Dua Zaidi Kwa Samatta .

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,249
Samatta amecheza mechi ya 14 tangu ajiunge na Genk akitoka kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na TP Mazembe pamoja na kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika.

Katike mechi hizo, ambazo saba tu ndiyo ameanza, mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam, amefunga mabao manne tu..........mbaya zaidi alianza kuaminiwa kucheza 90 sasa ndio hivyo tena

SAMATTA ACHEZA KWA DAKIKA 45 TU, GENK YAPIGWA 2-1

Na Mwandishi Wetu, ROESELARE

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amecheza kwa dakika 45 tu, timu yake KRC Genk ikifungwa mabao 2-1 na KV Oostende katika mchezo wa Ligi ya mchujo Ubelgiji kufuzu michuano ya Ulaya usiku wa Jumamosi Uwanja wa Schiervelde mjini Roeselare.

Samatta alitolewa baada ya kipindi cha kwanza na nafasi yake kuchukuliwa na Mgiriki Nikolaos Karelis, wakati huo Genk inaongoza 1-0 kwa bao la Mbelgiji Thomas Buffel aliyefunga dakika ya 25.

Samatta amecheza lkwa dakika 45 Jumamosi KRC Genk ikifungwa 2-1

Lakini akiwa benchi, Samatta aliishuhudia Genk ikifungwa mabao mawili kipindi cha pili la kwanza na Mzimbabwe Knowledge Musona dakika ya 71 na la pili na Jordan Lukaku dakika ya 90 na ushei.

Samatta leo amecheza mechi ya 14 tangu ajiunge na Genk akitoka kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na TP Mazembe pamoja na kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika.

Katike mechi hizo, ambazo saba tu ndiyo ameanza, mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam, amefunga mabao nne, moja katika kila mechi Genk ikishindia 2-1 ugenini dhidi ya wenyeji SV Zulte-Waregem, 4-0 na 4-1 dhidi ya KV Oostende na 3-2 dhidi ya Club Brugge mchezo wa kwanza.
 
Tutamuombea lakini naye asibweteke
Samatta amecheza mechi ya 14 tangu ajiunge na Genk akitoka kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na TP Mazembe pamoja na kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika.
Katike mechi hizo, ambazo saba tu ndiyo ameanza, mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam, amefunga mabao manne tu..........mbaya zaidi alianza kuaminiwa kucheza 90 sasa ndio hivyo tena
 
hiyo Genk nayo anaeingia sub ya Samata wa kawaida sana...Knowledge musoma alikua mfungaji bora South Africa sio mzuri kivile ila kapewa namba hapo ya kudumu anatupia tuu...mimi nashindwa kumuelewa yule kocha wa Genk wachezaji wanaonesha hali ya kumuamini Samata ila yeye sijui labda maujuzi yake...
 
najua Asamoah alikubalika sana lakini kwa kuwa alikua anakosa sana magoli akauzwa na ndio kasumba ya makocha wengi
 
najua Asamoah alikubalika sana lakini kwa kuwa alikua anakosa sana magoli akauzwa na ndio kasumba ya makocha wengi
Asamoah aliuzwa wapige hela mkuu China kumbuka aliuzwa bei gani...Giroud asingecheza Arsenal au welbeck maana wanashika vichwa hawa jamaa hatari..
 
hiyo Genk nayo anaeingia sub ya Samata wa kawaida sana...Knowledge musoma alikua mfungaji bora South Africa sio mzuri kivile ila kapewa namba hapo ya kudumu anatupia tuu...mimi nashindwa kumuelewa yule kocha wa Genk wachezaji wanaonesha hali ya kumuamini Samata ila yeye sijui labda maujuzi yake...
Samatta tatizo anakosa sana magoli ya wazi
 
asibweteke kama hasheem thabit...aongeze juhudi zaidi.. asishindane na alikotoka...+ pombe
 
...huyo kocha ndio amejaa presha,mchezaji yeyote mpe nafasi acheze angalau dakika 70,hiyo sub aliyofanya ni uoga tu hajiamini,hope atajifunza kwa hicho kichapo.
 
huyo kocha sio wewe mzimbabwe katika iyo timu waliyoifunga Genk amepewa mikoba yote na atoki na ni mchezaji wa kawaida daa samata mzee utadhani mchezaji wa kawaida tuu sub ya kwanza yeye na yabaki magarasa tuu ndani...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom