Duh! Hii hatari sasa.......

mansolata

JF-Expert Member
Aug 8, 2016
503
317
Habar wakuu
Karibuni

Miezi ya hivi karibu maisha yamekua magumu sana kwa upande wangu! .. Siteuliwi kushiriki semina..michongo ninayopanga inatibuka...Ofisini vikao haviishi...dah! kero tupu.........Ooooooh Tanzaniaaaaa!

Baada yakuona mambo yanazidi kubana nikakumbuka kujizimua labda betri low!
Weekend iliyopita nikaanza safari ya kwenda kijijini kwa MGANGA wangu aliyenisaidia kupata kibarua hiki kinachofanya wengi wetu tuishi mjini .....
Nilipokaribia kijiji husika nilishtuka kuona private car ya Boss wangu ikiwa imepak hatua chache kutoka kwa MGANGA.....haraka sana niligeuza na kukasweka porini kausafiri kangu huku nikishusha pumzi na kutafakari " loooh! kumbe huyu boss nae anajizimua!....niliwaza...
Nilijaribu kupeleleza nikagundua kua Boss alikuja na mkewe ambae pia ni mfanyakazi mwenzetu tena hua haipiti miezi 3 bila kufika pale...na hata nyumba anayoishi MGANGA kwa sasa ni kwa hisani ya Boss .....Nikawaza MGANGA huyu hatonisaidia tena bali atanidanganya tu.......
Niligeuza gari yangu na kwenda kwa MGANGA mwingine jirani na kijiji kile...Nikiwa reception ya MGANGA huyu ...ghafla gari ya Boss ilitia team wasaidizi wote wa MGANGA walikwenda kumlaki...
..Boss alifika kilingeni huku akitoa shukrani nyiiingi na pongezi kwa kazi alizowai kufanyiwa na MGANGA huyu nae!!! " nikikooa tu wote kimya " Boss alisikika akisema..Boss alifungua begi lake na kutoa kitita kisicho pungua million 10 kwa uzoefu wangu... na kutumbukiza kikapuni kilicho pembezoni mwa MGANGA..

MGANGA alimuamuru msaidizi wake atueleze sisi tunaosubiri huduma turudi makwetu hadi siku inayofuata kwa kua mizimu imepata ugeni Mkubwa...
.Nilipofunuliwa kipande cha kaniki ili niweze kutoka nje ya kilinge macho ya Boss yalikutana na macho yangu hafla akawa mpole .. Nikainuka na kutoka nje ,,,,,,,Boss alinifuata!!!!!

Boss: unakujua huku?
Mimi: ndiyo
Boss: iwe siri basi
Mimi:sawa
Boss: tutayapanga tukiwa ofisi
Mimi: sawa Mkuu (nikawasha gari na kuanza safari

Jumatatu ilipofika nilipata wito ukinidai nifike Ofisini kwa Boss.....
Nilifika Boss aliniahidi mengi sanaili nisitoe siri....
Leo hii nimepata barua ikinitaka nishiriki kwenye semina nje ya nchi mwezi ujao ...
Hapa nipo kwenye maandalizi ya safari .....

NB: Ushirikina umekithiri jamani hususan maofisini ....wanajidai wanafatamiongozo ya dini kumbe hatareee......!!!!!
 
Waganga wapo na nguvu za kiganga zipo.
Ila tu ukutane na mganga wa kweli ila ukikutana na matapeli ni taabu tupu.
 
Back
Top Bottom