ile kadi ni halali coz katenda kosa la 2 palepale mbele ya refa wakati anapewa yellow card
Kwahiyo refa alitoa maamuzi ya haki kwenye ile mechi, eti eeh?
ile kadi ni halali coz katenda kosa la 2 palepale mbele ya refa wakati anapewa yellow card
Asante Kaka kwa kunisaidia kuwaelezea hawa Watindiga(Wapenzi wa Simba) wa kizazi cha 1990s wasioijua Historia ya nchi hii, wao kazi yao ni kushangilia usajili wa kina Ngassa,Akuffor na wengineo tu uliofanikishwa na yule Mhaini...sijui hata nani alimfungulia bora angeishilia kulekule
Soka la bongo fitna kubwa kabisa!!wamejaa mafisadi wa soka na wanunua marefa,wachezaji ili kuboronga na kuhujumu mechi!woote wanajulikana!
Kama ilivyotarajiwa na wengi wale wachezaji wa kukodi No. 12 na No. 13 waliowawezesha Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Tanzania Bara Simba S.C kutoka droo ya goli 1 - 1 na Mabingwa wa kusakata kabumbu ukanda mzima wa Africa ya Mashariki mpaka kule kwa nchi waalikwa Dar Yong Africans wameadhibiwa na Shirikisho lenye dhamana ya kuendesha mchezo huo hapa nchini kwa kuvurunda, wakati Akrama (Pichani chini) akiondolewa kabisaa kwenye Ligi Msaidizi wake Mzee wa offsides yeye amepewa onyo kali,habari kamili hii hapa:-
Na Prince Akbar wa Bin Zubeiry
KAMA ilivyotarajiwa na wengi, refa Mathew Akrama wa Mwanza aliyechezesha ovyo mechi ya watani wa jadi katika soka ya Tanzania, Simba na Yanga, Jumatano wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam amekwenda na maji.
Taarifa ya Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura imesema kwamba, Kamati ya Ligi imewaondoa marefa watatu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kutokana na kuvurunda.
Mbali na Akrama ambaye Yanga hawana hamu naye tangu siku hiyo, wengine ni Paul Soleji wa Mwanza aliyechezesha mechi kati ya Simba na Tanzania Prisons, na mwamuzi msaidizi namba mbili kwenye mechi hiyo Mwarabu Mumbi wa Morogoro, wakati mwamuzi msaidizi namba mbili wa mechi ya Yanga na Simba, Ephrony Ndissa wa Dar es Salaam amepewa onyo.
Kamishna wa mechi namba 28 kati ya Yanga na African Lyon, Pius Mashera ameondolewa kwenye orodha ya makamishna wa ligi hiyo kwa kuchelewa kufika kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (Pre match meeting) na uwanjani.
Vilevile Mashera kwenye ripoti yake aliwasilisha malalamiko dhidi ya msimamizi wa kituo cha Dar es Salaam, na kwa vile suala hilo ni la kinidhamu ametakiwa alipeleke kwenye Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF.
Nayo Simba imepigwa faini ya jumla ya sh. 600,000 kwa kuchelewa kufika kwenye pre match meeting ya mchezo wao dhidi Tanzania Prisons (sh. 100,000) na kwa washabiki wake kuwatupia chupa za maji waamuzi wa mechi hiyo (500,000).
Pia Kamati ya Ligi imeagiza kuwa kwa vile suala la kipa Shaabani Kado wa Mtibwa Sugar kudaiwa kumpiga kiongozi mmoja wa Ruvu Shooting mara baada ya mechi kati ya timu hizo iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex ni la kinidhamu lipelekwe kwenye Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF.
wangemfungia na yule mnywa viroba BABOON!
Mkuu Masuke umewasilisha mpaka Bhaaaaaaaaass. Sio kosa lake alitumwa magoli bila ya kupewa mbinu za kiufundi, alifikiri Okwi Magoli akifunga huwa anakaa nyuma ya mabeki, akamuulize Nsajigwa na Chuji kilichowapata mwezi wa Nne mwaka huu huu mpaka wengine wamestaafishwa bila kupenda.Nafikiri kuna haja ya kulifukuza benchi nzima la ufundi la Yeboyebo FC kwa kushindwa kumfundisha Bahanuzi jinsi ya kuvunja "offside trick" za wachezaji wakimataifa kama wa Simba SC. Chezea Mnyama weweeMarefa mnawachagua wenyewe ili wawabebe, kawabeba hambebeki sasa mlitaka achukue mpira yeye mwenyewe autumbukize kwenye kamba ndo mngeona ni refa bora, timu yenu mbovu ile si ya kulipa tano kajipangeni tena acheni kubwabwaja, Huyo Bahanuzi wenu muda wote yuko nyuma ya mabeki unategemea nini? Na kama ataendelea hivyo hivyo ataishia kufunga magoli ya penati tu lakini ya move atayasikia kwa akina Sunzu, Okwi, Ngasa na Boban.
