Duniani kuna kipi cha maana mpaka ushukuru wazazi kukuleta?

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
15,300
23,022
Huwa nashangaa kweli watu tukishukuru Wazazi hasa Mama eti kwa kukuleta duniani.
Kuna kipi hasa cha maana huku duniani mpaka uwashukuru hao wazazi?

Yani tumetengeneza kitu kwamba huko ulikokuwepo hapakuwa sehem nzuri kuliko dunian.

Kama dunia kwako imejaa Mateso kwanini isiwe Lawama kwao? Hivi kwanza uliwaomba hao wazazi wakuzae?

Mi naona hakuna haja ya kushukuru mzazi yoyote katika hili. Kwasababu hamkukubaliana kukuleta duniani, walifanya kwa malengo yao, hivyo wao ndio walipaswa kukunyenyekea kukuleta huku.

Maisha hayana maana yoyote ile kwani mwisho wa siku kuna kufa, baada ya kufa kila ulichokifanya hakina maana tena kwako.

Ndo maana mtoto akizaliwa tu hua ana lia maana hapa dunian ni uwanja wa fujo, cha ajabu tunaogopa kufa wkt hatupendi kuzaliwa.
 
Hizi stress zako tuu mkuu!

Probability of being you was 1 out 1.2 bilions number of sperm cells in a single ejaculation..

Unfortunately it happened to be you! Then why would you need to complain on the innocent parents?

I guess you are wrong..
 
Ndugu siyo watu wote waliopitia katika maisha magumu. Vile vile hata yule mwenye maisha magumu siyo wakati wote alikuwa na maisha magumu , wakati mwingne anakuwa na furah na kutamani kitu kisimalizike kwisha. Kwa nini usishukuru wazazi Kwa vitu hivyo.
 
Hizi stress zako tuu mkuu!

Probabilit of being you was 1 out 3 bilions number of chromosomes...

Unfortunately it happened to be you! Then why would you need to complain on the innocent parents?

I guess you are wrong..
Sasa kwann niwashukuru?
 
Hizi stress zako tuu mkuu!

Probabilit of being you was 1 out 3 bilions number of chromosomes...

Unfortunately it happened to be you! Then why would you need to complain on the innocent parents?

I guess you are wrong..
1:3 billions chromosomes, how?
 
Huwa nashangaa kweli watu tukishukuru Wazazi hasa Mama eti kwa kukuleta duniani.
Kuna kipi hasa cha maana huku duniani mpaka uwashukuru hao wazazi?

Yani tumetengeneza kitu kwamba huko ulikokuwepo hapakuwa sehem nzuri kuliko dunian.

Kama dunia kwako imejaa Mateso kwanini isiwe Lawama kwao? Hivi kwanza uliwaomba hao wazazi wakuzae?

Mi naona hakuna haja ya kushukuru mzazi yoyote katika hili. Kwasababu hamkukubaliana kukuleta duniani, walifanya kwa malengo yao, hivyo wao ndio walipaswa kukunyenyekea kukuleta huku.
Le general hatushukuru wazazi kutuleta duniani.Tunashukuru kutulea na kutukuza.Hivyo vya kuletana duniani hata wanyama wanafanya.
 
Tuko duniani kwa KUSUDI LA MUNGU! yaani iko sababu ya mimi na wewe kuwepo duniani. Tunapswa tuitafute hiyo sababu ili tuijue na tuiishi !

Hakuna sababu yeyote ya kuwashukuru wazazi, bali tunapaswa kuwaheshimu.

after all, life is treasure regardless its burdens.
 
Hii mada ni nzito,hutakiwi kucomment kwa wepesi...
Umenena vyema, mada ngumu majibu myepesi, nami nimejikuta nikiwa kwenye mawazo kuwa kwanini binadamu tumezaliwa, ni kweli tupo duniani tumtumikie Mungu kisha turudi kwake mbinguni basi hakuna kingine? kama ni hivyo lengo lake nini? Huyo Mungu, kuna Siri gani katika kuzaliwa-kuishi-kufa. Maisha yana maana gani . Na mengine mengi.

Mpita njia na Porojo za mtaani
 
Ki ukweli mi mwenyewe huwa naona the whole point of living is useless, dunia imejaa struggle nyingi za kijinga tuu

Ubinadamu kazi
Maisha yanaanza kuwa na maana pale utakapojiuliza na utakapopata majibu ya maswali haya matatu:
1-WEWE NI NANI.
2-NI KWANINI UKO DUNIANI.
3-NINI KITAFUATA BAADA YA MAISHA HAYA.

tofauti na hivyo, life is meaningless!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom