Dunia hadaa walimwengu shujaa

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
31,636
37,850
Wakuu katika kuperuzi peruzi mitandaoni nimekutana na hii kitu, nikasema basi sawa kizuri kula la nduguzo.. karibuni.

DUNIA HADAA WALIMWENGU SHUJAA

Yupo wapi Paul Makonda

Lile bwana lililojiona ni Alfa na Omega katikati ya Jiji la Dar, alijifanya yeye ni kila kitu, akatangaza watu wa mikoani kuto kuingia Dar bila kuoga? Akatangaza kupima wanaume tezi dume kwa Nguvu, akatangaza kufanya doria guest na Lodge kutazama wanao lala mchana , akatangaza kuchapa viboko Watumishi watakao dai Nyongeza ya Mishahara kwa serikali!

Huyu bwana ndio aliye bomoa Bilicanas Club ya Mh Freeman Mbowe miaka nenda Rudi, huyu ndio alievamia Clouds Media Group na Mabaunsa kwa mitutu ya bunduki, ndie aliemfukuzisha kazi kwa aibu Nape Nauye wizarani, na walinzi wake kumtolea bastola hadhalani leo anaishi Arusha Mkoani, akisafiri anakwenda Mwanza Kutazama miradi yake, hana cheo tena, hawezi kushurutisha watu kama watoto wake, hawezi kusindikizwa na ving'ora (escort) hakuna media zinamtafuta tena kutaka habari.

Yupo wapi Humphrey Polepole huyu ndie alie ikana katiba baada ya kupewa cheo na Makufuli, huyu ndie aliyemshauri Makufuli kuzuia mikutano ya kisiasa, huyu ndio aliye ratibu kukata majina ya wenyeviti wa mitaa na Uchaguzi Mkuu wapite bila kupingwa, huyu ndio katibu Mwenezi mwenye dharau na kibri...alikuwa akipiga picha yupo kwenye V8 huku akituuliza "mnaijua V8 ninyi!" Leo yukwapi ... alikuwa anauwezo wa kuingia mda wowote Ikulu na kutoka leo ni Mbunge vitumaalumu, anauliza swali la Nyongeza kwa Devid Silinde, Patrobas Katambi, Pauline Gekul,Mwita Waitara na Dr Molel

Sio tena polepole yule aliekuwa akiwasha mziki pale ofisini Lumumba anakata viuno akicheza kwa mbwembwe na Madaha, kiburi cha Madalaka, Leo hii wanapishana na Jerry Slaa kwenye chumba cha Maadili, amekosa nidhamu, Leo Polepole anatamani kupata Uhuru hata kwa kuonyesha uwezo wake wa kujenga hoja anakosa kibali hicho, Leo hii maisha yake yapo chini ya Ndugai na SSH kaona afunguwe "Darasa la Uongozi" kwenye Facebook yake😂😂😂

Yupo wapu Dr Bashiru Ally Katibu Mkuu CCM na Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu aliyehudumu kwa kipindi kifupi kuliko yeyote toka kupatikana kwa Uhuru, huyu ni Katibu Mkuu alie tumia cheo kama fimbo kwa chama chake ndie alikata majina 90% ya wana ccm walioshinda kura za maoni na kupachika wakwake, katibu ambae alikuwa anafanya Maamuzi pasipo vikao, katibu aliejaa kiburi na majigambo, Katibu aliyeitangaza ulimwenguni kuwa CCM itashinda hata kwa kutumia Dola.

Leo yupo Bungeni hana tena cheo kama Kibajaji Mbunge wa Mtela, hana tena Nafasi kama Deo Sanga wa (Makambako) toka ameingia hana sauti tena , hajawai kuuliza hata swali la Nyongeza, amekaa tu kwenye siti yake kama Mbunge wa Moshi Mjini, yupo kimya kama Mbunge wa Bahi, maisha yake yamebaki hayo.

Yupo wapi Lengai OLE Sabaya mtoto wa mjini! Mmasai alieamua kuwakata masikio vijana pale Hai akishirikiana na genge lake la kihalifu, kijana alieweza kulala hoteli yeyote bila kulipa bili, Kijana ambae anaweza kuondoka na Mrembo yeyote amtakae, kijana anaweza kuja kwako na kuchukua Kiasi Chochote cha pesa na huna pa kwenda kushtaki? Kijana anae weza kwenda Mkoa wowote na kumchukua yeyote bila mkuu wa Mkoa Kujua na asiulizwe na mamlaka yeyote!

Kijana aliyevamia Hotel ya Freeman Mbowe "Aishi Hotel" kwa mitutu ya bunduki na kuwapiga walinzi wa Hotel, kijana anaye weza Kubadili pletnumber za Gari yake na kuweka za UN kisha kuvamia Hotel wala wa kuhoji hakuna!

Huyo ndiyo Legai Ole Sabaya kijana aliyekuwa anajinasibu yupo Hai kwa kazi maalum na wala hakuna wa kumfanya chochote.

Leo yupo Mahabusu Kisongo pale Arusha yeye na Mabaunsa wake, maisha yanaendelea....

Yupo wapi Albert Chalamila yule Bwana aliejiona yeye ndio Mwamba wa Mbeya, yule aliejichukulia umaalufu wa kuchapa watu, yule aliepiga marufuku madaktari kutoa taarifa ya magonjwa ya mlipuko, yule alie injinia Mawakala wa sugu kwenye Uchaguzi kuwatoa na kuwatangaza wengine Ushindi kwa Mtutu wa Bunduki, yupo wapi .... Unajua watoto alio wafukuzisha Shule wanaishije mtaani , Hivi anakumbuka kauli aliyoisema kuwa "walokole wakitaka nao wanywe pombe mbombe tamu" baada ya kulalamikiwa kuwa Bar wanaoiga mziki mkuwa na kuharibu usikivu wa Ibada.

Kuna watu waliona Mtawala yule angeishi Milele na wao wakitesa maisha ya Madaraka milele alipo ondoka maisha yao yamekuwa magazeti kila mtu anataka kuyasoma, unapopata Madaraka jitaidi kuwa mtenda haki... "Haki na Ubaya vyote ni Mbegu vinaota na kutoa matunda."

Leo Mbowe yupo Segerea akisota Maabusu ya Magereza eti kwa makosa ya Ugaidi na uhujumu uchumi, walio na Madaraka kwa sasa wametamani iwe hivyo wakifikiri aliyepo watakuwa nae maisha yao yote.

"Madaraka ni kama mchanga. Jinsi unavyoukumbatia kiganjani ndivyo unavyokuponyoka"
 
Yuko wapi gaidi mbowe alichezea ruzuku na mabaunsa wakimzunguka ,akiwaaambia watu kunjangumikunga ngumi

Alisema watake wasitake katiba inapatikana

USSR
 
Hamna cha ajabu hapo boss , walikuwepo akina Napoleon , Hitler , na wengine wengi , washasahaulika , Nyerere mwenyewe amebak kwenye makaratasi hata hao waliopo ni suala la mda Tu watakaa pembeni , na kumbu kumbu Lao litasahaulika ,
 
Yuko wapi gaidi mbowe alichezea ruzuku na mabaunsa wakimzunguka ,akiwaaambia watu kunjangumikunga ngumi

Alisema watake wasitake katiba inapatikana

USSR
wenzako majina wanayo na bata wamekula mpaka dakika hii.

wewe na pepo lako la kiswahili,unahubiri kushuka kwao.
Mko wapi Mataga na sukuma gang! Mlizoea kuishi kwa posho ya buku 7 kwa siku, leo hii mnaishi kwa tozo kama sisi!
 
Yuko wapi gaidi mbowe alichezea ruzuku na mabaunsa wakimzunguka ,akiwaaambia watu kunjangumikunga ngumi

Alisema watake wasitake katiba inapatikana

USSR
acha fitna ndugu, maana hata chama chako kina mwiko unaosema " Nitasema ukweli daima fitna kwangu ni mwiko"
 
wenzako majina wanayo na bata wamekula mpaka dakika hii.

wewe na pepo lako la kiswahili,unahubiri kushuka kwao.
Masikini ni watu wapumbavu sana mkuu!

Fikiria mleta mada anawazodoa Polepole, Bashiru na Makonda?

Hao wako kwenye mrija wa fedha, ila kwa upumbavu wa mleta mada ana hisi wanashindia dagaa kama ilivyo familia na ukoo wake.
 
Maisha hubadilika,hayawezi kua yale yale,nahii ni toka enzi na enzi.
Sioni cha ajabu hapo,hao sio watu wa kwanza Duniani kubadilika katika maisha yao ya vyeo,
Umeandika kishabiki zaidi pengine labda umeamua kua mbunifu wa kujipa faraja kwa kujifariji.

Aksante kwa kuwafunza hawa vijana.
Hayo yapo enzi na enzi, zamani alikuwepo mmoja anyeitwa mfalme Nebkadreza wa Babiloni. Yeye alikuwa na nguvu nyingi sana. Mpaka akawaza kujenga mnara kwenda mbingu. Lkn madaraka yake yakachukuliwa na YULE mwenye nguvu zaidi ambaye humpa mamlaka yule ampendaye yeye. Akabaki bila mamlaka na kupewa adhabu ya kukaa mwituni na kula nyasi na kupigwa na jua, umande kama hayawani wa kondeni.
Kwa kifupi, mambo yanabadilika.
 
acha fitna ndugu, maana hata chama chako kina mwiko unaosema " Nitasema ukweli daima fitna kwangu ni mwiko"
Chama kitamjua wapi mtu mpuuzi kama huyu? Wenzake wanatoa facts yeye analeta hisia! Unamwita mtu gaidi wakati kesi anaendelea???
Nikujulishe tu kwamba hukumu ya MUSIBA ni leo, hukumu y sabaya ni 15.10.2021 na ile ya case ndogo ya mbowe ni 19.10.3021.
Kaa kwa kutulia
 
Maisha huwa yanabadlika kwa mtu yoyote yule naona we umeangalia kisiasa tu tena kwa upande wa chama kimoja
Lakin tukianza kuulizana wako wapi usikite hata we kuna mtu anauliza uko wapi ktokana na mambo flanflan uliyowahi kufanya na unayo yapitia kwa sasa
 
Na ndipo huwa naheshimu uwepo wa Mungu kwani hucontroo Hata vitu ambavyo Binadamu hatuwezi ili tu kubalance maisha
 
Masikini ni watu wapumbavu sana mkuu!

Fikiria mleta mada anawazodoa Polepole, Bashiru na Makonda?

Hao wako kwenye mrija wa fedha, ila kwa upumbavu wa mleta mada ana hisi wanashindia dagaa kama ilivyo familia na ukoo wake.
Kwanza umekosea kumuita mwenzio mpumbavu sababu tu huamini alichokisema. Pili kwa wao kama wanasiasa wamefeli na wanajilaumu, Bashiru hakutimiza hata mwezi kwenye ukatibu mkuu. Naamini Bashiru na Polepole walikuwa hawatumii mishahara yao kwenye maisha yao ya kila siku, leo hii wanamtegemea Ndungai. Sabaya na Makonda kiumri bado wadogo na wangehudumu kwenye siasa muda mrefu sana, anaglia watu wenye mipango kama Mkamba Jr. Na inawezekana wote hao ndio ikawa baibai kwenye siasa kwasasa.
 
Wakuu katika kuperuzi peruzi mitandaoni nimekutana na hii kitu, nikasema basi sawa kizuri kula la nduguzo.. karibuni.

DUNIA HADAA WALIMWENGU SHUJAA

Yupo wapi Paul Makonda

Lile bwana lililojiona ni Alfa na Omega katikati ya Jiji la Dar, alijifanya yeye ni kila kitu, akatangaza watu wa mikoani kuto kuingia Dar bila kuoga? Akatangaza kupima wanaume tezi dume kwa Nguvu, akatangaza kufanya doria guest na Lodge kutazama wanao lala mchana , akatangaza kuchapa viboko Watumishi watakao dai Nyongeza ya Mishahara kwa serikali!

Huyu bwana ndio aliye bomoa Bilicanas Club ya Mh Freeman Mbowe miaka nenda Rudi, huyu ndio alievamia Clouds Media Group na Mabaunsa kwa mitutu ya bunduki, ndie aliemfukuzisha kazi kwa aibu Nape Nauye wizarani, na walinzi wake kumtolea bastola hadhalani leo anaishi Arusha Mkoani, akisafiri anakwenda Mwanza Kutazama miradi yake, hana cheo tena, hawezi kushurutisha watu kama watoto wake, hawezi kusindikizwa na ving'ora (escort) hakuna media zinamtafuta tena kutaka habari.

Yupo wapi Humphrey Polepole huyu ndie alie ikana katiba baada ya kupewa cheo na Makufuli, huyu ndie aliyemshauri Makufuli kuzuia mikutano ya kisiasa, huyu ndio aliye ratibu kukata majina ya wenyeviti wa mitaa na Uchaguzi Mkuu wapite bila kupingwa, huyu ndio katibu Mwenezi mwenye dharau na kibri...alikuwa akipiga picha yupo kwenye V8 huku akituuliza "mnaijua V8 ninyi!" Leo yukwapi ... alikuwa anauwezo wa kuingia mda wowote Ikulu na kutoka leo ni Mbunge vitumaalumu, anauliza swali la Nyongeza kwa Devid Silinde, Patrobas Katambi, Pauline Gekul,Mwita Waitara na Dr Molel

Sio tena polepole yule aliekuwa akiwasha mziki pale ofisini Lumumba anakata viuno akicheza kwa mbwembwe na Madaha, kiburi cha Madalaka, Leo hii wanapishana na Jerry Slaa kwenye chumba cha Maadili, amekosa nidhamu, Leo Polepole anatamani kupata Uhuru hata kwa kuonyesha uwezo wake wa kujenga hoja anakosa kibali hicho, Leo hii maisha yake yapo chini ya Ndugai na SSH kaona afunguwe "Darasa la Uongozi" kwenye Facebook yake😂😂😂

Yupo wapu Dr Bashiru Ally Katibu Mkuu CCM na Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu aliyehudumu kwa kipindi kifupi kuliko yeyote toka kupatikana kwa Uhuru, huyu ni Katibu Mkuu alie tumia cheo kama fimbo kwa chama chake ndie alikata majina 90% ya wana ccm walioshinda kura za maoni na kupachika wakwake, katibu ambae alikuwa anafanya Maamuzi pasipo vikao, katibu aliejaa kiburi na majigambo, Katibu aliyeitangaza ulimwenguni kuwa CCM itashinda hata kwa kutumia Dola.

Leo yupo Bungeni hana tena cheo kama Kibajaji Mbunge wa Mtela, hana tena Nafasi kama Deo Sanga wa (Makambako) toka ameingia hana sauti tena , hajawai kuuliza hata swali la Nyongeza, amekaa tu kwenye siti yake kama Mbunge wa Moshi Mjini, yupo kimya kama Mbunge wa Bahi, maisha yake yamebaki hayo.

Yupo wapi Lengai OLE Sabaya mtoto wa mjini! Mmasai alieamua kuwakata masikio vijana pale Hai akishirikiana na genge lake la kihalifu, kijana alieweza kulala hoteli yeyote bila kulipa bili, Kijana ambae anaweza kuondoka na Mrembo yeyote amtakae, kijana anaweza kuja kwako na kuchukua Kiasi Chochote cha pesa na huna pa kwenda kushtaki? Kijana anae weza kwenda Mkoa wowote na kumchukua yeyote bila mkuu wa Mkoa Kujua na asiulizwe na mamlaka yeyote!

Kijana aliyevamia Hotel ya Freeman Mbowe "Aishi Hotel" kwa mitutu ya bunduki na kuwapiga walinzi wa Hotel, kijana anaye weza Kubadili pletnumber za Gari yake na kuweka za UN kisha kuvamia Hotel wala wa kuhoji hakuna!

Huyo ndiyo Legai Ole Sabaya kijana aliyekuwa anajinasibu yupo Hai kwa kazi maalum na wala hakuna wa kumfanya chochote.

Leo yupo Mahabusu Kisongo pale Arusha yeye na Mabaunsa wake, maisha yanaendelea....

Yupo wapi Albert Chalamila yule Bwana aliejiona yeye ndio Mwamba wa Mbeya, yule aliejichukulia umaalufu wa kuchapa watu, yule aliepiga marufuku madaktari kutoa taarifa ya magonjwa ya mlipuko, yule alie injinia Mawakala wa sugu kwenye Uchaguzi kuwatoa na kuwatangaza wengine Ushindi kwa Mtutu wa Bunduki, yupo wapi .... Unajua watoto alio wafukuzisha Shule wanaishije mtaani , Hivi anakumbuka kauli aliyoisema kuwa "walokole wakitaka nao wanywe pombe mbombe tamu" baada ya kulalamikiwa kuwa Bar wanaoiga mziki mkuwa na kuharibu usikivu wa Ibada.

Kuna watu waliona Mtawala yule angeishi Milele na wao wakitesa maisha ya Madaraka milele alipo ondoka maisha yao yamekuwa magazeti kila mtu anataka kuyasoma, unapopata Madaraka jitaidi kuwa mtenda haki... "Haki na Ubaya vyote ni Mbegu vinaota na kutoa matunda."

Leo Mbowe yupo Segerea akisota Maabusu ya Magereza eti kwa makosa ya Ugaidi na uhujumu uchumi, walio na Madaraka kwa sasa wametamani iwe hivyo wakifikiri aliyepo watakuwa nae maisha yao yote.

"Madaraka ni kama mchanga. Jinsi unavyoukumbatia kiganjani ndivyo unavyokuponyoka"
Usimsahau Kangi lugola waziri wa mambo ya ndani aliyemfukuza kikaoni mkuu wa magereza kwa kosa la kuchelewa
 
Kwanza umekosea kumuita mwenzio mpumbavu sababu tu huamini alichokisema. Pili kwa wao kama wanasiasa wamefeli na wanajilaumu, Bashiru hakutimiza hata mwezi kwenye ukatibu mkuu. Naamini Bashiru na Polepole walikuwa hawatumii mishahara yao kwenye maisha yao ya kila siku, leo hii wanamtegemea Ndungai. Sabaya na Makonda kiumri bado wadogo na wangehudumu kwenye siasa muda mrefu sana, anaglia watu wenye mipango kama Mkamba Jr. Na inawezekana wote hao ndio ikawa baibai kwenye siasa kwasasa.
Kwahiyo wamekomolewa?
 
Back
Top Bottom