Duru: Matukio na habari za Dunia

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
14,869
Points
2,000

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
14,869 2,000
Riot police members block Yellow vests protesters near the Champs Elysees avenue in Paris on December 8, 2018 © AFP
French police fired the first batches of tear gas on Saturday as massive crowds of Yellow Vest protesters swarmed into the heart of the capital on the 4th weekend of unrest. Hundreds were detained prior to and at the rally.
The figure was announced by Prime Minister Edouard Philippe. According to him, 481 people were detained by police and 211 remain in custody
====
Ufaransa inawaka 'moto'. Kauli ya Macron kuwa EU itengeneze Jeshi lake yaweza kumgarimu! US wana mbinu nyingi za kuwashughulikia wanaokwamisha maslahi yake.
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
14,869
Points
2,000

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
14,869 2,000
1544292926083.png
DW.com
More than 30 people were injured during clashes with police on Saturday in Paris

15:09 Turkish President Recep Tayyip Erdogan has hit out at the "excessive force" used against protesters in Paris."Those who accused our police of oppression should see what their [French] police are doing now," he told supporters in Istanbul. The "scenes of chaos" show Europe has failed "the test on democracy, human rights, and freedom."
===
Polisi wa Ufaransa nao wameanza kutoheshimu haki ya kuandamana.
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
14,869
Points
2,000

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
14,869 2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,479
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,479 2,000
JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
HATUA ZISIPOCHUKULIWA JUMUIYA ITAVUNJIKA

Awali ya yote niwatikie heri ya Mwaka mpya tukishukuru kwa mjaliwa ya kuuona

Katika habari zilizopuuzwa ni kuhusu kuahirishwa mara mbili kwa mikutano ya waku wa jumuiya ya A.Mashariki
Sababu kubwa zinatokana na nchi za Burundi na Rwanda kutokuwa katika utengamano

Historia ya EAC inajulikana kuanzia miaka ya 1927 hadi 1967 na kifo chake 1977 kisha kuzinduliwa tena
Nchi wanachama kwa muda wote zimekuwa ni Tanzania, Kenya na Uganda

Kuijenga upya EA marais walioshiriki ni Moi, Mwinyi na Mseveni
Kwa muda wote jumuiya imekuwa ikiendelea vizuri hatua kwa hatua

Wazo la kuongeza Rwanda na Burundi lilikuwa na shinikizo kutoka Uganda huku Tanzania ikilaumiwa kutolikubali

Watanzania wengi walieleza kupitia maoni na tume kuwa nchi hizo zinaweza kuwa tatizo mbele ya safari

Hoja kubwa ya Watanzania ilikuwa, Rwanda na Burundi si nchi zenye utangamano na bado zina migogoro

Uwepo wao ndani ya jumuiya utaondoa maridhiano na kuirudisha jumuiya nyuma

Kwa haya yanayoendelea ni Tanzania ilikuwa sahihi kabisa.

Uwepo wa Rwanda na Burundi sasa unatishia suala zima la utangamano miongoni mwa wanachama kiasi kwamba ada za kuendesha jumuiya na hata ushiriki vimekuwa ni tatizo

Haitegemewi katika hali kama hiyo jitihada za kuiunganisha jumuiya zitazaa matunda
Ikiwa wakuu wa nchi hawawezi kukutana, ni vipi tunaweza kuongelea umoja wa fedha, forodha na ushuru?

Ni kwa mantiki hiyo viongozi wa nchi kuu zinazounda jumuiya, kwa maana ya Tanzania , Kenya na Uganda wanapaswa kuchukua hatua za lazima na za dharura kuiepusha Jumuiya na dhahma inayoinyemelea

Moja ya hatua hizo ni pamoja na kusimamisha uanachama wa Rwanda na Burundi hadi zitakapomaliza matatizo au zitakapokubaliana na usuluhishi kutoka ndani ya Jumuiya

Hatua hiyo itapeleka ujumbe mahususi kuwa Jumuiya ya Afrika mashariki inaweza kusimama na wanachama wake wa asili na kwamba wanaoomba kuingia wasichukulie fadhila hiyo kama haki bali fursa

Tusemezane
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
14,869
Points
2,000

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
14,869 2,000
Arrest of Yellow Vest leader Drouet slammed as ‘abuse of power’ & ‘dictatorship’
====
West hawawezi tena kutufundisha democracy, utawala bora, uhuru wa kutoa maoni na mambo mengine kama hayo. Ufaransa imetoa mfano mbaya. Kwa kuwa Ufaransa ni mmoja wa mataifa ya EU na EU haijatoa tamko la kuionya Ufaransa basi kwa tafsiri ya kawaida EU imeonyesha rangi zake halisi kupitia matendo yanayofanywa na madikteita wa Ufaransa dhidi ya raia wanyonge wa Ufaransa (wanavizibao vya njano).
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
14,869
Points
2,000

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
14,869 2,000
Si kulitendea haki jukwaa na hasa uzi huu ,kwa kukaa kimya juu ya mazungumzo aliyofanya Mh. Lissu ,ambaye amesema bado anaumwa, na Steve wa Hardtalk.

