Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,638
- 220,409
Usemi huu wengi hawauelewi maana yake hasa. Mimi binafsi kwa miaka niliyoishi hapa duniani na maisha niliyopitia nimejifunza kuwa kila unachokifanya hapa duniani malipo yake ni hapa hapa duniani. Na hii ndiyo dhana ya kuwa dunia ni duara.
Unapo mbagua, kumnyanyasa au kumyanyapaa mtoto kwakuwa hukumzaa. Kuna siku matendo uliyomfanyia yule mtoto yatakurudia wewe au watoto uliowazaa.
Unampata mtoto mdogo ambae wazazi wake wamekuamini na kukukabidhi kwakuwa tu hawana uwezo na wameona wewe kukaa na yule mtoto na kumlipa ujira kidogo kutawasaidia na wao kupata hela ya mafuta ya taa.
Mtoto yule unamruhusu kwenda kitandani saa tano usiku na awe ameamka saa kumi na moja alfajiri. Akikosea unampiga, yeye ndiye mla vipapatio mkichinja kuku. Akiumwa unamwambia huna hela za kumtibu unamrudisha Kwa wazazi wake.
Kuna habari niliisoma mitandaoni, inahusu kijana wa kiume wa miaka 15, baada ya kumaliza shule ya msingi aliondoka kijijini kwao kwenda kutafuta maisha mjini. Alifika Morogoro na alipata ajira kama house boy kwenye familia moja. Ilikuwa familia ya baba, mama na watoto watatu. Walikubaliana ujira na aliridhia kufanya kazi.
Mama alisafiri na watoto wake na kumuacha kijana awe anaandaa chaakula cha baba wa nyumba. Baba alianza kummendea yule mtoto alimuahidi kumpa pesa ya ziada mbali na mshahara wake. Yule mtoto alihamia chumbani kwa baba mwenye nyumba na kuwa kama mkewe. Anasema siku za kwanza alipata maumivu makali kwani hakuwa anafahamu mambo hayo kabisa.
Mke alirudi baada ya mwezi, aligundua uhusiano wa mume wake na yule kijana na mama alimfukuza kijana kazi. Yule kijana anasema yeye hana hisia kufanya mapenzi na wanaume wenzake ila ni shida ndiyo zilipelekea afanye vile.
Fanya hayo ukijua kuwa dunia ni duara .