DRC: Kanisa katoliki lapinga waliopata ujauzito kurudi shule

DRC: Kanisa katoliki lapinga waliopata ujauzito kurudi shule

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, limepinga agizo la serikali, kuwataka wasichana waliopata mimba kuendelea na masomo.

Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki CENCO, limesema Shule zake hazitatekeleza agizo hilo la serikali.

Kupitia barua ya wazi, walioijibu serikali kupitia Wizara ya Elimu, Kanisa Katoliki ambalo lina Shule zaidi ya 18, 000 linasema, agizo hilo la serikali linakwenda kinyume na kanuni za kupata elimu nchini humo.

Aidha, Kanisa hilo linasema kuwaruhusu wasichana waliopata mimba kuendelea na masomo, wakiwa wajawazito, kutasababisha upotofu mkubwa wa maadili na nidhamu miongoni mwa wanafunzi.

Kanisa hilo linasisitiza kuwa halitakuwa tayari, kuwa na msichana mjazito darasani, na badala yake, watakaokuwa katika hali hiyo, watahamishiwa kwenye shule za serikali.

Mvutano huu unakuja wakati huu Katiba ya DRC, ikitoa usawa wa watu wote kupata elimu lakini kwa muda mrefu wasichana wajawazito wamekuwa wakitengwa na kuacha masomo
 
Kanisa Katoliki pekee yake linazo shule 18k yaani; halafu muhuni mmoja utakuta kashiba zake kahawa na kababu, atakwambia Congo ina mfumo Kristo, inazuia wa dini ya myaazimungu wasisome; pumbafu
 
Hapa sasa ndio tawajua vizuri wanafiki.

Hili aliwahi kulipitisha jiwe huku na alikosewa sana tena saaaana.

Ngoja nikae kwa huu uzi ili nione rangi za ndugu zangu watz zilivyo.
 
Wakatoliki bhana,mara injili kidogo,mara siasa kidogo ,mara mimba za shuleni kidogo, duh!
 
Si wanasema katoliki ni la wote hadi wenye dhambi wanakaribishwa? Vipi tena mimba iwe dhambi isiyosameheka?
 
Back
Top Bottom