Dully sykes: Wasanii wengi hawajitambui

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Dully.jpg

Dully Sykes amewachana wasanii wenzake kwamba kinachowafanya washindwe katika tasnia ya muziki ni kutojitambua pamoja na kutokuwa na heshima.

Dully ameeleza hayo kutokana na uwepo wake wa kipindi kirefu bila ya kupotea au kupoteza kiwango chake katika suala zima la uimbaji tofauti na wasanii wengine ambao walikuwa pamoja kipindi cha nyuma lakini kwa hivi sasa wamepotezwa na upepo.

"Mimi najitunza, najielewa kama msanii, najitambua kwa kutengeneza 'status' yangu vizuri lakini wasanii wengi hawajitambui, mimi najitambua kuwa ni nani", alisema Dully

Kwa upande mwingine, Dully amewaasa vijana wa sasa wakubaliane na maisha wanayoishi ili waweze kuepukana na vishawishi vya utumiaji wa dawa za kulevya ambapo kwa sasa imekuwa ni janga la kila mahali.

Chanzo: EATV
 
Ni kweli kajitahidi sana kudumu kwenye muziki bila kuingia kwenye unga kama kina TID na wengine, mtoto wa uswahilini kuhimili vishindo vya muziki wake kupanda na kushuka bila kujilipua kweli anastahili pongezi, maana hata Makonda hakuwa na sababu za kumtaja kwenye list ya wahusika wa madawa, hataki utajiri wa haraka wala kulazimisha sifa..Tangu salome itoke niko shule mpaka leo aaaaa..mimi nampongeza kweli anajitambua.
 
Yeye pia mbona hajitambui? Mtu ana miaka zaidi ya 40 lakini anaishi kama mtoto mdogo.tabia za kitoto na hatabl kuimba hajui mbona? Sema wabongo wengi hawapendi msanii anayefanya muziki mzuri,wanapenda wasanii wanaoimba hovyo
 
Dully Sykes amewachana wasanii wenzake kwamba kinachowafanya washindwe katika tasnia ya muziki ni kutojitambua pamoja na kutokuwa na heshima.

Dully ameeleza hayo kutokana na uwepo wake wa kipindi kirefu bila ya kupotea au kupoteza kiwango chake katika suala zima la uimbaji tofauti na wasanii wengine ambao walikuwa pamoja kipindi cha nyuma lakini kwa hivi sasa wamepotezwa na upepo.

"Mimi najitunza, najielewa kama msanii, najitambua kwa kutengeneza 'status' yangu vizuri lakini wasanii wengi hawajitambui, mimi najitambua kuwa ni nani", alisema Dully

Kwa upande mwingine, Dully amewaasa vijana wa sasa wakubaliane na maisha wanayoishi ili waweze kuepukana na vishawishi vya utumiaji wa dawa za kulevya ambapo kwa sasa imekuwa ni janga la kila mahali.

Chanzo: EATV
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom