Dunia ya sasa haina Matusi

Dunia ya sasa haina Matusi

Author

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2014
Posts
1,745
Reaction score
8,230
Habarini wadau,
Nimetafakari kwa kina na nikagundua kuwa kwa dunia tunayoumishi sasa hakuna matusi kwa maana kwamba lugha ambazo zilikuwa zinazungumzwa zamani watu walikuwa wana hofu ya kutaja baadhi ya maneno hadharani ila siku hizi yameshakuwa ni kama lugha ya kawaida na yamezoeleka kiasi kwamba hata yakitamkwa watu wameona ni jambo la kawaida kwenye maisha ya kila siku. Tena kwa siku hizi yametokea na maneno mangine makali hata kutamka yakimaanisha matusi yale yale ambayo yalitamkwa zamani. Ukiwa popote iwe sokoni, stendi, barabarani, kwenye gari, ofisini imeshakuwa ni kawaida sana...zamani ilikuwa ikionyeshwa picha, au video mbaya mzazi aliwafunika watoto macho wasione au kuzima tv ila siku hizi wanakutana na watu waliovaa hivyo kila kona mpaka waalimu mashuleni...Imeshakuwa kawaida...Zamani ilikuwa tusi ila siku hizi sio tusi tena. Hata ipigwe nyimbo yenye maudhui mabaya utaona hata watoto wakiwekewa wacheze wakati zamani ilikuwa kwenye watoto wana disko toto lao hukooooo....Siku hizi tunaenda na watoto club, kwenye show za comedians ambao wanaongea lugha za matusi lakini kwa kuwa imeshakuwa lugha ya kawaida hakuna anayejali....Mdau utakubaliana na mimi kuwa siku hizi hakuna matusi...matusi ilikuwa zamani.
 
Back
Top Bottom