Drone saba za Yemen zashambulia Saudi arabia

Drone saba za Yemen zashambulia Saudi arabia

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,190
Reaction score
24,620
'Drone' za Yemen zashambulia maeneo muhimu ya Saudia
Mei 14, 2019 11:36 UTC
Jeshi na kamati za kujitolea za wananchi wa Yemen zimelipiza kisasi cha jinai zinazofanywa na Saudi Arabia na wavamizi wenzake nchini humo, kwa kushambulia maeneo muhimu ya Saudi Arabia kwa kutumia ndege zisizo na rubani 'drone'.
Duru za kijeshi zimeiambia kanali ya televisheni ya al-Masirah kuwa, vikosi vya Yemen vimetumia 'drone' saba kutekeleza mashambulizi hayo.
Hata hivyo vyanzo hivyo vya habari havijatoa maelezo kuhusu maeneo hayo ya Saudia yaliyolengwa, wala wakati ilipofanyika hujuma hizo.
Vikosi hivyo vya Yemen vimesisitiza kuwa, maadamu vikosi vamizi vinaendelea kuiweka chini ya mzingiro nchi hiyo maskini ya Kiarabu, navyo vitaendelea kufanya mashambulio ya aina hiyo.
Saudi Arabia ikisaidiwa na Marekani, Israel, Imarati na nchi nyingine kadhaa iliivamia kijeshi Yemen mwezi Machi mwaka 2015, na hadi sasa maelfu ya raia wasio na hatia wa nchi hiyo wameuawa na mamilioni ya wengine wamelazimika kuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi hiyo.
Mbali na mauaji, mzingiro mkubwa wa Saudia na waitifaki wake dhidi ya Yemen umeifanya nchi hiyo maskini ikabiliwe na uhaba mkubwa wa chakula, dawa na milipuko ya magonjwa ya aina mbalimbali na hivyo kusababisha maafa ya kibinadamu nchini humo.
4bshf1f5a81cdc1f5sv_800C450.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom