...dude wa bongo dsm umenena yaliyo mema..........

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
...Jana usiku nilifanikiwa kukinasa kipindi kimoja kinachochambua movie za kibongo kwenye CLOUDS TV chini ya mtangazaji mmoja Zamaradi Mketema kama sijakosea...Na mgeni mmojawapo alikuwa Dude..Katika ya moja ya maswali aliyoulizwa ilikuwa,Je unaionaje tasini ya Movie za Kibongo na wasanii wake kwasasa? Jamaa alijibu kuwa fani imevamiwa na machangudoa na wahuni..akasema badala ya wasanii kuwa kioo cha jamii sasa wamekuwa ni wachafuzi wa jamii..Na moja kwa moja akatolea mfano wa huyu mdogo watu na dada yetu LULU..akasema ni mtoto mdogo lakini mambo anayofanya ni aibu kwa jamii..akaendelea kusema jamii ya sasa imekosa maadili,maana wanashabikia ujinga na ushenzi anaofanya huyu binti..akasema namnukuu "WASANII WAKUBWA WANAMCHUKUA HUYU BINTI KWENDA KUFANYA NAE KAZI,BADALA YA KUFANYA KAZI WANAMTUMIA KAMA SEHEMU YA KUJISTEREHESHA" akaendelea kusema sasa hivi ukiwa mweupe ndio unaonekana unafaa kuigiza, na kwasababu hiyo machangudoa ndio wanapata nafasi ya kutamba kwasasa kwenye hii tasnia kwa kuwa wanatumia madawa ya mchina kuongeza weupe wao...na hata wanaume kwasasa wanautafuta weupe kama ambavyo mnaona...kimsingi huyu jamaa alinigusa sana kwasababu ya kinachoendelea kwasasa kwenye bongo movie...Jaribu kufatilia kashfa za hawa mabinti ni kinyaa...badala ya hawa wasanii kuwa kioo sasa wanakuwa giza mbele yetu...
 
Ni kweli kabisa alichokisema,wengi wao siyo wote ni kuuza sura tu,nakumbuka kuna siku nilikuwa naangalia tangazo la kipindi cha Bongo Movie, kuna muigizaji mmoja jina limenitoka akasema kama mwanamke huna mvuto na mengineyo hufai kuwa muigizaji,nimenukuu hapo,kwani kuigiza kwa mtu katika tasnia hiyo ni kuvitia watu au nakuelimisha jamii unamvutia mtu upande upi,katika kuhakikisha unaitendea haki tasnia hiyo au kutaka uonekane una mvuto kimapenzi.

Hili ni janga na matokeo yake wengi wasipoangalia si wote,kwa wale ambao wanafikiri hiyo ni ajaira ya kwenda kutembeza kilichofunikwa na nguo ya ndani tutawazika kwa magonjwa ya Zinaa ikiwemo UKIMWI.
Kweli inasikitisha sana

Hongera DUDE kwa kuliona hili na usichoke kukemea tabia mbaya za hawa watu kwa kutumia fursa hii kama ajira na baadaye kuidhalilisha.
 
ni kweli kabisa alichokisema,wengi wao siyo wote ni kuuza sura tu,nakumbuka kuna siku nilikuwa naangalia tangazo la kipindi cha bongo movie, kuna muigizaji mmoja jina limenitoka akasema kama mwanamke huna mvuto na mengineyo hufai kuwa muigizaji,nimenukuu hapo,kwani kuigiza kwa mtu katika tasnia hiyo ni kuvitia watu au nakuelimisha jamii unamvutia mtu upande upi,katika kuhakikisha unaitendea haki tasnia hiyo au kutaka uonekane una mvuto kimapenzi.

Hili ni janga na matokeo yake wengi wasipoangalia si wote,kwa wale ambao wanafikiri hiyo ni ajaira ya kwenda kutembeza kilichofunikwa na nguo ya ndani tutawazika kwa magonjwa ya zinaa ikiwemo ukimwi.
Kweli inasikitisha sana

hongera dude kwa kuliona hili na usichoke kukemea tabia mbaya za hawa watu kwa kutumia fursa hii kama ajira na baadaye kuidhalilisha.

siku hizi haifunikwi hata na hiyo nguo ya ndani! Unaweza kuwazia ni jinsi gani imekuwa rahisi kuifikia na kuipata
 
Elimu zero ulimbukeni mia kwa mia. Kipato kidogo kulinganisha walikotoka kinawachanganya na kusahau misingi ya kazi yao na umuhimu wa maadili ya jamii. Elimu jama elimu!
 
Shida yao hawa wasanii wa kibongo wanataka cheap popularity. Siyo tu huyo Lulu, pamoja na wasanii wengine kibao, hawajali kuelimisha jamii, wao wanachotaka ni kujulikana. Na ndio maana wengine wakiact hupati feeling kwamba unaangalia something real, inakuwa kama unamuona vile pembeni ya camera akihangaika.
 
Nyingi kwanza ni copy and paste from Nigeria.Alafu wanatafuta umaarufu usio na tija.Then wengi nafikiri frm4 point32 kwa hiyo nafikiri wengi ni mamc kwenye sherehe na k.party.Kwa hiyo usitegemee kupata movie yenye maadili kabisa.
 
Ni kweli kabisa alichokisema,wengi wao siyo wote ni kuuza sura tu,nakumbuka kuna siku nilikuwa naangalia tangazo la kipindi cha Bongo Movie, kuna muigizaji mmoja jina limenitoka akasema kama mwanamke huna mvuto na mengineyo hufai kuwa muigizaji,nimenukuu hapo,kwani kuigiza kwa mtu katika tasnia hiyo ni kuvitia watu au nakuelimisha jamii unamvutia mtu upande upi,katika kuhakikisha unaitendea haki tasnia hiyo au kutaka uonekane una mvuto kimapenzi.

Hili ni janga na matokeo yake wengi wasipoangalia si wote,kwa wale ambao wanafikiri hiyo ni ajaira ya kwenda kutembeza kilichofunikwa na nguo ya ndani tutawazika kwa magonjwa ya Zinaa ikiwemo UKIMWI.
Kweli inasikitisha sana

Hongera DUDE kwa kuliona hili na usichoke kukemea tabia mbaya za hawa watu kwa kutumia fursa hii kama ajira na baadaye kuidhalilisha.

huyo ni RAY alisema iyo ki2
 
bongo movies zinahamasisha ngono tu hamna lolote. Mamlaka zinazohusika kuscreen movies zimesinzia mpaka basi!
 
Huwa siangalii kabisaa! Hata bongoflavor sijui kama nimeipatia! yani tangu kipindi kile sugu,afande,baloz,nature,nk wanaimba music halisi kizazi kipya ndio nilikuwa nasikiliza laki tangu waingie hawa wanaobana pua na kujichubu nimeamua kuwa muumini wa rege!
 
Ni kweli kabisa nowdays naona wasanii wanachukua advantage na ndio mwisho wa dunia kwa kweli,maana kuna movie inaitwa PRETTY GIRL NA OFF SIDE kuna huyu IRENE UWOYO kuna part kavaa nguo lakini chupi zinaonekana na nguo zingine kavaa maziwa yanaonekana hata bra hajavaa kabisa kwa kweli imeniudhi sana na hizi movie hazifai kuangalia mbele ya watoto, ni movie chafu kabisa

Kitu kingine kingereza wasanii wetu hawajui kabisa na wanaudhi sana wanavyochanganya kingereza na kiswahili kama wanataka waongee lugha moja kama ni kiswahili basi iwe kiswahili na kama ni english basi iwe english....
 
unajua wa TZ tumeingiwa na shetani mbaya saaana hii hata makazini. mwanamke akiwa na makalio makubwa na akiwa mweupe au akiwa navyo vyote basi ataonekana ni almasi kazi nzuri atapata km akifanikiwa kuonyesha live alichopewa na mama yake yaani kugawa uroda. na wanawake type hiyo washajua udhaifu wa wanaume atajirahisi ili umtimizie anachotaka. kinachotokea kwenye bongo movies ni hicho hicho ma producer karibu wote na hawa akina kanumba na ray wakikutana na msichana wa aina hiyoo ili wampate kirahisi watamsifia jinsi alivyo na kumchomekea kwamba akiingia kwenye uigizaji atabamba saaana na wao wana uwezo wa kuwatoa mpakawakaja kuwa almaarufu. demu kwa ahadi hizo ataachia kitumbua halafu anaingizwa kwenye game baada ya hapo ni sisi watazamani wa hizo movies kubata ushungu tu ni maonesho tu ya ma bambataa yao vimini na kukaa nusu uchi. sasa mtu km wema sepetu kila baada ya miezi miwili ana bwana mpyaa kweli atapona huyu na kanumba ndiye aliyemwingiza kwenye game.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom