Dunia ya Soka impe Luka Modric heshima yake

Christopher Wallace

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
1,410
3,548
Bila kumung'unya maneno wanazi na wazandiki wa soka duniani hawamtendei haki Luka Modric. Wamekuwa wakimu-underrate na kumuona mchezaji wa kawaida.

Lakini kwa misimu kama mitatu Luka yupo katika ubora wa kipekee aking'arisha vilivyo safu ya kiungo ya Real Madrid.

Ila bahati mbaya, wazandiki wa soka wanawasifia viungo wa kawaida kama Pogba, Fabregas, Kroos, na Rakitic.

kikosini Real Madrid, wachezaji wanaosujudikiwa ni Ronaldo, Marcelo, Sergio Ramos na Casemiro. Wanamsahau mtu ambaye yuko nyuma ya pazia ya mafanikio ya hao wengine.

Kwanini dunia ya soka haimpi heshima yake Luka?
 
Modric huyu kijana wa Kicrotia Fundi sana sijui anatumia Petrol jinsi unavyomkuta kila kona ya uwanja na zile pasi zake za outer kwa kifupi anajua kusakata kabumbu.

Sitasahau goli alimfunga De Gea UEFA champions league pale OT
Siku haipiti bila kuisema MANUTD..UKOME.
Anyway nashangaa sn wanavomu under rate Luka....Kwangu mm ni mmoja kati ya viungo bora wa wkt huu
 
Siku haipiti bila kuisema MANUTD..UKOME.
Anyway nashangaa sn wanavomu under rate Luka....Kwangu mm ni mmoja kati ya viungo bora wa wkt huu
Una hisa nini pale Man utd?apo utakua umeniingilia uhuru wangu wa kuongea/kusema chochote la msingi sivunji sheria.

Kwa kifupi ni Shabiki mzuri tu Man utd ila hakuna game iliniuma kama ile hasa yule refa toka uturuki kumpa kadi Nyekundu Nani.

Kati ya viungo bora kuwahi kutokea Modric naye yupo tena sasa Zidane kampa uhuru zaidi baada ya Casemiro kuwa kiungo mlinzi na Modric kupewa jukumu la kucheza huru akizungukwa na Kroos anajua kulinda sana mpira ukiwa miguuni mwake kuuchukua labda umchezee rafu kariba ya akina Iniesta,Xavi
 
kila mchezaji ana malengo yake kama kupata vikombe na pesa sasa huoni kama hapo Madrid kapata vikombe vya Uefa 2, Super cup 1 wakati tot huko hata Epl tu wanashindwa kuchukua
Tatizo kubwa la Totenham ni kuuza wachezaji wao nyota...Modric na Bale walitosha kabisa kuwapa ubingwa endapo wangesalia kikosini.
Msimu huu atauzwa Kane we subiri uone.
 
Umaarufu wake ulipungua alipohama...pale Totenham alikuwa mchezaji wakutegemewa zaidi na alipewa heshimakubwa zaidi ya huku alipo sasa.

Mkuu naomba nitie neno hapo kidogo...unaposema luka alikuwa tegemezi spurs kulinganisha madrid unakosea sana kwa kuwa kitendo cha yeye kuanza kwenye 1st-eleven za Madrid ni kiashiria tosha cha kutegemewa...luka huanza venginevyo labda awe majeruhi...kingine kwenye timu kama Madrid mastaa ni wengi na hii ndo hufanya baadhi ya wachezaji kuonekana kawaida...na pale Madrid mchezaji unaweza kuwa fundi lakinii namba lazima uipiganie.
 
Modric huyu kijana wa Kicrotia Fundi sana sijui anatumia Petrol jinsi unavyomkuta kila kona ya uwanja na zile pasi zake za outer kwa kifupi anajua kusakata kabumbu.

Sitasahau goli alimfunga De Gea UEFA champions league pale OT
Ha ha ha
 
Luka kuna kipindi majeruhi yalimuandama sana, nadhani sasa hivi ametulia tulia. Tatizo la Madrid ni kumuona ronaldo ndie kila kitu, akiondoka pale hawa wengine wataanza kuheshimiwa.

Sijawahi kumpingaga huyu bwana ndani ya uwanja ila kroos namuona ni wa kawaida ila Modric na Casemiro ni wa pekee.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom