Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,488
- 16,646
Benjamini Netanyahu amejisifu kuwa ramani mpya ya mashariki ya kati inaenda vizuri.Katika kujisifu huko ametaja jinsi ambavyo Hamas na Hizbullah zimedhoofika.
Makamanda wake nao hasa waziri wa Ulinzi wamekuwa wakitoa kauli za kujiamini kiasi kama hicho zinazoenda sambamba na kuvunja maeneo muhimu ya makazi ya wapalestina kote Gaza na kote maeneo yaliyo ndani ya Israel ambako PA wamepewa madaraka kudhibiti wenzao.
Hayo yametokana na kuamini kuwa mfadhili mkubwa wa makundi hayo .ran naye amedhoofika na kuahidi kumpiga hivi karibuni ambapo hakutakuwa tena na upinzani wowote katika kuichora ramani mpya ya mashariki ya kati.
Ukweli ni kwamba ramani hiyo haitokamilika kwani makundi yote kuanzia Hamas ,Hizbullah na serikali mpya ya Syria hawajakubali kwamba wameshindwa hata kama wamedhoofishwa.
Kwa upande wa Iran ambao wameshafanya urafiki mkubwa na China na Urusi nao wamejitayarisha vya kutosha.Kwa mujibu wa Khamenei na makamanda wake jeshi lote limeshapewa amri ya kuweka tayari silaha zao ili kuzitumia dhidi ya Marekani na Israel kwa pigo la mwanzo tu la Marekani ambayo imepania kuipiga Iran kwa visingizio kadhaa ikiwa ni kumsaidia Netanyahu kukamilisha mchoro wake wa Mashariki ya kati.
Wapo makamanda wakuu wa Iran ambao tayari wameshauri na kumshinikiza Khamenei atoe amri ya kuzishambulia ndege za kivita za Marekani za B2 na B52 ambazo zimeshawekwa kwenye visiwa vya Garcia karibu na Yemen kabla hata hazijaruka kuwalenga wao.
Israel itakaposhambuliwa hata kwa kiasi kidogo itaumia pakubwa na makundi yote yaliyoumizwa kwa muda mrefu yatakuja juu kuishambulia na haitaweza tena kujitetea na kuidhibiti mashariki ya kati.