Duru: Matukio na habari za Dunia

Duru: Matukio na habari za Dunia

VITA YA ISRAEL-HAMAS

Tuliahidi kujadili baadhi ya maswali katika bandiko hapo juu lakini awali ya yote tuangalie yaliyojiri leo

1. Egypt na Jordan Abdulla wamekataa kupokea Wakimbizi wa Palestina katika nchi zao
Rais wa Egypt alisema wakimbizi watashambulia Israel na Israel itajibu kwa kuwashambulia wakiwa Misri. Hataki

Ukweli ni kwamba nchi za Kiarabu hazitaki kuwapokea kwasababu kufanya hivyo kunaipa Israel nafasi ya kuwaondoa katika ardhi yao ya asili. Jordan kwa sasa ina Wakimbizi takribani nusu ya nchi.
Njia rahisi ni kukataa kuwapokea ili Israel ibebe mzigo huo. Japo ni hatua yenye maumivu , kwa muda mrefu ni nzuri

2. Israel ime endelea kuibomoa Gaza kwa makombora , leo imepiga kanisa la Orthodox na kuua watu
Picha za shambulio la jengo moja zimeonyesha maiti 7 za Watoto kupitia Televisheni za Mashariki ya kati

Kushambulia Kanisa kunatoa taswira kwamba Israel ilihusika katika kupiga bomu Hospitali ya Anglican

Pamoja na jitihada zote za vyombo vya magharibi kuweka ''ushahidi' sehemu kubwa ya Dunia imekataa kuwaamini
Taswira ya Israel imezidi ni mbaya kuliko Hamas , ndiyo maana Rais Biden kahutubia na kusema ''maneno'

3. Rais Biden amehutubia Taifa akiomba Bunge liidhinishe pesa kwa ajili ya Ukraine na Israel. Biden amejaribu kuleta ' suluhu' akieleza machungu ya pande zinazohusika. Biden ameitaka Israel ifungue njia za misaada na iache hamaki na makosa na ifuate sheria za kivita. Kauli ya Biden imechukuliwa na vyombo vya habari vya mashariki ya kati kama kukiri kosa la klipua Hospitali.

4. Marekani imedai kuzuia makombora yakitoka Yemen kuelekea Israel.
Ikiwa ni hivyo na si propaganda za vita, makombora hayo ni 'cruise missiles' yanayojiongoza.
Marekani inadai ni ya kundi la 'Huti' linalosaidiwa na Iran. Huenda vita imeingia hatua nyingine na Marekani inaweza kujikuta imeingia, jambo ambao Raia hawataki wakikumbuka ya Afganistan na Iraq

5. Hezbollah wameshambulia kaskazini mwa Israel kwa makombora yenye shabaha.
Wameshambulia miundo mbinu ya mawasiliano na Israel imejibu mashambuli kwa vijiji villivyo karibu.
Mzozo huu wa kaskazini unaonekana kufungua njia nyingine ya vita, Israel haipendi kwani jeshi litasambaa

Wadadisi wanasema hatua ya Hezbollah ni kuiyumbisha Israel katika hatua za kuingia Gaza.

6. Israel yajiandaa kuingia Gaza.
Ni wiki Israel ikijiandaa kuingia Gaza kuwasaka Hamas. Kuna sababu mahususi kwanini Israel imesita sana

Kwanza, kuwanyima 'Hamas' na Wapalestina maji, umeme, matibabu na chakula ili kuwadhoofisha

Pili, kupiga maeneo ya majengo ili kupunguza msongamano na kuepuka vita ya mjini '' Urban war' na vifo vya askari

Tatu, kuna 'mateka' na Israel inataka kuwaokoa lakini inachelea kuingia Gaza watauawa

Nne, Kuna kikosi cha uokoaji kipo kazini kwa mazoezi (simulation) na ili kukipa kikosi muda na nafasi ni lazima hayo matatu juu yafanyike

Tutajadili maswali ya liyotangulia bandiko lijalo
 
1. Ni kweli zaidi ya 90% ya mijadala ya Watanzania ni Simba na Yanga, sijui tulikosea wapi? Ni vigumu kujadili mambo ya kitaifa au ya kimataifa ambayo yanatuathiri moja kwa moja. Tunaathirika.
2. Kuhusu ukatili wa Israel wakati mwingine mimi nafikiri tatizo ni waarabu wenyewe ambao wameshindwa kuungana dhidi ya Israel. Wakati makaburu walipokuwa wanawatesa waafrika kule SA, Waafrika ya akina Nyerere, Kaunda, Mugabe etc waliungana licha ya kuwa hawakuwa na nguvu za kijeshi mpaka makaburu wakaangushwa. Ni nini kinachowashinda Waarabu. Unaambiwa Saudia au misri inapatana na Israel kuliko inavyopatana na Syria.
 
1. Ni kweli zaidi ya 90% ya mijadala ya Watanzania ni Simba na Yanga, sijui tulikosea wapi? Ni vigumu kujadili mambo ya kitaifa au ya kimataifa ambayo yanatuathiri moja kwa moja. Tunaathirika.
2. Kuhusu ukatili wa Israel wakati mwingine mimi nafikiri tatizo ni waarabu wenyewe ambao wameshindwa kuungana dhidi ya Israel. Wakati makaburu walipokuwa wanawatesa waafrika kule SA, Waafrika ya akina Nyerere, Kaunda, Mugabe etc waliungana licha ya kuwa hawakuwa na nguvu za kijeshi mpaka makaburu wakaangushwa. Ni nini kinachowashinda Waarabu. Unaambiwa Saudia au misri inapatana na Israel kuliko inavyopatana na Syria.
Kamili , hoja zako nitaziunga na maswali ya bandiko#60 kwasababu zinawiana sana

1. Mijadala Watanzania imejikita kwa yasiyogusa Taifa au kimatifa. Watanzania wanaungalia mgogoro wa Israel-Palestine kwa jicho la udini. Wengi wanadhani tatizo limeanza October 7,2023, humeza habari kutoka vyanzo vya aina moja. Kizazi cha vijana kimekosa utamaduni wa kujisomea , kujifunza, kudadidisi na kuyatazama mambo kwa upana.

