only83
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 5,343
- 2,525
...Jana usiku nilifanikiwa kukinasa kipindi kimoja kinachochambua movie za kibongo kwenye CLOUDS TV chini ya mtangazaji mmoja Zamaradi Mketema kama sijakosea...Na mgeni mmojawapo alikuwa Dude..Katika ya moja ya maswali aliyoulizwa ilikuwa,Je unaionaje tasini ya Movie za Kibongo na wasanii wake kwasasa? Jamaa alijibu kuwa fani imevamiwa na machangudoa na wahuni..akasema badala ya wasanii kuwa kioo cha jamii sasa wamekuwa ni wachafuzi wa jamii..Na moja kwa moja akatolea mfano wa huyu mdogo watu na dada yetu LULU..akasema ni mtoto mdogo lakini mambo anayofanya ni aibu kwa jamii..akaendelea kusema jamii ya sasa imekosa maadili,maana wanashabikia ujinga na ushenzi anaofanya huyu binti..akasema namnukuu "WASANII WAKUBWA WANAMCHUKUA HUYU BINTI KWENDA KUFANYA NAE KAZI,BADALA YA KUFANYA KAZI WANAMTUMIA KAMA SEHEMU YA KUJISTEREHESHA" akaendelea kusema sasa hivi ukiwa mweupe ndio unaonekana unafaa kuigiza, na kwasababu hiyo machangudoa ndio wanapata nafasi ya kutamba kwasasa kwenye hii tasnia kwa kuwa wanatumia madawa ya mchina kuongeza weupe wao...na hata wanaume kwasasa wanautafuta weupe kama ambavyo mnaona...kimsingi huyu jamaa alinigusa sana kwasababu ya kinachoendelea kwasasa kwenye bongo movie...Jaribu kufatilia kashfa za hawa mabinti ni kinyaa...badala ya hawa wasanii kuwa kioo sasa wanakuwa giza mbele yetu...