Binafsi nimesikiliza clip nzima ya mazungumzo yale. Kwa kifupi, kwenye mazungumzo yale nimemkosa Mh. Lissu wa kutoa majibu yenye ukweli unaoambatana na ushahidi husiyotiliwa shaka. Nimejikuta namtazama Mh. Lissu niliyewahi kumueleza mwanzo humu jamvini yaani mfanya uanasheria wa kiharakati na si mfanya uaharakati kisheria.
===

 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
14,869
Points
2,000

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
14,869 2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,479
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,479 2,000
MAALIM SEIF AHAMIA ACT
CUF YAFIKIA HATMA YAKE KAMA NCCR NA WENZAKE

Baada ya tukio la Mh Lowassa kurejea nyumbani CCM tukio lingine la kisiasa lililotanda ni kwa Maalim Seif, kiongozi wa CUF kuhamia chama cha ACT Wazalendo

Tukio hilo lina maana nyingi kimfumo wa utawala na kisiasa

Ni wazi kuwa kuhama kwa Maalimu kunahitimisha matamanio ya kurejea Ikulu kufuatia uchaguzi uliokuwa na utata wa mwaka 2015 ambao CUF wanadai kushinda na kuporwa ushindi

Kwa upande wa CCM kuhama kwa Seif kumetoa nafasi ya muda kufuatia hofu ya shinikizo la kimataifa kuhusiana na uchaguzi. Lengo la CCM na serikali yake ilikuwa kuivuruga CUF
Kwasasa CUF ya Lipumba haitaweza kuwa na madai yoyote kufuatia uchaguzi wa 2015

Mbinu za CCM na serikali yake hazikufanikiwa kisiasa bali kwa kutumia nguvu nyingine
Uwepo wa mgogoro wa CUF ulishadidiwa sana na CCM kama njia ya kuipunguzia CUF kasi

Tumeshuhudia Bungeni kwa msajili wa vyama na kwingineko kukiwa na kila shaka ya kia jambo
Mkutano wa juzi wa CUF kukiwa na suala mahakamani kunaeleza kitu zaidi
Katika mazingira ya kawaida haikuwa sahihi, katika mazingira maalumu iliwezekana

Mh Lipumba aliungwa mkono katika kila hatua ikiwa ni sehemu muhimu ya mpango
Kwa ufupi tatizo la CUF halikuwa kubwa limekuzwa na wala halikupaswa kwenda mahakamani

Lakini pia kwa upande mwingine, Maalim Seifa anapaswa kujilaumu kwa kutoa nafasi ya kushambuliwa. Baada ya Lipumba kujiuzulu taratibu za kiofisi zingefuatwa hali isngekuwa ilivyo

Hili ni somo kubwa kwa vyama vya siasa, kwamba, mambo yaende kisheria. Katika hali isiyokuwa ya kawaida makosa hayo yanajirudia rudia na kutoa nafasi ya ''kushambuliwa''

Swali lililobaki kwasasa, ni je, mwendo wa Maalimu ni sahihi na kwa wakati sahihi?

Inaendelea...
 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,479
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,479 2,000
Sehemu ya II, MAALIM SEIF

Katika sifa za uongozi , weledi pekee haumfanyi kiongozi kupewa madaraka.
Kuna kitu kinaitwa ''charisma' kwa kiswahili cha mitaani kimeazima na kuita kisimati

Kuna watu wanazaliwa wakiwa na haiba ya uongozi. Hawa huwa na kitu hicho cha charisma
Yaani wanapendwa tu kwa busara zao lakini pia wanapendwa tu

Maalim Seif ana charisma, kwamba, anapendwa tu na wafuasi wake na humwamini kile anachosema. Hicho ndicho kimempa sifa ya uongozi wa upinzani katika mazingira magumu

Imekuwa rahisi Maalim kupata ''taarifa' zote kwani hata ndani ya mahasimu wake wapo wanaopenda haiba yake kwa jicho la charisma. Wapo serikalini wapo ndani ya CCM

CUF ilisimama kwa charisma ya Maalimu Seif. James Mapalala, Hamada Rashid na wengine hawakuweza kumhujumu kwasababu Maalim ana charisma ambayo wao hawanayo

Ni kwa jicho hilo, ni dhahiri shahiri chama cha wananchi CUF kimefikia hatma siku ya leo

Lipumba hana charisma na siyo 'natural leader''. Uwepo wake unategemea nguvu nyingine

Kitendo cha Maalim kuondoka masaa machache baada ya hukumu ya mahakama hakikuwa cha bahati mbaya. Maalimu alikuwa na plan A,B,C na D mkononi.

Plan A; ni hiyo ya mahakamani aliyoiona kama bahati nasibu hasa katika nyakati tulizo nazo

Plan B; Seif alitambua kuendelea na shauri kutatoa nafasi ya kupitisha muda kuelekea uchaguzi na lingetoa nafasi ya sheria ya vyama vya siasa ikumbana kugombea popote

Kumbuka sheria ya Msajili na muda wa uanachama na uongozi

Kwahiyo alifikiria kuwa katika chama kipya ndani ya miaka 2 ili kukwepa kikwazo

Plan C; Maalim aliona kuhamia chama kama Chadema kutazua mtanziko ''tension' kuhusu uongozi na huenda kikawa kikwazo kingine hasa kwa kuzingatia yaliyotokea kwa Lowassa

Kahiyo Seif aliiona nafasi yake ndani ya CDM inajadilika na si ''guarantee''
Hilo ndilo lilimpeleka ACT Wazalendo ambako uhakika katika uongozi upo

Plan D; Maalim anafahamu CUF ya Lipumba itatumika kwa ruzuku za Bunge.
Kwa mantiki hiyo Wabunge wa CUF wataendelea kuwepo, muda si mrefu wataachia ngazi na kumwacha Prof mwenyewe.

Prof ''atawezeshwa'' lakini si kwa kiwango kile kwavile kazi yake imekwisha

Kwacharisma ya Seif, kutakuwa na wimbi kubwa sana la wanachama watakaomfuata

ACT Wazalendo itaimarika sana kwa gharama ndogo ya kifo cha CUF

Hili litakuwa tatizo jingine kwa CCM,sasa itahangaika na mahasimu wawili, CUF na CDM.

Ndiyo maana tulisema mkakati uliotumiwa na CCM na serikali yake ni wa kutuliza maumivu si kutibu ugonjwa

Kisiasa Maalimu Seif anaijua hadhra yake, ana uwezo wa kusoma mazingira kwa wepesi na kwa kina. Ukichanganya na charisma yake, alichofanya ni 'smart move'

Tusemezane
 

kamili

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2011
Messages
950
Points
500

kamili

JF-Expert Member
Joined Feb 10, 2011
950 500
Sehemu ya II, MAALIM SEIF

Katika sifa za uongozi , weledi pekee haumfanyi kiongozi kupewa madaraka.
Kuna kitu kinaitwa ''charisma' kwa kiswahili cha mitaani kimeazima na kuita kisimati

Kuna watu wanazaliwa wakiwa na haiba ya uongozi. Hawa huwa na kitu hicho cha charisma
Yaani wanapendwa tu kwa busara zao lakini pia wanapendwa tu

Maalim Seif ana charisma, kwamba, anapendwa tu na wafuasi wake na humwamini kile anachosema. Hicho ndicho kimempa sifa ya uongozi wa upinzani katika mazingira magumu

Imekuwa rahisi Maalim kupata ''taarifa' zote kwani hata ndani ya mahasimu wake wapo wanaopenda haiba yake kwa jicho la charisma. Wapo serikalini wapo ndani ya CCM

CUF ilisimama kwa charisma ya Maalimu Seif. James Mapalala, Hamada Rashid na wengine hawakuweza kumhujumu kwasababu Maalim ana charisma ambayo wao hawanayo

Ni kwa jicho hilo, ni dhahiri shahiri chama cha wananchi CUF kimefikia hatma siku ya leo

Lipumba hana charisma na siyo 'natural leader''. Uwepo wake unategemea nguvu nyingine

Kitendo cha Maalim kuondoka masaa machache baada ya hukumu ya mahakama hakikuwa cha bahati mbaya. Maalimu alikuwa na plan A,B,C na D mkononi.

Plan A; ni hiyo ya mahakamani aliyoiona kama bahati nasibu hasa katika nyakati tulizo nazo

Plan B; Seif alitambua kuendelea na shauri kutatoa nafasi ya kupitisha muda kuelekea uchaguzi na lingetoa nafasi ya sheria ya vyama vya siasa ikumbana kugombea popote

Kumbuka sheria ya Msajili na muda wa uanachama na uongozi

Kwahiyo alifikiria kuwa katika chama kipya ndani ya miaka 2 ili kukwepa kikwazo

Plan C; Maalim aliona kuhamia chama kama Chadema kutazua mtanziko ''tension' kuhusu uongozi na huenda kikawa kikwazo kingine hasa kwa kuzingatia yaliyotokea kwa Lowassa

Kahiyo Seif aliiona nafasi yake ndani ya CDM inajadilika na si ''guarantee''
Hilo ndilo lilimpeleka ACT Wazalendo ambako uhakika katika uongozi upo

Plan D; Maalim anafahamu CUF ya Lipumba itatumika kwa ruzuku za Bunge.
Kwa mantiki hiyo Wabunge wa CUF wataendelea kuwepo, muda si mrefu wataachia ngazi na kumwacha Prof mwenyewe.

Prof ''atawezeshwa'' lakini si kwa kiwango kile kwavile kazi yake imekwisha

Kwacharisma ya Seif, kutakuwa na wimbi kubwa sana la wanachama watakaomfuata

ACT Wazalendo itaimarika sana kwa gharama ndogo ya kifo cha CUF

Hili litakuwa tatizo jingine kwa CCM,sasa itahangaika na mahasimu wawili, CUF na CDM.

Ndiyo maana tulisema mkakati uliotumiwa na CCM na serikali yake ni wa kutuliza maumivu si kutibu ugonjwa

Kisiasa Maalimu Seif anaijua hadhra yake, ana uwezo wa kusoma mazingira kwa wepesi na kwa kina. Ukichanganya na charisma yake, alichofanya ni 'smart move'

Tusemezane
Mh. Nguruvi, asante kwa mada zako chambuzi na zenye kufikirisha. Baada ya wengi kupatwa na mzizimo wa kutoa mawazo huru na kuchambua mambo ni furaha iliyoje kuona bado unaandika.
Hapa nyumbani yapo mengi ya kuchambua lakini najua changamoto zake.
Kule mashariki ya kati tafrani ya Iran na Marekani imeongezeka labda kushinda siku za nyuma. Hebu naomba tuchambulie nini hatima ya tafrani hii. Na je hamaki ya mataifa haya ina weledi au inawapeleka kubaya zaidi?
Tafadhali...
 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,479
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,479 2,000
Mh. Nguruvi, asante kwa mada zako chambuzi na zenye kufikirisha. Baada ya wengi kupatwa na mzizimo wa kutoa mawazo huru na kuchambua mambo ni furaha iliyoje kuona bado unaandika.
Hapa nyumbani yapo mengi ya kuchambua lakini najua changamoto zake.
Kule mashariki ya kati tafrani ya Iran na Marekani imeongezeka labda kushinda siku za nyuma. Hebu naomba tuchambulie nini hatima ya tafrani hii. Na je hamaki ya mataifa haya ina weledi au inawapeleka kubaya zaidi?
Tafadhali...
Kamili, suala la mzozo unaoendelea nimeliongelea HAPA
Mgogoro unaoendelea haukuanza awamu hii ni wa muda mrefu kidogo
Marekani na Israel wanaitazama Iran kama ''super power'' ya mashariki ya kati inayotishia usalama wa Israel. Hii ni baada ya kufanikiwa kumuondoa Saddam Hussein

Kama utakumbuka Israel iliwahi kushambulia Iraq kwa kile ilichosema kiwanda cha Nyuklia
Ukweli ni kuwa haikuwa Israel pekee, bali ilitumiwa na mataifa ya Marekani kumdhiti Saddam

Na utakumbuka katika vita ya ghuba Saddam Hussein alituma kombora Israel ambalo halikujibiwa. Israel haikujibu kwa makusudi kwani kufanya hivyo kungetoa picha ya vita ya kidini kati ya Wayahudi na Waislam. Hilo lingeathiri vituo vya Marekani na ushirika na nchi za kiislam

Baada ya Saddam, Iran inaonekana kuwa tishio kwa Israel namna nyingi
Kwanza, Iran ya Waahemi ni taifa la Shia na huwaunga mkono Izbollah ya Lebanon
Izbollah iliwasumbua sana Waisrael katika vita ya miaka akribani 10 iliyopita

Kumbuka kuwa Izbollah ya Hussein Nasrallah ipo katika eneo la kusini na si nchi nzima
Pili, Israel inahisi kuwepo kwa mbabe Iran kutamweka mahali pagumu kiusalama

Tatu, Iran ni nchi iliyoendelea kiteknolojia tofauti na nchi nyingine za mashariki ya kati
Iran inatengeneza makombora na silaha nzito zinazoweza kuwafikia Wayahudi kikamilifu

Kwa kuchelea hilo nchi za magharibi zikaunda zengwe zikitaka Iran isitishe utengenezaji wa silaha za Nyuklia. Vikawekwa vikwazo bila mafanikio na utawala wa Obama ukaamua kuwa na ''deal'' inayojulikana kama ''Nuclear deal'' ikishirikiana na nchi za Ulaya na Urusi

Inaendelea...
 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,479
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,479 2,000
Nuclear deal
Hii ililenga kuwasimimisha Iran kurutubisha madini ya Uranium kufikia kiwango cha silaha
Mbadala wake ukiwa ni kuondolewa vikwazo vya uchumi na nchi hizo za magharibi

BB Nayahu wa Israel hakupenda deal kwani alichotaka ni nchi za magharibi zikiongozwa na Marekani kumtandika Iran kabisa na pengine kubadilisha utawala na kuweka wao kama ule wa Shah

Hilo likazua mgogoro kati ya Obama na Nayahu. Obama hakutaka vita nyingine kwani alikuwa nazo za kutosha Iraq na Afghanistan. Lakini muhimu ni kuwa Iran siyo Afghanistan, vita ingesambaa na kauthiri sana uchumi wa dunia hasa mafuta kupitia ghuba ya Hazmut iliyopo Iran

Rais Trump akaahidi kufuta mkataba wa Nuclear deal akaiingia madarakani. Hilo amelifanya, na leo inajulikana alilifanya kama kufuta rekodi ya Obama, kwa mujibu wa balozi wa UK nchini Marekani. Ukweli wake unaonekana kwani hakuna mbadala wa nuclear deal

Nchi za Ulaya zinataka kubaki na nuclear deal wakati Marekani ikikaza vikwazo vya uchumi kwa Iran. Ili kufanikiwa likaundwa zengwe jingine na Israel kuwatisha majirani wa Iran ambao ni nchi za kiarabu kama Saudi Arabia, UAE n.k. kwamba Iran ya Washia inataka kuondoa utawala wa Sunni wa Saudia

Kwasasa kuna ushirikiano wa siri wa MBS mwana wa mfalme wa Saudia na Israel ukiunganishwa na Jared Kushner mkwewe Trump

Hivyo ugomvi unaouona si wa Marekani na Iran, bali Israel na Iran, wakati ambapo Israel imejificha nyuma ya mgongo wa Marekani. Kuna sababu za kufanya hivyo
Israel inajua mgogoro baina yake unaweza kuchukua sura ya mashumbulizi dhidi ya Waislam

Ukizingatia mgogoro wa Palestina, na kuchukua milima ya Golan kutoka Syria, ni muhimu Marekani akatangulia kuliko Israel kwani hali inaweza kubadilika na kuwa vita ya kidini

Vita ya dini itakuwa na maana moja, kwamba, Waislam wa mashariki ya kati wataungana
Marekani yenye vituo vyake itakuwa na wakati mgumu huku vita ikirindima mashariki ya kati kuanzia Iraq na kwingine kwenye Washia kama kule Yemen kwa Wahuti

Mashambulizi ya Saudi Arabia kwa Yemen yamelenga kuwamaliza Huti wanaoungwa mkono na Iran. Saudia inahisi kuwa Yemen ikianguka mikononi mwa Iran kama ilivyo Qatar utawala wa Saudia utakuwa matatani. Hapo ndipo Saudia inapolazimika kununua misilaha Marekani, kuwa na ushirika na Israel ili kuidhibiti Iran

Inaendelea...
 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,479
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,479 2,000
EU wanasemaje?
EU wanasema nuclear deal ilikuwa inafanya kazi vizuri na hivyo ilindwe. Hawakubaliana na hatua ya Marekani ya kuvunja makubaliano

Marekani wanasema Iran inawasadia magaidi. Katika takwimu na ushahidi hakuna mahali ambapo Iran inasaidia makundi ya magaidi. Kukwepa ukweli huo Marekani wamebadili kauli na kusema Iran inaleta mtafaruku mashariki ya kati, kwamba, inakuwa mbabe na si Saudia

EU wanataka deal na Iran kwasababu kadhaa. Kwanza, wameikatalia Uturuki kuwa mwanachama
Uturuki( Turkey) wakaamua kuelekea mashariki ya kati na moja ya washirika wakubwa ni Iran

Saudia ikiwa na mgogoro na Qatar na kuwawekea vikwazo vya uchumi kama vyakula, Turkey iliwasaidia sana ikishirikiana na Iran kiasi kwamba vikwazo havikuwa na maana

Hivyo, EU wanaona kuvunja nuclear deal ni kuiacha Iran huru na hivyo kujenga ushirika na Turkey. Kumbuka, ushirika huo una maana Iran kupitia Turkey watakuwa karibu sana na EU
Kama Iran itakuwa na nuclear basi mpaka wake na EU utakuwa mpaka wa EU na Turkey

Hatari kubwa ni kuwa Iran kupitia Turkey itakuwa inapumua uani kwa Israel na kuwa hatari kuliko ilivyo sasa. Bahati mbaya, Marekani kwa kuchagizwa na Israel wanataka kulianzisha

Uingereza inaingiaje katika mgogoro?
Nchi za EU zimemwekea vikwazo Assad wa Syria ambaye ni mshirika wa Iran wa karibu

UK wakaiteka meli ya mafuta ya Iran iliyokuwa inakwenda Syria kwa kisingizio cha kwamba Iran inakiuka vikwazo dhidi ya Syria, kwamba, Syria haipaswi kupata mafuta ya Iran
Wakati huo huo Iran inataka kuuza mafuta kukabiliana na vikwazo vya uchumi inavyokumban navyo. Kwahiyo UK imetumika na US kumdhoofisha Iran kwa kisingizio cha Syria

Iran ikajibu mapigo kwa kutaka meli za UK ikidai meli yake iliyokuwa safarini kwenda Syria iachiwe.

Kwahiyo mgogoro sasa ni wa Marekani, Israel, na UK dhidi ya Iran
Iran nayo imetangaza kuongeza kasi ya kurutubisha Uranium ili kuwalazimisha UE kuishauri Marekani iligeze vikwazo.

Inaendelea...
 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,479
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,479 2,000
Mwelekeo ni upi?
Marekani haitaki vita na Iran kwa kuangalia masilahi yake na nchi za mashariki ya kati hasa Uarabuni. Kuingia vita na Iran ni kuingiza mashariki ya kati katika mgogoro mzito sana

Israel inataka sababu za kuishambulia Iran ikitumaini kuharibu vinu vya silaha za Nuclear
UK haitaki vita kwani ina matatizo makubwa kama Brexit, lakini inatoa msaada kiana kwa US

Urusi inamchagiza Iran aendelee kukomaa kwasababu ni mshirika muhimu
China haitaki Iran ishambuliwe kwasababu ya mafuta ya bei nzuri kwa uchumi wake
Dunia haitaki vita kwani mlango wa bahari za mashariki ya kati ni Hazmut inayomilikiwa na Iran

Je marekani wanaweza shambulia Iran?
Yes wanaweza, wana vituo majini na nchi kavu katika nchi za kiarabu. Wana teknolojia kubwa na vifaa vizito. Wanaweza kupiga mabomu, lakini mabomu hayo yatakuwa na gharama kubwa ya vita pengine kubwa kuliko ya Iraq. Wanasita

Israel haiwezi kusimama yenyewe dhidi ya Iran. Inaweza pale tu Marekani inapokuwa nyuma yao. Obama alipokataa kuipiga Iran, Israel haikuthubutu wala kujaribu

Mashambulizi yote ya Israel yakitokea, ni mashambulizi ya Marekani kwa jina la Israel
Kama itazuka vita, Israel itakuwa mhanga, huku Hezbollah wakitoa usaidizi wa chini chini

Ni kwa msingi huo, akina Macaron na Merkel wanahangaika kuzuia mtafaruku lakini pia Marekani haitaki kuingia vita hiyo. Huu mgogoro utaendelea na kumalizwa kidiplomasia

Vita ya mashariki ya kati ni suluhu mbaya itakayovuta mataifa mengine yenye interest zake

Tusemezane
 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,479
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,479 2,000
SHAMBULIO LA SAUDIA ARABIA
MAREKANI YAPELEKA MAJESHI

Katika matukio ya dunia wiki hii, kumetokea shambulio la vituo vikuu vya mafuta Saudia .

Shambulio hilo limefanywa na 'ndege' zisizoendeshwa na binadamu ''drone''

Hilo limeathiri uzalishaji wa mafuta kwa asilimia 50 na kupelekea upungufu soko la Dunia

Kundi la 'Huti' la Yemeni limechukua dhamana ya shambulio hilo kama kulipa kisasi kwa Saudia.

Ni muda sasa Ufalme wa nchi takatifu umeshambulia nchi ya Yemeni kwa mabomu na ndege.

Kwa wanaofuatilia mabandiko huko nyuma tulieleza mahusiano miongoni mwa nchi za Kiarabu na majirani zao. Shambulio hilo limehusishwa na Iran kwa tuhuma za Marekani bila uithibitisho.

Iran ni Shia katika imani ya Kiislam huku Saudia ikiwa ni Sunni.
Mgogoro wa Shia na Sunni ulichagizwa sana na Marekani ilipoingia Iraq kwa kuwagawa

Katika mgawanyiko wa Sunni na Shia, Mashariki ya kati imekuwa katika wakati mgumu.

Makundi hayo yana yenye Imani moja yakiwa na madhehebu tofauti na ndivyo wananchi wake walivyogawanyika pia. Hivyo basi, Shia na Sunni wametawanyika na kuingiliana sana kijamii

Marekani ilikuwa inatafuta sababu hasa baada ya Iran kukataa kukaa meza moja kujadiliana nao kwa kile kinachojulikana kama 'Nuclear Deal''.

Nchi za Magharibi na hasa za Ulaya zinamlaumu Rais Trump kwa kufumua deal bila kuwa na mbadala mezani. Ni wazi , sasa hivi Marekani ina haha kutafuta majadiliano na Iran

Ingawa shambulio linaweza kutokuwa na ushahidi wa moja kwa moja, kiuchambuzi hili linachagiza kuamini Iran inayounga mkono Huti wa Yemeni ambao ni Shia ipo nyuma ya tukio.

Teknolojia iliyotumika ni ya juu kiasi kwamba, Huti kama kundi wasingeweza kufanya.

Ikiwa ni hivyo kwanini Huti wamechukua dhamana mapema?
Jibu ni rahisi, kuwaondoa Iran katika lawama. Na kama Iran ipo nyuma, ni kwanini?

Iran inakabiliwa na vikwazo kiasi cha kutoweza kuuza mafuta yake.
Hili linapelekea wao kuleta upungufu wa mafuta na huenda kuwarahishia vikwazo.

Lakini pia kuna kupeleka ujumbe kwa Saudi Arabia kwamba, licha ya kununua silaha kutoka Marekani na usaidizi wa Israel, Iran ina uwezo mkubwa kukabiliana nao.

Wengi walitarajia vita itazuka hasa ikichagizwa na Marekani.

Vita katika eneo hilo si rahisi kama inavyodhaniwa.
Sahambulizi dhidi ya Iran litaamsha makundia ya Washia mashariki ya kati.

Ni shambulio litakaloonekana linafanywa na Marekani na Israel kwa kutumia Saudia kuhujumu '' Waislam''. Na kwamba, kushambulia Saudia kutatafsiriwa kama shambulio la eneo Takatifu

Lakini pia Saudi Arabia ni nchi inayoangaliwa kamatakatifu kiimani za dini.
Kuingiza nchi hiyo katika vita kunaweza kusambaza vita nyingine isiyotarajiwa kwingine duniani.

Uhusiano wa Saudia na Israel na Marekani ni jambo linalowakera baadhi ya watu wa mataifa ya kiarabu. Hilo linaoonekana kama Usaliti dhidi ya Waislam na Saudia inabaki njia panda.

Na hapa mhanga mkubwa wa vita mashariki ya kati ni Israel huku Marekani ikitishiwa kimaslahi

Ni kwa mantiki hiyo kumekuwa na kusita kuishambulia Iran kwasasa.
Marekani imegawanyika kuhusu vita nyingine eneo hilo baada ya ile ya Iraq.

Rais Trump aliingia madarakani kwa hoja ya kutopeleka majeshi nchi nyingine.

Tulijadilia hapa kwamba, majeshi yanapelekwa si msaada bali maslahi ya Marekani na kwamba uelewa wa Rais Trump ulitia shaka sana kama kweli anazifahamu siasa za kimataifa

Rais Trump ameidhinisha kupelekwa majeshi kusaidia Saudi Arabia jambo alilowashambuliwa watangulizi wake kwamba halikuwa sahihi kupigana vita za dunia zisizoisaidia Marekani.

Majeshi ya Marekani si kwa vita bali kuilinda Saudia. Tukio hilo linazidi kuwaunganisha Waislam wa makundi kwa maana ya kwamba, Marekani inakwenda kulinda nchi Takatifu.
Kuungwa mkono kwa Saudia kutapungua.

Kwa maelezo hapo juu utabaini kuna ''kujichanganya' kwa hoja, tutafafanua
Hali ilivyo kama vita itatokea au kinachozuia vita kutotokea ni hii:
Wapo watakoichukulia vita kama;
- Shia na Sunni kiimani tu. Kwamba hawa ni shia nasi ni Suni
-Watakoangalia vita kwa jicho la kushambuliwa Saudia kama nchi Takatifu. Hivyo tu!
-Watakaolingalia kama shambulio la mahasimu wa Uislam dhidi ya Waislam wa Iran
-Watakaoliangali kwa jicho la Wazaioni wa Israel kunyanyasa nchi za Kiislam
-Watakaolingalia kiuchumi,Marekani inataka utajiri wa kuuza silaha za kuua Waislam.

Iran inaweza kushambuliwa na Saudi Arabia kwa msaada wa Israel na Marekani.
Hilo linawezekana na lipo katika uwezo. Tatizo ni madhara ya vita hiyo.

Vita itaenea kutoka Misri hadi Afghanistan. Qatar hadi Iraq na maeno baina ya hayo.
Masilahi ya nchi za Magharibi yatakuwa majaribuni kote duniani

Vita hiyo haitakuwa ya silaha, itaathiri utoaji wa nishati dunia na kama waswahili wasemeavyo, mafahali yakipigana ziumiazo ni nyasi, na huenda nchi masikini kama Tanzania zikawa nyasi.

Tusemezane
 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,479
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,479 2,000
QASSEM SOLEIMANI AUAWA NCHINI IRAQ

HALI YA MASHARIKI YA KATI NI TETE

Katika mabandiko 35 kuendelea na yaliyopita tumeeleza hali ya kisiasa mashariki ya kati
Wakati Rais Trump anaingia madarakani tulijadili pia kuhusu changamoto ya M.Kati

Katika wiki kadhaa Marekani imeishutumu sana Iran kuchagiza vikundi vya ''kigaidi''
Shambulio lililomuua Al Baghadad kiongozi wa ISIS lilifanyika miezi michache iliypita

Shambulio hilo limefanywa ''siri'' katika baadhi ya maelezo kama vile ndege zilizomshambulia Al Baghdad zilitokea wapi kwani eneo alilokuwepo lilikuwa mbali na majeshi ya Marekani.

Inaibainika kuwa intelejensia ilisaidiwa sana na serikali ya Iraq, lakini shambulio lilitokea Israel
Inafichwa sana ili kuitenga Israel na mgogoro wa Iran na Waislam wa mashariki ya kati

Israel imechagiza sana Marekani ishambulie Iran baada ya Marekani kujitoa katika nuclear deal
Tulieleza huko nyuma kuwa Marekani ilikuwa inatafuta sababu za kumshambulia Iran

Msaada mkubwa unatoka kwa nchi za Kiarabu kama Saudi Arabia na Israel
Saudia inalazimika kufanya kazi na Israel kwa hofu kubwa ya Iran kuwa mbabe wa M.Kati

Kamanda wa juu wa intelejensia wa Iran Qassem ameuawa akiwa katika airport ya Iraq
Inaripotiwa kuwa Qassem aliuawa akiwa anatoka safarini.

Qassem alikuwa mtu muhimu sana aliyeunganisha vikundi vya SHIA mashariki ya kati kama Hezbollah na vingine vinavyopata misaada kutoka Iran vikiwemo vya Kuds

Kuuawa kwa Qassem kumefanywa na Marekani iliyokiri hivyo, lakini suala hilo limeacha hali ya taharuki Mshariki ya kati kwani Iran inasema itajibu shambulio hilo.

1. Iraq imejikuta kati kati ya mzozo huo. Iraq ina Shia ambao kwa sehemu kubwa walikuwa tatizo kwa Marekani wakiongozwa na Murtada Al Sadr.

Stability ya Iraq inategemea Marekani na Iran. Hata hivyo, Iran ina ushawishi kupitia Shia.

2. Makundi ya Shia Mashariki ya kati kama Hebollah ya Sheikh Hussein Nasrallah na kwingine yanayomuheshimu sana Qassem yamechukizwa na hali hiyo.

3. Israel haitakuwa salama kwani wengi wanaamini yote yanatokea kwa shinikizo la Israel

4. Nchi wanachama wa EU na Washirika wa Marekani hawakujulishwa kuhusu Shambulio

5. Nchi za Mashariki ya kati zenye Shia nazo zina tatizo kukabiliana na hasira za Shia

Kuna hali ya wasi wasi kwamba Iran ikijibu mapigo huenda ukawa mwanzo wa vita nyingine
Tofauti na ile ya Iraq, vita ya Iran itakuwa na athari kubwa katika eneo lote la mashariki ya kati.

Inaendelea....

kamili
 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,479
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,479 2,000
QASSEM
Sehemu ya II

Haitakuwa rahisi Iran kujibu mapigo haraka, kitakachotokea ni kuchukua muda na kupitia makundi yao yaliyosambaa mashariki ya kati kuna jambo litatokea.

Kwa kuelewa hilo Marekani imeamuru Raia wake walioko Iraq kuondoka na kupeleka majeshi zaidi eneo la mashariki ya kati.

Marekani wametoa tahadhari kwa sehemu zenye masilahi yao zikiwemo balozi n.k.

Qassem hakuwa mgeni katika duru za kiintelejensia za Marekani.
Ingawa Marekani wamamwita gaidi, huyu alikuwa kamanda wa nchi ya Iran

Marekani haijaweza kueleza kwanini tawala zilizopita zilimwacha Qassem.

Rais Trump akiwa Rais aliwahi kumtuhumu Obama kwa kutaka kuanzisha vita na Iran kwa kile alichosema ''hawawezi majadiliano na kwamba alitaka kupata namna ya kuchaguliwa tena''

Inaonekana Rais Trump amaechukua hatua hiyo kupunguza joto la kisiasa la Impeachment
Lakini pia kuchukua credit kwamba anashambulia magaidi na kufanikiwa kuwaua

Kuna tatizo linalomsubiri. Kwanza, Trump amaechukua hatua bila kuwashirikisha wabunge wa genge la 8 (Gang of 8") badala yake kuwataarifu wapambe kama Graham.
Joto linapamba DC taratibu huku wakimtaka aeleze usahihi wa shambulio.

Kuelekea uchaguzi, vita ni hoja ngumu sana kuitetea ikizingatiwa Wamarekani wengi wamechoshwa na vita zisizo na mwisho.

Ikiwa itatokea vita, Trump atakuwa na wakati mgumu kueleza umma. Hoja yake ilikuwa kumaliza vita na kuondoa majeshi mashariki ya kati jambo alilowatuhumu watangulizi wake kushindwa

Marekani itakuwa na wakati mgumu kwa kuzingatia jiografia ya mashariki ya kati, maeneo ya vituo vyao vya majeshi na jinsi jamii ya mashariki ya kati isivyotabirika

Presha inatoka Iraq kwa sasa ambayo serikali yake inapata kutoka kwa wananchi wake

Mgogoro utaivuta Israel kwani kama kuna kitu kinachowaunganisha watu wa mashariki ya kati ni vita na Israel kwa mgongo wa dini. Hilo pia litawagawa washirika wa Marekani kama Saudia.

Vita itapigwana Iraq, Iran, Syria, Yemen, Jordan, Afganistan, Pakistan, Lebanon kwa uchache wa kutaja.

Hatua ya kumuua Qassem haikuangaliwa kwa mtazamo mpana wa siku za baadaye.

Ikiwa wapo wanaosema kifo kitaifanya Marekani salama, iweje leo wananchi wake waamuriwe kuondoka na nchi hiyo kupeleka askari 3000 zaidi mashariki ya kati?

Kama kuna nchi zenye hofu nchi hizo zitakuwa Iraq, Israel na Saudi Arabia.
Hizi zipo katikati ya mgogoro huo zikiwa na masilahi kwa pande zote.

Kwa vigezo vyote, mgogoro huu wa kifo cha Qassem ni mbaya na madhara yake yatakuwa ya muda mfupi na muda mrefu na mabaya.

Mgogoro utaathiri uchumi wa dunia kwani utahusisha ukanda maarufu wa nishati ya mafuta.

Tusemezane
 

Forum statistics

Threads 1,382,249
Members 526,314
Posts 33,823,114
Top