Mabibi na mabwana inasemekana kila mtu kwa namna moja au nyingine hufanana na mtu mwingine angalau mmoja hapa duniani.
Ukimwangalia Trump jinsi alivyoshuighulikia misingi iliyokuwa inabeba utambulisho wa taifa la Marekani duniani kisha ukamwangalia Magufuli na iliyokuwa misingi ya utambulisho wa Mtanzania, haichukui muda mwingi kutambua kuwa wawili hawa ni baba mmoja, mama mmoja.
Kwamba leo Marekani kuna Rais ambaye walio wengi wana mtazamo ule walio nao kumwelekea yeye?
Kwamba leo Marekani pana Rais akifungua mdomo, hali ya hewa inaweza isitabirike?
Kwamba leo Marekani iliyokuwa mshirika muhimu katika amani, haki na Uhuru wa dunia wana rais asiyetabirika kiasi kile?
Kwamba leo rais wa Marekani akifungua mdomo hakuna ajuaye atakachosema kinaweza kuwa na madhara gani, kwa kiasi gani na hadi wapi?
Hiyo si Marekani iliyokuwa ikijulikana kama taifa kubwa, super power na custodian wa nguvu za nyuklia ambazo wapuuzi wengine hawakuruhusiwa kuwa nazo kwa usalama wa dunia yote.
Kwamba leo Tanzania tuliokuwa na ushawishi ule wa kuwafanya wengine duniani kujifunza kutoka kwetu, leo ndiyo hapa tulipo kidiplomasia?
Kwamba leo nchi hii ambayo hatukuwahi kuwa na mtu yeyote ukimbizini, leo hii wenzetu kwa usalama wa maisha yao ni heri wakatafuta hifadhi nje ya nchi na mapema iwezekanavyo?
Kwamba leo umuhimu wa kukaa mezani kutanzua tofauti zetu haupo tena. Ila marungu na risasi za moto za vyombo vya dola dhidi ya watu wasio na hatia?
Kwamba tuliokuwa machampioni wa kutetea haki za binadamu na kuwa wa kupigiwa mfano kote duniani, leo hii ndiyo tumekuwa wa kunyooshewa vidole kwa uvunjifu wa haki hizo uliopitiliza tokea duniani kote?
Kwamba leo chaguzi si zinazotupelekea kupata viongozi bali hao wanaweza kutangazwa hata wasipochaguliwa?
Kwamba badala ya uchaguzi kumekuwa ni vilio. Kuna waliokamatwa, kupigwa na hata kuuwawa na mamlaka katika jitihada zao za kutetea uhuru na haki tu katika uchaguzi huu?
Kwamba nini tusikie kwenye vyombo vya habari au nini tusome kwenye mitandao, limekuwa la kuamriwa na mamlaka? Kwamba Magufuli anatumia Twitter lakini hataki sisi tusikie wala kufika huko?
Tuliokuwa vinara wa kuhamasisha, kushawishi na hata kusimamia maridhiano kwingine, leo yametushinda. Tumekuwa watu kubebeana nyundo za chuma kuuwana bila ya huruma wala aibu?
Marekani kwao wameliona na kulitanzua bila ya kusubiri tena. Wameshamfunga paka kengele. Alipo kesha tulizwa kikasuku! Pongezi kwao kwa hilo zimetolewa tokea kwa viongozi wengi duniani na ati na Magufuli akiwamo.
Sisi Je? Aaaah Wapi!
Ni muhimu tukashirikiana sote akiwamo mh. Magufuli mwenyewe. Misingi ya utanzania wetu si ya kufanyiwa mchezo hata kidogo.
Kwa hakika misingi ya taifa letu tunalolipenda sote tuliyoachiwa na mwasisi wetu siyo hii tunayo iishi sasa!