Duh! Wapogoro na sangura

Dini pekee ambayo haikupumbazwa na wageni kuacha na kudharau tamaduni zetu za asili ni KANISA KATOLIKI. wanajua tofauti ya maneno ya Mungu na tamaduni za waliotuletea imani

1. Kuna baadhi ya dini hasa walokole wanataka kujilinganisha na kumuiga mzungu mpaka anavyoshindwa kutamka vizuri kiswahili mfano mzungu hawezi kusema Jioni ya leo , yeye atasema chioni ya leo. Sasa unakuta liswahili jeusi tii kama lami linahubiri na lenyewe linasema CHIONI YA LEO , au CHINA badala ya jina. Ni kanisa katoliki pekee mtoto hubatizwa kwa jina la kimila na sii kuchukua kila kitu kwa wazungu.

2. Unakuta baadhi ya watanzania wamedharau kabisa tamaduni zao na wanajiona wao ni waarabu, kwa mavazi, lugha ndio kabisaa kila akiongea anatafuta msamiati wa kiarabu ili kujionyesha kuwa amestaarabika. Mbaya zaidi kuna watangazaji wa tv na redio ndio unakuta wanajikanyaga kwelikweli kutafuta msamiati na kiarabu kwenye matangazo. Lazima tukumbuke kuwa Mungu aliumba kila jamii na makusudi yake na akaipa mila na lugha ili wawasiliane wao kwa wao na wawasiliane na Mungu.

Sasa Mungu anatushangaa katupa utajiri wa Lugha, kisukuma, kirangi , kinyaturu , kichaga ,kihaya, kiha kimanyema, kingoni kizaramo, kinyakyusa nk lakini tunakomaa kusali kwa kutumia kilatini, kiingereza na kiarabu basi Mungu badala ya kuleta baraka kwetu anapeleka kwa wale tunaotumia Lugha na mila zao
 
Back
Top Bottom