Dukani bei ya kilo moja ya mchele ni sawa na ya unga dukani

Eddy Love

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2011
Posts
13,655
Reaction score
8,584
Sasa hali tete haijawai kutokea kilo moja ya mchele kulingana na ile ya unga wa mahindi,hakika tutaisoma namba haswa maana mpaka sasa serikali haijatuambia sababu ya unga kupanda bei na kuwa sawa na bei ya mchele ambayo ni 1500/=
 
Hili swala la unga hata mm huwa najiuliza kuna nini? Toka uanze mwaka huu bei ilikuwa 1200 na haijawahi kushuka zaidi ya kupanda
 
Acha na wakulima tufaidi ndugu mwaka huu mahindi yamecheza kwenye 10,000 hadi 15,000 kwa sasa na hio ni bei ya mikoani kwa debe moja. Nyie mnapenda tulime kwa gharama halafu tuuze 7000 kwa debe moja? Hapana, acha nasi tufanye ya maana na hio ndio sababu kubwa kwa nyie wanunua sembe kuuziwa bei juu.
 
Mbna bei ya ugali na wali ni sawa kwa mamalishe tangu kitamboooo mbna hukushangaa. Fanya vya muhimu siyo kila kitu kupost tu
Watanzania bwana kwa kulalamika hatujambo. Nashangaa hapa ninapoishi India kuna tatizo la pesa hata benki unapiga foleni Na mwisho unaambiwa zimeisha. ATM hakuna kitu ila sioni manung'uniko. Ingekuwa Bongo nadhani JPM ashakimbia nchi. Wenzetu wanaendelea na kazi zao. Tujenge tabia ya kuvumilia.
 
Mbna bei ya ugali na wali ni sawa kwa mamalishe tangu kitamboooo mbna hukushangaa. Fanya vya muhimu siyo kila kitu kupost tu

Ingredients nyingi za wali na ugali ni tofauti kabisa kwa maana wali unazo nyingi kuliko ugali. Kwa hiyo bei ya unga na mchele kuwa sawa haziwezi kupelekea ugali na wali kuuzwa sawa labda kama bei ya chumvi au mafuta au maji itakuwa imeshuka au bei ya hivyo vyote kushuka. Pia aina ya energy inayotumika kuandaa vyakula hivyo yaweza kuchangia ongezeko la bei la ugali.
 
Hili swala la unga hata mm huwa najiuliza kuna nini? Toka uanze mwaka huu bei ilikuwa 1200 na haijawahi kushuka zaidi ya kupanda
hapo ndipo mie panaponishangaza hata mazao yaongezeke vipi bei haishuki ila inapanda
 
Maisha bora kwa kila Mtanzania. Tunafanya savings ya kujenga viwanda.Ngoja tumalizane na tumbuatumbua, kunyoosha wawekezaji uchwara, kunyoosha watumishi wa umma, kunyoosha ukabila na ukanda, endless!!!! Viwanda .....viwanda...😡😡🙁🙁🙂
 
Acha na wakulima tufaidi ndugu mwaka huu mahindi yamecheza kwenye 10,000 hadi 15,000 kwa sasa na hio ni bei ya mikoani kwa debe moja. Nyie mnapenda tulime kwa gharama halafu tuuze 7000 kwa debe moja? Hapana, acha nasi tufanye ya maana na hio ndio sababu kubwa kwa nyie wanunua sembe kuuziwa bei juu.
kama bei imekuwa hiyo it means mahindi uzalishaji umepungua
 
Ingredients nyingi za wali na ugali ni tofauti kabisa kwa maana wali unazo nyingi kuliko ugali. Kwa hiyo bei ya unga na mchele kuwa sawa haziwezi kupelekea ugali na wali kuuzwa sawa labda kama bei ya chumvi au mafuta au maji itakuwa imeshuka au bei ya hivyo vyote kushuka. Pia aina ya energy inayotumika kuandaa vyakula hivyo yaweza kuchangia ongezeko la bei la ugali.
ni ngumu kukuta wali na ugali bei sawa kwa mama ntilie huyo jamaa mpuuzie
 
Ingredients nyingi za wali na ugali ni tofauti kabisa kwa maana wali unazo nyingi kuliko ugali. Kwa hiyo bei ya unga na mchele kuwa sawa haziwezi kupelekea ugali na wali kuuzwa sawa labda kama bei ya chumvi au mafuta au maji itakuwa imeshuka au bei ya hivyo vyote kushuka. Pia aina ya energy inayotumika kuandaa vyakula hivyo yaweza kuchangia ongezeko la bei la ugali.
kwani ugali na wali ni kipi chenye ingredients nyingi mkuu
 
Michele umeshuka nilitegemea unga ushuke zaidi nimejifunzs ungs muhimu zaidi Michele mijini tu
 
Afadhali, sasa hakutakuwa na sababu kwanini hatuli wali wakati ni sawa tu na kula ugali
 
Back
Top Bottom