DRC: Jaji aliyemhukumu Katumbi adai alishinikizwa na Majasusi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
140501174620_moise_katumbi_640x360__nocredit.jpg

Jaji aliyemhukumu Katumbi adai alishinikizwa
Jaji mmoja wa mahakama ya juu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekiri kuwa alishinikizwa na majasusi na wakuu wake katika idara ya mahakama kumpata na hatia kiongozi wa upinzani Moise Katumbi.

Jaji Chantal Ramazani alikuwa miongoni mwa jopo la majaji waliokuwa wakisikiza kesi hiyo dhidi ya katumbi ambaye hakuwa mahakamani.

Jopo hilo la majaji lilimpata Katumbi na hatia na kumhukumu kifungo cha miaka mitatu gerezani kwa kuuza mali kinyume cha sheria.

Bi Ramazani, sasa hivi yuko mafichoni. Anaamini kuwa kauli hiyo ya mahakama ilikusudia kumzuia kiongozi huyo wa upinzani katika kinyang'anyiro cha kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Uchaguzi mkuu nchini humo umepangwa kufanyika mwezi Novemba. Haikuwezekana kupata maoni ya viongozi wake mkuu wa idara ya mahakama wala idara ya ujasusi nchini humo kuhusiana na madai ya jaji huyo.

Bwana Katumbi kwa upande wake anasema kuwa anakusudia kurejea nyumbani DRC mwishoni mwa juma.

Chanzo: BBC
 
Bila katiba madhubuti serikali za nchi za afrika zitaendelea kutumia mahakama na bunge kama taasisi zake.Yaani Jaji anaamrishwa maamuzi na serikali au mtawala.Nakumbuka hapa mheshimiwa alifuta kesi ya lipumba Mara baada ya kuonana nae ikulu
 
Hata tuwe na katiba gani haitawezekana kuna laana fulani nadhani tuliachiwa na mababu zetu .tunahitaji kufanya matambiko ili kuondoa huo mkosi.
 
mahakama ni mhimili mkuu sana katika nchi yoyote ile duniani, sasa kama inafikia nayo inaanza kuingiliwa tujue moja kwa moja hakutakuwa na haki kwa na hasa kwa wanyonge ambao ndio tulio wengi
 
Ni fedheha kubwa sana , kumpa mtu kesi eti ili mrad asipate nafasi ya kugombea .. Cjui leo hii hao waliomshinikiza jaji wanajiskiaje ? Sisi waafrica hata kama katiba itatoka mbinguni na kila mtu anaiona ila lazima tutaibaka tu...
Kweli huyu alieturoga alijipanga.
 
Na ameshajufa pia.
 
Bila katiba madhubuti serikali za nchi za afrika zitaendelea kutumia mahakama na bunge kama taasisi zake.Yaani Jaji anaamrishwa maamuzi na serikali au mtawala.Nakumbuka hapa mheshimiwa alifuta kesi ya lipumba Mara baada ya kuonana nae ikulu
Halafu wanakutana AU meeting na kuishutumu vikali ICC! Afrika ni bara lenye watawala hovyo sana.
 
Back
Top Bottom