSE
LINDSYE GRAHAM AMRUHUSU SENETI, TRUMP HATAKI HOUSE
Kuna taarifa Mueller yupo katika majadiliano ya kufika mbele ya kamati ya House mwezi huu
Majuzi, mwenyekiti wa senate judiciary committee Seneta Lindsey Graham alisema ikiwa Muller atapendelea, anaweza kwenda kuongelea simu yake na AG Barr na si vinginevyo
AG akihojiwa mbele ya kamati ya seneti alisema haoni tatizo kwa Mueller ku-testify hadharani
Rais Trump ame tweet haoni sababu za Mueller kuhojiwa na kamati za Bunge
Mtiririko huo unaturidisha katika hoja ya msingi. Ikiwa taarifa ilikuwa ''total exoneration'' kama Trump alivyosema na ikiwa AG Barr aliwasilisha taarifa sahihi, na ikiwa hakuna kilichofichwa nini kinahofiwa kwa Mueller kuieleza taarifa yake?
Seneta Lindsey anasema Mueller aende kueleza maongezi ya simu. Hii ni baada ya kusema kamati yake haitajadili tena suala hilo akitumia maneno ''it's over''
Lindsey anajua tayari ameshamtibua Mueller ambaye inaelekea atakwenda kamati ya House
Hivyo anataka kumpooza kwa kumpangusa na si kumpa fursa ya kueleza nini kilichomo
AG Barr kusema hana tatizo na Mueller kueleza taarifa yake huku Rais akimshawishi kwa tweet Mueller asiitwe tayari wanajichanganya. Ikumbukwe wiki iliyopita maamuzi ya Mueller kwenda mbele ya kamati Rais Trump aliyaacha mikononi mwa Barr
Kwanini hawataki Mueller aende mbele ya kamati?
Kwanza, ni wazi Mueller ataiumbua taarifa ya kurasa 4 ya Barr na utetezi wake wote
Pili, Mueller ataeleza ni kwanini aliamua kumuandikia barua Barr kueleza kutoridhishwa naye
Tatu, Mueller ataeleza nini kilichomo ndani ya executive summary na kumuumbua Barr
Nne, Mueller atafafanunua hasa kipengele kinachohusu obstruction of justice
Tano, itabidi aeleze kuhusu memo ya Ms Anne Donaldson ambayo ni mwiba kwa Trump
Sita, itabidi afafanue kuhusu utata wa nani anapaswa kuchukua hatua, congress au Barr
Hofu kubwa ya Rais Trump ni kufikiri kuwa Mueller atajibu mapigo ya matusi ya ''hoax'' angry democrats, Mueller ni conflicted n.k.
Na kwa uhakika kabisa Mueller ameishika karata ya Rais Trump WH.
Hahitaji kurasa nne, anatakiwa aseme kwa mistari miwili tu ''ndiyo kuna abcd'
Huku joto la shinikizo kutoka kwa waendesha mashtaka zaidi ya 500 wakisema kuna uhalifu uliofanyika na kwamba katika hali ya kawaida Trump angefikishwa mbele ya grand jury
Kama tulivyowahi kusema vile vikaratasi 4 vya Barr (bandiko 765) vililenga kuwapunza wakimbiza ''mwenge'' wasiojua siasa za viunga vikubwa vya DC. Ngoma ndiyo kwanza inaanza
Tusemezane
Naam bado mbichi sana ndani ya DC na viunga vyake, tulisemaTrump na wapiga debe wake wamekuwa wakishangilia kwamba ripoti haijathibitisha kuhusu tuhuma COLLUSION na urusi. Lakini walipoingia mkenge na kuja kushituka baadae ni kwamba ripoti ya Mueler pamoja na kutosema wazi kuhusu collusion, imeanika ushahidi wa kutosha kuonesha kosa la OBSTRUCTION OF JUSTICE ambalo kisheria ni serious zaidi mtu anaweza kushtakiwa nalo.
Ndio maana hawataki full report (unredacted) ya Mueller ipelekwe bungeni sababu wanajua yatakayoanikwa humo hata wao watashindwa kumtetea mtu wao.
Ngoma bado mbichi!
Mkuu Nguruvi3, taarifa za ndani zinasema Mueller ni kiboko. Hizi jitihada zote za Trump na AG wake, Mueller alijua (ali-foresee) kwamba zitatokea na alihisi njama zitafanyika kuzuia ripoti yake isitoke kama ilivyo. Alijua uwezo na ujanja wa Trump katika kula njama kuhusu mambo muhimu aliyoshauri kwenye ripoti kutatafutwa mbinu za kuzipotosha kumnusuru Trump kwa tuhuma zinazomkabili kwani anamjua vizuri Barr.Jitihada zinazofanyika ni kufunika na kuendeleza muda muda, mwisho wa yote uchafu wa Trump dhidi ya Marekani utawekwa hadharani, ni suala la muda
Bavaria impeachment kwasasa hivi haitatokea kwasababu zifuatazoTrump will be impeached soon.
Asante mkuu kwa maelezo yako.Bavaria impeachment kwasasa hivi haitatokea kwasababu zifuatazo
1. Ili kuandika article of impeachment na ipitishwe lazima kuwe na ridhaa ya House na senate
Kwahouse Dems ni majority na ipo hofu kwa Republicans ambao wanaweza kuongeza idadi
Tuliona wakati wa mjadala wa taarifa ya Mueller, Republicans wote ndani ya house waliunga mkono taarifa hiyo iwekwe wazi
Katika senate, majority ni Republicans na inahitaji 2/3 ambayo ni sawa na maseneta 67
Kwa woga aliowajengea GOP kupata maseneta 18 kuunga mkono hoja ni ngumu sana
2. Hilo ndilo linasababisha AG Barr afiche taarifa ya Mueller, Rais Trump akiweka executive privilege kwa taarifa, huku akikataa mashahidi muhimu sana kutokwenda mbele ya kamati akiwemo Mueller
Trump anafahamu taarifa iliyofichwa kwa kisingizo cha grand jury inaweza kubadilisha kabisa mawazo ya baadhi ya maseneta kama Richard Burr ambaye sasa anamtaka Don Jr
Kwa mantiki hiyo Democrats wanaogopa kwamba impeachment haitatoa matokeo tarajiwa na hilo linaweza kumjenga Trump kuelekea uchaguzi mkuu kama ilivyokuwa kwa Bill Clinton
Lakini pia kukiwa na siku si zaidi ya 500 kuelekea uchaguzi , kuna uwezekano impeachment ikatumiwa kama hoja ya kumshindwa Trump katika sanduku la kura na kutaka kumuondoa kwa kutumia Bunge