Manumbu ni kweli tumeshafikia huko. kuna mwandishi wa habari na mpiga picha photojournalist alishinda tuzo ya Pulitzer award kwa picha bora ambayo ilikuwa inamwonyesha mtoto mwenye utapiamlo mkali ambaye alikuwa hawezi hata kutembea, alikuwa anatambaa kwenda kwenda kwenye kituo cha kutolea msaada wa chakula km moja hivi mbele yake. Tai kwa kujua kwamba lazima atakufa kabla hajafika kambini wakawa wamejaa angani wanamsindikiza ili akifa wale mzoga wake. Jamaa alipiga picha akapata zawadi, lakini baadae wakamwuliza alifanya nini baada ya kupiga picha kuhakikisha kwamba anachangia katika jitihada za mtoto yule kupata msaada? hakujibu maana yeye alisepa zake kuwahi town kutuma picha CNN, BBC, Reuters na kwingineko. nafsi ilimsuta sana maana anajua fika dogo ajigeuka mlo wa wale scavengers, akaamua kujiua!! Nadhani kuna watu wanajua hii stori watatuwekea link yake hapa.