Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,760
Wakongwe wa siasa za maji marefu CUF wamelitibua tena jeshi la polisi na kuhakikisha wamefanya kile walichokusudia kwa amani huku wakiwachezesha polisi kifura.
Polisi ambao walionekana kupania na kulinda kila kona walikuwa kila wanapotahamaki wanajiona wamechwa kwenye mataa ,mwisho walisikia habari kutoka kwa wasamaria wema kuwa CUF wameshatinga kwenye wizara na kuwasilisha rasimu sifuri ya Katiba.
Sasa wanangangari hao ambao wanajulikana kama dume la mbegu kwa sababu ya kutoa wanasiasa mashuhuri kwenda kwenye vyama vingine kama akina Shaibu Akwilombe,Wilfred Lwakatare Tambwe Hiza ,Jidawi na wengineo ambao wamepata umaarufu wa ksisiasa kupitia chama hicho cha CUF.
Msemaji wa CUF amesema sasa wametoa tena mbegu hiyo ya kufanya maandamano na vyama vingine viwache stori stori nyingi na blah blah ,viingie barabarani kwa salama na amani bila ya kuleta vurugu kwani maandamano ya amani yaliyofanywa na CUF hakukutokea malalamiko yoyote ya uharibifu au uvunjifu wa amani,ila kukurukakara ndogo tu ya kufurahishana na polisi ,jambo ambalo wanauzoefu nalo na wanalifanya kwa ustadi mkubwa kabisa.Hii ni mara ya tatu kwa wanangangari hao au kwa jina lingine wekundu wa Tanzania kufanya maandamano na kufikia lengo lao.