Si bure utakuwa umeamka muda si mrefu, kanawe uso kwanza wenzako wanajibu hoja wewe umeanza matusi. Shauri yako wenzako walianza rafu refa akawabeba kilichowatokea kawaulize akina Sufiani wenu bado wanalia.Yanga ni moto wa kuotea mbali, mtasingizia sana marefa mwaka huu, na bado. Kumkata simba sharubu mwaka huu ni jambo lililo wazi. Simba ni kenge blue hawazi kuifanya kitu yanga, tena mechi ijayo achezeshe Ismail Aden Rage.!
Huo moto wa kuotea mbali wa Yanga unaonekana wapi na sisi tukaote au kwa sababu ni wa kuotea mbali utatupata huku huku, Hebu tujikumbushe msimamo wa ligi tuone huo moto wa Yanga wa kuotea mbali.Yanga ni moto wa kuotea mbali, mtasingizia sana marefa mwaka huu, na bado. Kumkata simba sharubu mwaka huu ni jambo lililo wazi. Simba ni kenge blue hawazi kuifanya kitu yanga, tena mechi ijayo achezeshe Ismail Aden Rage.!
Mkuu Masuke kweli moto wakuotea mbali nimeuona, yaani pamoja na makelele yote ya usajili watu wanahemea kupata nafasi ya nne! Hivi na moto wa kuotea Morogoro upo au umezimika maana naona miwa inazidi kuchanua tu. TeheteheteheteheeeeHuo moto wa kuotea mbali wa Yanga unaonekana wapi na sisi tukaote au kwa sababu ni wa kuotea mbali utatupata huku huku, Hebu tujikumbushe msimamo wa ligi tuone huo moto wa Yanga wa kuotea mbali.
View attachment 67455
Mngeanza na Mtibwa SC kwanza halafu Simba SC wakafuatia. Kufunga magoli nane na wewe ukatundikwa sita (GD = 02) hapa naona moto wa mshumaa tu, moto wa gesi upo Simba SC wewe sisi tumetundika watu magoli kumi, tumefungwa magoli mawili tu na la penati ya kupewa moja.Yanga ni moto wa kuotea mbali, mtasingizia sana marefa mwaka huu, na bado. Kumkata simba sharubu mwaka huu ni jambo lililo wazi. Simba ni kenge blue hawazi kuifanya kitu yanga, tena mechi ijayo achezeshe Ismail Aden Rage.!
Mtani vipi au wewe hujui kama "Nyota njema huonekana asubuhi" na "Biashara asubuhi" au wewe unafuata kale kamsemo "Fainali uzeeni"Mambo ya ajabu sana haya mnashangilia ligi ikiwa round ya 5!!!!
Karaga bao, yanga tumewashika, tena tumeshika pabaya, lazima tumkate mnyama mkiaMngeanza na Mtibwa SC kwanza halafu Simba SC wakafuatia. Kufunga magoli nane na wewe ukatundikwa sita (GD = 02) hapa naona moto wa mshumaa tu, moto wa gesi upo Simba SC wewe sisi tumetundika watu magoli kumi, tumefungwa magoli mawili tu na la penati ya kupewa moja.
Naona umeishiwa na wadau pia wameliona hilo. Endelea kusema "jamani napiga njooni mniamulie' kumbe umepigwa wewe roba ya mbao halafu mchizi aliyepiga amekauka anataka mpaka aone ngama imetoka ndipo akuachie.Karaga bao, yanga tumewashika, tena tumeshika pabaya, lazima tumkate mnyama mkia
Unataka tushangilie ikiwa raundi ya ngapi? au tuanze kushangilia pale mtakapo lipa kisasi cha magoli matano bila au yale ya Dar mpaka Moro?Mambo ya ajabu sana haya mnashangilia ligi ikiwa round ya 5!!!!