Upeo wa kuielewa dunia ni jambo muhimu katika ushindani wa duni. Huwezi kutenga mgogoro wa Mid East na maisha au Kazi au Biashara popote alipo mwanadamu.

Jaribu kuuliza Watanzania uliza swali hili '' kwanini dollar imeadimika'' majibu utakayopata yatakushangaza.

2. Kuna swali ; Kwanini Israel inakingiwa kifua na Mataifa ya Magharibi?
Israel iliundwa na nchi za Magharibi 1948, saa 11 baada ya kujitangaza Utaifa , Rais Truman wa US aliitambua na kudharau kamati ya Uingereza-Marekani iliyopendekeza nchi mbili 'two sates' solution''

Pili, Wayahudi wanamiliki uchumi wa nchi za Magharibi, kubwa zaidi wanamiliki vyombo vya habari.
Mafanikio ya kibiashara na umiliki wa vyombo vya habari unawapa nguvu sana za kuamua siasa za mataifa.

Katika mgogoro unaoendelea CNN , Fox na MSNBC vimekuwa vyombo vya propaganda vya Israel. Habari zao ni biased hazina weledi wa kiuandishi na zimelenga kuipa Israel eneo la propaganda bila kusikiliza Wapalestina

Marekani kuna taasisi ya Waisrael inayoitwa AIPAC (America-Israel Public Affairs committee.
Ushawishi wa Taasisi hii kifedha na njia za habari ni sehemu muhimu sana ya Uchaguzi wa Marekani.

Wasrael wapo katika serikali za magharibi na wanafanya maamuzi mengi.
Waziri wa mambo ya nje US wa sasa ni Muisrael na wengi tu katika idara na taasisi mbali mbali muhimu

Wakati wa Rais Trump, waandamanaji wa kizungu (white supremacist) walibeba mishumaa na mabango yasemayo ( Jews will not rule us) yakiimanisha Wayahudi hawatutawala. Hawa niWaamerika Wazungu wanaosema hivyo.

3. Kwanini Iran inaunga mkono vikundi vinavyopingana na Israel?
Vikwazo vya nchi za Magharibi kwa Iran ni kutokana na Iran kuendeleza sayansi ya nuclear inayoweza kutoa Bomu.

Israel ina wasi wasi na Iran kwasababu ya nguvu za kitaaluma katika viwanda na Sayansi.
Tumewahi kujadili hapa kwamba Iran ikiwa na SHIA ina Raia walioelimika sana mashariki ya kati

Iran ina rasilimali za mafuta na inazitumia kwa kuelimisha Raia wake takribani Milioni 86 mara 12 ya idadi ya Israel.

Iran ina mpaka na Israel na nchi rafiki kama Syria na Lebanon kupitia makundi ya SHIA.
Iran ni tishio kwasababu haitegemei teknolojia ya Magharibi kujiendeleza na Israel inapata tabu kuipeleleza.

Kuuwa kwa kingozi wa Nuclear Bw Mohsen na Kamanda wa Jeshi Qasem ilitekekelezwa na Israel kwa juificha nyuma ya Marekani. Israel inatambua vita na Iran ni mchezo tofauti kabisa na huu wa Hamas, na huitumia Marekani

Iran imeshapata mashambulizi ya Israel kwa mauaji ya viongozi wake, inajibu mapigo kuipitia vikundi mbali mbali kama Hezebollah, Huti n.k. Kwavile 'adui yao ni mmoja' Iran na Hamas (SUNNI) wanashirikiana

Hamas kimsingi walitakiwa kuungwa mkono na Saudi Arabia, kwa kutoswa wameamua kushirikiana na Iran
Hii haina maana Hamas na Hebollah wanaiva, la hasha, wanaiva dhidi ya adui wa pamoja ''common enemy'

4. Waarabu wameitosa Palestina ? Kwanini Saud Arabia inataka 'normalization''
Ni kweli Palestina imetoswa na nchi za Kiarabu kwasababu moja, hofu ya nani mbeba Mashariki ya kati.

Saudi Arabia ina Sunni wengi kama tulivyowahi kusema. Iran ina Shia wengi. Pakistan , Afganistan, Qatar, UAE, Kuwait, Yemen , Lebanon , Syria , '' Misri , Morocco, Tunisia , Algeria' zenye Waarabu zimegawanyika kwa mrengo wa Shia na Sunni. Kuna vita ya 'dominance' ya mashariki ya kati , Saudia ikipoteza ushawishi

Tutaendelea tulipoishia '' kupoteza ushawishi''
 
Inaendelea kutoka bandiko #63

Ili kufahamu vema mahusiano ya nchi za kiarabu , pitia uzi huu hapa ( Mgogoro wa Qatar vs Saudi Arabia)

Nchi za Kiarabu kama Qatar, UAE , Saudi Arabia, Syria majority ni Sunni. Nchi kama Bahrain , Iran , Iraq ni SHIA.

Iran ina nguvu za kitaaluma, teknolojia na ushawishi mkubwa kiasi cha kuzifanya nchi nyingine ziingie wasi wasi.

Saudi Arabia inahofia ushawishi wa Iran kuliko Taifa jingine, inapoteza ushawishi kama Taifa kiongozi

Israel inazitumia nchi za Kiarabu kama UAE, Kuwait na Saudi Arabia kurudisha mahusiano kwa kuitambua.

Kwa njia hizo huo utakuwa mwisho wa madai ya Palestina. Kwa maneno mengine Israel inataka Palestina kupoteza uungwaji mkono na nchi kubwa za Kiarabu

Nchi ya Saudi Arabi ilikuwa karibu kufikia makubaliano ya ''normalization' yaani kurejesha mahusiano na Israel.

Kilichokwimisha hatua za mwisho ni takwa la Saudi Arabia kutaka ulinzi wa Marekani na pia kujengewa mtambo wa Nuclear. Mtambo huo ni kwa lengo moja, kukabiliana na Iran.

Saudia kama nchi kiongozi ilikuwa tayari kuwatosa Wapalestina ili kujilinda dhidi ya Iran kupitia Israel na US

Kama kuna kiongozi wa Saudia aliyaaewahi kuharibu taswira ya nchi hiyo ni MbS mrithi wa Ufalme.

Huyu kupitia Jerad Kushner aliyeoa mtoto wa Trump na ambaye ni Myahudi wameshirikiana sana katika kupoteza hadhi ya falme kuu ya nchi za kiislam (Saudia)

Mvurugano wa nchi za kiarabu umeharibu jitidaha za Palestina kujikomboa.

Hamas hawakufanya shambulio kwa bahati mbaya, walikuwa na sababu.

Kwanza wamelazimu Saudi Arabia kusitisha mpango wa 'normalization' na Israel.
Saudia imechelea ' vijana wasije leta spring revolution' kwa yanayoendelea Gaza
Pili, Hamas wamerudisha agenda ya two states solution mezani.

Kwa kumaliza ni kwamba, tofauti za nchi za Kiarabu hasa katika madhehebu zimewavuruga sana.
Palestina ni mhanga wa mvurugano huo wa nchi hizo kama tulivyoona.

Hata hivyo, vita inayoendelea imeibua kizazi kipya kinachotaka mabadiliko. Mkutano wa Cairo jana na leo ulikuwa na lengo moja , kutuliza munkari na hasira za vijana wa kizazi cha leo wanao ona Wazazi wao wamewasaliti Wapalestina.
 
3. Rais Biden amehutubia Taifa akiomba Bunge liidhinishe pesa kwa ajili ya Ukraine na Israel. Biden amejaribu kuleta ' suluhu' akieleza machungu ya pande zinazohusika. Biden ameitaka Israel ifungue njia za misaada na iache hamaki na makosa na ifuate sheria za kivita. Kauli ya Biden imechukuliwa na vyombo vya habari vya mashariki ya kati kama kukiri kosa la klipua Hospitali.
Hivi ni kweli Biden anawahurumia wa Palestine, Ili Hali, kwake wagonjwa wanaweza kufika mlangoni mwa hospitali kisa wamekosa fedha za matibabu ? Tuhuma hizi za mgonjwa kufika mlangoni huko US amezitoa Rais wa Russia.

 
Hivi ni kweli Biden anawahurumia wa Palestine, Ili Hali, kwake wagonjwa wanaweza kufika mlangoni mwa hospitali kisa wamekosa fedha za matibabu ? Tuhuma hizi za mgonjwa kufika mlangoni huko US amezitoa Rais wa Russia.

Nadhani hukunisoma vizuri au umesoma hukuzingatia alama . Nilisema hivi Biden anajaribu kuleta '' SULUHU''
Neno suluhu lina alama '' '' hiyo inaeleza kifungu kizima

Hata hivyo kwa minajili ya mjadala, jibu ni kwamba Biden hana utetezi wowote kwa Wapalestina.
Tunachokiona ni kutafuta kura kutoka kwa '' Immigrant' katika majimbo muhimu ya uchaguzi kama Michigan.

Kura za awali za uchaguzi wa Democrats zinaonyesha Michaigan kuna kundi la asilimia takribani 13 ni 'uncommitted' likisukumwa na hali ya kisiasa mashariki ya kati. Hali ni Mbaya zaidi Minnesota ambako asilimia 19 ni uncomitted.

Kwanini tunasema hana msaada kwa Wapalestina
1. Biden amewapa Israel Mabomu yasiyo na shabaha ' precision' ambayo Israel imeyatumia kuua na kuua raia wasio na hatia. Idara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imethibitisha kwamba haiwezi kutumia mabomu hayo na mara ya mwisho yalitumika Afghanistan tena kwa idadi isiyofikia 10. Israel imepewa ya kutosha.

2. Biden ana uwezo wa kulizamisha Israel ifungue mipaka ili misaada ya kibinadamu ifike Palestina. Tofauti na hilo ameamua kurusha chakula kwa ndege kitu ambacho hakitoshelezi hata 1/10 ya matumizi bali kujikosha

3. Biden ametumia turufu ya Veto kuikingia kifua Israel ili isilazimike kusitisha mashambulizi kwa Raia.
Kwa maana kwamba Biden anarusha chakula kwa ndege, halafu anawapa Israel mabomu yasiyo na shabaha na kisha kukinga kifua UN.

Haya ni kwa uchache tu, yatosha kusema hana lengo la kuwasaidia Wapalestina hasa watoto na Wanawake.

Hata Waisrael wenyewe wanapinga mashambulizi yanayoendelea lakini Biden anacheza na akili za watu katikati ya misiba.

Kuhusu Wagonjwa kufia mlangoni, well, katika nchi za kibepari mambo yanakwenda yakiwa yemenyooka.
Inaweza kuonekana ni ukatili lakini tujiulize mfumo wetu wa Bima ya Afya upoje?
Kuna tofauti gani ya mgonjwa kufia mlangoni na Mzazi kule Mwanza kujiufungulia sakafuni na hata kufa akiwa juu ya baiskeli.
 
Kuhusu Wagonjwa kufia mlangoni, well, katika nchi za kibepari mambo yanakwenda yakiwa yemenyooka.
Asante sana Mkuu kwa ufafanuzi. Nitarudi Tena kwa ajili ya kupanua mjadala huu katika masuala ya multipolars inayoanza kupigiwa debe na "wanyonge".
 
Hii kwa jicho lingine inaonekana kama grand corruption of all time in US! Unafutaje deni kubwa namna hiyo lakini unashindwa kuwapunguzia deni la mkopo wanafunzi wako wa elimu ya juu? Ilisemwa kuwa kwa sasa Ukraine ndiyo nchi inaoongoza kwa rushwa duniani....! Kwa mazingira haya accountability katika mfumo wa undeshaji wa serikali ya US unatia mashaka makubwa sana.

Ebu fikiria wanafunzi wa elimu ya juu wa nchini Marekani wanadaiwa $1.6 trillion hadi kufikia 2024. Sasa hizi $4.7 bilion si zingefanikisha kupunguza huo uchungu wa $ 1.6 trillion kwa wanafunzi?
 
There is little Trump can do at this point besides speaking out forcefully and demanding that the Biden administration “stand down,” but “they have nothing to lose,” he added.

“They've already lost. It’s like someone diagnosed with a terminal illness; they’re willing to take risks they might not have taken before,” Johnson argued. “He's going to be removed from office anyway in two months. Why does he care? I mean, he’s like a suicide bomber at this point.”
 
In a statement issued on Sunday evening, the president argued that his son was prosecuted “selectively and unfairly” because of his familial ties. He claimed that “people are almost never brought to trial on felony charges solely for how they filled out a gun form.”

“It is clear that Hunter was treated differently,” he said. The president went on to state that the charges against his son were brought “only after several of my political opponents in Congress instigated them to attack me and oppose my election.” He blamed Republicans for sabotaging “a carefully negotiated plea deal” that would have been a “reasonable resolution of Hunter’s cases.”
====
Huu ndiyo Utawala Bora wanaotuhubiria. Utawala unaoingilia Mamlaka ya Muhimbili mwingine!!!

Hii ni bad precedence katika kuheshimiana mihimili Tena Kwa nchi kama Marekani inayojinasibu kwa demokrasia na Utawala Bora.
 
MGOGORO WA IRAN NA US

Hali katika mashariki bado ni tete na hainekani kuimarika katika siku za usoni
Mazishi ya Qassem, Kamanda wa kikosi cha mapinduzi yamefanyika nchini Irani

Umati uliojitokeza ni mkubwa kuwahi kuonekana katika miaka ya karibuni ukiachilia wakati wa kurejea kwa kiongozi wa kiislam Ayatollah Khomeni. Umati ulijawa na jazba ya kisasi

Kama tulivyowahi kusema si rahisi Iran kujibu mapigo kwa wakati huu wa mshtuko mkubwa.
Iran wanafahamu Marekani watakuwa wamejiandaa kukabiliana na kisasi chochote

Kwingine mashariki ya kati kama Lebanon, kauli za kisasi ndizo zilizotanda kumuadhimisha Qassem. Viongozi kama Nasrallah wa Hezbollah na makundi mengine wameapa kisasi

Hasira za watu zimeelekezwa kwa Israel pia ambayo nayo imesifu mauaji hayo
Inaeleweka shambulizi hilo limechagizwa pia na Israel inayotaka kuona Iran inapunguzwa nguvu

Israel inahofia kuwa nguvu za Iran katika mashariki ya kati zitaiweka katika wakati mgumu
Kwamba, makundi kama Hezbollah na Hamas yatapata nguvu licha ya Iran yenyewe

Nchini Iraq Bunge limeatoa azimio kwa majeshi yaMarekani kuondoka nchini humo
Marekani inajikuta katika wakati mgumu kimkakati.

Kuondoka Iraq kunapunguza nguvu za Marekani kimkakati (strategic position) kwasababu Iran na Iraq ni majirani, hivyo uwepo wa majeshi yake Iraq unafanya kazi kuwa rahisi .

Hofu ya Marekani ni kuwa kuondoka Iraq kutatoa nafasi kwa Shia wa Iraq kuungana na wenzao wa Iran, wale wa Qatar na kwingineko katika mashambulio dhidi ya Marekani kama ikitokea.

Rais Trump anatishia kuweka vikwazo Iraq, wachunguzi wanasema hilo litaileta mashariki ya kati karibu zaidi kwa kuwa na ''adui'' mmoja kwa wote

Marekani isingependa kwenda vitani na Iran kutokana na funzo la Iraq.
Hofu kubwa ni kuhusu mihemuko ya Rais Trump anayeweza kuamua jambo bila kufikiri

Iran sasa imejitoa katika nuclear deal na nchi za Ulaya ingawa inasema ipo tayari kuzungumza
Shambulio la Qassem limewapa nafasi (upper hand) katika majadiliano na nchi za Ulaya

Lengo na mkakati wa Marekani ni upi? Je, leo baada ya Qassem ipo salama kuliko jana?

Tusemezane

Turejee mabandiko ya nyuma yaliyoelezea mtifuano wa mashariki ya kati (Israel-US vs Iran)
 
Nguruvi,
Nimekuwa nikiifuatilia Iran from time to time tangu 2011 au 2012 walipoweza kudungua ndege mbili zisizo na rubani za Israel ambazo kwa kawaida hazionekani kwenye rada, halafu baadae waliweza kui divert na kuishusha drone ya Marekani ikiwa nzima baada ya kufanikiwa ku intercept mawasiliano yake. Ninachokiona japo sina hakika kama niko sahihi ni kuwa:
1. Iran wameendelea sana kijeshi japo si kiasi cha kuishinda Marekani au Israel lakini yeyote atakayejaribu vita na Iran atapata ushindi wenye majuto makubwa na ya muda mrefu. kwa maana nyingine huyu ni mbabe anayekuwa kwa haraka sana mashariki ya kati na ni tishio kwa Marekani, Israel na washirika wao kama Saudia.
2. Rais Trump anafahamu vikwazo vya tangu 1979 havikufanikiwa kuidhoofisha Iran kiasi cha kushindwa vita kwa urahisi. Na anafikiri labda katika utawala wake atumie njia zozote kuhakikisha anauondoa utawala wa kiislam ili mbabe abaki Israel peke yake. lakini si kuuondoa tu bali kuruhusu makundi ya kigaidi ambayo yatahakikisha Iran haitulii kama ilivyo Iraq, Syria na Libya.
3. Inafahamika kwamba tangu kabla ya 2010 Israel imekuwa ikiishinikiza Marekani iishambulie Iran, lakini Marekani siku zote imesita kufanya hivyo. Hofu ya Israel ni maendeleo ya technologia ya Iran ambayo huenda ikaisumbua Israel baadae.
4. Siamini kama kweli Trump alitaka kumuua Soleiman halafu iishie hapo. nadhani anatafuta sababu za kuanzisha vita na Iran ili apate fursa ya kuisambaratisha Iran na kisha kuweka kibaraka wao.
5. Baada ya mashambulizi ya Iran hakujatolewa habari za uhakika kuhusu madhara ya mashambulio hayo, lakini swali la msingi ni je mfumo wao kutungua makombora wa Marekani kwa nini haukutumika? au tuseme haukugundua makombora yote 22?
6. Iran imechokezeka. na huenda Trump akatumia mwanya huu kucheza kamari na Iran. Kamari ambayo haitabiriki.
mwisho nimekuwa nikivutiwa sana na diplomasia ya Iran ikiongozwa na Zariff, laiti dunia ingekuwa inamsikiliza huenda mashariki ya kati pangekuwa salama.
Kamili aliandika haya!
 
Kamili Iran ni mbabe wa muda mrefu. Kilichomzuia ni uwepo wa kibaraka wa Marekani Mfalme Shah.
Baada ya 1979 Imam Khomeni alijaribu kuibadilisha Iran na kuirudisha katika ubabe.

Vita ya Iraq na Iran ilichagizwa sana na Marekani na hasa Israel.
Baada ya msaada wa mafunzo Saddam akawageuka Wamarekani na kuwa tishio kwa Israel
Kilichofuata ilikuwa kumtafutia sababu na kwa bahati mbaya Saddam akaingia katika mtego.

Baada ya Saddam ambaye unakumbuka alituma Qasam kule Israel, Iran ilichukua ukanda.
Tofauti na Iraq, Iran inawekeza sana katika elimu siyo ya jeshi hata sayansi na teknolojia.

Angalia popote duniani, Shia ni wazuri sana katika mambo ya kielimu ukilinganisha na wenzao kama Sunni au Sufi.

Iran wametumia uwezo wao wa fedha kusaidia makundi yanayohusiana nao na kujitanua sana mashariki ya kati. Jambo hilo limetia hofu mataifa mawili, Israel na Saudi Arabia.

Israel inaona makundi kama Hezbollah na Hamas yanayopata ufadhili wa Iran ni tishio kubwa.
Vita ya Israel na Lebano ya Imam Nasrallah miaka 10 iliyopita ili ieleza Israel kuna tatizo.

Jitihada za Israel ni kutaka kuona Iran inasambaratishwa na hasa suala la Nuclear
Kama unafuatilia nyuzi zetu tumeeleza mara nyingi, Marekani ilikuwa inatafuta sababu za kumpiga Iran si kwasababu ni tishio bali ''maagizo'' ya Israel

Saudia ina hofu kwamba kujitanua kwa Iran ni kuruhusu Shia kutawala mashariki ya kati.
Hofu siyo Shia kutawala maeneo ya Sunni, bali ushawishi wa Shia dhidi ya Saudia Kingdom.
Wasi wasi wa Saudia si kwa masilahi ya Sunni au makundi mengine, ni masilahi ya Kifalme.

Kwa kuelewa hilo, Wasaudia ambao miaka dahari wameongoza jamii ya Waislam dhidi ya Israel wamengana na Israel ili kumkabili Iran. Haya si kwa amasilahi ya dini ni kwa kulinda Kingdom tu.
Saudia wamewatosa Wapalestina kwasababu tu ya kulinda ufalme.

Kwamba Israel ina nguvu, kuna hoja mbili. Israel wana utalaamu na teknolojia ya juu sana.
Kijiografia, ukubwa wa eneo na population Israel hana nguvu kwa Iran bila msaada wa Marekani. Ndiyo maana Israel wanataka Iran ashambuliwe, wao wenyewe hawasimami .

Kwamba, Iran imeendelea hilo halina mjadala. Wana teknolojia na utaalam sana hasa ukizingatia wapo katika vikwazo kwa miaka zaidi ya 10.

Bandiko hili liliandikwa January 20 , 2020 na kila kinachotokea sasa hivi kilielezwa hapa

Tulieleza nguvu ya Iran isiyoonekana, kwamba, Israel au US wanaweza kushambulia lakini watakumbana na upinzani mkali. Ndicho kinachotokea

Katika mabandiko tulieleza Utaalam walio nao SHIA wa Iran na kwamba si wa kubezwa.
Tulieleza lengo la figisu za Nuclear si uwepo wa silaha bali sababu za kumshambulia Iran.

Lipo bandiko linaloeleza Israel kupiga Hospitali wakati wakipigana na Hamas,. Tulieleza kwamba suala hilo litairudi Israel, Marekani na Nchi za magharibi mbele ya safari. Well, leo kombora la Iran limetua karibu na Hospitali. Israel inalalama wakisahau jinsi Israel ilivyovuruga Hospitali za Gaza kwa makusudi ili kuua Wapalestina. Katika moja ya ukatili, Israel walipiga bomu mitambo ya Oxygen kisha kuzima jenerata.

Leo imekuwa siku ngumu sana kwani Nchi za Magharibi zilizokubali Israel kupiga Hospitali huku zinaongelea uvunguni Hopsitali ya Israel kupigwa. Hiyo ndiyo kanuni ya asili isemayo '' what goes around comes around''

Nchi za magharibi zinaonyesha Israel inavyoshambulia Iran, jhazionyeshi kifusi kilichotokea Tel Aviv.
Nchi hizo zinaaminisha watu kwamba anayeonewa ni Israel (victim) na si aliyeshambulia. Hili ni kutengeneza uhalali wa kuishambulia Iran.

Je, Israel ilifanya uamuzi wa busara au ilikuwa hesabu fyongo! tutajadili
 
MASHARIKI YA KATI

ISRAEL IMEVURUGA NA KUVURUNDA! HASIRA ZA MKISI ....


Rejea uzi huu kuanzia mabandiko# 30 kuendelea tulipo ongelea hali ya mashariki ya kati

Tumeeleza ugumu wa siasa za eneo hilo zikitawaliwa na makundi ''secretarians'' si kwa Waarbu na Waajemi bali pia kwa Waisrael pia. Mathalani, watu hawana ufahamu juu ya uwepo wa Israelite, Jews na Zionists.

Vita inayoendelea Gaza imeiweka Israel katika wakati mgumu sana tofauti na ilivyodhani. Ni siasa za mid east !

Turudi nyuma kwa ufupi. Kwanza aliondolewa Saadam Hussein kwa kusingiziwa silaha za maangamizi.
Ushahidi usio na shaka wa video unaonyesha ilikuwa mission ya BB Nyahu miaka 25 iliyopita.

Akaondolewa Ghadaffi kwa sababu ya ' Spring revolution' lakini haikuwa hiyo, Ghadaffi alituhumiwa kutengeneza silaha na kosa alilofanya ilikuwa kukubali kuacha matengenezo. Ushahidi US na Israel ziilichochea Waasi

Marekani ikamuua kamanda wa Majeshi ya Iran Gen Qaseem lakini waliotekeleza mpango ni Israel

October 7 Hamas wakashambulia Israel na hiyo ikawa fursa ya Israel kuivuruga Gaza.
Hata kabla ya Oct 7 Wapalestina waliuawa kwa mashambulizi ya Israel, si sahihi kusema hali ilikuwa shwari kabla

Israel ikamuua kiongozi wa Hamas, Ismail Haniya akitokea Qatar kwenda Tehran kwenye mazishi ya Rais wa Iran Bwan Rahis. Iran ikajibu kwa kutumia drone kwa shambulizi lisilokuwa la Vita.Ni shambuli hilo liliwapa Israel kiburi kwamba Iran ni dhaifu kwasababu ilitumia drones tu bila madhara

Israel ikaona ni fursa ya kuwashambulia Hezbollah kwa kutumia electronics kinyume na matakwa ya umoja wa Mataifa. Hilo likaachwa lipite kama lile la Israel kuua kiongozi wa Hamas akiwa Falme za Kiarabu UAE kwa kutumia passport za UK, Australia n.k.

Israel ikaona kuna firsa nyingine ya kumuodoa Asaad wa Syria. Israel na Marekani wakawatumia magaidi kumshambulia Asaad aliyekuwa msaada wa Iran. Wakamuondoa

Lakini pia Israel ilisha shambulia Ubalozi wa Iran nchini Syria na kuua makamanda wa Iran. Iran haikujibu

Israel ikaona Hezebollah ni dhaifu, Asaad kaondoka, Ghadaffi hayupo, Saadam hayupo ilikuwa mwafaka kumshambulia Iran. Israel kwa msaada wa nchi za mgharibi wakatekeleza shambulio dhidi ya vinu vya Nyuklia.

Iran ikajibu mapigo kwa namna isiyotarajiwa ikawalazimu Israel waombe msaada wa Marekani kumaliza vita

Hayo yakiendelea vita ya Ghaza ilikuwa inaendelea watu wakifa kwa mabomu na njaa!
Waandishi wa habari wakiuawa na kuzuia misaada yote kufika kwa Wapalestina.

Majuzi, Israel ikashambulia Qatar ikitaka kuua viongozi wa Hamas wanaoshiriki mazungumzo ya amani

Shambulio la Qatar limebadili siasa za mashariki ya kati kabisa zikiunganisha makundi na kuiweka Israel na Marekani katika wakati mgumu sana. Tutaeleza ni kwa vipi bandiko lijalo

Itaendelea
 
MASHARIKI YA KATI

Israel ilivyojichanganya.... kutoka bandiko # 74

Shambulio la Israel kule Qatar limebadili mwelekeo wa siasa za mashariki ya kati. Kabla ya shambulio Israel ilikabiliwa na shinikizo la Kimataifa kwa kuzuia misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula na kupelekea vifo

Mataifa ya Magharibi yali ionya Israel kwamba yataitambua Palestina kama 'state'' ikiwa itaendelea na ukiukaji wa haki za binadamu. Wiki hii mataifa hayo mbele ya UN yametangaza kutambua Palestina isipokuwa Marekani.

Shambulio la Qatar likiwalenga viongozi wa Hamas waliokwenda kujadili makubaliano limeonyesha kwamba Israel haina nia ya kusitisha mapigano. Shambulio lilichukua sura ile ya lile la Iran ambako viongozi wake waliokuwa wanajadili mkataba wa Nyuklia waliuawa kwa wakati mmoja. Coincidence?

Qatar ni msuluhishi wa yanayohusu mashariki ya kati lakini pia kituo kikubwa cha anga cha Marekani.
Ni kile kituo kilichorushiwa makombora na Iran. Ingawa haisemwi , kombora la Iran liliharibu ''radar' za kambi hiyo ikiwa ni ishara ya usahihi wa makombora yake

Shambulio la Qatar limeziamsha nchi za kiarabu. Maswali wanayojiuliza, ilikuwaje Israel ikashambulia Qatar bila Marekani kujua ikiwa kuna kituo kikubwa cha anga? Jibu linajieleza. Swali la pili, ikiwa Israel inashambulia kila nchi bila kuchukuliwa hatua nani yupo salama? Iran, Qatar, Yemen, Tunisia, Lebanon, Syria n.k. wameshambuliwa

Nchi za kiarabu zinaanza kuelewa kwanini Iran ilijibu mashambulizi ya Israel. Pakistani iliunga mkono Iran wakati huo, nchi za Saudi Arabia, Jordan na vituo vya Marekani Iraq vikisaidia kutungua makombora ya Iran

Hali baada ya shambulizi la Qatar imebadilika, nchi za kiarabu zenye ''military base'' zimeiambia Marekani isitumie vituo ndani ya nchi zao kushambulia nchi nyingine. Hii maana yake ni moja, kwamba vituo hivyo havitakuwa na msaada kwa Israel

Katika vita ya Israel-Iran, Waisrael walitumia vituo vya Cyprus kwenye British military base, Saudi Arabia, na Iraq kushambulia Iran.

Waarabu wanaungana, kuna mkataba wa Pakistan na Saudia wenye kipengele cha '' shambulio kwa mmoja ni shambulio kwa wote''. Nchi za kiarabu zinaanza kuwaelewa Iran na kurejesha mahusiano yao.

Marekani inatambua hali ilivyo, vituo vikiondolewa nafasi itachukuliwa na Russia au China na Marekani haitakuwa na ushawishi mashariki ya kati kijeshi.

Ni kwasababu hizo, Rais Trump kwanza ameikataza Israel isichukue west bank ya Palestina.
Pili, Trump amekutana na viongozi wa nchi za kiarabu na tatu, Rais Trump anakwenda mashariki ya kati kuweka mambo sawa

Israle imetengwa na jamii ya kimataifa kutokana na yanayoendelea Ghaza. Israel imetoa ''ushindi'' kwa Hamas kwasababu licha ya kupoteza watu na mali, katika hali ya kuchukizwa Mataifa mengi yakiwemo ya Magharibi yameitambua Palestina na kuiacha Marekani peke yake.

Na kwasababu ya hasira za kushambulia hovyo, Israel ilipopiga Qatar imewaleta Waarabu pamoja na si kwa afya ya taifa hilo. Na tano Marekani kwa kuangalia masilahi yake inaanza kuitosa Israel kwenye senate, congress na jamii kwa ujumla.

Ndio maana tunasema hasira za mkisi.. Israel imepoteza kwasababu ya hasira ! Mazungumzo sasa si Hamas ni Israel na yanayoendelea. Kutambuliwa Palestina ni hatua kubwa na ya kutisha kwa upande wa Israel.
Vita na Iran imeonyesha udhaifu wa IDF na Mossad kinyume na iivyofikiriwa.
 
MASHARIKI YA KATI
ISRAEL YAIOMBA RADHI QATAR

Waziri mkuu wa Israel bw Nyahu alikutana na Rais Trump white house kujadili mwenendo wa mashariki ya kati.

Hii ni ziara ya 4 mwaka huu kwa BB Nyahu nchini Marekani. Sijambo la kushangaza kwa nchi hizo kwani masuala ya vita wanayaendesha pamoja. Israel inategemea sana Marekani kidiplomasia kama kura ya VETO na Silaha kali.

Serikali ya Israel haifnyi jambo bila kupata idhini ya Marekani, ndio maana wachunguzi wa mambo wanajiuliza ilikuwaje Israel ikashambulia Qatar bila idhini ya Marekani na iliwezaje kuingia anga lenye vituo vya Mareakani

Hata hivyo kwa hasira za Marekani kuhusu Qatar imemlazimu BB Nyahu aombe radhi Qatar.
Sababu ni kama zilivyoelezwa bandiko #75 na zizonamlazimu Rais wa Marekani aende mashariki ya kati kuzima moto. Wiki moja iliyopita Nyahu aliongea kwa kiburi kwamba atawafuata adui zake popote walipo

Hii pia inaeleza kwamba hata Marekani imeanza kuchoshwa na maamuzi ya Israel yanayohatarisha masilahi mapana ya Marekani mashariki ya kati.

Israel imeingia katika mzozo na nchi ya China jambo lisilo la kawaida. Israel ipo katika ugomvi na Spain na Italy miongoni mwa Mataifa yasiyotegemewa zikiwemo Brazil, Argentina, Columbia, Korea n.k.

Je Marekani itafanikiwa kurudisha mahusiano yaliyovurugwa na Israel Mashariki ya Kati?
 
HALI TETE MASHARIKI YA KATI
VITA YA IRAN NA ISRAEL PENGINE IKAIHUSISHA MAREKANI

Vita ya siku 12 kati ya Israel na Iran imebadilisha suwiano wa nguvu za kijeshi eneo la mashariki ya kati
Marekani ya Trump ililazimika kusitisha vita, kwamba makombora ya Iran yaliilemea Israel

Israel ilifanya makosa ya kiitelejensia, Waziri mkuu Nyahu amekiri hivyo. Kwamba, nguvu za Iran zilikuwa katika 'drones' pengine na makombora machache yasiyo na nguvu.

Kosa la pili ni kudhani anguko la Bashir wa Syria na ku uwawa kiongozi wa Hezbollah kumedhoofisha muungano wa '' axis of resistance'' ukiongozwa na Iran. Israel iliona ni fursa nzuri ya kumaliza na Iran

Makadirio mabaya bila kujali uwezo wa akili (IQ) ya Waajemi ulipelekea Marekani kusitisha vita.
Mfumo wa anga wa Israel ukiongozwa na Iron dome, ikisaidiwa na David sling na Arrow vilishindwa kudhibiti makombora mazito ya Iran. Maeneo yote nyeti ya Israel yalipigwa ikiwemo kambi ya anga ya Nevatim air base

Marekani ikiisadia Israel ilishambulia vinu vya Nyuklia. Katika kuonyesha ina uwezo, Iran ilipiga kambi ya Qatar tena ikiwa imetoa taarifa ya mpango mzima( Televised). Kitu wengi hawakifahamu ni uwezo wa shabaha za makombora uliopiga radar ya Marekani kule Qatar, ikiashiria usahihi wa makombora (precision)

Nchi za Saudi Arabia, Jordan, Iraq , UK na France zote zilishiriki kwa namna moja au nyingine kuisadia Israel.
Uwezo wa makombora ya Iran yanayosemekana ni ya miaka mingi umeitisha sana Israel

Israel inamtaka Marekani na Washirika wa Magharibi waweke masharti si ya Nuclear tu bali kuizuia Iran isiwe na makombora yanayozidi KM 300 au kwa lugha nyingine yasiyoweza kufika Israel.

Israel inahofu kwamba kinu cha Nuclear hakikufumuliwa na urutubishaji wa madini ya Uranium kutengeneza bomu la Nuclear unaendelea Iran. Tatizo linaloisumbua Israel na Marekani ni kukosa taarifa za ndani

Wakati wa makubaliano ya JCPOA '' wasimamizi' wa Kimataifa ambao waliwemo makachero wa Israel na Marekani walipeleka habari ikiwemo majina ya wataalamu wa Nuclear na maeneo wanayoishi.
Ni kwa msingi huo Israel ilifanikiwa kuua Wataalam wa Nuclear na Makamanda kwasababu walikuwa na taarifa

Israel imeisukuma Marekani ipigane vita na Iran . Rais Trump ana wasi wasi kwamba shambulio dhidi ya Iran litapelekea machafuko mashariki ya kati na kuuingiza Marekani.

Trump ali kampeni kupinga vita. Kubwa zaidi ni kuhofia uwezo wa Iran hasa makombora yanyoweza kuiabisha

Kuna kutofautiana mawazo kati ya Trump na Ben Nyahu wa Israel. Marekani inataka majadiliano na Iran, Israel inasema la hasha lazima washambuliwe. Israel insisitiza, kipaumbele si Nuclea ni makombora (Missile)

Iran imetambua mgawanyiko huo na inasema suala la makombora halina mjadala, na kwamba ipo tayari kupigana. Marekani inakabiliwa na tatizo, kwamba, Iran inasema itapiga yoyote atakayesaidia mashambulizi.
Nchi nyingi zinasita!

Kwanini kuna vitisho vya Marekani na Iran ?

Inaendelea
 
HALI TETE MASHARIKI YA KATI
ISRAEL INAIVUTA MAREKANI KATIKA VITA

Vita ya siku 12 kati ya Israel na Iran imebadilisha uzani wa nguvu za kijeshi ''balance of power'' mashariki ya kati
Iran i ilifanya kile wengi walidhani hakitatokea, kuipiga Israel katika maeneo nyeti ya kijeshi kwa usahihi

makombora ya Iran yalifika kila mji au jiji la Israel. Kwa eneo la Israel hilo ni tishio kubwa sana kiusalama.
Inafahamika jeshi la Israel (IDF) kitengo cha Jeshi cha ujasusi (military intelligence)m kitengo cha ujasusi cha nchi (MOSAD) ni vitengo vikali, hata hivyo, Iran ilipenya na kukusanya taarifa kinyume na matarajio ya Israel.

Jaribio la Israel la kuvunja vinu vya Nuclear halifanikiwa, msaada wa Marekani kuvunja vinu haukufanikiwa pia.

Israel ilifanikiwa kuishambulia Iran kwasababu nyingi zikiwemo;
Kwanza, kushtukiza wakati Iran ikitambua Israel haina uwezo wa kuifikia bila kufikiri kwamba Marekani ipo nyuma.

Ndege za kujaza mafuta angani zilizotumika zilikuwa za Marekani. Kwa lugha nyingine, Iran walikuwa ''off guard'' kwa matarajio ya kuona maandalizi kabla ya kushambuliwa

Pili, makubaliano ya Iran na Nchi za magharibi ( JCPOA) yaliruhusu waangalizi wa kimataifa kukagua maeneo ya Nuclear kuona Iran haikiuki mkataba. Wakaguzi walikuwa makachero wa Israel , Marekani , UK na France.

Pamoja na kukusanya habari, wakaguzi walipata majina ya Wanasayansi nguli. Hili liliwezesha kuuawa kwa wakati mmoja kwasababu Israel ilijua kila mmoja anapoishi

Nne, Israel ilipenyeza makachero kwa kutumia wafanyakazi wa kigeni kutoka nchi jirani kama Pakistani waliotoa habari muhimu. Hujuma za za kulipua ulinzi wa anga zilifanywa na watu wa ndani kama mawakala wa MOSAD

Kwa wakati huu hali ni tofauti, Iran imepitia kila kosa na kulifanyia marekebisho.
Hili limeiweka Israel katika wakati mgumu wa kusimama katika vita na Iran hivyo kuiomba Marekani iingilie kati.

Israel imewapa Wamarekani masharti magumu sana kama watakubaliana na Iran.
Kwamba, Iran isiwe na Nuclear kabisa hata ya matumizi ya kawaida( Zero enrichment). Pili, Iran isiwe na makombora yanayozidi KM300, Iran iache kuunga mkono vikosi kama Hezebolla, n.k.

Masharti yanalenga kufanya mazungumzo kati ya Iran na Marekani kushindikana.
Iran inasema suala la makombora halijadiliki. Kwamba kwanini izuiwe wakati nchi jirani kama Turkey zina makombora ya masafa. Kwamba, isizuiwe kurutubisha Nuclear kwa matumizi ya kawaida.

Kwa ugumu wa majadiliano, Trump anaweka nguvu za kijeshi kama kuitisha na kuishinikiza Iran.

Nyuma ya pazia Trump hataki vita wakati BB Nyahu anataka Iran ishambuliwe.
Trump anahofia madhara ya vita mashariki ya kati na vifo vinavyoweza kutokea kwa askari wake.
Wananchi wa Marekani wamechoshwa na vita isiyowahusu

Kwa hali ilivyo vita haiepukiki , Iran haiwezi kukubali yale ya Ghadafi wala kukubali isiwe na silaha ili Israel iishambulie. Vita ikitokea Israel haitakuwa salama kwasababu Iran inajua si vita ya Marekani, ni ya Israel

Itaendelea..
 
Back
Top Bottom