Dunia inayumba, watawala nao wameshindwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dunia inayumba, watawala nao wameshindwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiby, Oct 16, 2011.

 1. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Kama vile ilivyo asili ya kila kitu, ni kwamba kuna wakati wa kuzaliwa kwa kila kitu na wakati wa ukomo(kufa) kwake. Hata hivyo kabla ya kufikiwa kwa ukomo huo kuna vipindi vya nyakati vitakavyopitiwa; mfano kama tukimchukua mtu, yeye atakuwa na wakati wa utoto baada ya kuzaliwa, ujana, uzee na hatimae kufa. Hiya yanatimia kuhalalisha ukweli kwamba kila chenye mwanzo kina mwisho wake. Tuna kitu kimoja tu kisicho na mwanzo, hicho ni Mungu peke yake, na hivyo hakina budi kisiwe na mwisho. Mfumo wa utawala wa binadamu, kama tunavyojuzwa na maandiko matakatifu ni kwamba, Mungu alikuwa akiwaongoza wanadamu kwa njia ya nabii wake. Lakini tunajuzwa kuwa watu kwa ukaidi wao, walitaka wapewe mtu juu yao yaani mfalme anaetokana na wao atakaewatawala, ili pia aweze kuwaongoza pamoja na mambo mengine ikiwamo vita.
  Mungu hakuwakatalia matakwa yao, bali alimweleza Samweli aweze kuwaeleza consequences zitakazo tokana na mfalme wanaemtaka. Miongoni mwa mambo mengi na ya ukandamizaji ni kwamba mfalme atachukua kila kilicho cha kwanza kwao(kodi). Pia watakuwa watumwa kwa mfalme wakimtumikia (1Samweli 8:1-22).
  Sasa siku za mwisho yametabiriwa yale tunayoshuhudia leo yakitokea, mfano mabadiliko makubwa ya kimaumbile kama matetemeko, Vita, Njaa, ndugu kusalitiana, Kupenda pesa, watu kujifanya wataua huku wakizikana nguvu za Mungu nk. Kizazi cha Adamu kuja hapa tulipo kimepitia nyakati mbali mbali na mifumo mingi, katika kujiongoza, na kibaya zaidi ule mfumo wa kibepari ambao umekuwa kimbilio la wengi katika zamani zetu hizi, una kila dalili ya kuanguka. Ujamaa uliangika, ufashisti umeshindwa, ukomonisti umeshindwa, ubepari ndio huu unashindwa. Tunashuhudia maandamano kote duniani sasa hivi yenye kauli mbiu ''OCCUPY'' ambayo ni dhidi ya ubepari katika zile nchi tunazoziita tajiri. Ni dhahiri sasa, siasa za wanadamu zimeshindwa, viongozi wao nao wameshindwa, dini zao nazo zimeshindwa. Ndipo linapokuja swali ambalo sote tunatakiwa kuliwajibikia, je kuna haja ya kuingia katika fahamu zetu na kumrejelea Mungu ili atuongoze? Maana katika ile 1Samweli 8:7b inasema ''... Kwa maana hawakukukataa wewe [Samweli], bali wamenikataa mimi [Mungu] ili nisiwe mfalme juu yao''
  Nawakilisha!
  .
   
 2. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu.Hili swala linaweza kuangaliwa katika mitazamo mingi.
  Unapoliangalia katika mtazamo wa dini linahitaji kuomba muongozo kwa Mungu.
   
 3. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Your analysis of events ni sahihi.Lakini kabla Mungu mwenyewe hajaingilia kati,atamruhusu yule asi atawale kwa muda mfupi,to be exact for seven years.These seven years will be terrible times.Na kwa jinsi mambo yanavyo kwenda, hatuko mbali sana,jamaa ataiteka dunia.Mungu anafanya hivyo makusudi ili tufundishwe adabu, kwa vile tumemkataa. yeye.
   
 4. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  .
  Mkuu nimejikuta nikilazimika kulitizama katika mtizamo wa Ki- Mungu zaidi baada ya kutafakari na kuona Dini zimeshindwa kwa maana zipo nyingi na zinahitilafiana mno katika masuala ya msingi hata kufikia kuuana kwa sababu za tofauti zao. Siasa zimeshindwa kwani mifumo yote imeprove failure. Watawala wameshindwa maana hawakuweza kusimamia check and balance kwa watu.
  Ndipo wazo likaja Mungu ndio pekee hajawahi kushindwa, hivyo itakuwa sasahihi kwake na wakati muafaka kuchukua usukani.
  .
   
 5. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  .
  Mkuu naona wewe umejikita zaidi kwenye unabii wa wakati wa mwisho, hasa katika kipindi cha dhiki kuu. Hivi kipindi cha dhiki kuu kitakuwa miaka saba ama ni mitatu na nusu?
  .
   
Loading...