Dreamliner ATCL yatumwa Sudan

Dreamliner ATCL yatumwa Sudan

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
29,969
Reaction score
34,096
May 16, 2019
Dar -es-Salaam, Tanzania

Ndege ya ATCL aina ya Boeing 787 Dreamliner yaenda Sudan kupeleka wanajeshi ktk jimbo la Darfur kulinda amani. Boeing 787 Dreamliner ya ATCL ni ndege mahsusi ya abiria yenye uwezo wa kwenda masafa marefu lakini hii ni mara ya kwanza kushiriki ktk operesheni za kijeshi kwa ajili ya ulinzi wa amani.

Akizungumzia ushiriki wa Tanzania ktk kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa, mkuu wa operesheni na mafunzo ktk JWTZ, Major General Alfred Fabian Kapinga amesema huu ni mwaka wa 12 mfululizo toka Tanzania ihusike ktk kampeni za ulinzi wa amani chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa.

Tanzania ina vikosi chini ya Umoja wa Mataifa kulinda amani ktk nchi za Lebanon, Central African Republic, Sudan na DR Congo. Na katika kupeleka vikosi imekuwa ikitumia ndege za JWTZ na zingine zilizokodishwa na Umoja wa Mataifa. Hii ni mara ya kwanza ATCL kutumika na kutakuwepo mwendelezo wa ATCL kutumika ktk misheni za ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa ATCL amesema wamefarijika shirika kupata tenda ya Umoja wa Mataifa kusafirisha walinzi wa amani. Amelishukuru jeshi JWTZ na wadau wengine waliofanikisha kupata kazi hii inayoshindaniwa na mashirika mengi ya ndege duniani ktk kufanya kazi za Umoja wa Mataifa.
 
Mkuu tunataka tujumlishe wenyewe mapato maana mabeberu wanatudukua, so tujulishwe kabisa ATC wameweka kimbindoni shi ngapi..
 
Where is uniformity? Nchi yetu imechoka kiasi cha kushindwa kuwapa wote ma-backpack ya kijeshi ya aina moja? Naona wengine wanaingia na asante mmachinga kwenye ndege!
 
Yaani kodi za wananchi ndo zinachezewa hivi, shenzi kabisa
 
May 16, 2019
Ndege ya ATCL aina ya Dreamliner yaenda Sudan kupeleka wanajeshi ktk jimbo la Darfur kulinda amani.

Akizungumzia ushiriki wa Tanzania ktk kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa, mkuu wa operesheni ktk JWTZ Major General Alfred Fabian Kapinga amesema huu ni mwaka wa 12 toka Tanzania ihusike ktk kampeni za ulinzi wa amani chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa.

Tanzania ina vikosi chini ya Umoja wa Mataifa kulinda amani ktk nchi za Lebanon, Central African Republic, Sudan na DR Congo. Na kati kupeleka vikosi imekuwa ikitumia ndege za JWTZ na zingine zilizokidishwa na Umoja wa Mataifa. Hii ni mara ya kwanza ATCL kutumika na kutakuwepo mwendelezo wa ATCL kutumika ktk misheni za ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa.
UN watakua wamelipia ,sio mbaya
Ni
 
Ndege yetu ikatokea inatunguliwa,lawama kwa nani?! Kwa nini wasipelekwe na ndege za UN ambazo zinatambulika na kisheria haziruhusiwi kushambuliwa?!

Tumekosa safari za kimataifa zenye tija hadi tuvizie mara kupeleka mbuzi Dubai na sasa wanajeshi Sudan?! Je safari hizo ni endelevu kwa wiki ama mwezi mara ngapi?!
 
Ndege yetu ikatokea inatunguliwa,lawama kwa nani?! Kwa nini wasipelekwe na ndege za UN ambazo zinatambulika na kisheria haziruhusiwi kushambuliwa?!

Tumekosa safari za kimataifa zenye tija hadi tuvizie mara kupeleka mbuzi Dubai na sasa wanajeshi Sudan?! Je safari hizo ni endelevu kwa wiki ama mwezi mara ngapi?!
Tulia mkuu! Kama tumelipwa kwa usahihi hamna shida,tuombe waendelee kutupa dili kuliko kuziacha ziozee uwanjani,kila biashara ina risk zake,ikitunguliwa basi ni ajali kazini! Ila labda tu tuambiwe ile 10 percent imeenda kwa nani! Maana ni obvious
 
Back
Top Bottom