Dunia miaka 117 iliyopita, Unadhani miaka 100 ijayo itakuwaje?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
1:Kabla Coca -Cola hawajaanza kutumia CAFFEINE, Ile Ladha tamu wakati ule ilikuwa ni COCAINE product, mwaka 1903 iliondolewa.

2:Asilimia kubwa ya madaktari walikuwa hawajaenda shule, na wale walioenda shule mara ya kwanza kwanza walilaumiwa kuwa hawajui kitu

3:Speed Limit ya majiji mengi duniani enzi hizo ilikuwa 16 Km/H

4:Wastani wamwanamke kuosha nyele zake ilikuwa ni mara moja kwamwezi/wenye nywele ndefu.

5:Kati ya watu 10 wawili walikuwa hawawezi kusoma na kuandika, afrika kwetu nadhani ilikuwa ni balaa zaidi.

6:Jengo refu kuliko yote ulimwenguni ulikuwa ni mnara wa Eiffer nchini ufaransa.

7:matumizi ya Cocaine tu ndio ilikuwa kinyume cha sheria marekani,Bangi zilikuwa zinapatikana katika maduka ya madawa na madaktari walikuwa wanawaandikia Heroin wagonjwa kama sehemu za dawa.

8: Idadi ya watu mji wa Las vegas marekani ilikuwa ni watu 22 mwaka 1900.

9:Kwa marekani 95% ya wanawake walikuwa wanajifungulia nyumbani

10:Nchi huru afrika nzima zilikuwa mbili tu Liberia na Ethiopia

pitia zaidi hapa kwa marekani
21 incredible facts about the world 100 years ago

unadhani miaka 100 ijayo mabo yatakuwaje...
 
Endapo kama Mungu atakuwa amenijalia heri nitakuwa na miaka 125
Nitashuhudia dunia itakavyokuwa na nafikiri Mungu aniwezeshe niwepo.
Endapo kama kuna Mungu na watu wasemavyo Mungu husikilia maombi basi nitakuwepo.
Thanks Mungu kama upo uniwezesha maana wakati huo tutakuwa tunaishi mars
 
Kitakacho kuwatu watu watakua waepungua sana , wendi watakua wamemuacha mungu, ushoga utakuwa kawaida ya dunia, teknolojia itafikia mwisho watu watarudia asili.
 
Hapa tanzania itakua, mchaga atakua ameongoza nchi, kilimanjaro itakua icon ya africa,dodoma itakua kama dar, dar itakua kama katesh, chadema haitakuwepo ccm itafanya jubilee ya 150 kanisa katoliki litakua na miaka 300, kizaz changu watakua 120
 
Endapo kama Mungu atakuwa amenijalia heri nitakuwa na miaka 125
Nitashuhudia dunia itakavyokuwa na nafikiri Mungu aniwezeshe niwepo.
Endapo kama kuna Mungu na watu wasemavyo Mungu husikilia maombi basi nitakuwepo.
Thanks Mungu kama upo uniwezesha maana wakati huo tutakuwa tunaishi mars.
Mkuu fanya hesabu ndogo tu jumlisha miaka 100+miaka yako+life style yako ukipata jibu angalau utakuwa matumaini kidogo ya kuwepo!
 
Back
Top Bottom